Duru: Hatima ya Muungano na dalili za kuvunjika mapema

jitegemee , umeleta hoja nzito sana

Hakuna shaka mgogoro wa muungano ni wa kiuchumi. Wapo watakaopindishaukwelikukidhi haja zao.
Kwetu sisi,madai ya wazanzibar
ni azma yao ya kujitegemea kiuchumi na kunufaika kiuchumi ndani ya muungano


Kujitegemea Wmeanza bila kushirikisha Tanganyika. Mfano,wanapoamua kuunda taasisi zao lengo ni kujiwezesha kiuchumi. Wana bandari,mashirika yao na taasisi zao ambazo kimsingizikiwa za muungano zingeathiri chochote.

Ugomvi mkuu ulikuwa gesi na mafuta wasiyotaka yawe ya JMT


Kwa mfano, hakuna sababu za kuwa na shirika la umeme zeco wakati bili zinabebwa na Tanesco.
Zeco ni chaka la wezi,mzigo unaotokana na wizi huo ni wa Tanganyika kwa jina la JMT


Katika kunufaika kiuchumi ndani ya muungano, hapa ndipo lilipo tatizo. Watanganyikawanapaswa kuwashukuru wazanzibar waliofungua ‘pandora box' na kuelewa mengiyenye utata yasiyo na manufaa kwao

Umezungumzia suala la BoT katika uzi ulioonyesha. Hisa za BoTzimetumika kufanikisha azma za utegemezi kiuchumi.

Mathalan, 7% wanayopata wznz,awali ilidaiwa ni hisa za muungano. Tumeuliza, hesabu zimepigwa kwa njia ganihakuna jibu


Tukaambiwa ni kutokana na misaada na mikopo. Nako tukauliza, hesabu zimezingatia nini, hakunajibu.


Tumeambiwa 7% ni sehemu ya pato la taifa. Tumeuliza, ni patola Tanganyika ambalo ni takribani Trillion 12 kwa mwaka huu au ni bajeti ya JMTambayo ni trillion 19. Hakuna jibu lililopatikana.

Hivyo, unaweza kuona hisa zisivyoelezeka, na yote yakiwa kwa gharama za Mtanganyika

Tumeongelea 21% ya ajira ambalo ni uchumi. Tumeuliza, namba imepatikana kutokana na nini na akina nani walikaa kitako. Jibu ni hakuna namna, ila tunajua waliokaa ni wznz na kuamua

Tumeona hiyo 21% ndiyo inawapa wznz 1.75Bilion kwa mwezi kama kodi za wafanyakazi wa muungano.
Tumeuliza, ni wafanyakazi wangapi wa znz katika muungano wanaoweza kulipa kodi ya Bilion 1.75? Hakuna jibu.


Tumeuliza je serikali ikipunguza ukubwa kiasi hichokitapungua au ni fixed, hakuna jibu.

Tumehoji, je kodi hizo zinahusu wafanyakazi wa znz katika muungano katika wizara 4 au ni pamoja na wizara, idara, taasisi na mashirika yasiyo ya muungano? Hakuna mwenye jibu.

Wapo wapuuzi wachache wanaosema ni kutokana na misaada namikopo!!!
Tumehoji ni nini znz inaleta ndani ya muungano Zaidi yamanung'uniko? Hakuna jibu lilillopo ni mikopo na misaada.

Tena wapuuzi wanasemaTanganyika inafaidika kwa jina la Tanzania. Tukasema kwanini znz isikope yenyewe?

Na Tanganyika ambayo haipo itakwepaje jina la Tanzania ikiwa haipo? Hakuna jibu.

Ukiangalia hayo na mengine tuliyoacha kuyasema, muundo wasasa na wa Chenge hauwezi kutoa jibu hata siku moja. Kitakachoendelea ni Znz kuwa tegemezi na tatizo.

Ni tatizo kwasababu haina uwajibikaji, hawaelewi gharama auuchungu wa muungano
Hivyo, kila sikuwatakuja kudai vyeo, madaraka na nyongeza za posho.

Itafika mahali hawatapaswa kufanya kazi kwani ruzuku wanazopata zinatosha kabisa kuwaendeleza.
Kwa hali ilivyo, Tanganyika imeanza kuchoka na hilo ndilo litachochoea kifo cha muungano siku moja

CCM inayoshikilia muungano kwa njia za hila zisizo na majibuimeshaanza kupoteza nguvu za kisiasa, kiutawala na ushawishi.

Ramani ya tawala imebadilika na muda si mrefu hakutakuwa na majadiliano bali kugawana kilichopo kama kipo, muungano kwisha

Tusemezane
 
Last edited by a moderator:
UNAFIKIUNAPOTAWALA
WATANGANYIKAMUMESIKIA WANAYOSEMA?

Unafiki nihali ya mtu kujifanya ana maadili kinyume na tabia yake halisi.
Mtu atendayehayo huitwa ‘hypocrite'' Hivyo, unafiki si tusi ni tabia au hulka kama zilivyo nyingine


Kuna ignorance ‘ujuha' ni kukosa uelewa na ufahamu. Nalo pia si neno la tusi

Upo ubinafsi,'narcissism' ukimaanisha umimi, kama hali ya kujipenda bila kujali wengine
‘Traitor' ni mtu ananyesaliti Jami, misingi,urafiki au hata nchi yake

Tanganyika:Ni majuha ‘ignorant', wameanishwa muungano ni sehemu muhimu ya ustawi wao.
Kwamba, bila uwepo wa Zanzibar,Tanganyika haisimami.

Kuwa , znzni muhimu ndani ya muungano nani hakiya Tanganyika kubeba Muungano Peke yake kwa gharama kubwa

Ni majuha waliokubali kuwekeza znz bila kujua malipo ya uwekezaji .
Wameelezwa, kuhudumia znz ni wajibu wao, na kwamba, haki yao ni ya wote.


Wanaoshiriki kuwaaminisha ujuha huo ni Watanganyika wenzao wasowaeleza ukweli.
CCM wanaoficha ukweli wa mzigo walioubeba wamuungano.
Ndio wanaitwa wasaliti ‘traitor'.

Ni wasaliti kwa kuwakana wananchi na nchi yao. Hawapo tayari kusimamia Tanganyika.

Wamekaa pembeni wapiga kura wao wakibeba mizigo isiyowahusu na huu wamuungano ni mmoja wapo.

Wazanzibar:
Hawa ni wanafiki ‘hypocrite' na wabinafsi ‘narcissism '' na majuha ‘ignorants'


Ni wanafikikwasababu, miezi michache iliyopita jina la Nyerere lilikuwa ni ushetani likitajwa.
Hakuna kiongozi aliyewahi kusimama na kukemea, Leo wanataka S2 za Nyerere wanaymlaani


Ni wanafik ikwasababu walidai hawataki muungano, muungano unawanyonya na wanataka mamlaka kamili

Leo ukiwasikiliza, yale ya Nyerere ndio wanayapigia debe, hoja za muungano zimebaidlika na sasa ni Watanzania.

Wana unafikikwasababu utanzania wao si wa moyoni, ni Utanzania wa masilahi, baada ya hapo znz kwanza.

Wana ubinafsi kwasababu hoja zao za kuonewa ni za uongo na wanajua hilo.

Na mwisho ni majuha ‘ignorants'kwasababu haieleweki nini wanataka.


Tunayasema haya si kwa kashfa, matusi au kejeli. Ni kwa ukweli, na maelezo haya kuto kagazeti la Habari leo likimkariri Naibu katibu mkuu wa CCM Zanzibar yanatutetea

Soma habarihii aya tatu za mwisho na kisha endeleana sehemu ya II

http://www.habarileo.co.tz/index.php/habari-za-kitaifa/36045-cuf-yahofiwa-kukwamisha-mafuta-zanzibar
 
Sehemu ya II

Naibu katibumkuu Vuai anasema, vijana watambue ajira nyingi zinatoka Tanganyika, na kwambaSMZ ya mapinduzi haiwezi kuwapatia ajira kiasi hicho.

Katika mkutanowa kibandamaiti akiwa na Rais Shein, Vuai alisema wanafunzi wa znz wanasomeshwana Tanganyika, wengi kuliko wale wanaosomeshwa na SMZ

Vuai anasema tunachosema kila siku, ingawa haendi mbali kuonyesha ukubwa wa tatizo kwa Taganyika

Vuai anachosema,madai ya wznz kuwa muungano unawanyonya ni uongo.
Kwamba,kelele ni unafiki, akijua moyoni kunyonywa si kweli na hakupo

Anafahamu znz haina mchango, na kwamba anachotaka S2 kumbebesha mzigo Mtanganyika kwajina la JMT.

Ni jina hilo wanalotumia wznz kudai ni koti la muungano, huku nyuma wakirudi kusema wanataka ubaki kama ulivyo! Unafiki


Kama Vuai anachosema ni kweli, iweje basi znz idai 21% ya ajira za muungano ikiwawanafaidika kwasasa.
Je madai ya ajira za muungano si unafiki!


Kama siunafiki, iweje znz hiyo inayonufaika na ajira, idai kupewa Bilioni 1.75 kwamwezi, kodi za wafanyakazi ikiwa Vua anajua ajira hizo si za muungano, nakwamba zinawasaidia bila hata kudai senti!


Narcissim. Ni ubinafsi kwasababu Vuai huyo huyo yupo znz akiweka sharia za kumzuia Mtanganyika kufaidika na fursa kama anazosema wao wanafaidika. Leo Mtanganyika anajulikana kama raia wa nchi jirani.
Vuai haoni unafiki huo, ubinafasi huo na ujuha huo


Lakini Vuai anawaeleza Watanganyika walivyo majuha. Kwamba, wanasomesha watoto wao kwa kodiza bure, wanapata ajira za Watananyika, na Watanganyika wanawalipa wznz kwakutoa nafasi hizo kwa gharama za watu wake

Vuaianawaeleza Watanganyika, ni majuha, wabunge wa znz ,mwaziri, wakurugenzi n.k. nisehemu ya ajira za wznz, kwani kwao znz kwanza na Tanzania ni ajira

AnawaelezaWatanganyika ujuha wa kudhamini mikopo ya znz, lakini pesa ni za znz.
Kwamba,Watanganyika wabebe mzigo usiowahusu kwasababu ni majuha


Wasichotambuawznz kama Vuai ni kuwa, huo ujumbe umefika. Ipo siku Watanganyikawataacha ujuha na usaliti wa nchi yao

Vuai anaeleza mfumo wa S2 ulivyo na matatizo kwa Tanganyika.Kwamba, muungano nishamba la ajira, madaraka na vyeo kwa wznz, mzigo wa gharama mgongoni mwaMtanganyika

Ipo sikuWatanganyika watahoji kauli za majigambo, tambo, na dharau za akina Vuai.

Watahoji haki yao
inaanzia wapi na inaishia wapi, na haki ya mzanzibar inaanzia wapi na kuishia wapi.

Watahoji maswali tunayohoji kila siku bila majibu.


Siku hiyomuungano utakuwa glass ya kioo iliyoanguka. Utafikia tamati

Tusemezane
 
VUAI WA CCM: PAZA SAUTI WATANGANYIKA WANAKUSIKIA

ULIKUWEPO TANGANYIKA IKITUPIWA VIRAGO, LEO NI SHUJAA WA MUUNGANO

MAJUHA YANAZINDUKA, NI MUDA TU!

Tumezungumzia dhana nzima ya unafiki na wanafiki. Tutaendelea kuonyesha unafiki unaotendwa ndani ya muungano
Mwaka 2010 wazanzibar walikaa pamoja wakapitisha katiba yao. Ni katiba iliyoua muungano kiroho ingawa kimwili upo

Ni katiba iliyojali masilahi ya znz na kuyapiga teke ya Tanzania. Iliyoiacha Tanzania ndani ya Tanganyika
Mabadiliko yalilenga uchumi na fursa za waznz kwa waznz na si Tanzania.

Mabadiliko yaliyomfanya rasmi Rais wa JMT mgeni ndani ya nchi ya znz.

Ni mabadililo yaliyoipa znz nguvu za kuamua bila mawasiliano na mshirika wa muungano. Wakaondoa maeneo ya kicuhumi kama bandari, anga, mafuta na gesi,ardhi n.k. kwa hofu tu kuwa kila kinachopatikana znz ni cha wazanzibar si Tanzania

Yaliamuliwa kwa kiburi cha upande mmoja,kwa kuamini kuwa znz ni muhimu katika muungano kuliko Tanganyika

Mabadiliko yalisimamiwa na akina Karume, Seif Idd, shamsa Nahodha ,Vuai n.k. Leo Vuai wanajitokez anapenda muungano kwavile unatoa fursa. Si kupenda muungano kwa kama jambo jema, bali ni kwavile unatoa fursa kwa wazanzibar.

Hawakukemea uhuni uliovunja muungano kiaina. walisimama kutetea znz huru yenye mamlaka kamili, znz kwanza!
Huu kama si unafiki ni kitu gani kwa lugha nyingine?

Hao hao waliotetea znz huru, wakilaani mkoloni mweusi, ndio wamegeuka na kuwa mashujaa wa muungano tena S2

Hawataki tena mamlaka kamili, na wala hawazungumzii koti la muungano alilovaa Tanganyika

Wanaamini muungano huu unaolindwa na Polisi utaendelea kudumu katika mazingira nyefu yaliyopo

Warioba na tume walitoa fursa kwa znz na Tanganyika kuwa nchi zenye mipango yao,ile ya pamoja iratibiwe kwa utaratibu. Mfano, walisema Raia wa Tanzania ni wa Tanzania yote na ana haki popote

Rasimu ya Chenge inasimama kule kwa katiba ya 1977 ambayo haielezi wala kuweka mipaka ya washirika.

Wasichojua wznz ni kuwa hadhi ya kuwa mshirika katika muungano inatoa fursa na milango ya maelewano kuliko hadhi ya kujipa ya uzanzibar na Utanzania

Watanganyika wameamka, japo wengine wapo usingizini hakika wameshanawa nyuso.
Walichokibaini ni kuwa muungano huu ni wao, wenzao wanautaka wakihitaji mafao baada ya hapo, znz kwanza.
Ndipo wanajiuliza Tanganyika kwanza ipo wapi?

Mambo mengi yamefanywa kwa makubaliano ya viongozi yakilenga kulindwa na Polisi na wala si ridhaa ya wananchi.

Leo hatujui ni sheri gani iliyoanzisha 21% ya ajira kwa wznz na wala si watu wa Kigoma, au Arusha.

Tunajua wznz walikaa kitako na kuamua wenyewe kwa kile walichosema kamati ya muungano.
Kamati hiyo ilikuwa chini ya Gharib, Mkakamu wa Rais, Seif Idd(makamu znz), Samia(waziiri muungano), Saada Nkuya.

Kikao kikaamua asilimia 21 ni yao bila kujali kitu kingine. Kikao kikaamua lazima znz ipewe 1.75 Bilioni kila mwezi kama adhabu kwa Watanganyika kuwaajiri raia wa nchi jirani ya znz.

Wapo wenyewe wanapanga hatma ya nchi yap, wanapanga hatma ya Tanganyika. Tanganyika, majuha wametulia

Haijulikani, wale wznz 1024 wanaodhaminiwa na HESLB ambayo ni ya Tanganyika wanadhaminiwa kwa utaratibu gani

Wala haijulikani kwanini Mtanganyika aliyekopa HESLB. Haijulikani kwanini wahitimu wa chuo kimoja wa nchi moja wawepo wenye nafasi maalumu(21%) na kuwe na utaratibu tofauti wa kukopa.

Haijulikani, 7% ya pesa zinazokwenda znz zinatoka eneo gani la muungano. Na wala haijulikani kwanini wznz wanaopewa fursa Tanganyika, waadhibu walipa kodi wa Tanganyika kwa fadhila hizo(1.75Bilioni)

Kwa vile hayo yamefanyika katika mikutano ya viongozi, wananchi hawajui.
Siku watakapotaka kujua hakutakuwa na jibuWananchi wataingiwa na hasira, na hapo liwalo na liwe

Ndio maana tunasema akina Vuai wanajua kilichopo mbeleni?

S2 zinalindwa na Polisi, wanajua ipo siku watanganyika watasema na iwe iwavyo?

Kauli za kina Vuai zitasaidia kama ushahidi

Muungano utavunjika kama kio cha taa ya fanusi

Tusemezane
 
WATANGANYIKA NI ‘MATEKA' KATIKA MAAMUZI YANCHI YAO
WAFANYE MAAMUZI MAGUMU ILI KUSONGA MBELE

MUDA WA KUSIKILIZA ZNZ NI KUPOTEZA MUDA NAFURSA

Sehemu ya I

Mwaka 2010wazanzibar wote walikaa kikao cha kubadili katiba
Walifanya bilakujali athari katika muungano. Ilikuwa kudharau muungano,kuidhalilisha na kuivunja katiba

Mabadiliko ya 2010 yalileta msukumo kudai katiba mpya ya JMT,ambayo sehemu kubwa inawahusu Watanganyika

Tume yaWarioba ikaja na mapendekezo ya wananchi kuhusu hatma ya muungano, ikawekawazi, ili kuepuka matatizo kama ya 2010 mamlaka ya nchi husika na ushirikiano yabainishwe

Znz ina katiba na vyombo kama serikali na nchi. Hivyo, katiba ya JMT haiwagusi kwa kutazama katiba ya znz ya 2010.

Kukwama kwakatiba ya JMT kunawaathiri Watanganyika zaidi ya wazanzibar

Mkwamo,umekuja kutokana na kubadilika badilika kwa mitazamo ya znz.

Walewaliokaa 2010 na kuvunja katiba, ndio hao hao wanaosimamia katiba ya Chenge
Walewaliokaa 2010 kupinga uonevu wa S2 ndio hao hao wapiga debe wa S2

Katiba yaChenge haitoi nafasi kwa uwepo wa nchi ya Tanganyika.
Hii maana yake, katiba ya JMT yenye matatizo inalenga kuwaathiri Watanganyika

Katiba yaJMT itategemea znz wanataka na kuamua nini.
Kwa mfano,walipopiga kelele za muungano, imetulazimu kubadili katiba kukidhi haja zao

.Lakini, katba ya 2010 haitoi nafasi ya mabadiliko yao kuwemo katika JMT.


Ili, mabadiliko yawepo lazima kuwe na 2/3ndani ya BLW na 2/3 kura ya maoni.

Warioba aliwekakipindi cha mpito cha miaka 4, lengo ni kutoa nafasi kwa pande zote kuweka utaratibu wa kujiendesha.

Hili lilikuwa ni kutoa nafasi kwa Tanganyika kuunda katiba yao kwa mambo yanayowahusu

Inaendelea..
 
Sehemu ya II

Katiba yaChenge, imekopi ya Warioba kwa kutoa kipindi cha mpito cha miaka 4.
Kukiwa hakuna mabadiliko ya mfumo wa muundo wa muungano, wala kupungua kwa mambo ya muungano, hakukuwa na haja ya kuwa na kipindi cha mpito.

Kipindi cha mpito cha katiba ya Chenge kimewekwa ili kukidhi haja ya wazanzibar kubadili katiba yao ili iakisi katiba ya Chenge wanayodhani ina masilahi kwao licha ya mappungufu mengi yakiwemo kuwapora madaraka kidogo waliyo nayo

Kuna tatizolisiloonekana. Hakuna uwezekano wa katiba ya znz ya 2010 kufanyiwa marekebisho kwasiasa za znz .

2/3 haiwezekani ndani ya BLW au kura ya maoni.

Maana yakeni kuwa, Watanganyika watabaki na katiba yao Chenge isiyoridhiwa kwa muda usiojulikana.

Jaribio lakuvunja serikali ya umoja wa kitaifa znz halina matokeo yoyote.
Ili kuvunjaGNU ni lazima 2/3 BLW na kura ya maoni, hilo halitatokea znz

Katika mkanganyiko huu, waliobaki na hasara ni Watanganyika.

Leo wangekuwa na bunge la katiba la Tanganyika, tungalikuwa na ubushani juu ya changamoto za taifa lao.
Huo ungekuwa mjadala endelevu na wenye manufaa.

Kinyume chake, Watanganyika wamewekwa mateka wa kujadili hatma ya nchi yao kwasababu tu wanatakiwa kwanza wakubaliane na namna ya kuishi na kuhudumia znz.

Hili nitatizo kubwa sana ambalo lazima Watanganyika walifanyie kazi

Kuishi na znz kama nchi moja ni katika kujenga nguvu tu ya pamoja.

Kwa muundo ulivyo na miaka 48 kuna kila sababu inayoonyesha, uwepo wa znz ni mzigo na si hazina katika muungano.

Kwamba,Tanganyika si kuwa inafanya investment kubwa sana, lakini pia hakuna maelezo investment hiyo kwenda znz inaleta manufaa gani kwa Watanganyika

Matokeo ya hali iliyopo kwa Tanganyika ni mabaya sana

Kwanza,Tanganyika imebaki kuwa mateka katika nchi yao.
Kwamba haiwezi kufanya maamuzi ya maendeleo ya wananchi wake bila kusikiliza wznzwanataka nini

Pili,Tanganyika itabaki katika lawama kila siku kutokana na malalamiko ya wznz ambayo tumeona hayana maana wala mashiko kwa kigezo chochote
.

Tatu,Tanganyika itabaki kuyumba kutokana na kuyumba kwa wznz.
Leo wanaamua hili kesho wanapingana na kuamua lile.

Maamuzi yao yanaathiri sana ustawi wa Tanganyika.
Si kwamba,yanaathiri kwavile znz ni muhimu, ni kwasababu taratibu zilizopo hasa za S2 zinaiondolea Tanganyika uwezo wa kuamua hatma yake

Kwa hali ilivyo, kuna umuhimu Watanganyika wakaa chini na kufanya maamuzi magumu.
Maamuzi ya kupanga taratibu za maisha na nchi yao bila kujali uwepo wa znz

Endapo znz wataona kuna umuhimu wa kuwa pamoja na Tanganyika, wawe washiriki na si kujificha katika koti la JMT, wakiendelea kuzuia Tanganyika kuamua hatma yao

Kwa Watanganyika, mwaswali yakujiuliza ni haya, miaka 49 ya kujitolea imeleta tija gani kwa Mtanganyika.

Na ni liniTanganyika itaondoka katika ‘umateka' wa znz ambao kimsingi hawana athari ya aina yoyote chanya kwa maisha ya Mtanganyika.

Kuna tatizo gani wznz, wakipewa nafasi ya kuamua hatma yao, na si kama ilivyo ambapo znz ni tatizo badala ya mtaji?

Tusemezane
 
MUUNGANO: MZOZO WA KQ UNATOA PICHA YA TWENDAKO

MBELE YA SAFARI MGOGORO MKUBWA, HATIMA YA MUUNGANO MATATANI

Shemu ya I

CHANZO CHA MZOZO HADI KUHUSISHA MUUNGANO

Mzozo wa shirika la ndege la Kenya kupunguziwa safari zake umetoa picha wasiyoiona viongozi wetu

Mzozo ulihusisha kibiashara kati ya Kenya na Tanzania, ulianza kwa Kenya kuzuia magari ya Tanzania kuingia uwanja wa ndege wa JK

Waziri wa uchukuzi Sitta akatoa maagizo safari za KQ kupunguzwa kutoka 42 kwa wili hadi 14.

Kwa mujibu wa waziri, hakuna sheria yoyote inayopanga uwepo wa safari na mamlaka ya anga Tanzania (TCAA) imeamua kupunguza hadi marejeo ya makaubaliano ya nchi mbili kuhusu anga (BASA)

Hilo limetokea baada ya shirika la ndege la FastJet kuomba njia za anga tangu mwaka 2009 na Kenya kutofanyia kazi maombi hayo. Inaeleweka KQ wanataka kumiliki njia za anga bila ushindani(monopoly), FastJet ingekuwa ni tishio kwa biashara yao(competitor)

Waziri alibainisha. KQ itazuiliwa hadi yawepo maridhiano ya makubaliano(BASA) kati ya nchi mbili

Suala lilizua taharuki kwa KQ ambayo Tanzania ni sehemu kubwa ya biashara yao na kulazimu serikali ya Kenya kuingilia kati. Rais Uhuru akaomba mamzungumzo ya dharura na Rais Kikwete wakiwa Namibia

Kenya walitumia propaganda kuwa kuzuia KQ kutaathiri Zanzibar kiuchumi.

Walifanya hivyo wakielewa watachonganisha Tanzania bara na Zanzibar.

Ni Kenya hao hao waliozuia magari yanayochukua watalii kwenda KIA na kisha Zanzibar
Kwa maneno mengine, Kenya walishaathiri uchumi wa Zanzibar kabla ya tatizo la KQ

Kuzuiliwa kwa magari kulifanywa bila serikali ya Kenya kuingilia kati. Na hata ilipobidi, mazungumzo hayakuwa na matokeo mazuri kwa Tanzania. Ilipokuja suala la KQ, Kenya wakaingilia kati haraka sana ili kulinda shirika lao na masialhi mapana ya nchi yao. Wakaomba mkutano wa dharura na kwa masikitiko Rais akakubali

Rais alikubali baada ya shinikizo kutoka Zanzibar. MKuu wa sjirika la viwanja Zanzibar alisema, maamuzi ya waziri Sitta yataumiza Zanz kiuchumi na hilo ni tatizo kubwa la muungano.

Wazanzibar walidai kuwa hakukuwa na makubaliano au mazungumzo kati ya Tanzania bara a.k.a na Tanganyika Vs zanzibar na hivyo muungano unawaumiza kiuchumi

Kenya waliopoona udhaifu huo wakautumia vema kushinikiza masilahi yao na si ya Tanzania kwa kuchonganisha pande mbili, Tanzania bara na Zanzibar kupitia muungano

Inaonekana Rais Kikwete alifanya haraka bila kuzingatia ukweli wa mambo.

Katika kufanya hivyo, Rais alijikuta anawafurahisha Wakenya na Wazazniabr, anamdhalilisha waziri wake, anatelekeza masilahi ya nchi kwa shinikizo la muungano. Rais liwajali wznz zaidi kuliko Watanganyika walioathirika zaidi bila kutazama ukweli halisi wa madai ya wazanzibar na Wakenya

Pia Rais amedharau vyombo vyake na kuviondolea nguvu za kiutendaji na hapa ni TCAA(mamlaka ya anga)

Tuangalie kwanini Rais hakuzingatia masialhi mapana ya nchi

Inaendelea....
 
Sehemu ya II

UKWELI KUHUSU ZANZIBAR, SHIRIKA LA ANGA NA VIWANJA VYA NDEGE

SAFARI ZA KQ TANZANIA BARA NA ZANZIBAR

Shirika la anga la Tanzania (TCAA) ni moja. Mashirika ya viwanja vya ndege ni tofauti kwa Tanganyika na ZNZ

Tanganyika wana (TAA) na Zanzibar wana (ZAA). Wazanzibar walijiondoa katika TAA kwa madai wanataka kukusanya mapato ya viwanja vyao.

Hivyo kodi na mapato yote ya viwanja vya ndege Zanzibar ni mali ya Serikali ya mapinduzi(SMZ)

Wazanzibar hawakujiondoa TAA kwa kutambua mzigo wa gharama za kujisajili kimataifa.

Hivyo, wakaamua kujibanza ili kukwepa gharama wakati huo huo wakikusanya mapato yao bila mchango katika JMT

Mapato ya viwanja vya Tanganyika yanahudumia sehemu ya TCAA iwe kuiptia kodi au iwavyo

Hapa maana yake ni kuwa gharama za uendeshaji wa TCAA ni za Watanganyika, wznz wakitegemea kufaidika na huduma za TCAA bila gharama.

Ndivyo ilivyo kwa Tanzania maritime Org ambako Tanganyika ndiyo inayolipa kodi International Maritime Organization(IMO) kutoka katika vyanzo vya Tanganyika

Zanzibar wana ZMO ambayo hakusanya mapato tu bila mchango katika JMT lakini hutumia jina la Tanzania kusajili meli za zanzibar kimataifa (IMO). Hivyo ndivyo ilivyo katika mamlaka za anga

Pili, KQ ilizuiliwa kufanya safari za Tanganyika. Haikuzuiliwa safari za Zanzibar ambazo ni moja kwa siku.

Wazanzibar hawkuwa na sababu yoyote ya kualalamika kwasababu Tangazo la waziri wa uchukuzi Sitta haliwahusu

Haliwahusu kwa sababu hizi
1. Waziri Sitta hatambuliki Zanzibar , hivyo maamuzi yake yalizingatia masialhi ya Tanganyika

2. Zanzibar haikuathirika na zuio la ndege na madai kuwa wataathirika kiuchumi ni ya kipuuzi tu

3. Zanzibar haina mchango TCAA hivyo, hawana haki ya kimsingi ya kulalamikia maamuzi yanayohusu Tanganyika

4. Masilahi yaliyozingatiwa ni ya walipa kodi wa Tanganyika wanaoendesha TCAA

5. Zanzibar wa serikali na vyombo vyao, na walishajiondoa katika mambo ya muungano

Kwa mantiki hiyo, Rais hakupaswa kushinikizwa na Zanzibar wakati wa kusimamia maamuzi yenye masilahi kwa Tanganyika.

Na wala Tanganyika hailazimiki kufuata nini wanasema wznz kwa kuzingatia kuwa wana serikali yao, na katiba yao ya 2010 inawapa uhuru wa kuanzisha vyombo vyao.

Ni wakati sasa wazaznibar waanzishe shirika lao la anga, walihudumie, wapange safari zao na KQ bila kuathiri masilahi ya Watanganyika, au kuwafunga mikono Watanganyika kwa kutumia neno na malalamiko muungano

Inaendelea....
 
KAULI YA RAIS NI SHERIA

AMWACHA SAMWEL SITTA PORINI

TCAA SASA HAINA NGUVU TENA

Rais Kikwete ametoa amri ya kufuta tangazo la waziri wake Samwel Sitta kuhusu ndege za KQ
Haijulikani kama suala hilo halikujadiliwa ndani ya kikao cha baraza la mawaziri
Kinachoonekana ni rais kuchukua maamuzi yanayomdhalilisha waziri wake wa uchukuzi, Samwel sitta

Rais alifanya hivyo bila kuzingatia Kenya waligoma kuzungumzia suala la magari.

Katika hali isiyotarajiwa, Rais akaamua kuchukua uamuzi wa kunusuru biashara ya KQ akisema uchumi wa Tanzania utaathirika

Endapo alijua usafiri wa anga ni sehemu muhimu ya uchumi, Rais asingekubali kuona shirika la ndege la Tanzania linakufa katika kipindi cha utawala wake.

Hakuna ndege inayoruka kutoka na uatawala mbovu ambao yeye ameutea kusimamia shirika.

Inapofika mahali Rais anasema uchumi wa Tanzania unategemea KQ, kwakweli inasikitisha

Watanzania walisima na serikali katika uamuzi uliolenga kuwaambia Wakenya biashara ni maridhiano si ubabe au ubinafasi.

Kauli ya Rais hakusimama na Watanzania bali sehemu kuu mbili

1. Kuwafurahisha Wakenya kwa kuwapa wanachotaka tena wakichochea kupitia udhaifu wa muungano

2. Kuwafurahisha wazanzibar waliokuwa hawana lolote la kupoteza katika suala zima

Pamoja na hayo, kauli ya rais huwa ni sheria. Kitendo cha kuamuru KQ irudi katika safari zake ni kuondolea mamlaka ya anga uwezo wa kutenda siku zijazo.

Ni nani anayeweza kupinga kauli ya Rais siku za usoni. Mfano, Kenya wanaweza kuzuia FastJet au ATC kuingia Kenya.

Kwavile Rais ameshaondoa nguvu ya TCAA basi itabaidi Watanzania wakae kimya

Hatudhani kama kuna mtendaji wa TCAA anyeipenda kazi yake anayeweza tena kupinga kauli ya rais, na wala hatudhani kama yupo afisa wa serikali nayeweza kzungumzia tena makubaliano ya BASA

Hili limewaondolea wasaidizi wa Rais, yaani waziri Sitta na TCAA nguvu za kusimamia masilahi ya nchi

Lakini pia linatia shaka kama Watanzania watasimama na Rais wao kwavile maamuzi hayazingatii masilahi ya nchi

Tuna uhakika watanzania waliosimama na taifa kuhusu KQ watajiuliza sana ikitokea suala lingine

Hali hii inaligawa taifa na kulitia hofu

HITIMISHO

Matatizo ya KQ yanaonyesha udhaifu wa katiba ya sasa na hiyo ya Chenge

Kwanza, matatizo ya muungano hayajapatiwa dawa na hakuna namna tunaweza kusema yatatatuliwa

Zanzibar wanabaki kuwa kikwazo kikubwa kwa uchumi wa Tanganyika, wanabaki kuwa sehemu ya 'maadui' kama tulivyoona.

Katika timbwili hili la KQ znz wamesaidia sana Kenya bila kujali masilahi ya Tanganyika.
Hali hiyo itaendelea kwa muda mrefu kwasababu znz huangalia mambo kwa jicho la mafao ya muungano hata wasipohusika

Ni somo zuri kwa Watanganyika, masilahi yao yamefungwa katika muungano.

Kwamba, wamebeba muungano wenyewe wenzao wakijificha nyuma na pengine kushirikiana na mataifa mengine kuhujumu masilahi ya Tanganyika.

Utalii na uchukuzi si mambo ya muungano, kwa bahati mbaya Tanganyika inapaswa kulipa gharama za matokeo yoyote kwasababu tu ya jina Tanzania.

Rasimu ya Warioba ilitenga mataifa,leo tusingekuwa na tatizo la kuangalia masilahi ya znz ambayo hayana masilahi na Tanganyika.

Ni wakati watu waangalie matatizo ya siku za mbeleni. Hali hii haiwezi kuendelea kuvumiliwa na Watanganyika

Kama walivyo wznz na serikali yao, Watanganyika wanahitaji fursa ya kuangalia masilahi yao bila kelele au madai ya kipuuzi yasiyo na masilahi na nchi yao. Na wala hawatakiwi kufungwa mikono na znz, shemu isyo na mchango wa kicuhumi kwa namna yoyote

Zanzibar wapewe nafasi waanzishe shirika lao la anga, waendeleze utalii wao kwa njia zao bila kuathiri Tanganyika.

Mbeleni kuna matatizo na haya yatavunja muungano mapema sana

Tusemezane
 
KAULI YA RAIS NI SHERIA

AMWACHA SAMWEL SITTA PORINI

TCAA SASA HAINA NGUVU TENA

Rais Kikwete ametoa amri ya kufuta tangazo la waziri wake Samwel Sitta kuhusu ndege za KQ
Haijulikani kama suala hilo halikujadiliwa ndani ya kikao cha baraza la mawaziri
Kinachoonekana ni rais kuchukua maamuzi yanayomdhalilisha waziri wake wa uchukuzi, Samwel sitta

Rais alifanya hivyo bila kuzingatia Kenya waligoma kuzungumzia suala la magari.

Katika hali isiyotarajiwa, Rais akaamua kuchukua uamuzi wa kunusuru biashara ya KQ akisema uchumi wa Tanzania utaathirika

Endapo alijua usafiri wa anga ni sehemu muhimu ya uchumi, Rais asingekubali kuona shirika la ndege la Tanzania linakufa katika kipindi cha utawala wake.

Hakuna ndege inayoruka kutoka na uatawala mbovu ambao yeye ameutea kusimamia shirika.

Inapofika mahali Rais anasema uchumi wa Tanzania unategemea KQ, kwakweli inasikitisha

Watanzania walisima na serikali katika uamuzi uliolenga kuwaambia Wakenya biashara ni maridhiano si ubabe au ubinafasi.

Kauli ya Rais hakusimama na Watanzania bali sehemu kuu mbili

1. Kuwafurahisha Wakenya kwa kuwapa wanachotaka tena wakichochea kupitia udhaifu wa muungano

2. Kuwafurahisha wazanzibar waliokuwa hawana lolote la kupoteza katika suala zima

Pamoja na hayo, kauli ya rais huwa ni sheria. Kitendo cha kuamuru KQ irudi katika safari zake ni kuondolea mamlaka ya anga uwezo wa kutenda siku zijazo.

Ni nani anayeweza kupinga kauli ya Rais siku za usoni. Mfano, Kenya wanaweza kuzuia FastJet au ATC kuingia Kenya.

Kwavile Rais ameshaondoa nguvu ya TCAA basi itabaidi Watanzania wakae kimya

Hatudhani kama kuna mtendaji wa TCAA anyeipenda kazi yake anayeweza tena kupinga kauli ya rais, na wala hatudhani kama yupo afisa wa serikali nayeweza kzungumzia tena makubaliano ya BASA

Hili limewaondolea wasaidizi wa Rais, yaani waziri Sitta na TCAA nguvu za kusimamia masilahi ya nchi

Lakini pia linatia shaka kama Watanzania watasimama na Rais wao kwavile maamuzi hayazingatii masilahi ya nchi

Tuna uhakika watanzania waliosimama na taifa kuhusu KQ watajiuliza sana ikitokea suala lingine

Hali hii inaligawa taifa na kulitia hofu

HITIMISHO

Matatizo ya KQ yanaonyesha udhaifu wa katiba ya sasa na hiyo ya Chenge

Kwanza, matatizo ya muungano hayajapatiwa dawa na hakuna namna tunaweza kusema yatatatuliwa

Zanzibar wanabaki kuwa kikwazo kikubwa kwa uchumi wa Tanganyika, wanabaki kuwa sehemu ya 'maadui' kama tulivyoona.

Katika timbwili hili la KQ znz wamesaidia sana Kenya bila kujali masilahi ya Tanganyika.
Hali hiyo itaendelea kwa muda mrefu kwasababu znz huangalia mambo kwa jicho la mafao ya muungano hata wasipohusika

Ni somo zuri kwa Watanganyika, masilahi yao yamefungwa katika muungano.

Kwamba, wamebeba muungano wenyewe wenzao wakijificha nyuma na pengine kushirikiana na mataifa mengine kuhujumu masilahi ya Tanganyika.

Utalii na uchukuzi si mambo ya muungano, kwa bahati mbaya Tanganyika inapaswa kulipa gharama za matokeo yoyote kwasababu tu ya jina Tanzania.

Rasimu ya Warioba ilitenga mataifa,leo tusingekuwa na tatizo la kuangalia masilahi ya znz ambayo hayana masilahi na Tanganyika.

Ni wakati watu waangalie matatizo ya siku za mbeleni. Hali hii haiwezi kuendelea kuvumiliwa na Watanganyika

Kama walivyo wznz na serikali yao, Watanganyika wanahitaji fursa ya kuangalia masilahi yao bila kelele au madai ya kipuuzi yasiyo na masilahi na nchi yao. Na wala hawatakiwi kufungwa mikono na znz, shemu isyo na mchango wa kicuhumi kwa namna yoyote

Zanzibar wapewe nafasi waanzishe shirika lao la anga, waendeleze utalii wao kwa njia zao bila kuathiri Tanganyika.

Mbeleni kuna matatizo na haya yatavunja muungano mapema sana

Tusemezane

Nguruvi3,

Kwa kweli nafurahishwa sana na style yako ya uandishi kwani imejikita katika kutoa ilmu kwa njia ya kulalamika na kunung'unika. Hiyo style ilikuwa inatumika enzi zile za utawala wa chama kimoja.

Hivi sasa style inayotumika katika kutoa darsa ni ile ya kuweka na hitimisho badala ya kulalamika na kunung'unika.

Mfano mzuri umeona TAMKO la Maaskofu wametoa darsa zuri sana na MWISHO walihitimisha kwa kusema wapige KURA YA HAPANA kwa katiba pendekezwa.

Kumbuka kuwa Znz hivi sasa ni TAABAN na vihoja vya muungano yaani wamechoka wamechoka na ndio maana unaona vitimbi vyote hivyo. Wanataka nanyi mchoke ili muweze kuzungumza lugha moja ya KILA MTU ACHUKUA MBAO ZAKE.

Jamani mna macho lakin hamuoni tu. japo hamuano hata vitendo navyo hamjagundua tu.

WAACHWE ZNZ WAPUMUE KWA RAHA ZAOOOOO

Poleni sana

 
MPANGO HUU KAMA NI KWELI, UTAHITIMISHA MUUNGANO

NI MAANDALIZI YA VURUGU MWEZI OKOTOBA

Baada ya kuahirishwa kura ya maoni ya katiba ya Chenge, Rais amekaririwa akiwa mjini Washington akisema, maandalizi ya BVR yatakamailika tayari kwa uchaguzi mkuu na kura ya maoni ya katiba ya Chenge

Ilieleweka wazi zoezi la kura ya maoni lilitakiwa kwanza lifanyike baada ya muafaka wa bunge maalumu la katiba.

Bunge lilivunjika wiki chache baada ya kuanza. Kilichoendelea ni maandalizi ya katiba ya CCM

Sheria ya mchakato wa katiba inasema , kulitakiwa kuwe na muda wa kujiandikisha, elimu kwa umma na kampeni.

Hata kwa kutumia uhuni, hayo yasingewezekana kwasababu muda wa uandikishaji ulizuia kila kitu

Ni wazi hakukuwa na uwezekano wa kura ya maoni ya katiba ya CCM licha ya ukweli kuwa haikuwa katiba ya watu

CCM walilazimisha ili waweze kutumia katiba hiyo katika uchaguzi ujao.

Hata hivyo, hawakuangalia ugumu wa kupata katiba hiyo kwa upande wa znz amabko katiba ya 2010 inataka jambo la muungano liridhiwe na BLW kwanza. Uwezekano wa kupata 2/3 ndani ya BLW haukuwepo

Katika kukwepa kikwazo hicho kimbumbumbu, CCM waliwekwa kipindi cha mpito cha miaka 4.

Tume ya Warioba iliweka kipindi hicho kwa kutambua kuwa katika hali ya maridhiano kipindi cha mpito kililenga kutenga shughuli za mtaifa mawili huru.

CCM walidandia wakijua kitaweza kuihalalisha katiba kabla ya uchaguzi.

Ni maono hayo mafupi ndiyo yamezaa hasara ya BVR ambayo ni wazi ingeweza kuepukika.

CCM wakiwa katika wakati mgumu wakachukua hatua za aibu na fedheha kwenda kuazima BVR.

Hii maana yake, hakukuwa na maandalizi ya maana isipokuwa kazi za zima moto ili katiba yao ipite kama walivyotaka

Rais aliposema katiba ya CCM itapigiwa kura katika uchaguzi mkuu, hakika ni jambo la kuangalia kwa umakini

Hawa CCM hawajali mustakabali wa taifa, wanataka wanachotaka kipatikane kwa njia zozote hata kama ni za maisha ya wanandamu.

Tuliona uhuni wa BMLK pale Dodoma ambapo 2/3 ilitafutwa kwa njia za kijinga, kipuuzi na kilaghai kama tulivyoshuhudia wazee wenye heshima zao wakivua nguo

Nia ya CCM kuweka katiba ya Chenge sambasamba na uchaguzi ni ile ile ya kuweka katiba ya CCM na uandikishwaji

Walichotaka ni kuwadanganya wananchi kuwa ukijiandikisha lazima upige kura katiba ya CCM

Baada ya hilo kukwama sasa wanataka kuunganisha mambo kwa wakati mmoja

1. Uchaguzi mkuu
2. Kura ya maoni ya katiba ya CCM
3. Uchaguzi wa madiwani

Kwa uapnde wa znz itakuwa na ongezeko la wabunge wa JMT

Hayo yote yanatarajiwa kuchanganywa ili kuweza kutengeneza mazingira mazuri ya kupitisha katiba yao

Yaani katika vurugu za uchaguzi, ni rahisi mwenyekiti wa tume kutangaza kura imepita

Hatari ya jambo hilo ni uchaguzi mkuu kuwa na vurugu na huenda nchi kuingia katika mtafaruku

Lakini pia, ni hatari kwasababu Rais anayeondoka hataweza kusaini katiba ya CCM, hivyo kumpa anayemfuata kazi ya ziada ya kukabiliana na upinzani wa wananchi, vurugu na kila aina ya mazonge zonge

Nchi haiwezi ikatulia kama Rais ajaye atapewa mizigo isiyomhusu na wala asiyoijua

Rai kwa wapinzani na wananchi ni kuwa hii kauli ya kuchanganya mambo mawili, uchaguzi na kura ya maoni ni ya kuiangalia kwa jicho kali.

CCM hawaishiwi mbinu na inaweza kuwa suprise.

Vinginevyo serikali ikanushe kuwa kauli ya Rais haikulenga wala haikuwa na maana tunayoizungumzia

Tusemezane
 
HISIA ZAJITOKEZA, UTAIFA WATAWALA ''WATANGANYIKA WAKITOA YA MOYONI HAPAKALIKI' WAZANZIBAR WATAWANYIKA, HAWANA KAULI, SASA NGUMI MKONONI
SEHEMU YA I

Ndugu wanaduru Bunge la katiba la CCM au Samwel Sitta linaendelea kwa kuunga unga, likipoteza mvuto maana na thamani. Wajumbe wameacha kazi aliyodai wanaifanya, sasa wageuza ukumbi eneo la mipasho dhidi ya UKAWA

Jitihada za kutoa zawadi ili kuungwa mkono zinaendele. Mwenyekiti Sitta akiahidi kutumia pesa za umma kama mali yake, vifungu nyeti kama cha 1 na 6 vikiwekwa pembeni ili kujadili vile venye mvuto hasa wa kupendeza wazanzibar

Kila kifungu kimejadiliwa kkidhi haja za Wazanzibar ili mradi 2/3 ya nguvu ipatikane. Vifungu ambavyo ni moyo wa katiba vimewekwa kiporo kuchelea Unyeti ''sensitivity' kulivunja bunge la CCM bila UKAWA au jambo jingine.

SINTOFAHAMU ILIANZA SIKU NYINGI

Wazanzibar waliondoka kwao na msimamo wa S3, msimamo uliosimamia mambo mengi yakiwemo kuvunja katiba, kuondoa mambo ya muungano, kupunguza madaraka ya rais wa JMT visiwani n.k.

Ni haki kusema bila kujali CCM au CUF msimamo wa S3 ni wao. Hata kura za maoni ikiwemo maoni ya tume yanaeleza hivyo.

Hulka ya wazanzibar ni wamoja kwa baadhi ya nyakati, lakini huwa wamoja zaidi dhidi ya 'adui' yao Tanganyika. Wznz hukumbwa na kihoro wanapotoka znz. Waliofika Dodoma, umoja wa S3 ukatawanyika. Pandu kificho akisema hakuwemo, waziri wa sheria akilalamika 'tulikubaliana'

UMOJA KATIKA UNAFIKI

Umoja wa wazanzibar una aina za unafiki. Kama tulivyosema, kuvunjika kwa msimamo wa S3 ni dalili moja.

Kujitoa kwa mwanasheria mkuu katika kamati ya uandishi wa katiba ya Sitta, nao unawakilisha unafiki. Maana yake, wapo wanaoamini maafikiano yao kabla, wanaoamini S3 na mkataba bila kujali mrengo wa kisiasa,kwa pamoja hawawezi kusema. Wapo UKAWA wanaosema na CCM wanaotetea mfumo uliopo.

Unafiki una mizizi,ni wznz wanaosema Tanganyika imewageuza koloni, wananyonywa, wanaibiwa na wanateseka ndani ya muungano,waasisi wa muungano wakitukanwa hadharani. CUF wakimshambulia Karume kwa ukatili, CCM&CUF wakimzodoa Nyerere laana .

Ni Wazanzibar wanaodai muungano hauna faida, laiti ingekuwepo nchi za jirani zingeshajiunga Na ni wazanzibar wanaodai, muungano umefunga fursa zao za kukigeuza kisiwa chao kuwa 'pepo' ya Afrika. Madai hayo yakiwemo matusi yanapotolewa, hakuna kiongozi wa CCM au CUF anayesimama kukemea.

Tena wapo wanaorudia maneno kama Nyerere! ilimradi wanazi wao waitikie Laanatullah Hakujatokea kiongozi yoyote kusimama na kukemea dhihaka na kejeli hizo. Leo wanapotokea wazanzibar wakitetea muungano eti kumuenzi Nyerere, duru hatuelewi ni unafiki wa kiwango gani. Kutokana na kutoelewana au kuelewa wanachokizungumzia, hamkani si shwari tena kwa upande wao

Inaendelea sehemu ya II...
Wanabodi,
Leo sikukuu ya Muungano, nafanya mapitio ya baadhi ya mabandiko ya muungano.

Japo waasisi wa muungano wetu huu adhimu ni Nyerere na Karume, muungano ni kama ndoa, kuna mtu ana proposes, mwingine anakubali, ndoa inafungwa. Kwenye muungano wetu huu adhimu, aliye proposes ni Nyerere, Karume akakubali. Nia ya Nyerere ni kwenda kwenye serikali moja. Wito kwa viongozi wetu, kama nia ya kweli ni kudumisha muungano, twende kwenye serikali moja. Tumuenzi Mwalimu Nyerere kwa kuyaishi maono yake!. Nawatakia Muungano Mwema.

Paskali
 
Wanabodi,
Leo sikukuu ya Muungano, nafanya mapitio ya baadhi ya mabandiko ya muungano.

Japo waasisi wa muungano wetu huu adhimu ni Nyerere na Karume, muungano ni kama ndoa, kuna mtu ana proposes, mwingine anakubali, ndoa inafungwa. Kwenye muungano wetu huu adhimu, aliye proposes ni Nyerere, Karume akakubali. Nia ya Nyerere ni kwenda kwenye serikali moja. Wito kwa viongozi wetu, kama nia ya kweli ni kudumisha muungano, twende kwenye serikali moja. Tumuenzi Mwalimu Nyerere kwa kuyaishi maono yake!. Nawatakia Muungano Mwema.

Paskali
Mkuu Pasco

Nukuu bandiko#392 ina maana leo zaidi kuliko siku nilipoandika

Unafiki wa Wazanzibar upo pale pale tuli taja wahusika ambao leo ni Washirika wa CCM

VP M.Othman alikuwa UKAWA, Pandu Kificho akiwa UKAWA usiku mchana CCM

Wote, akina Maalim, Jussa na timu yao hawakutaka S3, walitaka muungano wa mkataba
Walipouliza mkataba wa nini na Tanganyika hawakuwa na jibu wakarudi S3

CUF ndio ACT Wazalendo na wapo raha mstarehe na CCM , hawana habari na katiba mpya
Wazanzibar wapo kimya, mambo safi 'bili zinalipwa huko bara '' katiba mpya ya nini!

Siku mambo yakibadilika, Wazanzibar hawa hawa utawasikia na fukunyuku na kelele

Katika unafiki huu haiwezekani na Serikali1! kutakuwa na matatizo makubwa kuliko

Kuna hisia za Ubora kwa Wazanzibar!ndani ya serikali moja kutakuwa na ''ubora' wa kizanzibar utakaoleta distractions bila faida yoyote, leo ni hivyo seuse S1

Zanzibar haiwezi kukubali serikali moja kwasababu haitapata faida wanayopata sasa hivi

Ndani ya serikali moja Zanzibar itakuwa sawa na Ilala, kwasasa ina hadhi tofauti ndio maana tunaona upendeleo usio na mantiki

Ripoti ya CAG inaonyesha TRA wamekusanya Bilioni 200 ( less than 1/4 of Trillion)
TRA imekusanya Tanganyika Trilion 17 ambazo ni chini ya lengo ya Trilioni 20

Yaani hawajafikia hata robo ya Trilion halafu wanataka kuwe na account ya pamoja na Tanganyika. Unaweka 'senti 10 mwenzako sh 100'' halafu mnataka account ya pamoja!

Tazama Zanzibar inavyopewa mgao wa Trilioni 17 kupitia 4.5% ,
Zanzibar inavyolipiwa mikopo kupitia jina la JMT. Tangu mwaka jana wameshapata mikopo ya JMT zaidi ya bilioni 500 wakati makusanyo yao ni Bilioni 200.
Nani analipa! kama si Machogo

Ukiangalia mambo mengi sana ikiwemo fursa kuna upendeleo kwa Zanzibar kwasababu tu ina special status.

Jambo moja ambalo Zanzibar haina special status ni kuchangia Muungano , fursa na madeni! hapo huwaoni.

Kwa hali hiyo watakubali vipi serikali 1 na hata wakikubali Watanganyika a.k.a machogo watakubali haya yanayoendelea sasa hivi?

Turudi kwa Tume ya Warioba , serikali 3! kama haiwezekani hewala njia nyeupe Tanganyika haina cha kupoteza !
 
KAULI YA RAIS NI SHERIA

AMWACHA SAMWEL SITTA PORINI

TCAA SASA HAINA NGUVU TENA


Rais Kikwete ametoa amri ya kufuta tangazo la waziri wake Samwel Sitta kuhusu ndege za KQ
Haijulikani kama suala hilo halikujadiliwa ndani ya kikao cha baraza la mawaziri
Kinachoonekana ni rais kuchukua maamuzi yanayomdhalilisha waziri wake wa uchukuzi, Samwel sitta

Rais alifanya hivyo bila kuzingatia Kenya waligoma kuzungumzia suala la magari.

Katika hali isiyotarajiwa, Rais akaamua kuchukua uamuzi wa kunusuru biashara ya KQ akisema uchumi wa Tanzania utaathirika

Endapo alijua usafiri wa anga ni sehemu muhimu ya uchumi, Rais asingekubali kuona shirika la ndege la Tanzania linakufa katika kipindi cha utawala wake.

Hakuna ndege inayoruka kutoka na uatawala mbovu ambao yeye ameutea kusimamia shirika.

Inapofika mahali Rais anasema uchumi wa Tanzania unategemea KQ, kwakweli inasikitisha

Watanzania walisima na serikali katika uamuzi uliolenga kuwaambia Wakenya biashara ni maridhiano si ubabe au ubinafasi.

Kauli ya Rais hakusimama na Watanzania bali sehemu kuu mbili

1. Kuwafurahisha Wakenya kwa kuwapa wanachotaka tena wakichochea kupitia udhaifu wa muungano

2. Kuwafurahisha wazanzibar waliokuwa hawana lolote la kupoteza katika suala zima

Pamoja na hayo, kauli ya rais huwa ni sheria. Kitendo cha kuamuru KQ irudi katika safari zake ni kuondolea mamlaka ya anga uwezo wa kutenda siku zijazo.

Ni nani anayeweza kupinga kauli ya Rais siku za usoni. Mfano, Kenya wanaweza kuzuia FastJet au ATC kuingia Kenya.

Kwavile Rais ameshaondoa nguvu ya TCAA basi itabaidi Watanzania wakae kimya

Hatudhani kama kuna mtendaji wa TCAA anyeipenda kazi yake anayeweza tena kupinga kauli ya rais, na wala hatudhani kama yupo afisa wa serikali nayeweza kzungumzia tena makubaliano ya BASA

Hili limewaondolea wasaidizi wa Rais, yaani waziri Sitta na TCAA nguvu za kusimamia masilahi ya nchi

Lakini pia linatia shaka kama Watanzania watasimama na Rais wao kwavile maamuzi hayazingatii masilahi ya nchi

Tuna uhakika watanzania waliosimama na taifa kuhusu KQ watajiuliza sana ikitokea suala lingine

Hali hii inaligawa taifa na kulitia hofu

HITIMISHO

Matatizo ya KQ yanaonyesha udhaifu wa katiba ya sasa na hiyo ya Chenge

Kwanza, matatizo ya muungano hayajapatiwa dawa na hakuna namna tunaweza kusema yatatatuliwa

Zanzibar wanabaki kuwa kikwazo kikubwa kwa uchumi wa Tanganyika, wanabaki kuwa sehemu ya 'maadui' kama tulivyoona.

Katika timbwili hili la KQ znz wamesaidia sana Kenya bila kujali masilahi ya Tanganyika.
Hali hiyo itaendelea kwa muda mrefu kwasababu znz huangalia mambo kwa jicho la mafao ya muungano hata wasipohusika

Ni somo zuri kwa Watanganyika, masilahi yao yamefungwa katika muungano.

Kwamba, wamebeba muungano wenyewe wenzao wakijificha nyuma na pengine kushirikiana na mataifa mengine kuhujumu masilahi ya Tanganyika.

Utalii na uchukuzi si mambo ya muungano, kwa bahati mbaya Tanganyika inapaswa kulipa gharama za matokeo yoyote kwasababu tu ya jina Tanzania.

Rasimu ya Warioba ilitenga mataifa,leo tusingekuwa na tatizo la kuangalia masilahi ya znz ambayo hayana masilahi na Tanganyika.

Ni wakati watu waangalie matatizo ya siku za mbeleni. Hali hii haiwezi kuendelea kuvumiliwa na Watanganyika

Kama walivyo wznz na serikali yao, Watanganyika wanahitaji fursa ya kuangalia masilahi yao bila kelele au madai ya kipuuzi yasiyo na masilahi na nchi yao. Na wala hawatakiwi kufungwa mikono na znz, shemu isyo na mchango wa kicuhumi kwa namna yoyote

Zanzibar wapewe nafasi waanzishe shirika lao la anga, waendeleze utalii wao kwa njia zao bila kuathiri Tanganyika.

Mbeleni kuna matatizo na haya yatavunja muungano mapema sana

Tusemezane
Yanayotokea leo tuliyasema miaka 8 iliyopita. Soma bandiko hasa 'Hitimisho'
 
Nguruvi3,

Hakika Huko Ndio tuendako.
Nikianza na hoja yako juu ya moto unaozidi kuchochea ndani ya CCM, kwa kweli ni Vigumu kuelewa nini itakuwa ni hatima ya cheche hizo ndani ya chama. Kwa mfano Mdogo tu, Kabla ya kufunga kikao cha bunge usiku wa jumatatu iliyopita, Samuel Sitta aliwaeleza wajumbe Kwamba kila mmoja wao atapewa Cheti kilichosainiwa na rais Kikwete kuonyesha Kwamba mjumbe huyo amefanya "kazi muhimu na ya kihistoria ya kutunga katiba".

Ni Vigumu kuelewa iwapo mpango huo ulikuwepo tangia awali/Kabla ya mchakato kuingia nyongo, au ni mpango mpya ulioletwa na Sitta kwa ajili ya kuwalaghai wajumbe Kwamba watatambuliwa na rais. Wengi tunajiuliza, kwanini then rais Kikwete alifikia makubaliano na ukawa hivi karibuni Kwamba kwa muda na mazingira yaliyopo, katiba mpya haiwezi kupatikana; Kauli ya Sitta kuja baada ya kauli ya rais Kikwete iliyokiri Kwamba katiba Mpya haiwezekani Kabla ya uchaguzi 2015 maana yake ni nini? Je Ina maana Sitta Ana mamlaka makubwa zaidi ya Mwenyekiti wake na rais wa nchi juu ya suala Zima la katiba mpya?

Tayari watanganyika wengi wameanza kuona athari za mwenendo wa Sitta kwa Tanganyika, Zanzibar na muungano kwa ujumla, lakini sijui Kama wajumbe wa BLK wanaelewa nini kinafuatia kutokana na mwenendo wa Sitta na katiba mpya. Kwa mfano - Sitta ameingiza masuala ya ardhi, maji, viwanda, uvuvi, serikali za Mitaa, uwekezaji, na takukuru Kama masuala ya muungano. Tuangalie baadhi ya mambo haya kwa undani:

Tukianza na Ardhi - Kuchukua mambo ya Tanganyika Kama vile ardhi na kuyaingiza Katika katiba ya muungano, hii ni Kinyume na rasimu ya tume. Pia kufanya hivyo ni kurekebisha katiba iliyopo, huku sio kutunga katiba mpya. Kazi hii haipaswi kufanywa na BLK Bali bunge la JMT. Kwa mfano, katiba ya JMT (1977) inataja suala la umilikaji wa ardhi Katika ibara ya 24. Kila Raia wa JMT anayo Haki ya kumiliki Mali na ulinzi wa Mali yake, ingawaje Haki hii Ipo upande mmoja tu wa muungano.

Sheria ya ardhi ya mwaka 1999 Katika sura yake ya 113, kifungu cha 3(a) kinatoa Dira na Sheria kuhusu kanuni muhimu ya sera ya taifa ya ardhi. Kanuni hii imemkabidhi rais wa JMT usimamizi wa ardhi kwa niaba ya wananchi wa JMT. Pia Sheria ya ardhi ya kijiji sura namba 414 na Sheria ya kusajili ardhi Sura ya 334, hizi Ndio uongoza usimamizi wa matumizi ya ardhi kwa Mujibu wa Sheria na sera ya ardhi. Tatizo ni hili:

Pamoja na Kwamba Sheria hii Inahusu jamhuri ya muungano wa Tanzania, ni suala lililo wazi Kwamba Sheria hii haitumiki Zanzibar. Anachofanya Sitta kwa wazanzibari ni kuwaletea kitu kipya yani kuagiza Zanzibar kuruhusu ardhi Yao kutumiwa na Raia wa Tanganyika, suala ambalo wamelikataa Katika kipindi chote cha muungano, na kuliweka sasa itakuwa ni moja ya njiti za kibiriti zitazowasha moto na machafuko.

Masuala mengine Kama vile serikali za Mitaa, takukuru, vyama vya Ushirika, uwekezaji, viwanda, vijijini vya ujamaa, vitongoji, uvuvi, pembejeo, Kilimo etc, haya yote ni masuala yanayohusu Tanganyika moja kwa moja serikali ya Tanganyika. Ndio maana tume ya katiba ikayaweka haya Kando, nje ya muungano. Kama tunakumbuka vyema, haya ni sehemu ya malalamiko mengi ya wananchi Wakati wa ziara za tume ya katiba, ambapo wapo wananchi waliolalamika Kwamba haya mambo yanahusu Tanzania bara pekee (Tanganyika) lakini yanaendeshwa kwa kodi za wananchi wote wa Tanzania.

Tukichukulia mfano wa uwekezaji, kwanini TIC iwe ni ya muungano, huku taasisi hii kwa upande wa Zanzibar ibakie nje ya muungano? Wazanzibari ni mabingwa wa kusamehe kodi, kwa vile mjomba Tanganyika yupo kutoa fedha. Kitendo cha TIC kuwa Chombo cha muungano kitakuwa Kama uwepo wa TRA na ZRA Zanzibar, mzigo kwa Tanganyika.

Tukija kwenye suala la viwanda, sekta hii Ndio inayobeba matumaini ya Ajira kwa vijana wetu. Kufanya viwanda kuwa sehemu ya muungano, Wakati viwanda karibia vyote vitakuwa bara ni kujenga mazingira Kama yake ya 21% ya Ajira kwa wazanzibari; wazanzibari watadai vijana wao waajiriwe kwa quota Fulani Katika viwanda ambavyo haviwahusu, huku mtanganyika akiumia. Na kwa viwanda ambavyo vitashamiri znZ iwapo itatokea hivyo, watanganyika hawatopewa fursa kule.

Tukichukulia mfano TAKUKURU, Sitta na Kundi lake wanaigeuza kuwa ni ya muungano Wakati Chombo Hiki hakiruhusiwi kufanya kazi nchi Jirani ya Zanzibar. Nchi hii Jirani haitambui takukuru ni kiumbe gani, na Wala haimo Katika Orodha ya mambo ya muungano kwa Mujibu wa mkataba wa muungano (1964). Unga'ng'anizi huu wa Sitta na wenzake ni kuua muungano, sio kuboresha muungano.

Zanzibar wana Chombo kinachofanana na takukuru, kinaitwa - kamishen ya rushwa na uhujumu uchumi. Kitendo cha Sitta kuifanya takukuru kuwa ni suala la muungano ni kuzidi kuiminya Zanzibar, lakini pia kuongeza matumizi ya fedha za walipa kodi wa Tanganyika kwa nchi Jirani bila ya faida kwani gharama za kuendesha Chombo Hiki chini ya serikali Mbili, wazanzibari watasema Hilo ni la muungano (Tanganyika).

Nchi Mbili zinapoungana, hubadilika huwa nchi moja yenye mamlaka moja ya Kidola. Tofauti na hili, kupitia katiba yake ya 2010, chini ya uongozi wa Sitta na wenzake, Zanzibar imekuwa ni nchi huru. Ina bendera yake, Wimbo wake wa taifa, Ina serikali yake kamili inayoambatana na political autonomy, na Ina fiscal and policy autonomy.

Katiba yake inatambua Kwamba Zanzibar ni nchi, na Sitta na wenzake wanatambua Kwamba nchi hii Ipo ndani ya nchi nyingine ya Tanzania, lakini wanadhania Kwamba hatari hii watanganyika watapuuzia na suala hili litapita tu Kama upepo. Katiba ya Zanzibar imeruhusu nchi hii ya Jirani kuanzisha majeshi yake, ambayo yapo chini ya amiri jeshi mkuu wa nchi hiyo Jirani. Tuna uhakika gani Kwamba hatutaanza kutuniana misuli Kama Korea kusini na kaskazini kwa masuala ya rasilimali? Kitendo cha kuruhusu znZ kuwa ni nchi kamili, nchi hii itakuwa na Haki ya kutetea Kile inachoamini ni chake na hata Jumuiya ya kimataifa itaelewa hivyo.

Kitendo cha wajumbe wa BLK pale Dodoma kushabikia juhudi za Sitta kuzima serikali Tatu kitasababisha muungano kuingia Katika machafuko makubwa sana ndani ya kipindi kifupi. Kutaibua migogoro mipya ndani ya muungano, hasa baada ya watanganyika Kuamka na kujua nini kinaendelea. Hali hiyo itavunja muungano. The question that follows ni je, Nani atakuwa loser zaidi Kati ya Tanganyika na Zanzibar? Jibu ni dhahiri - ZANZIBAR.

Uzuri wa JF ni kutunza kumbu kumbuku. Bandiko hilo hapo juu lipo katika uzi huu na liliandikwa miaka mingi.
Soma Bandiko lote halafu Tafakari maneno yaliyokaziwa (Bold) aya ya mwisho.
 
NI 'DONDA' KUBWA LINALOHITAJI TIBA NA SI DAWA ZA MAUMIVU

Suala linalorindima nchini limezua tafrani likielezwa kama 'open a Pandora's Box'. Ukweli ni kwamba halikufungua Pandora, ukisoma uzi huu ni jambo lililokuwa wazi wala si la kubashiri, kutabiri au kuhijtaji akili.

Tabia za Watawala wetu ni kujiaminisha mambo yatakuwa kama wanavyodhani bila kujali nyakati na kizazi.

Rais Jumbe alilipa gharama kwa kuongelea Muungano. Tume zote za majaji na Wanasiasa zilizoundwa zilieleza pasi na shaka tatizo la Muungano. Miaka ya 90 likazuka jambo la OIC, tukio kubwa lililowahi kutokea tangu 1964 likiutikisa Muungano. Kundi la G55 liliundwa kudai Tanganyika.

Mazingira ni kama ya leo yakihusisha Zanzibar kupewa kipaumbele cha kukiuka katiba ya JMT.
Mwalimu Nyerere akazima hoja kwa nguvu za ushawishi tu lakini si hoja.

Mwaka 2014 Mzee Warioba na Tume alipendekeza Muungano uangaliwe.
Jaji Warioba alisema jambo lililoisumbua kamati ni la Muungano, kukiwa na makundi , kwamza likikataa muungano, la pili lserikali 2, serikali 1, la nne serikali 3 na lile la Mkataba.
Jaji akabainisha kwa masilahi mapana ya nchi Serikali ndhiyo jibu

Kwa mtazamo, Jaji aliamua hivyo kwasababu: Kuvunja Muungano ni kuvunja Utaifa, tatizo kwa Wananchi. Serikali 2 zimefeli kimuundo, serikali 1 haiwezekani kwasababu za Utaifa(Zanzibar), serikali 3 inawezekana ili kwa uwiano na usawa. Serikali ya Mkataba haiwezekani Tanganyika Itauliza mkataba utafaidisha vipi.

Rais SSH baada ya joto kali la Katiba mpya aliunda kamati ya Mkandala pengine kuua hoja ya Tume ya Jaji Warioba iliyopendekeza Serikali 3. Rais SSH anajua ugumu wa suala na asingependa kuligusa.
Hata hivyo kama ilivyokuwa awali, suala limepata dawa za maumivu kulituliza, SSH alijaribu yake pia.

Kwa bahati mbaya gonjwa limekuwa likisubiri mahali pa kutokea. Bandari likaonyesha ukubwa wa tatizo. Lakini si ukubwa tu uliojitokeza bali hali ilivyo hasa ya kuleta usawa wa Muungano bila kuleta usawa wa kuwajibika katika muungano.

Zanzibar inasikilizwa kwa kinachoitwa kero, Watanganyika wameduwaa bila kujua wanasimama wapi. Linapokuja suala la Masilahi tatizo linakuwa kubwa, Wazanzibar watatumia fursa za Utanzania iwe ni ajira , biashara n.k. wakijitenga kwa mambo mengi kwa kisingizo cha katiba yao kama hili la Bandari.

Zanzibar wamejipa uhuru wa kukiuka katiba ya JMT tangu mwaka 2010 ''with impunity' .
Suala la Bandari limetumbua tu jipu na kuonyesha ' reservations and resentment' kati ya nchi mbili.

Tufikirie kinadharia tu, kwamba Zanzibar haipo katika mkataba wa DP World, ina mkataba na kampuni za Oman kuendesha bandari. Hii ina maana moja, kutajengeka upinzani kati ya Tanganyika na Zanzibar.

Katika hali hiyo Tanganyika ni kubwa ilipakana na nchi 8 ni lango muhimu Biashara na utalii kwa Zanzibar. Ushindani wa Bandari utaiumiza Zanzibar kwasababu ya jiografia. Katika chuki iliyojejengeka ni vipi Zanzibar watarudi kuongea na Tanganyika ili kupata fursa na si ushindani?

Hali itakauwa hivyo katika maeneo yote hata ya ajira. Kwamba, Wazanzibar wataangaliwa kama 'nchi jirani''. Pengine kwa Wazanzibar hilo ni jema kwasababu ya Utaifa wao lakini je litawasaidia mbele ya safari?
JMT ni Mwajiri mkubwa wa Wananchi wa Zanzibar. 21% ya nafasi za muungano ni nyingi kuliko nafasi za SMZ.

Suala la Bandari limeansha majeraha kwamba popote Wazanzibar walipo pasipo pa muungano wataangaliwa kwa Uzanzibar na si Utanzania. Mfano, wengi hawakujua wizara ya uchukuzi inaongozwa na Wazanzibar.

Hali hiyo inawafanya Watanganyika wautafute Utanganyika wao na hivyo Utanzania unafifia.
Pasipo na Utanzania ni fursa finyu kwa Wazanzibar, kwa maana kwamba sasa hivi wanapata fursa kwasababu ya Utanzania, kwa hili la bandari hali itakuwa tofauti sana.
Watanganyika watakuwa na wivu wa nchi yao kama walivyo Wazanzibar! Hamkani si shwari tena

Ni katika mazingira hayo na ambayo Tanganyika ndiye mlezi na mbeba wa muungano hali itakuwa tete.
Uwezekana wa kuamka asubuhi moja bila Muungano si suala la ' kama inawezekana bali lini'.

Ni ukweli ambao viongozi hawataki kuusikia kama ule wa Mh Mbowe kwa maneno yake makini sana yaliyosemwa kwa busara lakini akashambuliwa. Matokeo yake sasa hali ni mbaya zaidi

Kuna nafasi moja ya kunusuru Muungano, si kwa silaha au vitisho kwasababu yote hayo yameshindwa.
Kuulinda Muungano kwa kuuliza Wananchi wa Zanzibar kwa kura ya maoni ikiwa bado wanataka Muungano.

Ni Zanzibar kwasababu malalamiko yanatokea kwao, na ndio wavunjaji wakubwa wa katiba ya Muungano lakini pia duniani kote mwenye malalamiko hupewa nafasi. Imetokea hivyo Scotland, Quebec, Timor na kusikilizwa kwa S.Sudan, Eritrea n.k. na sasa ni wakati Wazanzibar waulizwe.

Suala la Bandari limeonyesha ufa,limefunua chuki na manung'uniko tuliyodhani hayapo, limetikisa muungano.

Donda linahitaji matibabu si dawa za maumivu zilizoshindwa. Busara itumike!
 


Video hiyo ina maneno ya Prof Kabudi yanaelekea kutokea. Mwl Nyerere alikuwa kiongozi anayeona mbali.
Tunarudia tena kusema suala la Bandari pamoja na ukubwa na umuhimu wake limekuwa ni sehemu tu ya jipu lililovia . Bandari imeonyesha matundu makubwa hasa ya Katiba.

Suala la Katiba limepigwa dana dana sana, Rais Kikwete akiwa na fursa akaliahirisha. JPM hakutaka kulisikia akiamini 'mkono wa chuma'. Hili ni donda ndugu linalovuja damu .

Video hapo juu inaonyesha Watanganyika wakishangilia sana suala la Tanganyika likitajwa.

Kwa hili la Bandari jitihada za kumnanga Mh Mbowe kwa tahadhari zimewarudi CCM vibaya sana.

Ukitaka kuona ukubwa wa tatizo hasa la muungano, ni pale ambapo kuna CCM wachache wenye kelele sana na CCM wengi wakiwa kimya. Kuna CCM Zanzibar wakiwa kimya sana kana kwamba hali ni shwari.

Kuna ACT Wazalendo wakisema sana tena wakimshangilia Rais SSH, pale maskani Kisonge ni kimyaa .

Kuna janja inayotumika kurekebisha sheria na Tume za uchaguzi ili kuua hoja ya Katiba mpya.

Janja hiyo itafikia hatma kabla ya kuanza na huenda likatimka vumbi jingine.
Hili la Bandari halitoshi kuwa mfano? Hili la bandari halitoshi kueleza jambo ?

Bandari na mambo mengine yaliyotokea yamefunua vidonda, suala la Katiba mpya na muundo wa muungano vitabaki kama vijinga vya moshi!

king suleman Kalamu
 


Futailia Hotuba hiyo ya Mansour

Dakika 15.54 : Mansour anasema Bank iliyoanzishwa na Mh Karume sasa imeletewa kiongozi kutoka Tanga.
Dakika 16.51 : Mansour anasema wanaletwa Watanganyika , na sasa Wazanzibar wana nyang'anywa mamlaka yao

Hoja:
Maneno hayo yanasema bila kificho, hatujawasikia Wabunge wakisema ni uchochezi.
Akiyasema Mtanganyika kama Mh Mbowe kwa sataha akionya tatizo kama kiongozi wa chama hilo likawa nongwa.

Mbowe aliambiwa kusema Uzanzibar na Utanganyika ni ubaguzi, akisema maneno yale yale Mzanzibar ni haki!!

Mansour kasema wazi wanaletwa Watanganyika! Kuna tatizo gani Watanganyika wakisema kaletwa Makame Mbarawa na Katibu mkuu kusaini mkataba usio wa jambo la muungano!
Kwanini kuna kibali cha kusema kwa Mzanzibar na uharamu kwa Mtanganyika?

Dakika ya 18.00.: Salaum Bimani anasema kunahitajika muungano ulio sawa na wa heshima.
Akaendelea, chama cha Wanasheria wa Zanzibar ni ZNS na uchaguzi umefanywa na Rais katoka Tanganyika.
Bimani anasema chama cha wanasheria Tanganyika hakina Mzanzibar.

Hoja:
Muungano uliso sawa unakuja na uwajibikaji. Zanzibar inastahili heshima na usawa, ni kweli, lakini pia Zanzibar ionyesha thamani ndani ya Muungano.Zbar iwe mshiriki wa Muungano kwa kuwajibika na si kutaka 'nipewe'

Thamani ya Zanzibar ni ushiriki katika muungano. Huwezi kulipiwa umeme na Familia yako ukabaki na heshima. Huwezi kupewa pesa za walipa kodi wengine ukabaki na heshima.
Huwezi kukopa ukalipiwa deni na mtu mwingine ukabaki na heshima.
Huwezi kuwa na Wabunge wanaolipiwa gharama na mtu mwingine ukabaki na heshima na huwezi kuchangia sifuri ukadai 5 katika 10 na ukabaki na heshima. Heshima ni kuwajibika.

Bwana Bimani ana jazba tu na kusahau ukweli. Fatma Karume ni mjukuu wa Mzee Abeid Karume wa Zanzibar.
Fatma amekuwa mwanachama wa chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) na Rais wa chama hicho.
Sidhani kama Bimani hana taarifa! na kama anajua basi kuna jambo kuhusu Uzanzibar wa Fatma.

Katika dakika 16.51 Mh Mansour anafafanua kuhusu watu kutoka bara akisema hata Wazanzibar waliofanya kazi Tanganyika hawafai kupewa nafasi Zanzibar. Hapa kuna jambo, kwamba chuki dhidi ya Tanganyika inaanza kuwanyima haki Wazanzibar wanaotafuta riziki zao Tanganyika na si kwingine duniani.

Wanasheria wa Zanzibar wanaofanya kazi zao bara ni wanachama wa TLS. Hivi hili linahitaji Certificate!

Hoja hiyo ni kama ile ya Makamu Othman Masoud Othman aliyoitoa hivi karibuni akisema Wachezaji wa Mpira wa Zanzibar wanacheza bara na hivyo timu za Bara zinafanya vema.
Bwana Masoud anasema hilo ni tatizo linalotokana na Muungano na kwamba Zanzibar haiendelei.

Hoja:
Bwana Othman Masoud Othman (OMO) ni kiongozi mwepesi sana kujenga hoja nyepesi zisizolingana na hadhi yake akiwa amesimama juu ya viatu vya Almarhum Maalim S.S. Hamad.

Siku za nyuma Ligi ya Tanzania ilikuwa na timu za Zanzibar na timu za visiwani zilifanya vema kwa ushindani mkubwa. Tunakumbuka Navy, KMKM, Small Simba, Miembeni , Jamhuri n.k. na zilifikia hatua ya kuwakilishia Tanzania.

Jitihada za Alli Salehe na Mwenzake Farouk za kuziondoa timu hizo ili kuwe na ligi ya Zanzibar zilifanikiwa.

Jitihada za kuifanya Zanzibar iwe mwanachama wa CAF au FIFA zilifanyika tena zikiungwa mkono na Tanganyika.
Kwa bahati mbaya sheria za kimataifa haziitambui Zanzibar na hapo ndipo tatizo lililpo.

Kwa mantiki hiyo kuondoa timu za Zanzibar katika ushindani zimerudisha soka nyuma Zanzibar.
Hakuna faida yoyote Tanganyika inapata kupitia michezo Zanzibar kama tunavyoona timu zake zikifanya vema.
Fikra kwamba Tanganyika inaiminya Zanzibar ni za masikitiko, swali kwa OMO, ni ili iweje na kwa faida gani

Kuhusu wachezaji wa Zanzibar kuchezea timu za bara, Mh OMO anashindwa kuelewa michezo ni ajira.
Wachezaji wa Zanzibar hawashikiwi viboko wala hakuna sheria ya Muungano inayowataka wacheze bara.

Wachezaji wa Zbar wapo bara kwa masilahi yao lakini wanaweza kucheza popote duniani .
Masoud Othman akae na wachezaji wa Zanzibar na awashawishi wakacheze Mauritius, Comoro , Somalia au Eritrea. Hakuna atakayehoji wala kuuliza maana hiyo ni haki yao, lakini kusema Tanganyika inachukua wachezaji wa Zanzibar inafedhehesha. Kwanini ACT hawamwandai kiongozi wao katika mikutano?

Kusema kwamba Muungano ndio unasababisha wacheze Tanganyika ni jazba tu isiyo na msingi.
Si Wachezaji tu, hata ikiwezekana wafanyakazi wote waalioko bara warudi Zbar hilo ni wazo zuri na Mh OMO ana ushawishi, awaambie waondoke na kurudi visiwani. Tanganyika haina sababu za kuwazuia

Katika mazingira ya namna hii ambayo viongozi kama Bimani na OMO wanazua uongo, kuna kila sababu ya kutoa kura ya maoni kwa Wazanzibar waamue kuhusu Muungano. Chuki ya Wazanzibar dhidi ya watu wa Bara imefuruta.

Isisubiriwe Watanganyika wakajaa furutu maana hata nje ya muungano mataifa haya yamekaribiana.

Waswahili husema udongo uwahi ungali maji. Suala la Muungano si 'kama bali ni lini' ikiwa busara hazitatumika

Mwalimu Tindo
 
BANDARI INAZIDI KUFUKUA 'MASHIMO' NA NYUFA

Kama kuna wakati nyufa za muungano ziliwahi kuonekana bila 'darubini' ni kipindi hiki cha suala la Bandari

Nyaraka ya 'mkataba' au 'makubaliano ' ilipovuja vyama vya siasa vilitoa misimamo ya awali

CCM walitetea msimamo wa mkataba kama ulivyoelezwa na serikali. Kwamba hakuna tatizo
CHADEMA walieleza haja ya kuukataa mkataba kwa ifungu vibovu lakini pia wasi wasi wa Zanzibar kuachwa nje
ACT Wazalendo wakaeleza DP iwe na Mbia ambaye atakuwa ni Serikali ya Tanzania akimiliki Hisa

Msimamo wa CCM una matatizo kwasababu nyingi sana hasa za vifungu. Kuna vifungu vinavyohitaji wanasheria wafafanue baadhi vinahitaji akili ya kawaida tu ya mtu mwenye elimu yoyote.

Mathalani:
Mkataba au makubaliano hayajaelezwa kwa ufasaha, Spika akiwa na tafsiri inayobadilika, mwanasheria wa Wizara akiwa na lake , CCM wakiwa na lao , waziri lake n.k.. Haieleweki ni kitu gani nchi inahangaika nacho

CCM hawajaeleza, mkataba unasema ni kati ya Dubai na ''The united Republic of Tanzania'', iko wapi Zanzibar mshirika wa URT? Je, Dubai ingetoa pesa kwa URT ingalikuwa pesa ziwe za Tanganyika na Zanzibar haihusiki.

Kwa miaka mingi hilo ndilo limekuwa tatizo la muungano, lakini kwa mkataba Zanzibar haionekani inasema haihusiki. IIkiwa Zanzibar haihusiki, vipi mapato yanayotokana na rasilimali za Tanganyika kama bandari zake zote za bahari na mawaziwa zinazopelekwa hazina na kuhudumia Muungano?

Hoja ya Watanganyika si kudhulumiwa bali kueleza hisia kwamba kuvaa koti la muungano ni hasara kinyume na Wazanzibar wanavyoamini.

Mfano, mapato ya Tanganyika yanahudumia madeni ya nje na ndani ya JMT pamoja na SMZ.

Mapato ya Tanganyika yanahudumia wizara na taasisi za muungano.
Wafanyakazi wa muungano ambao asilimia 21 ni Wazanzibar wanalipwa mishahara na mafao yao ya sasa na uzeeni kwa pesa kutoka hazina ya Tanganyika inayojulikana kama Tanzania.

Kwa maneno machache, kuvaa koti ni kuhalalisha rasilimali za Tanganyika kuwa za wote na zile za Zanzibar kuwa Zao peke yao. CCM hawawezi kutetea hoja hiyo zaidi ya kumshambulia Mwenyekiti wa Chadema Mh Mbowe.
Mifano inayohusu CCM na kushindwa kutetea hoja ni mingi na orodha ni ndefu, inatosha kwa uchache kueleza hayo

Kwa upande wa CHADEMA, msimamo ni ubaya wa mkataba wote na wanataka ufumuliwe.
CDM hawaridhiki na Zanzibar kuondolewa kwa maana moja , kwamba kama kuna mafao ya mkataba iweje Zanzibar wasishirikishwe wakiwa ni sehemu ya JMT au The United Republic of Tanzania kama mkataba unavyosema?

Hoja hii inashadidiwa na hoja ya kwamba Tanganyika iwepo ili kama ilivyo Zanzibar nayo isimamie rasilimali zake.

Katika hili Chadema wanasema suluhu ni uwepo wa Katiba mpya itakayoitambua Tanganyika kama sehemu ya Tanzania na iwe na mamlaka ya kusimamia rasilimali zake kwasababu 'uchungu wa mwana ajuaye ni Mzazi'

Kwa upande wa ACT Wazalendo, msimamo wao umeingia mawaa. Jumapili hawakutokea katika mkutano uliozungumzia Bandari kule Temeke, badala yake chama kikasema bado kinafanya tathmini.

Huo ni msimamo unaopingana na hoja ya kiongozi Zitto aliyetaka serikali iwe mbia wa uendeshaji wa Bandari na huo ulikuwa msimamo wa ACT Wazalendo Tanganyika

Kubadilika kwa msimamo wa ACT kunachagizwa na ukweli kwamba suala la Bandari limeshangiliwa sana na ACT Wazalendo Zanzibar ambao kwao hiyo ni njia njema ya kufikia lengo lao ka kuvunja muungano au mamlaka kamili.

ACT inasimamishwa na Wazanzibar kwa wingi wao kama chama kikuu cha upinzani.
Kiongozi Zitto hana kauli yanapokuja masuala ya nchi kwasababu ACT Zanzibar ndio wenye nguvu.

Hili linaacha maswali ikiwa ACT ni chama cha Tanzania na si cha Zanzibar. Tunasema Tanzania kwa maana na Tanganyika. Kwa hali ilivyo suala la bandari na misimamo ya vyama imekiweka ACT njia panda.

Kwa kauli za kejeli , matusi na indhara kutoka kwa viongozi wa ACT Zanzibar kama Makamu Othma Masoud, Jussa, Duni na wengine dhidi ya Tanganyika, ni wazi ACT inapoteza ushawishi Tanganyika.

Kwamba, chama cha ACT Wazalendo hakina masilshi na Tanganyika, na ACT Zazibar wanaona Tanganyika kama adui yao. Mbele ya safari chama hicho kitabaki kuwa cha Zanzibar na kuathiri sana ustawi wake kisiasa Tamnganyika

Suala la bandari linazidi kuibua nyufa nyingi zilizokuwa zimejificha kama misimamo ya vyama, katiba mpya n.k.

Hata CCM wanachama kwasiri wanaamini uwepo wa Tanganyika kama wanavyoamini CHADEMA.

Watanganyika wanajiuliza ACT Wazalendo inasimama wapi? Na kauli za viongozi wa Zanzibar nini mustakabli wa chama hicho kwa upande wa Tanganyika ikizingatiwa chama kimeshindwa kutetea Tanganyika wakati kinahitajika!

 
WAZANIZBAR WAPEWE 'HAKI YAO' JUU YA MADAI

Wazanzibar wamedai kuongezwa mambo 11 ya mkataba wa Muungano yakifikia 22 na sasa ni zaidi ya 36

Madai ya Wazanzibar kwa kupitia chama cha ACT Wazalendo na CCM wanojificha yanabeba sura 2
Kwanza, ni madai yenye ukweli kwa kuangalia mkataba wa Muungano wa 1964
Pili, ni madai yenye uongo kwa hoja kwamba Tanganyika imeyaongeza ili kunufaika nayo.

Katika mambo 11 ya nyongeza, hakuna Mzanzibar anayejibu swali moja, kwamba, Tanganyika inafaidika vip. nayo.

Mfano, Elimu ya Juu si suala la Muungano. Kuongezwa kumewezesha Wazanzibar wasome vyuo vya kati na juu Tanganyika wakipewa nafasi za upendeleo maalumu kuingia na hata kitaaluma. Huu ni ukweli mchungu lakini ni ukweli. Wapo wanafunzi waliofeli wanaingia vyuo vikuu kwa Uzanzibar

Kupitia elimu ya juu, Zanzibar wanapata mikopo kutoka HESLB zaidi kuliko inayotolewa na ZHESLB
Pesa za HESLB zinatoka ni kodi za Watanganyika kupitia Hazina Dar es Salaam.

Kuna ushahidi wa kutosha kwamba kodi zinazokusanywa Zanzibar hazivuki bahari na BoT kupitia Gavana Marhumu Ndulu wameeleza wazi Zanzibar ina miongo zaidi ya 4 haichangii chochote katika Muungano.

Swali wasilojibu Wazanzibar ni moja, ni kwa njia gani Tanganyika inanufaika na ongezeko la mambo ya Muungano?
Swali hilo haliwezi kutatuliwa kwa majibu rahisi, linahitaji hatua madhubuti.

Ni wakati mambo yasiyo ya muungano Wazanzibar wasishirikishwe ili kuwatendea haki katika madai yao.

Hii ina maana moja, kwamba, Wazanzibar walioajiriwa sehemu zote zisizo za Muungano waondolewe ili kukidhi haja ya kubaki na mambo 11 ya mkataba wa Muungano. Haiwezekani kulalamika mambo kuongezwa halafu kuyatumikia mambo hayo. Haiwezekani 'Nguruwe awe haramu lakini mchuzi wake uwe halali'.

Hatua hiyo itawatendea haki vijana wa Tanganyika. Kwamba, nafasi zao zilizochukuliwa na Wazanzibar kwa kutumia 21% ya Uzanzibar , sasa ziwahudumie. Ikumbukwe vijana wa Tanganyika hawana nafasi hata 1% katika SMZ

Kuwaondoa Wazanzibar katika Wizara, Idara na Taasisi zisizo za Muungano kutatenda haki kwa sehemu zote.

Kwanza, Wazanzibar wataridhika kwamba mambo ya muungano ni 11 na yaliyoongezwa yameondolewa.
Pili, Watanganyika wataridhika kwamba mambo yasiyo ya Muungano yatahudumiwa na Watanganyika wenyewe.

Hoja za Watanganyika ni kwamba ikiwa Wazanzibar wanalalamika kuongezwa kwa mambo zaidi ya 11, kwani hawakatai nafasi zinazotokana na ongezeko la mambo yasiyo ya Muungano?

Mfano, Wizara ya Mawasiliano si ya Muungano vipi Waziri awe Mzanzibar? Je, huku si kuwadhihaki Wazanzibar wasiotaka mambo zaidi ya 11. Lakini pia Katibu mkuu aliyetokea Ofisi ya Rais Muungano ni kiongozi wa Wizara isiyo ya Muungano. Ni kwavipi hili linatokea. Huu si ubaguzi bali ni kwa mujibu wa Wazanzibar wanaotaka mambo si zaidi ya 11.

Kuna njama za kuwaingiza Wazanzibar ndani ya JMT kisha kuwapenyeza katika maeneo yasiyo ya Muungano. Wazanzibar wanalalamika na kusema hilo si sawa na kwa hili wana hakIi, na ni vema kuwaondoa ili tuwatendee haki

Tatizo la mambo 11 lina muendelezo mzuri. Kwamba Zanzibar itapewa 21% ya mambo 11 ya Muungano na SMZ iwajibike kulipa mishahara, marupu rupu na mafao ya Wazanzibar 21%. Haiwezekani kudai haki bila kuwajibika.
Haiwezekani kuwe na 21% ya Uzanzibar halafu gharama zinabebwa na walipa kodi wa Tanganyika.

Wazanzibar pia wachukue dhamana ya kulipa Wabunge wao wanaokuja Dodoma kwa ajili ya Zanzibar.
Wabunge wa Zanzibar wahudhurie mambo 11 na kisha waondoke. Haina maana kwa Wazanzibar kutumia gharama za Watanganyika kujadili Bandari, Afya, Mawasiliano, Elimu n.k. mambo yasiyo wahusu.

Kodi za Watanganyika zinatumika vibaya kuwalipa Wabunge wa Zanzibar takribani 100 kwa kukaa Dodoma kujadili mambo yasiyowahusu. Ikiwa Baraza la Wawakilishi lina Wabunge 50, kwanini Wabunge wa Zanzibar Dodoma wawe takribani mara 2. Ni kwanini kodi ya Mtanganyika imlipe Mbunge wa Zanzibar!

Wakati Rais SSH anaangalia masilahi ya Wazanzibar ni wakati pia aangalie uwajibikaji wa Wazanzibar ndani ya JMT. Ni mchango gani unaotolewa na SMZ kuendesha Muungano katika mambo 11 ambayo Wazanzibar wanayaafiki.

Watanganyika wanaeleza hisia, wamebeba muungano kama nchi moja kwa kutumiwa

Mfano, kuna hoja kutoka Zanzibar kwamba LESENI za kuendesha magari zinatolewa Zanzibar hata kwa Watanganyika kwasababu ni Watu kutoka nje ya nchi kama Kenya, Canada au Brazil.

Rais wa Zanzibar alisema Watanganyika watapewa ardhi kama Wageni wa nchi nyingine.
Kwa maana tuna nchi ya Zanzibar na Tanzania.

Wazanzibar hao hao wanaowaona Watanganyika kama Raia wa nchi nyingine wanataka bidhaa zao ziingie Tanganyika kama nchi moja kwa jinala JMT. Hii ni 'abuse' ya Muungano

Kinachosumbua akili za watu ni kuhusu nchi inayoitwa Tanzania ambayo Zanzibar imo.
Ni kichekesho kwasababu sheria za nchi mbili na moja ikiwa haijulikani zinakinzana.

Hoja ya Watanganyika , ni kwamba, Tanzania Bara ijulikane kama Tanganyika ikiwa na uongozi wake.

Kitendo cha Rais SSH kubariki MoU kati ya Tanzania na Zanzibar kuhusu madini kinaonyesha ufa uliopo na haja ya uwepo wa nchi inayoitwa Tanganyika.

Kwa maana noja, Zanzibar haiwezi kuwa Zanzibar na kisha kuwa Tanzania.
Hili linatoa Mwanya kwa Zanzibar kukwepa uwajibika na kuwa mzigo kwa Tanganyika.

Ni kwa njia hiyo tu Tanganyika itaweza kudhibiti rasilimali na kuzitumia kwa watu wake kama ilivyo Zanziba.
Tanganyika haitavaa KOTI LA Muungano ambalo kwake ni Mzigo Mzito sana.
Zanzibar haitajificha ndani ya KOTI na kutumia kivuli cha jina pale penye mafao tu ikikimbia kuwajibika.

Uwepo wa Tanganyika na Zanzibar utazifanya nchi zishirikiane kama itabid na kama kuna manufaa yoyotei.

Ni wakati Rais SSH awape Wazanzibar fursa ya wanachokitaka. Kwanza, aondoe mambo yaliyoongezwa kutoka yale ya mkataba. Pili aache kutoa ajira kwa Wazanzibar kwa mambo yasiyo ya Muungano kama Wazanzibar wanavyodai

Kwa Tanganyika hakuna malalamiko ya kuonewa na Zanzibar kuna kuchoshwa na mzigo wa Muungano na kutumika 'abused' kwa jina la Muungano ikiwemo matumizi ya rasilimali zake kwa nchi jirani kwa mujibu wa Wazanzibar.

Ili y kumsaidia Rais SSH katika jitihada zake, Chama cha ACT Wazalendo kiache siasa za kuwatusi na kuwatukana Watanganyika majukwaani kila uchao.

Ndani na nje ya Muungano Zanzibar itabaki kuwa jirani tu hivyo chuki inayojengwa na Wazanzibar haitawasaidi kwa kuzingatia jirani yao Tanganyika ni mkubwa kwa kila kitu. Chuki inayopandwa na ACT Wazalendo na kukaliwa kimya na Rais SSH ni kibali na ipo siku chuki hiyo itarejewa (referenced) kwa gharama kubwa itakayolipwa na Wazanzibar.

Badala ya kuhubiri matusi dhidi ya Watanganyika wengine wakiwa hawajui hata Zanzibar ipo wapi, chama cha ACT Wazalendo kijikite kuomba KURA YA MAONI ili kuamua ikiwa kuna haja ya Muungano.

Ni utaratibu duniani mdogo anapewa nafasi ya sauti kama ilivyo kwa Scotland, Quebec, East Timor , Eritrea, na kwingine walikotaka kujitoa katika serikali za nchi zao. Zanzibar ipewe nafasi hiyo na Rais SSH anaweza

Kuanza mchakato wa katiba kabla ya kura ya maoni ni kuahirisha tatizo. Tutafafanua bandiko linalofuata
 
Back
Top Bottom