Duru za Siasa: Marekani (U.S) Chini ya Donald J. Trump

MASHAKA MASOKO YA MITAJI
Tumewahi kueleza uchumi wa mataifa makubwa haupimwi kwa kwa thamani za masoko ya mitaji.

Kushuka na kupanda kwa masoko ni jambo la kawaida katika biashara za kila siku

Masoko ni sehemu tu ya picha nzima ya hali ya uwekezaji na si kupima afya ya uchumi kwa ujumla

Kuna vigezo vingi ikiwemo GDP, manufacturing index, Real estate, consumer confidence, job numbers n.k orodha inaendelea

Mtakumbuka tulisema wawekezaji ni 'sensitive' katika masuala ya kisiasa,kiuchumi na jamii

Tabia ya masoko, hayataki 'uncertainty'.

Uchumi ulipokuwa unajongea wakati wa obama masoko yalivunja rekodi.
Mfano, kutoka point 6,000 hadi 19000+ wakati anaondoka. Utulivu wa Obama ulisaidia

Kwa upande mwingine masoko hupenda 'uhuru'. Kuingia kwa Trump aliyeahidi kuondoa sheria kuliamsha ari ya wawekezaji na masoko kuongeza point hadi kufikia 20,000

Hili liliitwa Trump factor kwa maana wawekezaji waliona mazingira mazuri ikiwemo kuondoa 'Obamacare' , kwa baadhi ya wawekazaji na waajiri inaonekana mzigo.

Tuliwahi kujadili kuwa kauli za mgombea, au Rais mteule si thabiti na hazina uzito

Kauli za mtawala ndizo huongoza dira za kisiasa na kiuchumi.

Trump alipo tweet hakuna aliyemchukulia kwa uzito, alikuwa mgombea na Rais mteule

Baada ya kuchukua madaraka, kauli zake zina beba uzito kuliko inavyodhaniwa

Mfano, amri ya kutaka taasisi ziondoe 'burden ' kwa ACA (Obamacare) haikuwa na maelezo

Hilo lilitosha kuonyesha mashaka na kama tulivyosema masoko hayaki uncertainty

Kuondoa TPP na kupitia upya NAFTA kulipelekea mashaka, investors hawajui nini kitafuata

Ugomvi wa Trump na Mexico kuhusu wall umeongezeka mashaka kwani nchi zenye masilahi makubwa ya kiuchumi kutoka kila upande

Exec order ya marufuku ya wakimbizi, na visa yamepelekea mshtuko US na duniani.

Kuna tension kati ya US na nchi kama Iran na sasa Iraq ambazo ni washirika wa energy
Kwa ufupi 'tension' inawafanya investors waone risk katika investment

Hayo machache yanapelekea 'uncertainty' na inakuwa reflected katika masoko kama siku ya jana ambapo thamani zilishuka. Hilo haliwezi kuwa na athari kiuchumi kwa muda huu

Athari zitakuwepo mashaka yakiendelea siku hadi siku kama ilivyo sasa
Kwa muda mrefu wawekezaji wataingiwa na hofu kwa kile kinachosemwa global conflicts.

Kama hakuna investment uchumi utakuwa na matatizo na hasa suala la ajira.
Investment Trump anayofanyia kazi inaweza kutozaa matunda yanayotarajiwa

Trump effect ipo in both ways, positive and negative
Akiwa Rais hapaswi kuamsha hisia au tension . Kauli za Trump zina effect US na duniani

ACT AG AFUKUZWA KAZI

Inaendelea
 
Hali ya uchumi (kisekta na kitaifa) unaweza kupimwa kwa kuangalia masoko ya mitaji (capital markets) pia, yanaelezea hali ya uwekezaji, yanaelezea hali ya matumizi (consumer spending) n.k. Hali ya uchumi ikiwa mbaya mfano kwenye recession na hali ya masoko ya mitaji lazima yawe mabaya.

GDP = C + I + G + (Ex - Im)

“C” ni spending ya wateja
“I” ni uwekezaji wa kibiashara
“G” ni matumizi ya serikali
“(Ex - Im)” ni thamani ya exports kutoa imports.

Thamani ya masoko ya mitaji yakipanda ni wazi:
(a) Uwekezaji utaongezeka na kukuza GDP na ajira zitaongezeka (multiplier effect).
(b) Consumption itapanda maana watu wanakuwa na hela ya ziada ya kuspend (consumer confidence nayo inapanda) na matokeo yake GDP itakua.
(c) Kuna sekta zinafanya vizuri (mtu ukiangalia index ya Dow Jones, Nasdaq, S&P 500 unapata picha, companies ambazo zimekuwa included kwenye hizi index ni wakilishi) mfano real estate, manufacturing, aviation, construction, hospitality, technology, health, oil and gas n.k. Pia unaweza kuangalia masoko ya derivatives na bonds ukiacha hayo ya hisa.


Hisa za sekta nyingi zimepanda kama construction, regional na community banks, steel companies, oil and gas n.k. Wakati sekta au kampuni zingine zinafanya vibaya zingine zinafanya vizuri. Ndivyo soko lilivyo.

Huwezi kuwa na uchumi mbaya halafu thamani ya masoko ya mitaji yakapanda. Masoko yatakuwa tu bearish badala ya bullish.

Uncertainty huwezi kuikwepa,unadeal nayo tu, ndio maana kuna 'residual uncertainty' na level zake na namna ya kudeal nazo.

Ex. Order ya kuzuia utoaji wa US visa kwenye nchi 7 ipo in total effect na ni kitu cha kawaida kwa shares za Airline companies na companies zingine zinazodeal na hizo nchi kushuka thamani. Lakini hizo haziwezi ku-drive index zote kama vile uchumi ni mbaya.

Lakini hii ni national security issue, kwa US, national security interest inakuja mbele ya faida na 'certainities' zote. Kwa mfano, Obama alitumia mda mfupi kushinikiza sanctions kwa Russia (ingawa hili lilijawa siasa) na akatengeneza 'uncertainties' nyingi tu kwa wafanyabiashara wengi.


Akapitisha amri kali za climate change, extreme na burdensome banking regulations, bila kujali ni biashara ngapi za US atazimaliza kwa gharama kubwa za compliance, kushindwa kujiendesha kwa faida na kutengeneza ajira.

Kitendo cha Rais Trump kusababisha Dow Jones kuhit 20,000 kwa mara ya kwanza kinawapa kiwewe wapinzani wake, wanahangaika kuonyesha kuwa ni kitu cha kawaida ambacho hata Obama alijaribu kufikia, mara wanadai masoko yanapenda 'uhuru' n.k.

Lakini ukweli unabaki pale pale, vitu anavyofanya Rais Trump kwa ajili ya wafanyabiashara wa US na ajira za US, Obama alikua anaviota tu.

Kitendo cha kuonyesha nia ya kushusha kodi ya makampuni kutoka 35% hadi 15% Obama hakuwahi hata kukaa kufikiria, yeye alifikiria kuongeza kodi tu.

Trump anachofanya ni kustreamline regulations, ONE IN TWO OUT, Obama alikuwa anaziongeza tu bila kujali ugumu anaosababishia wafanyabiashara na ajira za US. Rais Trump ana experience kubwa sana ya biashara, Obama hawezi kumfikia hata robo.

Utakuta wanasema hayo makampuni yanayorudi kuwekeza US yalishapanga kurudi hata kabla Trump hajawa Rais. Lakini ukiwasikiliza hao CEOs wanasema wazi kuwa bila Trump kuwa Rais wasingerudi maana US ni nchi ngumu sana kwa wao kufanya biashara, kodi kubwa, sheria kibao zisizo na maana.

Obama hakuelewa hivyo vitu, asubuhi au jioni alikuwa akijichokea anaenda kucheza golf. Mwenzake anafanya kazi masaa 20 kwa siku!, kwa mshahara wa 1$ kwa mwaka.

Nchi zilizoendelea zipo strong sana pale nchi yoyote inapotaka kuingilia masuala ya ndani yake.

Waziri mkuu wa UK aliulizwa concerns zake kuhusu ujenzi wa ukuta kati ya US na Mexico, akasema haimuhusu. Obama alienda UK akajaribu ku-influence kura za Brexit alipondwa sana akawa mpole.

Brexit ikatengeneza uncertainties nyingi but it's none of any other country's business. Kwahiyo mtu anaposema kuwa Border Wall imeongeza mashaka kwa nchi zenye masilahi makubwa ya kiuchumi na US ana kumbukumbu fupi. Halafu sheria ya kujenga physical barrier kwenye border ilishapitishwa na Congress kitambo sana, Trump anafanya kuitekeleza tu.
 
Kuna hili suala la Rais wa 44 (Obama) kuingilia namna Rais Trump anavyotawala US na kutoa 'statements' na kuchochea maandamano.

Hili halijakaa vyema na anajishusha thamani. Huyu kiongozi anajiaibisha sana bora angekaa kimya akaendelea na vacation yake huko British Virgin Islands.

Kwani sio kitu cha kawaida Successor wake hajamaliza HATA WIKI MBILI yeye anajifanya kumkosoa wakati matatizo mengi anayoshughulikia Rais Trump yalisababishwa na Obama mwenyewe. This is rare!

Suala la refugees lilisababishwa na nani? Obama ndiye aliyechochea Arab spring huko Middle East na North Africa na kutengeneza hizi terror hotbeds. Akaja akazuia refugees wa Iraq kuingia US mwaka 2011 kwa miezi 6.

Mwenzake anatafuta suluhu ya kudumu yeye anajifanya ndiye anajua American values. Wakati ana-authorise drones kuua watoto na akina mama huko Middle East alisahau kuhusu hizo values? Je George W Bush aliwahi kumkumbusha kuhusu American values?

Rais Trump ameshinda uchaguzi kwa kutumia failures za Obama mfano Obamacare, unemployment, trade deficits, bad trade deals, national debt, immigration crisis, weak border, energy dependence, kusahau coal na viwanda vya steel, high regulations, mamilioni ya watu kuwa kwenye food stamps, unmodernised military, foreign policy blunders, high taxes, homeland insecurity, good jobs leaving US, yaani vitu vingi mno.

Marais wastaafu wenzake (Democrats and Republicans) wanaendelea na maisha yao, sio kwamba hawaoni kila kinachoendelea, ila wanatumia busara zao kukaa kimya. Sasa yeye Obama alivyokuwa hana busara anachochea maandamano. So disgraceful!

Kuna mdau alisema tusimzungumzie Obama humu kwa sababu hajulikani alipo. Mwenzake hajamaliza hata mwezi!!! Kama kuna kitu kinamsumbua Obama ni kule kuondoka madarakani bila kuacha legacy yoyote ya maana, Obamacare inatupwa, climate regs zake zinatupwa, hana kingine zaidi ya kwamba yeye ni Rais wa kwanza mweusi.

Cha ajabu huwa anapenda kujiaminisha kuwa amefanya kazi kubwa kuliko Marais wote waliomtangulia,funny!!
 
snapshot_chart_api.asp


Kwa ufahamisho tu...kwa siku kama mbili hivi Dow Jones imerudi pale pale ilipokuwa kabla ya Uchaguzi na inazidi kushuka...
El Jefe said:
Trump anachofanya ni kustreamline regulations, ONE IN TWO OUT, Obama alikuwa anaziongeza tu bila kujali ugumu anaosababishia wafanyabiashara na ajira za US. Rais Trump ana experience kubwa sana ya biashara, Obama hawezi kumfikia hata robo.
El Jefe, regulation alizokuwa anaziongeza Obama zilikuwa na sababu zake, na kwa wewe kudai alifanya hivyo bila kujali ugumu anaosababishia wafanyabiashara na ajira za US, humtendei haki hata kidogo. Hatua nyingi alizochukua Obama ndizo zimefanya Trump apokee nchi ikiwa haina matatizo kama alizorithi kwa mtangulizi wake..

Nikikusoma kati ya mistari naona kama vile you have an axe to grind linapofika swali la Obama. Hili si tatizo kwako tu nimeona wengi wa Watanzania hawampendi Obama na ukitazama kwa undani ni chuki ambayo inahusishwa na ile inayofukuta kati yetu na Wakenya kwa sababu tu Obama anahusishwa na nchi alikozaliwa baba yake.

Matatizo aliyorithi Obama akiingia madarakani mwaka 2008 huwezi kuyafananisha na ya sasa anapoondoka madarakani na hii ndiyo sababu Wamarekani wengi walimlilia akiwaaga. Nakumbuka Republicans walivyokuwa wakimtaka aache kumlaumu aliyemrithi na badala yake ajikite katika kuinusuru nchi na hali mbaya ya uchumi.

Nakumbuka kwa mara ya kwanza Dow Jones ilipoanza kupanda (toka 6,000 hadi 8,000) walivyomkejeli wakidai kupanda si dalili ya uchumi kuwa mzuri lakini leo wanashabikia hiyo hiyo Dow Jones kupanda kutoka 19,000+ hadi 20,000! Ajira zilipoanza kuongezeka badala ya kumpongeza walimkejeli wakidai ni watu tu wameacha kutafuta kazi.

Sababu nyingi na hatua nyingi Trump anazoahidi kuzichukua ndizo hizo hivo zilizosababisha Marekani kujikuta kwenye hali mbaya ya uchumi mwishoni mwa utawala wa Bush. Trump kwa upande wake alikuwa moja katika wafanya biashara ambao si tu walichangamkia hali hiyo bali walinufaika nayo kupitia migongo ya wanyonge masikini.

Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni...Obama aliinusuru Marekani kutoka kwenye recession.
 
"
Mag3, post: 19530082, member: 10873"]
snapshot_chart_api.asp
Mkuu nilicheka sana siku niliposikia 'Trump effect' nikajiuliza hivi watu wana ufahamu kweli. Leo husikii tena Trump effect pengine ni matatizo aliyosababisha Obama!!!

I can't make head or tail of.. Mfano, utasikia Trump anasahihisha makosa ya Obama.
Halafu 'Ban' ya immigration imewekwa na Obama si Trump.kuna kusahihisha nini hapo?
regulation alizokuwa anaziongeza Obama zilikuwa na sababu zake, na kwa wewe kudai alifanya hivyo bila kujali ugumu anaosababishia wafanyabiashara na ajira za US, humtendei haki hata kidogo.
Obama aliwahi kuuliza, kama sheria anazoweka zinasababisha matatizo, Marekani ilifikaje katika recession?

Watu wengi hawaelewi kuwa wakati wa Bush hakukuwepo na sheria na recession ikapiga

Hawaelewi kuwa kulegezwa kwa sheria kulianza wakati wa Clinton

Ilikuwaje recession ikatokea wakati hakukuwepo sheria za Obama? hawawezi kueleza​
Hatua nyingi alizochukua Obama ndizo zimefanya Trump apokee nchi ikiwa haina matatizo kama alizorithi kwa mtangulizi wake..
Ikiwemo vita mbili na jumla ya askari 100,000+ nje
Sheria za kubana wall street, na bail out ya auto industry ambayo Trump anapigia upatu
Nchi ikipoteza kazi katika kiwango cha 600 kwa mwezi,hawaoni miezi 74 mfululizo
Nikikusoma kati ya mistari naona kama vile you have an axe to grind linapofika swali la Obama. Hili si tatizo kwako tu nimeona wengi wa Watanzania hawampendi Obama na ukitazama kwa undani ni chuki inayofukuta kati yetu na Wakenya kwa sababu tu Obama anahusishwa .
Well unaweza ku criticize kama kuna substance.

Nimewahi kuuliza, wakati Obama anachukua nchi GDP ilikuwaje? Kulikuwa na ACA ipi? Real estate ilikuwa hali gani? Auto industry ilikuwaje?
Kulikuwa na challenge gani za usalama?

Hakuna majibu, wanaamini kwavile inasemwa!

Guess what, ameondoka approval rate ikiwa 50+ nyuma ya Reagan na Clinton kidogo.

Kumpinga Obama kwa ACA halafu kumsifia Trump kwa ACA ''hewa'' inakatisha tamaa.

Hivi kweli katika wiki moja Trump amefanya reform ya healthcare kiasi cha kusema kafanya vema!!! Real kwamba exec order imeeleweka na inafanya kazi vizuri!!
Matatizo aliyorithi Obama sakiingia madarakani mwaka 2008 huwezi kuyafananisha na anapoondoka madarakani, ndiyo sababu Wamarekani wengi walimlilia akiwaaga.
Jinsi alivyo handle challenges za uchumi na usalama na kijamii

Hakuna anayezungumzia Obama alianzia wapi! Wanazungumzia GDP inakuwa kwa asilimia ndogo stangu WWII.

Niliuliza kabla ya hapo GDP ikuwa katika kiasi gani? Hakuna jibu

Hesabu zinapigwa kwa 1.3% bila kujua ilianzia wapi

Nikauliza kulikuwa na recession nagpi kati ya WWII na 2008? Hakuna jibu.

Baada ya muda hoja zinatajwa hazielezwi
Sababu nyingi na hatua nyingi Trump anazoahidi kuzichukua ndizo hizo hivo zilizosababisha Marekani kujikuta kwenye hali mbaya ya uchumi mwishoni mwa utawala wa Bush.

Trump kwa upande wake alikuwa moja katika wafanya biashara ambao si tu walichangamkia hali hiyo bali walinufaika nayo kupitia migongo ya wanyonge masikini.
Trump kawajaza wall street aliowalaani sana!

ACA wanayotaka kuifuta ingawa hawana mbadala hadi sasa, ni kwa faida ya matajiri wanaoajiri na si masikini.
 
Nilishawahi kusema hapa watu wakanishambulia. Leo narudia tena,obama anathibitisha tu kuwa yeye ni mweusi..!! Marais wetu wa africa wakishakuwa madarakani huwa wanajiona wanaakili kuliko watu wote ndo maana huamua kujiongezea muda wa kutawala kwa kubadili katiba za nchi zao.

Obama hana tofauti na akina kagame. Tofauti yake ni moja tu obama ameongoza US hivyo asingeweza kusigina katiba ili ajiongezee muda wa kuongoza.

Alichokifanya ni lile jambo la aibu la kushupaa kumfanyia kampeni yule bibi ili aje kuendeleza utawala wake. Wamarekani siyo wajinga,wakampiga chini,akaanza kupitia mlango wa nyuma kushawishi maandamano. Lkn ktk hali ya kustaabisha zaidi amevunja itafaki ya marekani ya rais mstaafu kukosoa uongozi uliopo. Tatizo la obama anajiona yeye na mkewe wana akili kuliko trump. Hizo akili ni za watu weusi tu nikiwemo mimi...!

Na kwa sasa anaanza kumuandaa mkewe kugombea urais ili aje arudi ikulu. Yaani akili zilezile za akina museven..kazi kweli kweli...!!
 
YALIYOJIRI LEO

Hapo nyuma tulieleza tukio la shambulizi la masikiti kule Quebec. Habari za awali zilitaja watu wawili
Taarifa zilizopo zinamtaja mhusika kama Alexander Bissonete na Si Mohamed raia wa Morocco

Polisi wamegundua Mohamed alikuwa anatoa msaada kwa wenzake, alipoona Polisi hakuwatambua akakimbia hadi walipomkamata. Hivyo mtu aliyekamatwa na mhusika ni mmoja tu

Tulisema pia motive yake haipo wazi na hadi sasa haijaelezwa.
Kinachoelezwa ni kuwa alikuwa shabiki mzuri wa siasa na hasa Trump.

Katika kulichukua suala hilo ili kujenga hoja baada ya sakata la maandamano Sec of press Sean alisema shambulio lilifanywa na Rais wa Morocco katika kuonyesha kuwa hatua anazochuku Trump ni njema

Ofisi ya waziri mkuu wa Canada imekanusha habari za WH pamoja zile zilizoenezwa na Fox news

Sakata la immigration na Ban limezua mengi. Kila mbinu inatumika kulionyesha ni sahihi
Bila shaka ni sahihi wa mujibu wa exec order na sheria za US, hakuna tatizo na hilo

Tatizo lililojitokeza ni namna order ilivyotolewa bila mpangilio wa kiutendaji, bila ushauri wa kisheria
Matokeo yakawa vurugu katika viwanja vya ndege na kubadilika kwa 'amri' kutokana na nyakati

Hilo limepelekea Rais Trump kupingwa na Act AG kwa kukataa kutekeleza amri na kumfukuzwa kazi

AG S. Yates alijua madhara ya kufanya hivyo, hata hivyo alionyesha kutokubaliana na tamko, na kisha kutakiwa kwenda kutetea kile alichosema ni ukiukwaji wa katiba

Sakata linafukuta kukiwa na habari kuwa maafisa kwa mamia wa state dept wanaandika dissent note

Utetezi wa sakata hilo unatumiwa na serikali ya Trump kumtuhumu Obama.
Kwamba marufuku yalitokana na amri alizoweka 2011 ku ban nchi husika.

Hili linafanyika ku spin tu kwasababu Obama alikazia visa kwa Iraq hakuweka ban.

Utetezi wa pili unaotolewa leo ni kuwa hakuna 'ban kwa waislam'. Jumapili akiwa katika TV Rudi Gullian alisema Trump alianza na ban ya waislam, kisha wakabadilisha kuwa dangerous countries

Trump ametumia neno Ban siku 3 zilizopita kama alivyotumia S.Spicer
Leo wanasema hakuna neno 'ban' na wala si kwa nchi au Waislam

Siku chache zilizopita akihojiwa na TV ya wakristo Trump alisema wakati wa Obama Wakristo walikuwa na wakati mgumu kuja US. Madai hayo hayana uthibitisho kutoka mahali popote

Inaendelea
 
snapshot_chart_api.asp


Kwa ufahamisho tu...kwa siku kama mbili hivi Dow Jones imerudi pale pale ilipokuwa kabla ya Uchaguzi na inazidi kushuka...​

Hiyo graph ulioweka hapo ina lengo la ku-potray kwa mtu asiye makini kuwa dow imeshuka sana kwa kuweka nafasi kubwa kwenye hizo grids. Dow haijarudi ilipokuwa kabla ya uchaguzi, kindly check that.

Lakini hata hapo Dow ilipo leo 19,864.09 Obama hajawahi kusababisha kufika miaka yote minane aliyokaa madarakani. Hajawahi kusababisha hata Dow Jones kufika 18,300.

Mnakuja na data mara Obama alisababisha Dow kutoka 6,000 hadi 19,000 kwa miaka 8 . Kwanza Obama aliikuta Dow kwenye 8,900+ na siyo 6,000. Pili, hata hiyo 19,000 nani alisababisha ikafika hapo on Nov. 22, 2016 kama siyo ushindi wa Trump!

Mnachotakiwa kuja nayo ni data ya Dow kutoka Nov. 8, 2008 hadi Feb. 1, 2009 kwa ajili ya comparison. Significant impact ya soko kutokana na sera za serikali baada ya Nov. 8, 2016 zilisababishwa na Trump mkizingatia Trump alianza kufanya kazi na kudeliver hata kabla ya kuapishwa Jan. 20, 2017. Obama akiwa lame duck ali-influence soko
lipi la mtaji kupanda? kitu gani alichokifanya hadi ikapanda?

Kwahiyo nawa-challenge kwamba Obama hakuwahi kusababisha Dow kufika 19,000. Prove me wrong.
 
YALIYOJIRI

Kwa mtirirko huko wa matukio hasa mawili, kutumia amri ya Obama tofauti na ilivyokuwa kuficha na hoja ya kumtuhumu kuruhusu Waislam zaidi ya Wakristo yamezua jambo jingine.

Kauli ya Trump dhidi ya Obama ilionekana na Obama kama mwendelezo wa tuhuma za Uzawa alizopigia debe miaka 5 hata ushahidi ulipowekwa, zikichangiwa na hoja za 'kwamba ni mwislam'

Alichofanya Trump ni kuamsha base yake inayoona Obama kama Raia wa kigeni na mtu aliyependelea Waislam kuliko Wakristo (insinuate).

Hilo hakulifanya kwa bahati mbaya, alichotaka ni kubadili mwelekeo wa mazungumzo hasa ya waandamanaji ili hoja zinazotokana na amri yake zitoweke

Hayo ndiyo mambo yaliyomtibua Obama huko aliko.

Kwamba, rekodi na uongo unazushwa sababu Rais mstaafu hukaa kimya

Ni uongo hadi Trump atakapotoa ushahidi wa kupendelea dini moja dhidi ya nyingine
Au ushahidi kuwa kulikuwa na 'ban' kama aliyoweka yeye kwa nchi 7

Hivyo malengo ya Trump yalikuwa mwili

1. Kubadili mjadala kwa kuzusha kuhusu madai ya upendeleo aliyofanya Obama
2. Kuzuia wimbi la waandamanaji kwa kutumia sheria wanayodai ni ya Obama

Statement ya Obama haikumaanisha kingine chochote, ni ujumbe kwa Trump kuwa kubadili au kutumia jina lake vibaya kutakuwa na majibu licha 'kustaafu'

Ni kwa kutambua kosa hili, si Trump au surrogates wake waliojibu kama ilivyozoeleka iwe kwa taarifa au kwa tweet

Wanatambua, kumjibu sasa hivi rekodi zitawekwa wazi na hali inaweza kuwa tofauti

Huenda watamjibu lakini si wakati huu.
Popularity ya Obama imeshaandikwa ya Trump inajaribiwa

Kwanini Trump amesema hivi au Obama amesema vile siyo rahisi tu, kuna sababu

Tusemezane
 
KUTAWALA UMMA SI KAMPENI (I)

Tuliyosema yanajidhihiri taratibu

Wanajamvi, tulikuwa mbali kidogo kwa siku kadhaa, tunaendelea na mjadala

Kauli yetu siku zote ilionya kutawala umma si sawa na kuendesha familia, kampuni

Obama alisema'ukifika oval office kuna ufahamu wa maisha ya watu mikononi mwako''

Siasa za dunia ya leo zinahitaji uelewa wa kihistoria, kihoja na mantiki.

Hili haliwezi kumfanya anayejifunza kuwa zuzu hapana.
Sote tunajifunza nami nikijifunza sana kutoka kwa wenzangu

Kuna mwanajamvi aliongelea 'Gerrymandering'. Unaweza kudhani ni dhana ya US, ukweli, Tanzania inatokea, tofauti ni kukosa ufahamu. Fuatilia ugawaji wa majimbo utaelewa

Tuliwahieleza siasa za US hazihitaji ushabiki au unazi , zinahitaji uelewa zaidi
Pamoja na kejeli na matusi,tuliyojadili yanajitokeza bila shaka na ndiyo tunajadili sasa

1. Tulizunguzia mbinu za Trump ya kuleta 'controversy' katika hoja ili kupoteza watu

Baadhi ya media zimeliona hilo na leo kiongozi 'upinzani' Nancy Pelosi kaliongea

Katika mazingira ya ukweli, hoja inajidhihiri.

Wiki moja iliyokosa weledi Trump alidai wahamiaji 3.5-M walipiga kura isivyo halali.

Tulisema hapa ililikuwa kupoteza umma usijadili exec order iliyosababisha taharuki

Liliposhindika akatoa kauli ya kuunda tume kuchunguza kwa kusaini exec order
Leo ni siku ya 7 halijatokea na halionekani kama litatokea. Ilikuwa kupoteza umma tu

2. ACA a.k.a Obamacare:
Tulisema hawezi kuifuta siku ya kwanza kwasababu inagusa maisha ya watu
ACA inagusa uchumi na ustawi wa jamii na haiwezi kufutwa tu kwa kalamu siku moja

Siku ya kwanza alitoa exec order kuhusu ACA isiyo na maelezo.
Hili ni katika kupoteza watu wasiohoji ACA yake ipo wapi

Trump alijua lipo kundi lake litashangilia tu iwe Marekani au kwingine na tuliambiwa 'asifiwe kwa kufanya vema katika ACA' bila kuelezwa lipi limefanyika.

Ni siku 90 na zaidi ya miaka 2 Trump hajaonyesha mbadala wa Obamacare.

Kwasasa ana msuguano akisema 'insurance kwa wote'GOP wakisema 'accessible insurance'

Hadi itakapopatikana ACA mpya, na si viraka, ACA ni legacy ya Obama na hakuna mbadala hadi sasa

Inaendelea... 2
 
KUTAWALA UMMA SI KAMPENI (2)

3.
Wall:
Trump aliwaambia watu atajenga ukuta na Mexico watalipa.
Ali tweet na kujibiwa na Mexico kwa tweet Rais amefuta ziara yake US

Siku iliyofuata Trump akampigia simu tena
Jana kampigia simu akimweleza nia ya US kusaidia kupambana na wauza madawa

Obama alikuwa na sera kusaidi nchi za Latin Amerika kupambana na madawa
Kwamba ushirika mzuri na mataifa hayo niustawi wa US. Trump anakumbatia sera Obama

Hili la ukuta baada ya kukwama alisema ataweka kodi kwa bidhaa kutoka Mexico
Kwanza, ili kulinda na kurudisha ajira nchini Marekani
Pili, kuhakikisha pesa atakazopewa na congress zinalipwa kwa njia ya kodi

Tulijadili ni jambo gumu , badala ya Mexico, watakaolipa gharama ni Wamarekani
Mexico ni mshirika mkubwa wa biashara kati yake na US.

Kuweka vikwazo kutaumiza Mexico lakini kutakuwa na madhara kwa US.
Trump kwasasa anahangaika na Mexico badala ya kinyume

4. NAFTA: Ni hoja tuliyozunguzia kuwa kuifuta ni jambo lenye madhara
Trump katika kampeni aliita 'disaster' akiilaani kwa nguvu kama chanzo cha kufa ajira

Trump hakuelewa muasisi wa NAFTA ni Republican, Reagan.
Anasema NAFTA irekebishwa kuwa '' fair free', ameona madhara na umuhimu wake

5. IC: Tulisema mapema, uhusiano mbaya wa Trump na Intelligence com utaamuumiza
Ndivyo inavyotokea ambapo siri nyingi zinavuja zikiwemo simu zake na viongozi wengine

6. Simu na PM wa Australia:
Kulikuwa na sintofahamu hata Trump kuwataka watu wasijali 'hard call'.
PM wa Aussie amelifanya jepesi, hali haikuwa nzuri hadi Trump kubwaga simu

Inaendelea....
 
KUTAWALA UMMA SI KAMPENI (3)

Haya tuliandika huko nyuma na ndiyo yatajenga hoja yetu inayofuata

Kwa kuzingatia mahusiano mazuri sana ya Trump na Putin wa Russia, uhusiano wa kindugu US na Israel, Urafiki wa Iran na Russia, na ushirika wa Iran, Russia na China, pamoja na turufu ya Taiwan na North Korea, kuna tatizo mbele ya safari.

Rais Trump atakuwa na wakati mgumu kwa siasa za nje at least kwa mwanzo wa utawala

5. Israel
Tulisema siasa za US hubadilika lakini 'siasa core' zinazoongoza US
Uhusiano wa US na Israel ni wa kipekee.

Pamoja na matatizo yote Obama aliisaidia Israel kwa silaha kama watangulizi wake

Ujenzi wa makazi Israel si suala la kupingwa na Obama, bali ni kuanzia miaka 40 iliyopita
Tofauti ilikuwa US kutotumia kura ya Veto kupinga azimio la UN

Trump katoa kauli ya kutokubaliana na upanuaji wa ujenzi kwa lugha tofauti ikiwa katika sera za US kuhusu ujenzi kwa miaka nenda rudi

Jan 1 Trump alimwambia BB Nyahu wasubiri siku 20 atabadilisha mambo. Je ni kweli?

6. Russia
Balozi wa US UN ametoa kauli ya kulaani Russia kwa yanayoendelea Ukraine
Ukisoma nukuu yetu mwanzo, tulieleza mahusiano ya kimataifa.

Kulikuwa na hoja yenye mapungufu ya weledi US wanataka uhusiano mzuri na Russia
Leo imekuwaje ''washirika'' wakanyosheana vidole UN?

Sera za Obama na Clinton zilikuwa na mapungufu gani? Je hapa si kuzitekeleza!

7. Iran
Baada ya kauli ya jana ya kulaani majaribio ya makombora limetokea jipya

Trump ameeleza vikwazo zaidi kwa Iran. Ni Trump aliyelaani sana deal ya Iran
Alichosema ni kuwa deal ilifanya US kuonekana dhaifu.

Obama aliwahi kusema siasa za US zilikuwa za Diplomasia zikifuatiwa na nguvu za kijeshi.
Majadiliano kwanza na kila option ipo mezani

Iran ikarudi mezani na deal ya Nyuklia ikapatikana. Ni bora kiasi gani ni suala jingine
Trump anakaza vikwazo kwa Iran kuliko Obama akirudia kauli 'kila option ipo mezani'

Kwa maana anasimamia sera za Obama kwa ukamilifu. Sera hizo ni

ACA au Obamacare. Hakuna mstari hata mmoja ulioandikwa katika repeal and replace

Anasimamia masuala ya Israel kama alivyofanya Obama katika ujenzi wa makazi

Ana deal na Iran kama alivyofanya Obama

Hayo ni kwa uchache. Je yanamfanya dhaifu? Hapana, anakabiliana na ukweli
Ukweli kuwa kuendesha kampuni si kuendesha nchi.

Matatizo mengi yaliyotokea wiki mbili yalitokana na attitude kuwa anaweza kama alivyofanya kwa makampuni yake. Kutawala ni jambo jingine

Tusemezane
 
MATUKIO WIKI HII US

Kama wiki zilizotangulia, wiki imegubikwa na matukioya kisiasa katika utawala wa Trump
Jaji wa Federal ametoa hukumu ya kusitisha uzuiwaji wa visa kwa nchi 7 kwa muda

Hukumu ilitaja maeneo yote ya Marekani. Kwa sheria za Marekani limetokea

Mkanganyiko ukazuka kwa wale wenye visa 'valid' iwapo watapokelewa.

Kwa wale waliofutiwa inabidi waombe upya, jambo linatakalochukua muda

Wizara ya mambo ya ndani (Homeland security) aliagiza maeneo kutii amri ya mahakama

Jana, Homeland security wakaeleza kukata rufaa mahakama ya rufani ya Marekani

Hoja:

Zuio limeathiri sehemu kubwa ya wanavyuo kutoka nje wanaosoma Marekani.
Hili limepelekea wakuu wa vyuo kuandika barua ya kupinga agizo

Shirika moja la habari Canada limenukuu taasisi moja ikisema ongezeko la wanafunzi wa kigeni kujiunga na vyuo imefikia zaidi ya silimia 500

Wanasayansi wanaofanya kazi maabara za US au mashirika yanayotumia wageni, ambazo wameonyesha hofu kubwa

Agizo la Trump lilipingwa na Act AG Sally Yates ambaye alifukuzwa kazi
Muda unavyosonga, inadhihirika hakukuwa na mawasiliano ya Trump na wizara- DOJ

Tamkoalilitoa katika kuridhisha kundi lake kwamba anatimiza ahadi.
Trump hajafanya kosa kisheria, bali makosa ya kisheria yanayomweka katika hali ngumu

Katika kuficha udhaifu wa yaliyotokea, serikali ya Trump inasema nchi hizo zilikuwa katika orodha wakati wa Obama.

Kwa miaka zaidi ya 2 Trump amemshambulia Obama kwa udhaifu na sera mbovu

Iweje katika hili akumbatie sera zile zile alizosema ni mbovu?

Hata katika kukumbatia bado kuna makosa. Tweet yake ya Leo amemshambulia Jaji kwa kumwita 'the so called' kisha kusema hukumu ya 'Ban kama alivyoita' ni ya kichekesho.

Kumbuka ametumia neno Ban ambalo wasaidizi wake wamelikanusha kwa nguvu.

Hapa kuna hoja kati ya ' restriction na Ban'

Inaendelea
 
WIKI HII US

Inaendelea.

Serikali ya Obama iliweka restrictions kwa wananchi wanaotoka nchi kadhaa
Trump ame ban wananchi kutoka nchi zinazosemwa Obama aliziwekea restrictions

Kwanza, Restriction haina maana sawa na ku ban. Restriction katika muktadha wa Obama ulilenga kuchunguza zaidi na kwa kisheria kuhusu wananchi kutoka nchi kadhaa.

Haikuwa 'blanket ' kwa kila mtu , bali ilikuwa na zuio kwa baadhi ya watu kutoka huko

Ban ni kuzia watu kuingia US ambayo kisheria haina makosa. Kimantiki ni kuzuia kabisa

Pili, Obama hakutoa kipaumbele kwa misingi ya dini.
Alisema waliokuwa persecuted kwa njia yoyote wapewe hifadhi.

Trump anasema ban yake itawafikiria Wakristo ambao wamekuwa persecuted

Mfano mzuri wa 'Ban na restrictions' upo hapa TZ.
Waziri aliweka restrictions kwa wakimbizi kutopokewa kwa makundi.

Alisema wachunguzwe mmoja mmoja . Waziri haku ban walikimbizi, ali restrict

Hoja: Kimantiki Wakristo wamekuwa target ya makundi kama ISIS kule middle east

Kwa upande mwingine waliokufa zaidi kutokana na ISIS ni waislam i.e persecuted.

Trump anapotoa favor kwa kundi moja inashadidia hoja yake dhidi ya Waislam aliyotoa katika kampeni na siku za karibuni madarakani kama ilivyodhihirishwa na R.Guillin

Tatu, Obama hakupiga marufuku wakimbizi, Trump amepiga marufuku

Ni dhahiri kwa kutoshirikiana na idara ya sheria DOJ Trump hakupata ushauri wa kutosha

Trump alidhani kuendesha nchi ni sawa na kuendesha kampuni zake.

Matokeo ni mkanganyiko mkubwa, ukichagizwa na mahakama kupinga agizo kwa muda

Trump na wafuasi wanajificha vipi kwa utetezi wa Obama ikiwa walitumia muda mwingi kuponda?

Trump anawezaja kufuata sera za Obama alizoponda kwa miaka 2+?

Inaendelea......
 
Baada ya Jaji wa mahakama kuu kutoa uamuzi wa kusitisha amri ya rais kuwazuia raia wa nchi 7 kuingia marekani, Trumo amemshambulia jaji huyo ambaye aliteuliwa wakati wa utawala wa G. W. Bush na kupitishwa na bunge la chama chake! Kupitia twiter amemuita jaji huyo "so called judge" ikiwa ni namna fulani ya kumkashifu...

Taratibu watu wataanza kuamka na kukubali ukweli kwamba huyu jamaa ni mwehu...
 

Attachments

  • tweet.jpg
    tweet.jpg
    30.3 KB · Views: 9
Baada ya Jaji wa mahakama kuu kutoa uamuzi wa kusitisha amri ya rais kuwazuia raia wa nchi 7 kuingia marekani, Trumo amemshambulia jaji huyo ambaye aliteuliwa wakati wa utawala wa G. W. Bush na kupitishwa na bunge la chama chake! Kupitia twiter amemuita jaji huyo "so called judge" ikiwa ni namna fulani ya kumkashifu...

Taratibu watu wataanza kuamka na kukubali ukweli kwamba huyu jamaa ni mwehu...

Na hao watu 140K walio-like hiyo tweet ni wehu?

Masuala ya Judiciary kupishana na Executive ni mambo ya kawaida na sio mara ya kwanza kutokea.

Usishangae hili suala likafika Supreme Court na decision ikawa tofauti hata baada ya appeal ya DOJ kukataliwa na Appeals Court.
 
Na hao watu 140K walio-like hiyo tweet ni wehu?

Masuala ya Judiciary kupishana na Executive ni mambo ya kawaida na sio mara ya kwanza kutokea.

Usishangae hili suala likafika Supreme Court na decision ikawa tofauti hata baada ya appeal ya DOJ kukataliwa Washington State.
Trump ana followers zaidi ya 23M kwa hiyo suala la post kupata likes 140k sio shida. Pia kutofautiana kimtazamo na majaji nayo sio shida na inaweza kutokea mara kwa mara.

Shida ya Trump ni hulka anayoionyesha jinsi anavyokabiliana na wote ambao wanatofautiana na yeye kimtazamo. Kama hajakubaliana na uamuzi wa jaji haina shida lakini kufikia hatua ya kumdhihaki kwa kumwita "so called judge" ameonyesha kiwango kikubwa cha utoto kitu ambacho hakipaswi kuonyeshwa na mtu mzima yeyote sembuse rais wa taifa kubwa kama marekani. Na hii sio mara ya kwanza kufanya hivi, juzi hapa alimkatia simu waziri mkuu wa Australia baada ya kutokubaliana juu ya hoja za uhamiaji. Hakuna namna nyingine ya kuita tabia hii isipokuwa "utoto"!
 
Shida ya Trump ni hulka anayoionyesha jinsi anavyokabiliana na wote ambao wanatofautiana na yeye kimtazamo. Kama hajakubaliana na uamuzi wa jaji haina shida lakini kufikia hatua ya kumdhihaki kwa kumwita "so called judge" ameonyesha kiwango kikubwa cha utoto kitu ambacho hakipaswi kuonyeshwa na mtu mzima yeyote sembuse rais wa taifa kubwa kama marekani. Na hii sio mara ya kwanza kufanya hivi, juzi hapa alimkatia simu waziri mkuu wa Australia baada ya kutokubaliana juu ya hoja za uhamiaji. Hakuna namna nyingine ya kuita tabia hii isipokuwa "utoto"!

Wamarekani wamezoea kusikia au kuona Rais Trump akitoa maoni yake na kuzungumzia masuala kama yalivyo bila kufichaficha.

Kwahiyo sio 'utoto' kama ulivyoelezea, bali ni ujasiri wa kutoa maoni yake kwa namna ya kuonyesha kutokubaliana na maamuzi ya Jaji yanayoweza kugharimu maisha ya watu, ukizingatia analo jukumu la msingi la kulinda raia wa US.

Rais Trump aliona kama Jaji James Robert anachukulia kwa wepesi suala la ulinzi.

Mimi, wewe na Majaji wote wa US hatupati intelligence briefings ndio maana Congress imempa mamlaka POTUS ya kumtoa au kumzuia mtu yeyote kuingia US.

Kuhusiana na waziri mkuu wa Australia, Rais Trump anayo haki ya kuhoji hata kukataa deal yoyote alioingia mtangulizi wake ukizingatia mtangulizi wake alifanya blunders nyingi kwenye foreign policy.

Kwahiyo hamna kitu cha ajabu hapo. Mbona mtangulizi wake alipenda TPP, Rais Trump alivyoingia kaitupa huko? na vingine vingi. Inawezekana Malcolm Turnbull alitegemea Rais Trump ata-copy na ku-paste!!

Ni kawaida kila utawala mpya unapoingia US, kunafanyika review za programs na sera za mtangulizi, ndio maana unaona Rais Trump anatupa kule programs na sera nyingi za mtangulizi wake ambazo kiukweli hazisaidii nchi.
 
Baada ya Jaji wa mahakama kuu kutoa uamuzi wa kusitisha amri ya rais kuwazuia raia wa nchi 7 kuingia marekani, Trumo amemshambulia jaji huyo ambaye aliteuliwa wakati wa utawala wa G. W. Bush na kupitishwa na bunge la chama chake! Kupitia twiter amemuita jaji huyo "so called judge" ikiwa ni namna fulani ya kumkashifu...

Taratibu watu wataanza kuamka na kukubali ukweli kwamba huyu jamaa ni mwehu...
Hata waliokuwa die-hard supporters wa Trump wanaanza kuwa na mashaka na kuanza kujiuliza mara mbili mbili, is our guy serious? Time will tell but let me on a limb and stand by what I did forecast before, his day of reckoning is fast approaching and he better pull up his socks or the honeymoon is over.

Like Abraham Lincoln once said, "You can fool all the people some of the time, and some of the people all the time, but you cannot fool all the people all the time. Of course, for some obvious reasons, the gullible cannot be expected to see anything wrong with their hero Trump immediately!
 
Back
Top Bottom