Duru-Ulaya: Kura ya maoni 'Brexit'

Nguruvi3

Platinum Member
Jun 21, 2010
15,626
32,047
Wanajamvi kwa ujumla,

Tarehe 23 June 2003 ni siku ya tukio muhimu katika bara Ulaya. Britain itapiga kura ya maoni (referendum) kuamua ibaki Ulaya (EU) au itajiondoa. Hii si mara ya kwanza Britain kuwa katika mazingira kama haya kuhusu EU.

Huko nyuma UK si kuwa ilikataliwa kujiunga mara 3 lakini ilishaoiga kura ya maoni. Hivyo, ni tukio linalojirudia likiwa na sura tiofauti. Tutafafanua utata na historia EU, mikataba kama Rome treaty, Maastricht n.k.

Hoja ya kuondoka/kubaki EU inayojulikana kama BREXIT inasimamiwa na conservative.

Conservative walitumia manung'uniko ya wananchi kama platform ya uchaguzi dhidi ya Labor. Manun'nguniko yalijikita katika maeneo matatu

1. Kura ya maoni kuhusu Scotland kuondoka au kubali ndani ya UK
2. Kura ya maoni kuhusu UK kuondoka au kubaki ndani ya EU
3. Hoja ya nafasi kwa washirika wa UK kuwa na mamlaka Zaidi, England, Wales na Ireland

Moja la kura ya maoni ya Scotland limeshapatiwa majibu baada ya wengi kuamua kubaki. Kwasasa hoja ya washirika kupewa mamlaka yao kama Scotland linaendelea kwa kasi. Hata hivyo, kubwa ni hili la referendum kuhusu Brexit.

Referendum itaamua mustakabali wa Britain katika Ulaya, mahusiano na washirika kisiasa au kiuchumi kupitia mikataba mingine likiwa na impact kubwa future ya Britain. Referendum imewagawa Waingereza katika makundi makuu mawili. Wanaotaka kuondoa na wanaotaka kubaki ndani ya EU.

Hili si suala la chama bali la kila mmoja na maono yake, ndiyo maana conservative wanapingana na waziri mkuu, na nyakati Liberal au Labor wanaungana na conservative n.k. Ni suala huru kwasababu lina utaifa na busara zinaelekeza uhuru wa maoni.

Makundi mawili yamegawanywa katika hoja kuu tatu

1. Suala la Uchumi (Economy)
2. Mabadiliko ya jamii (Social Change)
3. Kupoteza alama 'utaifa' (identity)

Uzi huu utakuwa endelevu.

Tutaanza na sehemu ya I kwa kuangalia EU ilpoanzia miaka ya 1951, misuko suko ya 1957, 1958, 1967,1970, 1975 ikihusisha Zaidi Britain

Sehemu ya II tutaangalia kwa undani sababu zinazochagiza hali hii


Tusemezane
 
Sehemu ya I

EUROPEAN UNION (EU)

Kwasasa ina wanachama takribani 28. Wengi wanaiangalia EU kama kitu kipya

EU imekuwepo tangu mwaka 1951 ikiwa na waanzilishi 6(founders) ambao ni;
Luxembourg, France, Italy, Belgium, Netherland na west Germany

Haya ndiyo mataifa yaliyoitikia wito wa Schuman waziri wa mambo ya nje wa Ufaransa aliyetaka uwepo wa mamlaka ya kushugulikia makaa na chuma (ECSC).

Hofu ya soko la makaa ya mawe lilieta mtafaruku kuhusu matumizi ya nguvu za atomiki na kupelekea matafaruku kati ya Ufaransa na Ujerumani

Katika kutuliza hali , iliundwa 'European atomic energy community na European Economic community mwka 1957 kwa kupitia 'Rome Treaty'

Taratibu umoja ukaanza kuongezeka wanachama waliokuwa nje ikiwemo UK

UK ilipeleka maombi ya kujiunga mwaka 1960 pamoja na wanachama wengine.

Rais wa Ufaransa Charles DE Gaulle alipinga hatua hiyo akisema ni njama za Marekani kupitia Uingereza kuingilia umoja huo.

Unaweza kuona ni takribani miaka 10 ya EEC,UK ilivuta miguu

Mwaka 1967 UK iliomba tena kuwa mwanachama pamoja na washirika wengine
Hii ni baada ya Charles De Gaulle kuondoka ambaye ali veto sana UK kujiunga

Mwaka 1973 UK ikajiunga rasmi na EC(European Communites)wengi waliafiki EC
Kura ya maoni iliwagawa UK kiasi cha baraza la mawaziri kugawanyika

Hii ilikuwa ni kura kubwa ya maoni iliyowahi kufanywa na Britain kwa ujumla wake

Unaweza kuona UK ilikataliwa uanachama mara 3 na Ufaransa ndiyo ilikuwa kikwazo

Mwisho wa siku Ufaransa chini ya Pompidou ilikubali Britain kujiunga

Kwa muda wote, EEC ilikuwa ikiongeza idadi ya wanachama lakini pia baadhi wakijitoa

Mwaka 1992 ndipo EU ikazaliwa rasmi kupitia mkataba wa Maastricht.

EU ikachukua jukumu la kiuchumi na kisiasa katika ukanda wa Uropa.

Chini ya EU kukawa na mamlaka kama bunge la Ulaya, benki kuu, baraza la ulaya n.k.

Swali, je EU imeweza kuwaleta Waropa wote kwa pamoja katika mwamvuli wa uchumi na siasa? Tunauliza hivi kwasababu pamoja na uwepo wa EU bado kuna ushirika miongoni mwa wanachama kwa 'interest' tofauti

Tuangalie Shengen, Eurozone, EFTA na utaratibu wa opt-out

Vitu hivyo pamoja na vile tulivyosema , Economy, social change and national identity ndivyo vimetufikisha hapa pa referendum

Tuangalie sehemu ijayo
 
Mkuu Nguruvi, kuongezea mada yako sababu nyingine ya msingi kutaka kuungana ilikuwa kuepusha vita. Katika makubaliano ya awali the six members waliafiki iwapo kuna mgogoro wa kisiasa baina yao wote wachangie kutafuta suluhu kuliko kutandikana na kuleteana hasara kubwa baada ya somo walilolipata kupitia I and II World wars.

Pili hiyo Maastritch treaty ndio imesababisha UK kuulizana regardless ya matokeo baada ya kura ya maoni some aspects have to change.

Kwanini? Kwenye hiyo treaty wamekubaliana sera ya pamoja katika nyanja zifuatazo: sera ya pamoja kwenye mambo ya ndani, bargain ya pamoja kwenye international trade, ushirikiano wa pamoja wa intelegensia, sera ya mambo ya nje,ulinzi wa mipala na uraia wa EU usio na mipaka.

Kuhakikisha kila mtu ana comply kwenye Lisbon Treaty wakaongezea EU commission ndio body yenye power ya kutunga regulations and directive which all member states have to comply. Wameenda mbali zaidi na kuipa European Court of Justice having the final say on interpreting disputes kuhakikisha precedences mahakamani azipishani.

Hapo ndio waingereza walipokasirika ina maana sera zao nyingi kwa sasa zinatoka EU right now its 60%, sio bunge tu ambalo limeingiliwa kazi bali mahakama yao ya juu kwenye kutafsiri sheria na some precedence pia inabidi zifutwe iwapi kuna mgongano wa tafsiri.

Ndio wanajiuliza sovereignty yao ipo wapi. Kingine ni hiyo EU citizenship watu kuingia watakavyo na kufaidi kwenye welfare system bila ya kuchangia wakati serikari aiwezi ku control immigration hizo ndio sababu mbili za msingi wasizo kubali kwenye Maastritch treaty.

Hayo ya economy ata wakijitoa wanadai wata negotiate ni athari tu kwenye kujenga hoja za faida ya kubaki na umuhimu wa kushare intelligence. Lakini issue ni uhuru wa kujiamulia na immigration control. Ndio hapo unajiuliza huu muungano wetu wa EAC una maana gani wakati kila mtu anacheza na ngoma yake.
 
Mkuu Nguruvi, kuongezea mada yako sababu nyingine ya msingi kutaka kuungana ilikuwa kuepusha vita. Katika makubaliano ya awali the six members waliafiki iwapo kuna mgogoro wa kisiasa baina yao.........
Eric , ahsante sana kwa mchango wako

Kuhusu Brexit, tunaweza kusema kuna layers za sababu.

Hata hivyo, kama tulivyoonyesha hapo awali UK haikuwa na interest na EU kwa muda mrefu. Tulionyesha kuwa ilichukua miaka 10 kwa UK kutuma maombi ya kujiunga (1960), kukataliwa na kisha kuomba tena na tena.

Hata baada ya kukubaliwa bado wananchi walilazimika kupiga kura ya maoni 1975

Katika bandiko lako umesema 'issue ni uhuru wa kujiamulia na suala la immigration'

Ni kweli kuwa UK inaona nguvu za parliament na judicial system zinapokwa na EU.
Lakini hapa kuna suala jingine limejificha 'national identity'

Kujiunga na Eurozone inamaanisha kufikia mwisho kwa pound sterling, pesa inayoaminika kuwa ya zamani katika Ulaya tangu miaka 1600.
Wengine wanaona ni kupoteza identity

Ingawa wachumi wamefanya test nyingi kuhusiana na Eurozone, hakuna matokeo yanayoonyesha atahri kubwa kiuchumi

Kwa Wasomaji, Eurozone haina maana ya EU, ni muungano wa nchi za EU zinazotumia mfumo mmoja wa fedha 'monetary system' ambao si wanachama wote ni Eurozone

UK ilijitoa kufuatia kifungu cha mkataba wa Masaachtrit unayoipa UK op-out
Sababu kubwa ni uchumi wakidai mabadiliko ya Pound kwenda Euro yata destabilize uchumi wa ndani na kubebesha walipa kodi mzigo mzito unaotokana na washirika hasa katika mambo ya madeni ya mifuko ya jamii

Schengen: Ni ushirika wa wanachama wa EU kuhusu visa, kwamba EU iwe ni eneo huru kwa wanachama. Kama ilivyo Eurozone, Schengen si kila mwanachama, wapo wasio!

Na hakika hili ndilo limekuwa sababu kubwa, kwamba UK inataka iwe na uwezo wa kudhibiti mipaka yake (Border protection) ili kuzuia wahamiaji wa kiuchumi.

Wengi wanadhani wahamiaji ni kutoka Asia na Afrika. Gazeti la the Guradian limeripoti katika kipindi cha miezi mitatu wahamiaji takribani 300,000 wameingia na kutoka UK na wengi wakitokea nchi za Ulaya na hasa Ulaya Mashariki.

EU inawapa fursa za kushiriki shughuli zote za kiuchumi bila kuwa na ruhusu ya nchi husika. Hilo ndilo UK wanaona linaathiri soko la ajira.

Kwamba walio na ajira zisizo na uhakika wanaathirika kwa ushindani na pia mapato. Waajiri wamepata soko rahisi la waajiriwa na hivyo kukwaza kiwango cha mishahara.

Na mwisho ni social change , kwamba wahamiaji wengi watapoteza utamaduni wa UK kwa kuchagnayika, linawatisha wahafidhina wanaoona national identity itapotea na athari kwa culture and tradition

Hivyo ukiangalia kwa haraka ni ngumu sana kujua nini kinawakwaza UK katika EU

Hata baada ya majadiliano ya Brussels yaliyoongeza 'opt-out' bado sehemu ya UK haikubaliani na uwepo ndani ya EU.

Ukipitia maoni ya wachambuzi wengi hakuna kukubaliana kwa sababu moja kuu ya kwanini kuwe na Brexit.

Isipokuwa, kuna sababu nyingi zinazoorodheshwa ambazo ni Economy, social change na national identy zote zikichagizwa kwa nguvu na suala la immigration

Itaendelea..
 
BREXIT

Matokeo ya kura bado yanaendelea kupokelewa

Television ya ITV Uingereza inaonyesha kuwa asilimia 85 ya kampeni ya 'leave' yaani kuondoka EU ina uwezekano wa kushinda

Hadi sasa 'Leave' kampeni inaongoza kwa tofauti ya kura 700,000

Yamebaki ''majimbo 83'' kati ya 382

Tutaendelea
 
BBC nayo imefanya forecast: UK itaondoka EU

Matokeo ya vituo 327/382 yameshapokelewa, na kampeni ya 'leave' inaelekea kushinda

Tofauti ya kura sasa ni takribani milioni 1

Tufafanue kuwa vituo si kama tujuavyo. Kwa kura ya maoni UK miji imegawanywa na ndiyo inayotoa idadi ya 382

Lakini pia matokeo haya yanaangaliwa kwa ushirika wa UK
Scotland wamepiga kura kubaki EU kwa wingi takribani 62%

Kuna Engalnd, Ireland na Wales ambazo nazo pia zitaangaliwa kwa jicho kama la Scotland.

Mtinange mwingine wa siasa za UK utazuka.

Tutaendelea
 
Hali ilivyo kwa Ushirika wa UK

Mwaka 1975 kura ya kwanza kuhusu UK kujiunga na EU
Scotland iliegemea kidogo kubaki EU, 2016 Scotland imegeemea sana EU
Ireland, Mwaka 1975 iligawanyika nusu kwa nusu, Mwaka 2016 imegeemea sana EU

England, Mwaka 1975 iliegemea EU, 2016 Imeegemea kuondoka EU
Wales, Mwaka 1975 iliegemea EU, 2016 imeegemea sana kuondoka EU

Kiongozi wa SNP kule Scotland anasema, Scot inaanalia EU kama future

Hawa ndio washirika wa UK na jinsi walivyopiga kura

Mtinange unaofuata ni England, Wales kupewa mamlaka Zaidi ya mambo yao kama Scotland na Ireland. Hilo ndilo linalofuata na linaweza ku trigger jambo jingine kutokana na matokeo yalivyo hadi sasa.

Kura ya maoni ya UK imekuwa na madhara katika masoko ya dunia, wawekezaji wakiwa hawana uhakika na hali ya baadaye wenyewe wakisema market volatility

Pound imepoteza thamani kwa kiasi kikubwa tangu ilipotokea hivyo 1985

Mjadala uliopo, nini kinafuata sasa kwa UK na ushirika wake EU?

Wachunguzi wa mambo wanasema, kura hii inaweza kuwa na ushawishi kwa mataifa mengine kutokana na ushawishi wa UK ndani ya UE.

Swali, is this the beginning of the end of EU?

Tutaendelea...
 
BAADA YA KUJITOA, NINI HASA AKINAFUTA!

Tumeonyesha wascochina Wairishi walivyotaka kubaki EU, England na Wales wakiondoka

Takwimu zinafanyiwa kazi, chache zinaonyesha vijana walipendelea kubaki EU kuliko wazee. Ni mwendo ule ule wa British Pound ambapo wazee walikataa kutumia Euro

London kama sehemu ya England walipiga kura ya kubaki kwa wingi.
Na hapa ndipo walipo wahamiaji wengi. Hata hivyo maeneo ya nje yalitalka kuondoka

Ieleweke kuondoka kwa UK sijambo la siku moja.
Itachukua miaka 2 UK kuacha uanachama.

Katika miaka 2, UK haitashiriki maamuzi ya EU ingawa itafungwa na sheria za EU ''abide''

Waziri Mkuu Cameron ametangaza kuachia ngazi kabla ya Oktoba.

Ilitarajiwa angejiuzulu jana, hata hivyo wabunge zaidi ya 80 waliandika barua wakimtaka aendelee kwa muda katika kipindi cha mpito

Kujiuzulu kwake ni kutoa nafasi kwa wale waliongoza kampeni ya kujitoa kushika usukani kuelekea UK nje ya EU.

Waziri mkuu ajaye atakuwa na changamoto nyingi

1. SNP wa Scotland wanasema future ya scotland ipo EU
2. Sinn Fein ya Ireland wanasema, kura ya maoni inasisitiza zaidi United Ireland

3. England nao wanasema sasa ni muda wapewe fursa kama kuamua hatma yao, huku Wales wakiwa wapo wapo tu

4. Ndani ya UK kuna 'wazawa' BNP wanaotaka Uingereza isiyo na wahamiaji
Kuna UKIP ya Nigel Farage ambayo kimsingi ni kama BNP wakiwa na tofauti chache sana.

Kwa mantiki hiyo, siasa za UK zitabaki kuwa za mawaa kwa muda mrefu

Lakini pia kuna 'domino effects' yaani athari zinazoambatana na tukio.
Domino ni hali ya tukio moja kuchochea mtiririko wa matukio

Ujerumani na Ufaransa kuna 'wazawa' wanaouona ushindi wa 'leave' kama kichocheo

Kuondoka kwa UK kutazusha mzunguko mwingine kwa EU yaani domino effect na hilo litachukua miaka michache sana kutokea

Tusemezane
 
KIZUNGU ZUNGU CHA BREXIT CHAENDELEA

Masoko ya mitaji yamepoteza point kufuatia kura ya maoni ya UK iliyoamua kujitoa
Ndivyo ilivyo kwa pound sterling ambayo thamani imeshuka kwa kiwango cha 1985

Hofu kubwa ni wawekezaji kutojua hatma ya EU kwa siku za usoni na nini kitafuta

Kwa wasomaji wa duru, mabandiko ya mwanzo tumeeleza kuanzishwa kwa EU ikiwa na wanachama 6. Ikumbukwe UK haikuwa miongoni mwao hadi mwaka 1975

Tulieleza hilo makusudi ili kufahamu EU ina akina nani na nani wenye kauli

Leo wanachama waanzislishi sita wamekutana kujadili hatma ya umoja huo
Kauli yao ni kuharakisha mchakato wa UK kuondoka EU

Hili linafanyika ili kuzuia domino effect kwa mataifa mengine. Nationalists wa mataifa mengine wameanza kufikiria namna ya kushinikiza nchi zao kuwa na kura za maoni

Kura za maoni zina matatizo, hazikihakikishii taifa lolote mwelekeo sahihi na hugawanya watu wa mataifa hayo. Ndivyo ambavyo UK imeanza kugawanyika, Scotland na Ireland ambao wametaka kubaki EU sasa wakipiga chapuo la kura nyingine iwapo wajitoe UK

Hii haina maana kuwa wanadhamira ya dhati kuhusu EU. Ni malengo yao ya kisiasa ili kutenga nchi hizo kama ilivyokuwa shinikizo la kura za maoni za Scotland.

Katika hali iliyopo hakuna anayejua kwa uhakika hatma ya EU, na isingalitegemewa mataifa mengine kurukia hoja ya kubaki kama ilivyo Ireland na Scotland bila kuwa na hoja nyingine

Kura ya maoni ya UK si kuwa imezaa kizaa zaa katika nchi za ulaya na dunia tu, bali pia imezaa kiazaa ndani ya UK.

Kama tulivyoona, Mataifa mawili ndani ya UK yanataka 'kujitenga'

Ndani ya Taifa lingine la England hali si shwari. Kumekuwa na petition ya saini Zaidi ya milioni 2 zikitaka kura irudiwe tena.

Hawa ni vijana wengi wanaoona kujitoa ni kuminya fursa zao

Bunge la UK limesema litajadili suala hilo kwa undani. Hata hivyo, hakuna aliyelalamika kuhusu ukiukwaji wa kura za maoni na ni ngumu kurudia uchaguzi kwa mtindo wa 'jecha'

Nini kinafuata baada ya hapa, ni kizungu zungu kwa mataifa na UK yenyewe

Tusemezane
 
KIZUNGU ZUNGU CHA BERXIT CHAENDELEA

Kura za maoni zina matatizo, hazikihakikishii taifa lolote mwelekeo sahihi na hugawanya watu wa mataifa hayo. Ndivyo ambavyo UK imeanza kugawanyika, Scotland na Ireland ambao wametaka kubaki EU sasa wakipiga chapuo la kura nyingine iwapo wajitoe UK
Hiki kipande nimekipenda sana, nasubiri mgeuko
 
MKATABA WA LISBON

Mkataba wa Lisbon pamoja na mambo mengine unaeleza namana nchi inavyoweza kujitoa katika EU kwa kifungu maarufu cha 'article 50'

Kifungu kinaeleza utaratibu wa nchi inayotaka kuondoka EU.
Wasomi na wachambuzi wanakiita 'vague' hakifafanui utaratibu mzima

Kwa uchache kifungu kinaeleza anayeyjitoa aandike barua kwa baraza-EU

Britain inatakiwa kufikisha kifungu hicho kwa mchakato wa miaka 2

Kifungu hiki kiliandikwa katika mazingira ya kuleta ugumu wa kujitoa
Haikufikiriwa mwanachama kwa EU angaliweza kufikia hatua hiyo.

Jambo la kufikirisha,aliyeandika vifungu vya Lisbon Treaty ni Raia wa UK

Rais wa EU BwJuncker alisema ' si talaka ya urafiki, hata hivyo hakukuwa na pendo'
Not amicable divorce, but there was no love. ikieleza uhusiano wa EU na UK

Waziri mkuu Cameron amekataa ku-trigger article 50
Cameron anasema kiongozi ajaye ata- trigger the article 50.

Kuna article 49 inayoeleza mwanachama kujiunga tena baada ya kujitoa
Na article 48 inayoeleza uwepo wa majadiliano ya hatma ya ushirika baada ya talaka

Haya yanaisumbua sana UK sasa hivi. UK inataka majadiliano kuhusu ushirika wake na EU, wakati EU wanataka UK ku trigger article 50 haraka.

EU inataka Uingereza iondoke kwa sababu mbili

1. Kuondoa sintofahamu 'uncertainty' hasa ya masoko ya uchumi

2. Kuzuia domino effect inayoweza kutokea wakati wa mijadala ya article 50

Hali ya masoko imetulia, kinachosumbua ni hatma ya ushirika wa EU na UK.

Majadiliano ya mikataba ya biashara na uchumi, na hali ya wafanyakazi wa EU-UK, free movement na ushirika wa taasisi chini ya EU ni masuala nyeti yanayohitaji mjadala

Yakiendele, ndani ya UK kuna mitafaruku Scotland, Ireland na vyama vya siasa vya UK.

Ndani ya Labor wabunge wanamtaka Jeremy achie ngazi
Conservative wanamuona Boris Johnson kama tatizo la baadaye

Nigel Farage wa UKIP akikumbana na upinzani si UK tu bali katika EU.

Tutendelea na mjadala huu mrefu

Tusemezane
 
BORIS JOHNSON AACHIA NGAZI KABLA YA KUANZA

Mtifuano ndani ya UK unaendelea katika vyama na nchi kwa ujumla
Jambo moja la kushangaza ni kuwa wabunge wengi wa Westmister walipendelea kubaki EU

Vyama vya Conservative na Labour vilikuwa na wabunge katika kambi mbili
Ni chama cha UKIP cha Nigel Farage ndicho kilisimama kwa asilimia kubwa kujitoa EU

Swali, ikiwa wabunge wengi walipenda kubaki, iweje wananchi wengi walipiga kujitoa?

Jibu lake kina sehemu mbili

1. Wapo wanaosema wabunge walikuwa 'out of touch with constituents'
Kwamba,wabunge hawakuelewa ndani ya majimbo yao wananchi walitaka nini

2. Kile kinachoitwa 'perception ' kuliko reality.
Kwamba, kilichosemwa kilivutia kuliko uhalisia wa mambo

Ukweli umetimia, tumeona hamaki za kutaka kurudia kura ya maoni,jambo lililoshindwa
Takribani watu milioni 4 walijiandikisha wakitaka bunge litazame upya kura ya maoni
Hili haliwezekani kwasababu hakuna sababu za kufanya hivyo

Viongozi walioongoza kujitoa wanakabiliana na ukweli wa hali ya sasa na baadaye ya UK
Kiongozi wa Labour Bwana Jeremy anatuhumiwa kutoongoza kampeni ya kubaki vema
Anatahumiwa na wabunge wa chama chake

Kwa upande wa chama tawala, Cameron keshasema anaahcia ngazi.
Ilitegemewa kiongozi wa kujitoa Bw B. Johnson achukue uongozi

Leo naye kama Jeremy, ameonja joto ya Wabunge wa Westminister
Katika hali ya mshtuko, naye amesema hatagombea nafasi ya uwaziri mkuu

Nafasini kwa Bw M. Gove, waziri wa sheria na Bi Theresa May,waziri wa mambo ya ndani

Wengi wanaona changamoto mbele ya safari
1. Kuimarisha uchumi wa UK ikiwa nje ya EU
2. Kujenga mahusiano mapya na EU katika biashara na uchumi
3. Kutatua mtafaruku wa kugawanyika UK, kwa Scotland na Ireland

Tatizo linalojitokeza ni matumaini 'fake' yaliyokuwa hayana plan B.
Kwamba, wengi wangepiga kura ya kubaki.
Hata waliotaka kujitoa kwa uhalisia hawana plan B au kujiandaa na hatma ya nchi

Mparaganyiko wa kisiasa, hali ya uchumi vinatengeneza uncertainty.
Hili linaweza kuzua mtafaruku mwingine wa mdororo wa uchumi kama litabaki lilivyo

Tusemezane
.
 
NI ZAMU YA NIGEL FARAGE

'I want my country back, now I want my life back'

Kiongozi wa UKIP ametangaza kuachia ngazi za uongozi wa chama leo.

Hayo aliyasema leo akisisitiza, aliondoka katika buisness kujiunga na siasa za kuirejesha Uingereza 'I want my country back'

Na kwamba lengo limetimia, hana nia ya kuwa mwanasiasa

Amesema, kampeni imemgharimu pengine na waliokuwa karibu naye.
Amesisitiza kuwa ' I want my country back, now I want my life back'

Hili ni katika joto la umma linalopanda kila siku.
Yeye na Boris wanaona kiza kinene na hawajui hatma ya Uingereza ni ipi.

Ni watu walioamua kuogelea katika bahari wasiojua kina, na sasa wanarudi ufukweni na kuwaacha wenzao wakiendelea na safari.

Jahazi linakwenda kwasababu upepo upo, hakuna ajuaye litatia nanga wapi.

Manahodha wanachupa majini!

Tusemezane
 
Walilikoroga na sasa itabidi walinywe, Brexit yageuka na kuwa Bremain...tatizo moja tu, maziwa yamemwagika, je yatazolewa? Na yakizolewa yataweza kutumika tena? Hili limetoa funzo si kwa Waingereza tu, ni funzo kwa dunia nzima! Kukurupuka kuna madhara, je Watanzania tunajifunza chochote hapa?
 
Walilikoroga na sasa itabidi walinywe, Brexit yageuka na kuwa Bremain...tatizo moja tu, maziwa yamemwagika, je yatazolewa? Na yakizolewa yataweza kutumika tena? Hili limetoa funzo si kwa Waingereza tu, ni funzo kwa dunia nzima! Kukurupuka kuna madhara, je Watanzania tunajifunza chochote hapa?
Mkuu hali ya UK inatatiza. Jana wametangaza tax cut kwa corporate kwa 20% ? nadhani.

Hii ni kuwavutia wawekezaji wanaohamisha mitaji nje ya UK
Kwasasa Borse kule Frankfurt na Paris wanapokea wawekezaji kutoka UK

Kama ulivyosema, kuna mafunzo mengi sana na ndiko tunaelekea kujadili

Hayo yatakuwa katika sehemu hizi
Funzo la :
Maamuzi yanayogusa maisha ya watu
Wananchi kushangilia bila kujua wanashangilia nini
Wananchi kutoshiriki wakidhani wapo wa kuwasemea
Muungano: EAC,Tanzania, AU n.k.

Kuna mafunzo mazuri na mabaya kwa hili la UK, na afadhali limetokea

Maziwa yashemwagika, waliotakiwa kuongoza kuzoa zoa wanataka 'life back'
Alianza Johnson, sasa Nigel Farage

Ukweli ni kwamba, wanabanwa na Waingereza na hawana majibu.
Kwanza, wameambiwa wafanye trigger of article 50.

Hii ni sawa na kupewa kitanzi umfunge mtu shingoni
Pili, wameulizwa nini hatma ya Scotland na Ireland?

Scot wanataka second referendum kwavile matokeo ya 'Leave' haya present interest zao
Sinn Fein wameanza na habari za Ukatoliki na uprotestant, wanadai referendum pia

Johnson na Farage wanaulizwa, nini hatma ya haya? Mitini!

Halafu kuna suala la England na Wales.
Hawa nao waliahidiwa kupewa mamlaka yao. Down the road inaweza ku split zaidi.

England na Wales wanaweza kuwa pamoja, lakini England inayobeba washirika imechoka na choko choko za waliobebwa.

Mkanganyiko wa haya ndio kulikoroga kwenyewe, ili kuepukaka kikombe, wanaachia ngazi
 
HALI YA MASOKO BADO TETE

BREXIT YAITESA UK KIMAWAZO, MAJIRANI HOFU

Masoko ya mitaji yamedorora kwa kiasi na Pound kupoteza thamani tena wiki hii
Wawekezaji wana haha kutafuta mahali salama kufuatia sintofaham kila uchao

Kuna hoja kuwa kujitoa EU bado kunaipa UK nafasi katika soko la pamoja la Ulaya.
Na kwamba fursa ya watu kwenda popote ipo pale pale.

Boris Johnson aliyasema hayo baada ya kura kutangazwa za Brexit

Katika hali nyingine, EU wanasema UK imejitoa ili kuzuia wahamiaji nchini mwao.

Hii ikimaanisha UK imezuia free of movement ya watu, takwa muhimu la soko la pamoja
EU wanasema, ikiwa ni hivyo, ile free movement ya UK katika EU haitakuwepo

Kauli hizi zinapelekea kiwewe. Mathalani, UK ikiwa nje ya soko mambo kama tariff yata athiri biashara.

Athari ni kama za Wairishi wanaofanya biashara ya mamilioni ya pound kwa wiki na UK

Brexit ni mwiba kwa UK ku-settle mambo ya ndani, kwa majirani

Ni mwiba kwa wawekezaji wanaotafuta balance ya access ya single market na access ya 'financial hub'

Katika kubabaika wanaotegemewa kumrithi Cameron wamebadili kauli za kampeni.
Wanasema wahamaiji hawatafukuzwa UK, na wataendelea na shughuli zao.

Uchaguzi wa Conservative

Inafuata
 
WAZIRI MKUU AJAYE WA UK ATAKUWA MWANAMKE

Kinyang'anyiro cha kutafuta mrithi wa Cameron kimeendelea
Kura za maoni zimefanyika na kuondoa wagombea wenye kura chache

Sasa wamebaki wanawake wawili watakaopigiwa kura na mmoja kuwa waziri mkuu wa UK. Wakina mama hao ni Bi Teresa May na Bi Leadsome

Hayo yakiendeleahali ya masoko ni ya utata sana pound ikiendelea kuyumba
Wawekezaji wakiiangalia UK 'financial hub' kwa jicho la mashaka

Tusemezane
 
THERESA MAY NDIYE WAZIRI MKUU WA UINGEREZA

Bi May ndiye mgombea aliyebaki baada ya Andrea Leadsom kujitoa.

Kwa utaratibu wa chama cha Conservative, wabunge hupigia wajumbe waliojitokeza kura

Mgombea wa mwisho anaondolewa, na mchakato huendelea hadi watakapobaki 2
Katika hatua hiyo, wananchama wa Conservative wa wapatao 150,000 huachagua mmoja

Kwa bahati nzuri au mbaya, hatua hiyo haitafikiwa.
Andrea amejitoa akiwa amebaki na Theresa

Kwa mantiki hiyo, Theresa May hatapigiwa kura bali kuwa kiongozi wa Conservative

Kwa mfumo wa bunge la Uingereza ' British parliamentary system' kiongozi wa chama tawala ndiye waziri mkuu.

Waziri mkuu hachaguliwi na wananchi bali chama chama chenye viti vingi

Mfumo huo haukuanza kutumika leo, ni makubaliano yao ya jinsi ya kuongoza nchi
Bi Thatcher aliondolewa na John Major.Tonny Blair akaondolewa na Godown Brown n.k.

Wapo wanaosema hiyo siyo Demokrasi, ukweli ni kuwa ni demokrasi kwa sababu ndivyo walivyokubaliana. Jambo muhimu la kujiuliza, ni je wanaafiki makubaliano yao?

Hata kama kuna demkorasia nzuri kiasi gani, kama hakuna heshima juu yake ni upuuzi tu.

Lakini pia kuna la kuangalia. Cameron anaondoka kwasababu alishindwa kutetea alichokiamini yeye na serikali yake.

Hakulazimishwa, aliona umuhimu huo kwa kuweka masilahi ya nchi yake mbele.

Je, hiyo si demokrasia? Na wala hakuingilia taratibu za kumpata mrithi, je hiyo si demokrasia?

Theresa May amesema, Brexit ni Brexit, kwa maana anaheshimu maoni ya wananchi.

Je, hiyo si demokrasia? Hata pale wengi waliposema kura irudiwe, serikali ilisema kura imeshafanyika hakuna kurudi nyuma, je, hiyo si demokrasia?

Tusemezane
 
kuna mafunzo mengi kuhusiana na Brexit

Hayo yatakuwa katika sehemu hizi
Funzo la :
Maamuzi yanayogusa maisha ya watu
Wananchi kushangilia bila kujua wanashangilia nini
Wananchi kutoshiriki wakidhani wapo wa kuwasemea
Muungano: EAC,Tanzania, AU n.k.
Waziri Mkuu May amefanya ziara ya kwanza Scotland. Kama tulivyowahi kujadili, Brexit ina taathira kwa siasa za ndani na za nje ya UK. Scotland chini ya waziri kiongozi 'First minister' na bunge lao wanataka wabaki EU.

Wakati huo huo EU wanasema, hawawezi kukubali ombi la Scotland. Hapo panazuka mtafaruku kati ya 'UK' na Scotland, huku scot wakiadi kura ya pili ya maoni kuhusu ushiriki wao katika UK

Mtafaruku wa pili ni wa Ireland ambayo kama Scotland ilipiga kura kwa wingi kubaki EU. Pamoja na hayo, biashara ya Ireland na 'UK' iliyobaki ni kubwa.
Sinn Fein wataamua lipi?

Matafaruku wa tatu unahusu England na Wales zinazoona kuwa kwa kutokuwa na 'autonomy' kama Ireland na Scotland kunawapunguzia fursa na kuwaingiza katika mitafaruku isiyowasaidia. England ikiwa imebebea mzigo mkubwa wa kuendesha UK.

Mtafaruku wa nne ni kuhusu UK kwa ujumla. Waziri mkuu May anataka kujadiliana na EU kuhusu mahusiano mapya ya kiuchumi na kibiashara.
Kwa mantiki hiyo hataki kufanya kile wanachokiita 'Trigger of article 50 of Lisbon treaty.

Wakati EU ikitaka UK washughulikie article 50 ya Lisbon treaty haraka.

Hapa panahitaji ufafanuzi. Kwanini article 50? Iikiwa kura ya maoni tayari?

Tutaiangalia article 50 kwa mantiki yake na kisha kuingia katika mada halisi 'MAFUNZO YATOKANAYO NA BREXIT'

Inaendelea...
 
Back
Top Bottom