Duru-Ulaya: Kura ya maoni 'Brexit'

Nguruvi3

Platinum Member
Jun 21, 2010
14,084
2,000
ARTILCE 50 OF LISBON TREATY

Kifungu cha mkataba wa Lisbon, kwa ufupi kinaeleza

Kwanza,nchi inavyoweza kujitoa EU kufuatana na matakwa ya katiba zao

Kwa Uingereza isiyo na katiba rasmi, kura ya maoni iliyofanyika inaeleza hilo

Pili,nchi itakayojitoa itafikisha azimio baraza la Ulaya 'Eurpoean council' litakalofanyia kazi maombi kwa kukasimiwa madaraka na Bunge la Ulaya.

Majadiliano ni namna ya kujitoa na mahusiano ya siku za baadaye na EU

Tatu,Kuitoa kutakuwa na nguvu za kisheria kuanzia siku ya makubaliano, au miaka miwili baada ya hapo na upo uwezekana wa kuongeza muda katika mchakato wa kujitoa

Nne,kutokana na matakwa namba 2 na 3 hapo juu, mwanachama hatashiriki katika baraza la ulaya au kwa maamuzi yanayomhusu

Tano,Nchi ikiomba kujiunga tena itafuata utaratibu wa kifungu 49 cha mkataba huo.

Ieleweke, kura ya maoni peke yake ni mambo ya ndani ya UK,hayahusu ushiriki kwa maana siyo taarifa rasmi kwa umoja wa Ulaya.

Kinachosubiriwa ni taarifa ya UK kujitoa rasmi kufuatana na kifungu 50 cha mkataba. Ingawa kila mmoja anajua UK imejitoa, hakuna barua rasmi.

Barua hiyo ndiyo ita'trigger article 50' kwa mambo manne tulivyoyaorodhesha hapo juu

Cameron alikataa kuanzisha mchakato wa kifungu 50 kutokana na hali ilivyo UK.

Kuna hoja ya EU,UK wakiondoa wahamiaji wa EU,wananchi wake hawatakuwa na 'free movement' katika EU

Hili ndilo linamsumbua Waziri mkuu May. Hoja ya kujitoa ililkuwa kulinda soko dhidi ya Wahamiaji. Kuwaondoa ni ahadi waliyotoa.

EU ikizuia free movement ya waUK,waliokataa kujitoa wata ng'aka dhidi ya serikali yao.

May amesema hata trigger article 50 hadi mwakani licha ya shinikizo la EU.

Maana ya hii ni kuwa UK itaendelea kuwa mwanachama wa EU wakati inajipanga kujitoa. Kumbuka hadi watakapowasilisha article 5 bado ni wananchama

Theresa May anataka kuvuta muda wa kujipanga.

Kadri wanavyochelewa kuanzisha article 5 ndivyo wanavuta muda wa kuwa ndani ya EU wakijianda kuondoka, wenyewe wakisema 'Buy the time'

Tatizo, EU wamechukizwa na wanashinikiza article 50 haraka sana.

Swali, je, Theresa na akina Boris Johnson na Nigel Farage wataharakisha mchakato bila kujua wanakwenda wapi?

Kwa mantiki hii, tuangalie mafunzo yatatokanayo bandiko lijalo

Tusemezane
 

Nguruvi3

Platinum Member
Jun 21, 2010
14,084
2,000
BREXIT NA MAFUNZO YATAKANAYO

Kura ya maoni 'Brexit' imeacha mafunzo mazuri na mabaya kwetu sote

Funzo la 1
Wenye madaraka kuwaheshimu waliowapa madaraka.

Wananchi wa UK wamelalamika kwa muda mrefu matatizo yao ndani ya UK.
Hata kama ni kundi dogo sauti zao zilisikilizwa

Funzo la 2
Kuheshimu ahadi : Moja ya ahadi alizotoa David Cameron akiwakilisha sera za conservative ni , kwanza kura ya maoni ya Scotland.Pili, kura ya maoni ya ya EU.
Na tatu kutoa madaraka kwa England na Wales (devolution)

Mawili aliyetekeleza kwa bahati mbaya hakukamilisha la tatu
Hii ni ukomavu wa kisiasa na kidemokrasia kwa pande zote, wapiga na wapigiwa kura. Kwamba, kura ya mwananchi inaamua hatma yake na si viongozi.

Funzo la 3
Kuheshimu maamuzi ya wananchi
Hata pale matokeo yalipokwenda kinyume na matarajio, serikali ya UK ilisimama kuhakikisha hakuna uchakachuaji tofauti na kauli za wananchi

Funzo la 4
Kushiriki mambo ya siasa kwa wananchi bila kutegemea vyama
Kwamba waliotaka kubaki EU walikuwa wengi baada ya matokeo.
Maana yake hawakushiriki kupiga kura kwa mazoea tu. Waliojitokeza ndio waliopewa

Ni funzo, shughuli za nchi si za vyama au bunge,masilahi ya taifa yanapoingia matatani.

Mfano, katiba si suala la vyama au bunge, linatugusa wote. Ikiwa wananchi wataridhia au kudharau tu kwa kutojali, maamuzi ya katiba pendekezwa ya CCM yata athiri kila mtu

Funzo la 5
Masilahi mapana ya Taifa kuliko vyama au taasisi
Wananchi wa UK walipewa fursa bila kufungwa na itikadi za kisiasa.
Wapo Labor waliotaka kuondoka na conservative waliotaka kubaki
David Cameron alikampeni na Meya Khan wa London wa Labor jukwaa moja n.k

Kwamba suala lenye masilahi ya Taifa, Utaifa mbele bila kuwafunga watu midomo kwa kamba za vyama vya siasa

Kuvurugika mchakato wa katiba Tanzania ni zao la masilahi ya vyama badala ya Taifa.

Mchakato ulifanywa kwa mtazamo wa vyama, kuanzia bungeni na bunge la katiba.
Tume ya Warioba n.k. iliundwa kivyama badala ya uwakilishi wa Taifa. Tulifeli

Funzo la Sita
Mkumbo wa kisiasa
Wananchi wa UK walikumbwa na mkumbo wa kisiasa ambao haukueleza nini hatma yao. Kwamba, waliamini baadhi ya viongozi tu bila kufanya tathmini ya kauli zao.

Ni funzo kwetu, lazima tujenge utamaduni wa kushindanisha hoja kwa faida za umma.

Utamaduni uliozuka wa kutotaka mijadala, kutosikiliza , kuamini na kushangilia tu hatua bila kujiuliza hauna tija na utatuacha njia panda kama ilivyo kwa UK leo hii

Funzo la Saba
Viongozi kuheshimu nafasi zao
Cameron alifanya jitihada UK ibaki ndani ya EU, alishindwa baada ya kura.

Kwa kuheshimu maamuzi ya wananchi, Cameron amejiuzulu kutoa nafasi kwa wengine kusukuma mbele agenda.Hakusukumwa wala kulazimishwa

Kiongozi wa Labor Corbyn yupo katika wakati mgumu ndani ya chama chake wakimtaka ajiuzulu. Kwamba, naye kama Cameron alisimamam na EU, na kwavile wameshindwa ni muda aachie ngazi. Shinikizo linatoka ndani ya chama chake

Nasi kama Taifa tunapaswa kujifunza. Kiongozi anaposhindwa kusimamia agend , kwanza ambie ajiuzulu ikishindikana alazimishwe.Shinikizolitoke popote ikiwemo vyama vya siasa

Kuna wanasiasa Tanzania na hasa wa Upinzani wameongoza bila kutoa mafanikio.
Bado wapo madarakani wananchi na wanachama wakitegemea watafanya tofauti

Ni wakati viongozi hao washinikizwe kuachia ngazi.

Haya ni mafunzo ya kawaida na ya ujumla.

Tunaendelea na mafunzo (12) yanayotokana na EU, na mifano mingine ikiwemo wa AU, EAC, SADC na Tanzania

Inaendelea
 

Nguruvi3

Platinum Member
Jun 21, 2010
14,084
2,000
Funzo la nane
Uharaka usiozingatia mambo muhimu
EU ilikuwa imara walipokuwa wananchama wenye 'uwezo' Haraka ya kupanua EU ni sehemu ya tatizo.

Wanachama walio ongezeka wengi hali zao zilikuwa duni kiuchumi
Hilo likapelekea mataifa makubwa kubeba mzigo mzito

Kilichoangaliwa Zaidi ilikuwa 'hali' ya usalama badala ya uhalisia wa kiuchumi.

Tatizo la uhamiaji likazikumba nchi zenye uchumi mkubwa kama UK, Ujerumani

Tunaona haraka ya AU kutaka kuunda umoja wa Afrika bila kuzingatia hali za kiuchumi za mataifa.

Kwa bahati nzuri wazo hilo lilikataliwa na Tanzania ilikuwa kinara wa kupinga

Uharaka huo ulionekana EAC kwa shinikizo la kuingiza nchi nyingine kama Burundi, Rwanda na siku za karibuni Sudan Kusini

Matatizo yanayotokea Burundi na Sudan kusini yanatishia hali ya baadaye ya EAC.

Uharaka wa kutengeneza 'single currency' kabla ya kuimarisha maeneo mengine unaweza kuzua ya UK.

Inaendelea..
 

Nguruvi3

Platinum Member
Jun 21, 2010
14,084
2,000
Funzo la Tisa
Kubeba uzito wa muungano
UK wanasema, walibeba sehemu kubwa sana ya mzigo wa kuendesha EU.

Viongozi waliotaka ijitoe, walijenga hoja, kila mwezi UK ilipeleka Pauni milioni 350 EU, Pesa ambazo zingeweza kutumika kuimarisha huduma za jamii

Iwe takwimu hizo ni kweli au la , na zinapingwa, ukweli unabaki kuwa mataifa yenye uchumi mdogo yalibebwa na kwamba UK ilichangia kiasi kikubwa sana

Malalamiko mengine ni wimbi la wahamiaji lililoongeza mzigo katika sekta za kijamii kama afya. Hivyo, UK waliona wamebeba mzigo mzito katika EU

Hoja nyingine ni wahamiaji kukubali ujira wowote na kuathiri kipato cha UK

Hapa tunaona kwa nchi za EAC ni muhimu kuwepo kwa uwiano katika kuchangia

Tatizo la EU lilijitokeza Tanzania ilipokataa kuharakisha soko la pamoja.
Hoja zilikuwa kama zile za UK kuhusu soko la ajira

Kwa jicho jingine, viongozi-Tanzania na muungano wanaficha ukweli kuhusu malalamiko ya Tanganyika. Nao kama UK wana madai ya kubeba muungano

Kwamba rasilimali za kuendesha muungano ni za Tanganyika na bado wanalazimika kuchangia kuendesha serikali ya Zanzibar kama bajeti n.k.

Itakapotokea mtu akajenga hoja juu ya hili, sehemu ya jamii inaweza kuwa na mtazamo tofauti na hilo linaweza kutatiza muungano kwa kiasi kikubwa sana

Kwa Tanzania ni rahisi sana kujenga hoja. Kwamba, Tanganyika imebeba Wazanzibar wengi pengine nusu ya idadi yao.

Kwa Znz ambayo idadi ya wakazi ni chini ya nusu milioni, kiasi kinachotolewa katika muungano ni kikubwa kuliko eneo lolote la nchi

Pamoja na hayo, tuliona Zanzibar wakipinga hatua za JMT kuzuia ndege za Kenya.
Hoja ya Zanzibar ni kuwa zuio lingeathiri uchumi unaotegemea huduma za utalii.

Wakati Tanzania ikiwakilishwa EAC, kuna ufanano wa hoja ya Scotland na UK na Zanzibar na Tanzania ndani ya EAC

Ipo siku Tanzania itakuwa na msimamo wake ndani ya EAC, na Zanzibar itadai kuathirika kama ilivyo Scotland au Ireland katika EU.

Hilo litaweza kuamsha hisia za kura ya maoni kama anavyodai waziri wa kwanza wa Scotland Ms Sturgeon.

Viongozi wetu wanadhani ukifika wakati huo watatumia nguvu kuzuia.

Tunaona kwa uwazi jinsi nguvu ya umma inavyoweza kuwa kubwa kama ilivyotokea Turkey ambako mapinduzi yalizimwa na umma.

Inaendelea...
 

Nguruvi3

Platinum Member
Jun 21, 2010
14,084
2,000
Funzo la Kumi

Kuiga mambo bila kuzingatia uhalisia

Nchi nyingi zimejikuta zikiiga mfano wa Ulaya, kama muungano bora duniani.
Mifano ipo kama wa EAC, SADC, BRICKS n.k.

Kuiga tu bila kutengeneza jambo linaloshabihi maeneo husika hakuzai matokeo bora
Kwamba, ulaya wana umoja basi kila 'block' itengeneze kitu kama hicho!

Muungano wa aina yoyoteunapaswa kuangalia hali halisi ya eneo na vigezo kadhaa.
Kwa mfano, jiografia, uchumi, siasa na utamaduni na miingiliano ya kijamii.

Vigezo kama hivyo, hotofautiana kutoka eneo moja hadi jingine na hivyo ni muhimu kuviangalia na si kuangalia umbile 'structure'

Tunapotengeneza kitu kama EAC tunapaswa kuangalia kwanini tunataka, inatusaidiaje na tutaendeshaje. Si suala la kuangali EU wana Euro hivyo nasi tutengeneze kama wao
Leo wanaanza kusambaratika, sisi tutakuwa hali gani ikitokea hivyo?
 

Nguruvi3

Platinum Member
Jun 21, 2010
14,084
2,000
Funzo la 11

Nchi ni ya wananchi, watawala wanaongoza tu
Brexit inaonyesha hatma ya nchi ipo kwa wananchi si viongozi au vyama

Kwamba yapo yanayohusu Taifa, yanapaswa kushughulikiwa kitaifa
Hatma ya nchiipo mikononi mwa wananchi na si viongozi au vyama vya siasa

Viongozi wawasikiize wananchi wanasema nini hata kama hayawapendezi. Wajibu wao ni kukabiliana na changamoto licha ya tofauti za mitazamo

Conservative waliahidi kura ya maoni.
Ni uamuzi mgumu tunapoangalia matokeo na walitambua gharama yake

Hawakujificha au kutumia vyombo vya dola kuzima hoja
Walitambua, wasipokidhi haja, wataadhibiwa kwa fimbo ya sanduku la kura.

Tukiangalia EAC, maamuzi yanatoka kwa viongozi na si wananchi.
Viongozi walipoamua kuunda CoW ni ushahidi mzuri.
Kilichopaswa ni kusikilizana na hoja kuzijibu kwa mantiki.

EAC ikiendelea na mwendo wa viongozi,ipo tutasikia ''..EXIT' ya taifa moja.

Kwa upande wetu, viongozi wamekuwa wepesi kudharau kauli za wananchi.

Tulipoamua kuandika katiba, maoni ya wananchi yalipaswa kuheshimiwa.
Yupo ''mmoja'' amenukuliwa akisema, wapo katika maandilizi ya kura ya maoni

Katiba pendekezwa si maoni ya wananchi, ni ya CCM. Utaifa upo wapi?
Katiba ni ya wananchi si CCM. Kuendelea na mchakato ni kudhara wananchi

Uongozi si nguvu za kidola ni dhamana ya wananchi.
Hatutafanikiwa tukiwa vipande, na hatufanikiwi tukikimbia tatizo, kulificha au kulaghai.

Tutafanikiwa tukikabiliana na tatizo kama ilivyo UK kwa sasa.

Tusemezane
 

Nguruvi3

Platinum Member
Jun 21, 2010
14,084
2,000
ARTICLE 50 , LISBON TREATY

UK sasa ipo katika hatua za ku trigger article 50 ya Lisbon Treaty ikiwa mwanzo wa kujitoa EU kwa kufuata taratibu. Hii ni baada ya Bunge kuridhia

Tukio kubwa ni lile la Scotland kutaka kura ya maoni kuamua ima ibaki au kuondoka katika UK
Katika kura ya Brexit asilimia 60 ya Wascot walitaka UK ibaki wakieleza faida za kiuchumi ndani ya EU

'Waziri mkuu' anayejulikana kama First Minister amelieleza bunge la Scot kuhusu kumwandikia PM wa UK ili waruhusiwe kuamua hatma yao akiunganisha suala la Brexit na kura ya maoni ya kujitoa

Mzigo huo wa kumaua ametupiwa PM May na wachunguzi wanasema hilo linaweza lisitokee hadi pale mchakato wa article 50 ya Lisbon treaty utakapokamilika.

Katika kipindi hicho mengi yanaweza kutokea na kubadilisha mwelekeo, lakini hadi sasa Scotland wameng'ang'ana na msimamo wa kura nyingine ya maoni

SOMO
Kwa mara ya kwanza Scotland walipiga kura ya maoni baada ya kelele za muda mrefu
Ndivyo ilivyo hapa nyumbani na suala la Zanzibar ingawa hawajapewa fursa ya kura ya maoni

Scotland wamekaa katika bunge lao kama ambavyo ZNZ inaweza kukaa katika BLW
ZNZ ina nafasi ya kutumia BLW kutaka kura ya maoni ili waamue hatma yao badala ya kulalamika

Kwanini scotland inawezekana kujaribu kwa taratibu sisi tudhani hatuwezi kufanya hivyo?

Tusemezane
 

Nguruvi3

Platinum Member
Jun 21, 2010
14,084
2,000
MKATABA WA LISBON

Mkataba wa Lisbon pamoja na mambo mengine unaeleza namana nchi inavyoweza kujitoa katika EU kwa kifungu maarufu cha 'article 50'

Kifungu kinaeleza utaratibu wa nchi inayotaka kuondoka EU.
Wasomi na wachambuzi wanakiita 'vague' hakifafanui utaratibu mzima

Kwa uchache kifungu kinaeleza anayeyjitoa aandike barua kwa baraza-EU

Britain inatakiwa kufikisha kifungu hicho kwa mchakato wa miaka 2

Kifungu hiki kiliandikwa katika mazingira ya kuleta ugumu wa kujitoa
Haikufikiriwa mwanachama kwa EU angaliweza kufikia hatua hiyo.

Jambo la kufikirisha,aliyeandika vifungu vya Lisbon Treaty ni Raia wa UK

Rais wa EU BwJuncker alisema ' si talaka ya urafiki, hata hivyo hakukuwa na pendo'
Not amicable divorce, but there was no love. ikieleza uhusiano wa EU na UK

Waziri mkuu Cameron amekataa ku-trigger article 50
Cameron anasema kiongozi ajaye ata- trigger the article 50.

Kuna article 49 inayoeleza mwanachama kujiunga tena baada ya kujitoa
Na article 48 inayoeleza uwepo wa majadiliano ya hatma ya ushirika baada ya talaka

Haya yanaisumbua sana UK sasa hivi. UK inataka majadiliano kuhusu ushirika wake na EU, wakati EU wanataka UK ku trigger article 50 haraka.

EU inataka Uingereza iondoke kwa sababu mbili

1. Kuondoa sintofahamu 'uncertainty' hasa ya masoko ya uchumi

2. Kuzuia domino effect inayoweza kutokea wakati wa mijadala ya article 50

Hali ya masoko imetulia, kinachosumbua ni hatma ya ushirika wa EU na UK.

Majadiliano ya mikataba ya biashara na uchumi, na hali ya wafanyakazi wa EU-UK, free movement na ushirika wa taasisi chini ya EU ni masuala nyeti yanayohitaji mjadala

Yakiendele, ndani ya UK kuna mitafaruku Scotland, Ireland na vyama vya siasa vya UK.

Ndani ya Labor wabunge wanamtaka Jeremy achie ngazi
Conservative wanamuona Boris Johnson kama tatizo la baadaye

Nigel Farage wa UKIP akikumbana na upinzani si UK tu bali katika EU.

Tutendelea na mjadala huu mrefu

Tusemezane
Ule wakati umewadia, UK wame trigger article 50 ya Lisbon treaty kuondoka rasmi EU. Kinachofuata sasa ni mchakato ukiongozwa na article 48

Kama atahitaji kurudi mbele ya safari(unlikely) itabidi itumike article 49

Tunasema unlikely kwasababu kuna sintofahamu Scotland.
Bunge lao kimepitisha mswada wa kuondoka UK, ambapo PM Theresa akipinga

Hapa kuna machungu matamu.
Kuondoka EU ilionekana maamuzi ya wananchi, vipi Scotland kuondoka iwe tabu?

Katika kura ya maoni, Scot kwa asilimia 60 ilikataa kuondoka EU. Hili lilizingatia hali ya uchumi na umuhimu wa EU. Hata hivyo wanasiasa wanalitumia kama karata

Kwa upande mwingine England kwa wingi walikataa kuondoka EU pia

Kura ya maoni ilichagizwa sana na vitu viwili
Nationalists waliojitokeza kukataa EU
Wananchi waliodharau matokeo ya kura ya maoni wakiamini haitawezekana kutokea

Wananchi wa UK hasa wa England wana wasi wasi na hali ya uchumi
Ndiyo maana kuna jitihada za kurudisha ujirani mwema kama inavyoonekana ziara ya Duke of Edim. Prince William

Wakati huo huo PM May anakabiliwa na changamoto nyingine. Wakati akipooza suala la Scot linaloonekana kuchukua kasi, anahitaji kuwasikiliza washirika wengine wa UK

Kuna faida na hasara ambazo ni mapema mno kuzibaini

Tutajadili zaidi
 

General Mangi

JF-Expert Member
Dec 21, 2013
14,969
2,000
Mkuu Nguruvi3
Mjadala wa Brexit wazidi kupamba moto,

Theluthi ya wabunge waukataa mpango wa PM May kujiondoa Eu.

Kiongozi wa Upinzani awasilisha kura ya kutokuwa na imani na Waziri mkuu jana na kura inapigwa leo....

Je kuna hatima ya UK kuondoka EU hila negotiation yoyote na EU?

Mana muda ushaenda na mwisho ni 29th March

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Nguruvi3

Platinum Member
Jun 21, 2010
14,084
2,000
Mkuu Nguruvi3
Mjadala wa Brexit wazidi kupamba moto,

Theluthi ya wabunge waukataa mpango wa PM May kujiondoa Eu.

Kiongozi wa Upinzani awasilisha kura ya kutokuwa na imani na Waziri mkuu jana na kura inapigwa leo....

Je kuna hatima ya UK kuondoka EU hila negotiation yoyote na EU?

Mana muda ushaenda na mwisho ni 29th March
EU wametoa muda zaidi hadi July kama UK watahitaji ili kuweka mambo yao sawa. Hili suala ni gumu sana kwa kuangalia jiografia na interest za kiuchumi
Theresa May ame survive kura zote za kutokuwa na imani kwasababu chama chake kinasimama naye
Linapokuja sula la EU wabunge wa chama chake wanagawanyika na kuongeza nguvu kwa upinzani

Kwanini wanamuunga mkono Theresa na hawataki sera zake?
Wabunge wanafahamu kurudi katika uchaguzi na suala la Brexit conservative watapoteza sana
Hivyo wanataka kubaki na uongozi wa nchi kwa kumkumbatia May

Pamoja na hayo, wanaogopa kuwa mrengo wa kushoto ukichukua madaraka huenda Brexit ikafutwa

Hapa uelewe, conservative si kwamba hawataki Brexit, wapo wanaosema hawataki negotiations, yaani UK iondoke tu, wapo wanaosema kuwe na makubaliano na EU na wapo wanaunga mkono kutojitoa kabisa

Kinachotokea ni conservatives kutaka ku retain power na kuwa na leverage katika Brexit
 

Nguruvi3

Platinum Member
Jun 21, 2010
14,084
2,000
BREXIT YAMUONDOA THERESA MAY

Waziri mkuu wa UK Bi Theresa May atajiuzulu nafasi yake mwezi June, 7. Hii ni baada ya Brexit kutokuwa na majibu ya nini mwelekeo.

Kama tulivyowahi kujadili miaka 3 iliyopita, kujitoa Brexit si suala rahisi. Pamoja na ukuu na ukubwa wa uchumi mataifa bado yanategemeana. Kwamba, EU ilianza UK ikajiunga na kujitoa na kisha kujiunga tena. Hivyo wahafidhina walipaswa kuelewa nguvu iliyopo

Hakuna maafikiano, wapo wanaotaka kutoka bila deal kwasababu wanataka tu kutoka

Wapo wanaotaka kutoka lakini kuwepo na deal na EU kuhusu mahusiano ya maeneo kadhaa

Wapo wasiotaka UK ijitoe kabisa katika EU

Yapo makundi kama Ireland na Scotland yenye masilahi tofauti na England na Wales kule EU

Kujitoa EU si jambo rahisi kwakuzingatia masilahi ya UK.
Pamoja na fursa zote walipewa bado imekuwa ni jambo zito na lenye mitazamo tofauti

Lakini pia ni funzo kwa maeneo mengine ikiwemo Tanzania. Wale wanaoshadidia kuvunja muungano hasa wa visiwani wawe tayari kukabiliana na matokeo kama ya UK

Kwa eneo kama ZNZ ambalo kijiografia, utamaduni n.k. inafungamana na Bara kuliko UK inavyofungamana na EU, ikitokea kama ilivyokuwa UK yale yale ya UK yatajitokeza

- Wapo Wazanzibar watakaotaka kujitoa tu kwa matarajio ya misaada ya Oman n.k.
-Wapo Wazanzibar wanotaka muungano uendelee kwani unarahisisha maisha yao
- Wapo Wznz wenye masilahi yao bara ambao kwao kujitoa ni maafa

-Wapo Wazanzibar wanaotaka Zanz ijitoe lakini kuwe na mahusiano maalumu na Bara
Kundi jili limejificha katika kile wanachokiita muungano wa Mkataba.

UK ni taifa kubwa kiusalama na kiuchumi. Ndani ya EU, UK ilipewa fursa maalum ili kukabiliana na mazingira yao. Waliruhusiwa kubaki na pesa yao, taratibu za uhamiaji n.k.

UK ilipoamua kujitoa walioongoza mpango huo hawakuona nini kilicho mbele yao
Waliongozwa na umimi na usisi wakiamini wanaweza kusimama wenyewe
Kiongozi wa kujitoa Nigel Farage akiwaongoza akina Theresa May sasa maji yashingo

Haya tunayaeleza bila kuwa na maana ya kutozungumzia muungano au hata kuamua hatma yake. Hoja iliyopo hapa ni kuwa kila jambo linalofanyika lazima liangalie jamii kwa upana wake

Ni muhimu kuwa na plan A, B, na C ili muda ukiwadia kama utakuja yasitokee ya UK

Tusemezane
 

Kichuguu

Platinum Member
Oct 11, 2006
11,101
2,000
Ulaya (na marekani) sasa hivi zimegubikwa na umaskini ambapo wamekuwa wanatafuta mchawi. Trump aliwaambia wamarekani kuwa umaskini wao unatokana na wahamiaji. Ulaya nayo imejiaminisha hivyo: Brexit ilikuwa ni matokeo ya imani hiyo.hiyo. Watu waliozowea kutawala na kupata kila kitu rahisirahisi, moto umewawakia, inabidi wafanye kazi sana tena kwa bei ndogo ili washindane na wachina mambo yanakuwa hayaendi. Kwa hiyo wamebaki na lawama kila kona; jambo lililomfanya binti yule aache ngazi, ni kiburi cha waingereza. Wamesahau kuwa hawana dola ya dunia tena ila bado wanajiaminisha kuwa wanaweza kuitawala Ulaya. Binti kawaambia kwa kuwabembeleza kuwa wanayotaka hayawezekani lakini bado hawamskii;mwishowe ninti wa watu akaachia ngazi akilia,
 

Nguruvi3

Platinum Member
Jun 21, 2010
14,084
2,000
"
Kichuguu, post: 31633128, member: 348"]
Ulaya (na marekani) sasa hivi zimegubikwa na umaskini ambapo wamekuwa wanatafuta mchawi. Trump aliwaambia wamarekani kuwa umaskini wao unatokana na wahamiaji.
Katika kutafuta mchawi hawana mchawi wanayemjua ni hisi tu.
Marekani sasa hivi kuna mamilioni ya kazi yanayohitaji watu, tena kazi zinzolipa vizuri
Hawa Wamexico ni waokota machungwa na wapaua nyumba
Uchawi ni kuwa hizo ndizo zilikuwa kazi zao hivyo wanajikuta wakigombea na wahamiaji

Chuki kubwa ni pale mhamiaji anapokwenda na kujinyima akitafuta kwaelimu
Muda mfupi tu wanamuona huyoo anaanza kuchipua. Hili jambo linawatia kinyaa sana
Lakini ukiangalia kwa undani ni matatizo yao. Hivi mtu anawezaje kutoka familia isiyomudu kununua viatu akamwacha mzawa wa Marekani au Ulaya akihaha?
Ulaya nayo imejiaminisha hivyo: Brexit ilikuwa ni matokeo ya imani hiyo.hiyo. Watu waliozowea kutawala na kupata kila kitu rahisirahisi, moto umewawakia, inabidi wafanye kazi sana tena kwa bei ndogo ili washindane na wachina mambo yanakuwa hayaendi.
Ulaya nalo ni tatizo lile lile la kuamini wachawi ni wahamiaji. PM Tony Blair aliwaambia ikitokea wahamiaji wote wakaondolewa kuna sekta kama ya afya zita ''collapse'' kwa kukosa watumishi
Swali la kujiuliza ikiwa kazi za afya zinalipa, inakuwaje basi watoto wao wasisome na kuzichukua wakiwa na advantage ya lugha na rangi?
Kwa hiyo wamebaki na lawama kila kona; jambo lililomfanya binti yule aache ngazi, ni kiburi cha waingereza. Wamesahau kuwa hawana dola ya dunia tena ila bado wanajiaminisha kuwa wanaweza kuitawala Ulaya. Binti kawaambia kwa kuwabembeleza kuwa wanayotaka hayawezekani lakini bado hawamskii;mwishowe ninti wa watu akaachia ngazi akilia,
Binti May ni mmoja wa wafuasi wa Nigel Farage ambao ni ultra-right. May kama Farage aliamini kwa uyakinifu kabisa anaweza kuitoa UK ndani ya EU bila misuko suko, akaamua kumpiga kikumbo Cameron

Kilichowaponza ni kutoiangalia historia. Watu wengi wanadhani EU ya leo imeanza karibuni
EU imeanza miaka mingi, UK walichelewa kuingia kisha wakajitoa halafu wakarudi
Walishindwa kuelewa Ujerumani ina nguvu sana katika Ulaya na Angela akaweka ngumu

Kwa hali ilivyo wapo wanaotaka kujitoa tu kwasababu ya kubaki na UK yao na kwamba sheria zitungwe Westminster na siyo Brussels.
Wapo wanaotaka kujitoa lakini wakiamini ustawi wao upo katika ushirika na EU
Wapo wanaoona ni dhahma kujitoa waendelee na EU

Unapokuwa na makundi hayo matatu ni ngumu sana kupata muafaka wa kura
Kimahesabu ni kuwa kuna 1/4 ya wanaotaka EU ijitoe bila sharti, waende zao
Kuna 1/4 inataka wasijitoe kabia EU. Kuna 1/2 inayotaka wajitoe lakini kuwe na deal na EU

Hivyo basi hakuna 1/4 inayomeguka kuunga mkono 1/2 inayotaka kujitoa kukiwa nadeal
Kila kundi lenye 1/4 lipo intact na misimamo yao. Hapo ndipo kura inapogoma kila ikiitishwa

Lakini pia kuna factor nyingine, Ireland na Scotland wao wanataka kubaki na EU
Kwenda kinyume na ''nchi hizo mbili'' ni kutishia muungano wa falme ''union jack'

Ujerumani na Ufaransa wameongoza EU kwa kuweka mashrti magumu kwa UK makusudi
Kwasasa EU ni stable sana, vile vinchi vilivyokuwa vinataka kujitoa sasa vimekaa kimya
Baada ya baba yao UK kuhenyeshwa hatusikii sauti za kujitoa toa kama ilivyokuwa awali
 

Mwalimu

JF-Expert Member
Aug 21, 2008
1,543
2,000
Toka mwanzo wakati kina Nigel Farage wanaimba wimbo wa brexit walikuwa wakihanikiza zaidi zile beti tamu kwamba uingereza itakuwa paradiso ikijitoa EU. Walishindwa kuwa wakweli juu ya GHARAMA wanapaswa kuziingia kwa kwa kujitoa EU wakawa wanaimba tu kwamba wakijitoa tu basi mambo yatawanyookea! Matokeo yake ndio haya sasa reality inawatandika wamebaki na kizunguzungu.

Wimbi la brexit lilichagizwa na siasa za kihafidhina europe zilizopata nguvu kutokana na wimbi la wakimbizi wa syria na iraq... hapo ukiongezea na ujio wa trump ambaye amekiwa akihanikiza wimbo huo huo wa kuwachukia wahamiaji.

Momentum ya wahafidhina europe imepungua nguvu kidogo kutokana na uimara wa EU chini ya Ujerumani.... pia kushindwa uchaguzi kwa mhafidhina Marie Lepen wa Ufaransa dhidi ya Macron. Marie alikuwa ameahidi akishinda ataanzisha mchakato wa Ufaransa kujitoa EU (FREXIT) . Na kubwa zaidi ni watu kumuona trump katika rangi zake halisi kuwa sio kiongozi wanayeweza kumtazama kama reliable ally.
 

Bongolander

JF-Expert Member
Jul 10, 2007
5,051
2,000
Kinachoendelea sasa ni kuwa kati ya watu 10 wanaowania nafasi ya kuwaongoza Torries, nane wamewahi kutumia mihadarati. Kwa hiyo kuna uwezekano mkubwa kuwa UK itakuwa na kiongozi ambaye ni teja. Lakini issue ni kuwa Uingereza sheria sio msumemo, kwani wengine waliotumia mihadarati kama hao hawaruhusiwi kupata kazi popote na maisha yao yanaharibiwa kabisa, lakini hawa kwa kuwa wengi wao ni wazungu, wameruhusiwa kuwa mawaziri.
 

Nguruvi3

Platinum Member
Jun 21, 2010
14,084
2,000
JOHNSON NA BREXIT
AAHRISHA BUNGE KUCHUKUA NJIA YA MKATO

Sakata la UK kujitoa EU linaendelea likichukua sura mpya.
Waziri mkuu (PM) Johston ameamua kuahirisha Bunge hadi UK itakapojitoa October 30

Boris Johnson alichukua madaraka baada ya mama May kushindwa na fupa hilo kubwa
Kwa utaratibu wa UK, Waziri mkuu anatokana na chama chenye Wabunge wengi
Kwasasa Boris ana kura moja zaidi ya kumwezesha kufanya jambo (majority)

Hii maana yake ni moja, kwamba, hawezi kufanya lolote akapoteza hata kura moja.

Boris amechukua madaraka kutoka kwa May kwavile Conservative ndio wengi Bungeni
Kwa utaratibu wa kawaida, ili apate mandate inambidi aitishe uchaguzi.

Kwa kuangalia timbwili la Bexit , Boris ana uhakika huenda chama chake kikashindwa
Wabunge wamegawanyika na hivyo kupata 1/2 tu ni jambo gumu achilia mbali 2/3

Kwa mantiki hiyo, Boris ameamua kuahirisha Bunge baada ya kupata ''ridhaa' ya Queen.
Inelezwa chini chini Queen anataka UK ijitoe kwa kuchelea kupoteza nguvu za kimamlaka.

Nyuma ya Boris yupo Trump aliyeahidi kufanya biashara na UK ikiwa nje ya EU.
Huu ni mtego mkubwa kwani Trump haaminiki na mifano kama Japan, S.Korea n.k ipo

Kubwa zaidi ni kuwa biashara pekee haihakikishii maisha bora kwa mwananchi wa kawaida.
Biashara kama itafanikiwa itakuwa miongoni mwa Matajiri na serikali. Mwananchi Je?

''Free Movement of persons goods services and capital'' yanawaumiza vichwa Waingereza.

Kuna suala la North Ireland na Scotaland ambayo si tu yataeleta sintofahamu bali pia yanatishia uwepo wa UK kama Taifa moja

Ugumu wa kujitoa si jambo rahisi kiuchumi kama inavyoonekana kwa Boris

Alichokifanya Johnson ni kuahirisha Bunge hadi Octoba 31 siku moja baada ya Brexit ili kukwepa midahalo. Kwamba, Wabunge wakirudi mjadala umefungwa, wanasonga mbele.

Baadhi ya Wabunge wakiwemo mawaziri wakuu wamekwenda mahakamani kupinga hatua hiyo ya mkato anayotumia Boris. Haieleweki nini kitatokea kwani kila jambo linaelea hewani.

Kama atafanikiwa kuiondoa UK ndani ya Brexit, Boris itabidi aitishe uchaguzi ili apate ''mandate' ya wananchi wote. Johnson anafahamu hilo linaweza kuhitimisha u-PM wake hata hivyo ana mission moja kuiondoa UK.

Madhara ya kiuchumi yatakuwa na sehemu mbili, ya muda mfupi na muda mrefu.
Madhara makubwa yatakuwa ya muungano wa falme( UK).

Scotland bado si suala mtambuka mezani, N.Ireland itahisi maumivu kwa haraka na ukali sana

Wawili hao wanaweza kuleta tafrani katika muungano wa falme na kuchagiza England na Wallace nazo ziangalie masilahi yao. Hilo likitokea bendera ya Malkia '' The Union Jack' itakuwa njia panda

Tusemezane
 

Mwalimu

JF-Expert Member
Aug 21, 2008
1,543
2,000
Boris Johnson alisema lazima UK iondoke EU ikifika Oktoba 30 come what may hata bila deal yoyote. Na amefanya hivi kwa lengo la kushinikiza EU kulegeza msimamo wao kuhusu deal ya kujitoa iliyopo mezani ambayo bunge la uingereza imeikataa mara kadhaa. Bahati mbaya hawajajiandaa kwa ajili ya kujitoa bila deal yoyote na ndio maana Boris kaamua kupeleka mambo kibabe.
 

Nguruvi3

Platinum Member
Jun 21, 2010
14,084
2,000
BORIS JOHNSON AENDELEA KUGEGEDA FUPA
BUNGE LAMWEKEA NGUMU

Boris Johnson amekumbana na kizingiti kingine baada ya jaribio la kuahirisha Bunge
Kura zilizopigwa zilimgomea Boris kuitisha uchaguzi wa haraka ndani ya wiki sita

Boris aliamua kuitisha uchaguzi kwa kuelewa kuwa huenda angepata wabunge wengi zaidi.

Tatizo linalojitokeza ni kuwa katika Wabunge wa sasa sehemu kubwa iliungana na Wapinzani wa Labor mara mbili kupiga chini hoja zake za uchaguzi

Kuitisha uchaguzi ni katika kutapa tapa kwani ngoma ya kujitoa si nyepesi kama alivyodhani
Katika mazingira yalivyo ambayo Johnson anajua hata Uwaziri mkuu anaweza kupoteza, hii ilikuwa ni kamari kubwa kucheza.

Ni kamari ya ''liwalo na liwe' kwani mbele kumefunga nyuma hakuendeki.

Wabunge wengi hawataki kujitoa bila deal na EU, wakati Boris akisisitiza wajitoe tu.
Tena ameapa ni bora afie katika kidimbwi cha maji kuliko kuomba EU imueongezee muda

Hakuna anayeweza kutabiri hali ya baadaye ya UK itakuwaje kutokana na mfungamano unaoendelea ambao hauna majibu.

Wahafidhina wanasema kura ya kujitoa ilishafanyika na hawaoni sababu za deal.
Lakini pia miongoni mwa wahafidhina wapo wanaosema kujitoa sawa, lakini kuwe na deal

Waliberali na sehemu kubwa ya jamii inasema mahusiano na EU ni muhimu.
Kujitoa lazima kuwe na deal kulinda masilahi ya UK barani Ulaya.

Katika nchi ambazo kura inalindwa, inaheshimiwa na inasimamiwa suala la kupiga kura ni muhimu sana.

Ilikuwa wazi kwamba UK haitajitoa kutokana na kura za maoni na mitazamo ya wengi

Tatizo lilijitokeza kwa watu kutopiga kura kwa kuamini itatokea kama wanavyodhani
Hilo linawagharimu wa UK waliotoka kubaki ndani ya EU.

Lakini pia kupitia yanayoendelea tunajifunza mambo mengi ya siasa zilizokomaa

Kwanza, hakuna ubabaishaji katika kuhesabu kura za Wabunge.
Katika nchi masikini na zinazoendelea, ''maafisa'' wangehusika kupanga matokeo. Si UK

Pili, licha ya kuwatisha wabunge wa Conservative kwamba ''watakatwa'' majina wakati wa uchaguzi, bado Wabunge hao wamesimama kwa misimamo yao iwe kujitoa au kubaki.

Ni kupitia misimamo hiyo Wahafidhina wamemkwamisha Boris mara mbili ndani ya Bunge.

Wabunge wanaamini katika masilahi mapana ya nchi na si yao.
Kuwakata majina hakuzui kusimamia kile majimbo yanachokitaka bora kwa masilahi ya nchi

Sakata zima linaendeshwa kisiasa bila kuhusisha vyombo vya dola kwa namna yoyote
Kwamba siasa inachukua nafasi yake badala ya vyombo vya dola kuingilia kati, kuvuruga au kupindua maamuzi ya wananchi.

Tatu, UK ni Taifa kubwa kiuchumi, kisiasa, kiulinzi na hata kiutamaduni.
Ni taifa lililokuwa na makoloni yake yaliyobaki na alama ya commonwealth.

Pamoja na yote hayo UK inaishi katika kivuli cha EU kwa maana kuwa kuachana na EU si jambo rahisi kama inavyodhaniwa.

Mkanganyiko huu unatueleza jambo hasa nchi zenye mahusiano ya karibu.

Tusemezane
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom