Shukran ningekuomba wewe anzisha mada hiyo maana sielewi haswa unapokwazwa ama wanapokwazwa wengine. Maana ieleweke tu ya kwamba unapofanya mambo yote ya Muungano ina maana kila kitu kinaelezwa kwa ufasaha wake ktk Katiba ya nchi hivyo sheria za nchi zinapotungwa haziathiri sheria mama. Kuacha mambo mengine sio ya Muungano inaleta nchi moja inaweza kuandika na kupanga masharti wapendavyo ktk katiba yao maadam jambo hilo sio la Muungano.Mkandara,
Mimi naona kuna mjadala mpana sana kuhusu hiyo mifumo unayojadili au kupendekeza hapa. Kwani unaposema kuwa kila jambo liwe la muungano kuna mengi sana ya kujadili katika kuchambua faida zake na khasara zake kwa nchi hizo mbili huru zilizoamua kuungana.
Mjadala huo utajikita zaidi katika nyanja hizi:
1. Kiuchumi
2. Kijamii
3. Kisiasa
4. Kiutawala
Sasa mimi ushauri wangu kwako NI KUWA TUWEKE UZI MAALUM WA KUJADILI HOJA YAKO YA KILA KITU KIWE MAMBO YA MUUNGANO ili tupate muda na nafasi pana katika kujadili katika mada husika kuliko hapa katika uzi huu.
Kwani kwa kufanya hivyo nafikiri wengi sana watanufaika na kufaidia na mada hiyo. Na nataraji itakuwa ni moja ya mada bora sana katika barza hii kuhusu muungano kama watu wote watakaochangia watapunguza jazba, chuki na kuweka kando ushabiki na kujikita katika kutengeneza FACTS na hoja zenye mashiko.
Upande wangu insh'Allah japo nipo Ziara ya ibada hapa Madinat munawar lakin nitatafuta muda kuweka uzoefu na maoni yangu kuhusu utaratibu huo insh'Allah.
hayo ni maoni na ushauri wangu kuhusu hilo kwa nia ile ile ya kuilimishana na kuhabarishana ikiwemo kupeana mawazo na uzoefu mbalimbali kwa faida yetu sote.
Nikutakia siku njema.
Mkuu wangu hakuna athari zozote zinazoweza kutokea.Kuacha mambo mengine sio ya Muungano inaleta nchi moja inaweza kuandika na kupanga masharti wapendavyo ktk katiba yao maadam jambo hilo sio la Muungano.
Shukran ningekuomba wewe anzisha mada hiyo maana sielewi haswa unapokwazwa ama wanapokwazwa wengine. Maana ieleweke tu ya kwamba unapofanya mambo yote ya Muungano ina maana kila kitu kinaelezwa kwa ufasaha wake ktk Katiba ya nchi hivyo sheria za nchi zinapotungwa haziathiri sheria mama. Kuacha mambo mengine sio ya Muungano inaleta nchi moja inaweza kuandika na kupanga masharti wapendavyo ktk katiba yao maadam jambo hilo sio la Muungano.
Shukran, nitaifanyia kazi japo mimi sii mwandishi mzuri lakini nitajihidi kadri ya uwezo wangu. Ila nakuomba sana iwe baada ya Ramadhan maana hii kitu inabidi niikalie kwa muda kuiandika.Mkandara,
Mimi nilishauri kwa nia njema sana kuwe na uzi maalum wa hoja yako hiyo na TITLE maalum yenye kuuliza au kuelezea kwanini mambo yote yasiwe ya muungano katika Muungano wa TGK na Znz?
Na hapo ungejenga hoja zako kutushawishi na sisi vile vile tungejazia nyama na hata kutoa ufafanuzi mbalimbali katika mambo mbali mbali katika nyanja ya kiuchumi, kisiasa, kiutawala na kijamii.
Kwani kifupi kuna mambo mengi a kuzingatia kutokana na historia kwa nchi zote zilizoungana zilikuwa ni nchi huru. Lakin ukiangalia Znz ina eneo la SQ Km 2000 na TGK ina Sq Km 885,800 na vile vile Population ya TGK ni zaidi ya 45 Mil na Znz ni chini ya 1.5 Mil.
Kwa vigezo hivyo tunaweza kuichambua hoja yako katika mambo makuu manne. Utawala, kisiasa, kiuchumi na kijamii.
nafikiri ukiweka uzi maalum utakuwa uzi mzuri sana na mengi tutajifunza kwayo na nafikiri unaweza kuwa uzi wa Mwaka katika JF katika nyanja ya Muungano wa Tz kama watu watakuwa serious katika kuchangia na kuacha chuki, jazba na ushabiki.
Kazi njema
hata sikuelewi kabisa, kwani Zanzibar hawakuwa na katiba yao kabla ya mwaka 2010, na hiyo katiba tuliandika pamoja au? Tunacholaumu wengi wetu ni yale makubaliano baina ya Utawala wa CCM na CUF pasipo kuwashirikisha wadau wengine ktk jambo muhimu kama hili kupelekea kuandikwa kwa katiba mpya ya Zanzibar ambayo ilitokana na makubaliano hayo.Mkuu wangu hakuna athari zozote zinazoweza kutokea.
Kwasasa Zanzibar ina katiba yake na inaweka, kuondoa, kuvunja, kubagua n.k. hakuna kilichoharibika, vipi uone ujio wa Tanganyika ndio tatizo? Kwani huoni masharti ya katiba ya znz ya 2010 ilivyoandikwa 'wapendavyo' na tukiuliza tunaambiwa si jambo la muungano.
Tukiuliza, wewe Mkandara unasema ni haki yao. Tukiuliza unasema wao ni wachache n.k.
Hujaweza kukemea wlichofanya wznz unaanza kukemea kisichokuwepo! mkuu wangu !
Tanganyika ikizinduka, sheria zitawiana, ya upande mmoja sawa na mwingine. Hakutakuwa na mgogoro wa aina yoyote ile!
Mkuu Mkandara , makubaliano ya vyama hayo hayana uhalali wa kuathiri katiba ya nchi.hata sikuelewi kabisa, kwani Zanzibar hawakuwa na katiba yao kabla ya mwaka 2010, na hiyo katiba tuliandika pamoja au? Tunacholaumu wengi wetu ni yale makubaliano baina ya Utawala wa CCM na CUF pasipo kuwashirikisha wadau wengine ktk jambo muhimu kama hili kupelekea kuandikwa kwa katiba mpya ya Zanzibar ambayo ilitokana na makubaliano hayo.
Hivyo chama cha CCM wanakubaliana na mabadilliko hayo ambayo yanapelekea kuongeza zaidi mambo yasokuwa ya Muungano. Kwa hiyo usiseme wameandika katiba mpya wapendavyo, sio kweli kwani walipata ridhaa ya rais na baraza kuu la chama cha Mapinduzi wakiwemo wajumbe kutoka bara. haya ndio mapungufu ya katiba ya mwaka 1977 ambayo bado inawapa nguvu zote za kiutawala wa dola kuamua wayatakayo wao na ndio sababu ya kuitaka katiba mpya.
Na bado haitoshi kwao wana CUF ambao wanataka mambo yote yasiwe ya muungano ili Zanzibar ijitenge kama nchi huru ili tusiwe na muungano wetu bali tuwe na Shrikisho. Haya yote yametokana na sisi kushindwa kuwapa mamlaka kamili ktk utekelezaji wa shughuli zao pamoja na Uvaaji wa koti a Muungano. Ni muhimu kuwasoma watu wanataka nini kabla hujatoa maamuzi ama majibu. Kipi kinawezekana ama hakiwezekani badala ya ku react maana ndivyo wanavyotaka. Zipo njia sahihi zinazoweza kuondoa mgogoro huu na ndicho nimekuwa nikiandika muda wote lakini wewe una react kama vile huelewi gharama za kuunda Muungano na yapi yataathiri Umoja huu.
Unajua mkuu wangu wakati mwingine acha hata kuandika ama kujibu maana unapojibu ndio unatupoteza kabisa. sasa ikiwa wewe unaona makubaliano hayo hayana uhalali wa kuathiri katiba inakuwaje tena wewe unamtaka mume amtarakie mkewe? Wewe Mtanganyika ni sawa na mtoto alozaliwa ktk ndoa hiyo unataka vipi maswala walokubaliana mume na mke uyatolee wewe maamuzi kwa sababu tu unaathirika na ndoa yao.Mkuu Mkandara , makubaliano ya vyama hayo hayana uhalali wa kuathiri katiba ya nchi.
Hakuna mahali bunge letu lilitaarifiwa mbadiliko ya katiba ya zanzibar ya mwaka 2010. Hakuna! Kama wameongea katika vikao vya CCM hayo ni maongezi ya mke na mumewe chumbani hayana nguvu za kisheria achilia mbali mantiki.
Hakuna mahali penye kumbu kumbu za kuonyesha Wananchi wa Tanganyika walitaarifiwa kuhusu ajira,bandari, TBS,ardhi n.k kuondolewa katika muungano.
Kama unavyoona ilivyo ndivyo tume ziliyokutana nayo. Muungano ulilenga S1, nchi moja na taifa moja. Hilo halitawezekana kwasababu ya Narcissism ya Wazanzibar hata leo.Nguruvi3
Tuache kurudi nyuma kuendeleza Ubishani juu ya mambo tulokwisha yatolea maelezo, isipokuwa nakuomba wewe, UKAWA na wengine wote wanaosoma mada hii waniambie wanachokifahamu wao kwa nini tume zote walojaribu kuandaa muundo mpya wa JMT walikwama ilipofikia ' Tanganyika itaimeza Zanzibar' ikiwa zitaundwa serikali 1 au serikali 3 ni gharama kubwa.
1..Je kuimeza huko walikuwa na maana gani? itamezwa vipi, na utafiti wao ulionyesha nini huko kumezwa ama kudhihirika kwa hizo gharama kubwa za serikali 3 ktk uchunguzi wao.
2. Je, Mnaweza kutoa mifano kusherehesha majibu, kisha
3. Naomba pia mnambie leo hii huu ushirika wa Shirikisho na serikali 3 leo hiii zinatoa majibu gani tofauti ambayo miaka ya nyuma isingewezekana!.
Tafadhali tusirudishene nyuma ktk mjadala tulokwisha utolea maelezo, twende mbele na kwa kituo. Naomba maelezo ya swali langu kenu nyote halafu tuendelee maana haitakuwa akili kutoa maelezo kibao wakati swala lilotukwaza kwa miaka yote hatufahamu hata ilikuwa ikimaanisha nini..
Mfano huu ni irrelevant na usiwadanganye vijana wanaotusoma. Unawachanganya mkuu. Onea huruma viumbe vya mungu! Usitumie elimu yako kupotosha.Nguruvi3 Unajua mkuu wangu wakati mwingine acha hata kuandi
sasa ikiwa wewe unaona makubaliano hayo hayana uhalali wa kuathiri katiba inakuwaje tena wewe unamtaka mume amtarakie mkewe?
Wewe Mtanganyika ni sawa na mtoto alozaliwa ktk ndoa hiyo unataka vipi maswala walokubaliana mume na mke uyatolee wewe maamuzi kwa sababu tu unaathirika na ndoa yao.
Majibu yako yapo bandiko #470 . Sina namna ya kukupendeza na majibu isipokuwa kukueleza kile ninchotaka kukueleza na si kile unachotaka kusikia.Mfano huu ni irrelevant na usiwadanganye vijana wanaotusoma. Unawachanganya mkuu. Onea huruma viumbe vya mungu! Usitumie elimu yako kupotosha.
Mkandara, Tanganyika si mtoto wa muungano hata siku moja. Tanganyika ilikuwepo kabla ya muungano.
Tanganyika iliungana na Zanzibar mwaka 1964 na kuendelea kuwepo hadi 1967 ilipozaliwa Tanzania kutoka ubavuni kwa Tanganyika.
Wazazi walikuwa wawili, Tanganyika na Zanibar. Mkataba wa muungano haukuwahi kuitaja Tanzania hata sehemu moja.
Katiba iliyopo ni ya Tanzania ambayo Tanganyika ndiye ''yaya''. Sasa znz wanapofanya makubaliano na mtoto Tanzania, mzazi Tanganyika yupo wapi?
Tanganyika si mtoto hata siku moja, ni mzazi wa muungano.Hili limekwisha halina mjadala.
Nguruvi3 Unajua mkuu wangu wakati mwingine acha hata kuandika ama kujibu maana unapojibu ndio unatupoteza kabisa. sasa ikiwa wewe unaona makubaliano hayo hayana uhalali wa kuathiri katiba inakuwaje tena wewe unamtaka mume amtarakie mkewe? Wewe Mtanganyika ni sawa na mtoto alozaliwa ktk ndoa hiyo unataka vipi maswala walokubaliana mume na mke uyatolee wewe maamuzi kwa sababu tu unaathirika na ndoa yao.
Sii kinachotakiwa haswa ni wewe mtoto kutoka ktk nyumba hiyo ukaanze maisha yako? - Now utakwenda wapi ndio majibu yangu kwa hao kina Jussa watoto wa kufikia ila yanisikitisha hata nyie ndugu zangu mmejiunga nao kwa sababu ya mazoea. Na tutakapo gawana mabo sii bado utabakia na CCM au unadhani hiyo CCM itaondoka na Zanzibar maana humjui adui yako ni kunguni uliyemvaa na nguo zako. Na kibaya zaidi hao Wazanzibar usowataka na wanaopiga kelele ni samaki wadogo sana kwani mipapa yao yote yenye kuzua mgogoro huu makazi yao yapo Tanganyika na wamewekeza Tanganyika, Zanzibar ni kwenda kununua ardhi beach, mashamba ya karafuu na minazi. Hawa ndio wasotaka wewe ukanunue ardhi Zanzibar ili wao wakaiuze kwa Muuza unga wa Kitaliani au Mjarumani. Hawa watu hawanisumbui miye kwa sababu nawajua hila zao!
Tuache kurudi nyuma kuendeleza Ubishani juu ya mambo tulokwisha yatolea maelezo, isipokuwa nakuomba wewe, Barubaru, UKAWA na wengine wote wanaosoma mada hii waniambie wanachokifahamu wao kwa nini tume zote walojaribu kuandaa muundo mpya wa JMT walikwama ilipofikia ' Tanganyika itaimeza Zanzibar' ikiwa zitaundwa serikali 1 au serikali 3 ni gharama kubwa.
1..Je kuimeza huko walikuwa na maana gani? itamezwa vipi, na utafiti wao ulionyesha nini huko kumezwa ama kudhihirika kwa hizo gharama kubwa za serikali 3 ktk uchunguzi wao.
2. Je, Mnaweza kutoa mifano kusherehesha majibu, kisha
3. Naomba pia mnambie leo hii huu ushirika wa Shirikisho na serikali 3 leo hiii zinatoa majibu gani tofauti ambayo miaka ya nyuma isingewezekana!.
Tafadhali tusirudishene nyuma ktk mjadala tulokwisha utolea maelezo, twende mbele na kwa kituo. Naomba maelezo ya swali langu kenu nyote halafu tuendelee maana haitakuwa akili kutoa maelezo kibao wakati swala lilotukwaza kwa miaka yote hatufahamu hata ilikuwa ikimaanisha nini..
Mkuu wangu alhan Wasahlan, Kwanza Eid Mubarak,Mkandara,
Ahali yangu kuna mengi sana ya kuyaongelea katika huo muundo wa sasa wa muungano kwani kuna ukakasi mwingi sana na haiwezekani abadan, asilan kuuondoa ukakasi huo.
Kumbuka Muungano wa Tanzania una sura mbili kwa wakti mmoja. Kama ukibahatika kuutazama ukitokea Znz utauoana tofauti kabisa na ukiutazama ukitokea Tanganyika. Hilo ni tatizo kubwa kitu kimoja kuonekana tofauti kutokana na upande utakaotazama dubwana hilo muungano.
Lakin kubwa Znz ni nchi huru yenye mila, sirka utamaduni wake toka dahli na dahali na wana Historia yao . Vile vile Tanganyika ni nchi huru na wakaazi wake wana mila na desturi zao na historia zao. Je itawezekana kuzificha au kuzipoteza historia hizo na mila na desturi hizo.
Mfano mzuri ni mimi mwenyewe baba na mama yangu wote asili yao Oman na mimi nimezaliwa Znz na kubwa zaidi kuanzia darsa la nne mpaka chuo kikuu nimesomea Tanganyika na hata kazi miaka 8 nimefanya Serikali ya JMTz kwa upande wa Tanganyika. Lakin tunarudi pale pale sijaweza kusahau asili yangu lakin pia kupaenzi na kupatetea pale nilipo zaliwa Znz.
Lakin Kubwa Mkandara, pamoja na mambo ya kijiografia ya TGK na Znz lakin pia tazama population ya nchi hizo yaani Znz ni 1.5 Mil na TGK ni zaidi ya 45 Mil. Lakin lingine TGK ina eneo la zaidi ya 450,000 Sq Km na Znz eneo lisilozidi 2,000 Sq Km.
Hizo zilikuwa ni dondoo tu za kukuelekeza katika kujadili nchi hizi mbili.
Lakin kubwa mimi siamini kabisa kama kuna Gharama kubwa. Kwani kama mimi kama mchumi naona ni upotoshaji tu na hadaa kwa wananchi. Wachumi wanasema kila jambo zuri ni Gharama.. Unaona hata Bunge lenu la Katiba mpya si linatumia gharama katika kutaka kupata katiba mpya.. Hakuna kizuri bila gharama.
Mimi naamini NI BORA MPATE GHARAMA KATIKA KUUNDA CHOMBO BORA KULIKO KUKWEPA GHARAMA NA KUISHI KWA MAISHA YA MASHAKA , KUTUHUMIANA NA KUTOAMINIANA kama mlivyo sasa.
Kumbukeni maneno yanakua na yakishakomaa hakuna mwenye uwezo wa kuyazuia yasilete mush'kira.
Awali ya yote Eid Mubarak.Mkandara;10185722]Kwanza, nikwambie tu ya kwamba Zanzibar haikuwa huru ila baada ya Mapinduzi! hii kubali maana al Utanisamehe lakini kusema kwamba Uhuru wa mwaka 1963 wa Zanzibar hiyo ni sawa kabisa na Uhuru wa Rhodesia November 11 1963 hivi ndivyo inavyoonekana kwa waafrika wote regardless of their race or colour
Ndivyo Ian Smith alivyotawala akimtumia Askofu Abel Muzorewa.MMkandara;10185722Hivyo sitokushauri utumie sana asili yako kuhalalisha Uhuru wa Zanzibar kwani Sultan ndiye alikuwa mtawala kabla ya Uhuru na ndiye alokuja kupata ushindi ktk uchaguzi wa mwaka 1963 kwa mchezo mchafu wa kisiasa kama aloufanya Ian Smith
Huu ni ukweli usioweza kupingika. Laiti wazanzibar wasingekuwa na faida na muungano wangeshaondoka.Kijiografia, kibiashara, kijamii na kiusalama Zanzibar inategemea Tanganyika.Ushahidi wa kufadika ni nusu yao kuishi Tanganyika kuliko sehemu nyingine dunianikandara;10185722 Swala la Population,hapa mimi nakubaliana na wewe sana tu lakini nisichokubalianana wewe ni kipimo mnachotumia kwa sababu Zanzibar yenye watu 1.3 Mil wanaweza kufaidika na soko la Tanganyika na zaidi ya fursa na hapo ajira zinazopatikana
Kuungana kuwa serikali 1 hakuwezekani.Mkandara;10185722 Udogo wa Zanzibar .Udogo sio sababu kabisa kumezwa na Tanganyika ikiwa hatutakuwa tumeungana na kuunda serikali 1. Sidhani kama New York ama Hawaii hazikufaidika kutokana na udogo wao tena katika nchi 50.
Itawezekana tu ikiwa tutaunda serikali moja maana serikali moja naweza kuimeza Znz ikawa kama Mkoa tu kwani Zanzibar haitakuwa na seirkali yake tena bali serikali moja ya Muungano.
Hivyo Muungano wa serikali 2 au 3 unaondoa swala la kumezwa na ndio maana Zanzibar ina serikali yake leo hii ambayo kwa madai yenu inapewa asilimia 4.5 tu wakati mnasahau kwamba kwenye serikali ya Jamhuri Zanzibar bado ipo katika mambo ya Muungano ambayo bajeti yake huwashirikisha wabunge wa Zanzibar.
Na matumizi na wizara zote hizi za JMT, toka viongozi wake, watumishi hadi ofisi zake kote bara na Zanzibar hulipwa na serikali ya JMT sio serikali ya Znz. Kwa hiyo tusiwasikilize sana wanasiasa uchwara ambao hupotosha aidha makusudi ama kwa kutofahamu ya kwamba JMT ina mfuko wake tofauti na mfuko wa serikali ya Zanzibar na ndio maana tuna JMT kuhudumia nchi 2 na sii Tanganyika. Kwa maana ya kwamba ktk fungu la 10 ukitoa 2 za Serikali ya Znz, JMT inabakiwabakliwa na 8, hizi 8 sii za bara bali za serikali ya JMT ambayo matumizi yake hujadiliwa ktk bunge la JMT na huduma zake hufanyika pande zote mbili.
Ndipo usipotuelewa, tunasema hivi hata kama ni 0.00001 lazima wachangie. Kwa sasa ni sifuri.Mkandara;10185722 Na wala isifahamike kwa watu kwamba hizo 8 zilitakiwa kuwa za Tangayika (bara) kama wanavyofikiria kina Nguruvi3 kwa sababu tu ya mchango mdogo wa Zanzibar ktk mfuko wa taifa wakati wanashindwa kuelewa kwamba Wazanzibar mil 1.3 waishio zanzibar ni asilimia 2.9 ya watu mil.45 wa bara, hivyo Zanzibar ikichangia asilimia 3 tu ya mfuko wa Taifa wametuzidi bara (mathlan JMT imekusanya bil.10 - bil.7.7 ni a bara na Zanzibar .3) hapa huwezi kusema ati Zanzibar wananufaika.
Hawa wanaosema haya nao ni wapotoshaji wengine ambao somo la uchumi limewapiga magoli kama Brazil na Ujarumani.
Na hapa ndipo hueleweki. Kwani sasa hivi inapata wapi?Mkandara;10185722 Kuhusu Gharama.
Watu wengi wanachukulia swala hili juu juu tu kwa kwa sababu imependekezwa serikali ya JMT kuwa na mambo ya muungano 7 tu. Hii haiwezekani mkuu wangu wa sababu serikali ya JMT hutegemea fungu kutoka serikali zake kwa ajili ya matumizi ya nchi husika. Sasa ikiwa wizara zote zilizowekwa ktk mambo 7 ya Muungano hazizalishi ila ni matumizi matupu unafikiri hiyo serikali kuu itapata wapi fedha za kujiendesha?
Si kweli, sasa hivi Tanzania inadhamini asilimia 88 ya madeni ya Zanzibar ambayo haitambuliki kimataifa.Mkandara;10185722 Na kama serikali ya shirikisho haina mamlaka kabisa ktk mambo mengine hiyo serikali itaweza vipi kuweka dhamana juu ya maswala la maendeleo ya nchi hizo ikiwa nchi hizo hazitambuliwi kimataifa?
Si kweli, na wewe kupitia uzi wako umethibitisha kuwa inawezekana.Katika uzi huo umesema ili kuondoa matatizo ya muungano, Zanzibar iruhusiwe kukopa nje(Ushahidi upo wa maneno yako)Mkandara;10185722 Nani atakaye ikopesha Tanganyika ama Zanzibar pasipo mhuri wa TAIFA maana msidhani kujiunga na UN ni kutambuliwa Uhuru wa nchi na mtawala bali hupata ridhaa ya mataifa hivyo unaweza kukopeshwa ktk miradi ya maendeleo na ukafuata masharti ya kimataifa. Tangayika na zanzbar ni sawa na mtoto wa chini ya Miaka 18 na mzazi ni JMT nani atakaye kubali kumkoposha mtoto ilihali mzazi hayupo labda awe molester!
Mkuu rudi kasome rasimu uielewe kwanza.Mkandara;10185722 Nani atakaye ipeleka Zanzibar au Tanganyika mahakama ya Dunia ikiwa nchi hizo zitagoma kulipa mikopo yake ambayo JMT imewawekea dhamana. Je, rais wa JMT akikataa kudhaminia kitu ambacho anakiona hakina umuhimu kwa taifa itakuwaje?
Na hata nchi husika wakiamua kuzitumia vibaya fedha hizo huyo rais atakuwa na mamlaka gani ya kusimamisha matumizi hayo maana hayamhusu!. haya ndio maswali tunayotakiwa kujiuliza kwanza kabla ya kuvamia kupendekeza mambo 7 ya Muungano.
Mkuu usizunguke mbuyu. Kuna mambo 14 ambayo kila mshirika atabeba.Mkandara;10185722 Halafu, kumbuka lile swala la 10-2 ikabakia 8 ya JMT hili haitakuwepo tena kwa sababu JMT haitakuwa na 10 tena bali Tanganyika na 7.7 kwa sababu Zanzibar hawatachangiza .3 zao, hivyo wao watasubiri kipenga. Na wizara za visiwani/bara hazitapungua ila kutakuwa na ongezeko la matumizi kwa mabo yote isipokuwa hayo 7 ya muungano ni sawa na kusema kati ya 22 za mambo ya muungano toa 7 kuna mambo 14 yatakuwa mzigo mpya kwa bara na visiwani ambao ni maskini.
Mkandara, wewe umesema tumechukua mambo yote na kuyafanya muungano na hilo linawanyima wazanzibar fursa( bandiko lipo ukitaka kuliona).Mkandara;10185722 Ni rahisi sana kusema kwani asilimia .3 kitu gani, ila nakuhakikishia hiyo asilimia inaweza kuvunja muungano kwa sababu haitaonekana faida ya kuwa na mambo 7 yanayo wagharimu pande zote pasipo kuwepo vyanzo vya mapato yake yenyewe. itakuja swala la mtu una deep ndani ya mfuko wako kugharamia mambo 7 wakati kuna mambo 14 muhimu kwa wananchi wako ambayo yanahitaji fedha! huu wenzdawazimu.!.