Mchambuzi
JF-Expert Member
- Aug 24, 2007
- 4,850
- 9,405
Mchambuzi ahsante sana kwa ufafanunuzi. Hoja ya JFC inatumiwa kufidia mapungufu na kukwepa ukweli.
Tumeuliza sana, kama znz haichangii kwasababu hakuna JFC,ni mfuko gani unaoiwezesha kupata 4.5% ambayo sasa imepanda na kuwa 7%. Hakuna anayekuja na jibu, wanarudia hoja ile ile dhaifu
Tumeuliza, kwasasa znz inapata Bilioni 1.75 kwa mwezi. Je, zinatoka mfuko gani wa pamoja? Hakuna jibu, wanarudi na hoja ile ile isiyo na maana kwasababu hawana majibu.
Tumeuliza, watimishi wa muungano wanalipwa na frdha kutoka mfuko gani wa pamoja? Hakuna jibu, wanarejea hoja wanayojua haina mashiko.
Tunauliza, zile pesa za kusaidia bajeti ya znz kutoka JMT zinatoka mfuko gani? Hakuna jibu, wameshikilia pale wasipo na jibu
Inapofika wakati wa kudai masilahi wznz ni wazuri sana wa kuumba na kudai. Wakati wa kuwajibika, hukimbilia hoja za kipuuzi kama hii ya JFC.
Kwa mtu mwenye akili angejiuliza
Na mwisho, tumewauliza formuala gani zinatumika kwa znz kupata mafao ya muungano, ambazo haziwezi kutumika katika kuchangia muungano? Hakuna jibu, wanasema misaada na mikopo. Tumewaonyesha ni kiasi gani znz inapata kutoka muungano bila kujua kwanini na kwa njia gani. Hawana jibu, wanaturudisha kule kule kule wasiko na mjibu
Ni kwa msingi huo, utawasikia wznz wakizungumzia kugawana vyeo, kupata nafasi zaidi kwasababu mentally wanaaamini kuwa huu muungano unajiendesha kwa solar energy, na wajibu wa kuhudumia hiyo solar system ni wa Tanganyika.
Wao wanawajibu wa kukusanya tu.
Kwa sasa tunawaambia Watanganyika lazima mambo yatenge, na shughuli zishsughuikiwe na nchi husika. Tanganyika irudi, znz ikae kama mshirika mwenza katika kuzungumzia nafasi yake ndani ya muungano na si nani anakuwa spika, waziri au vyeo. Lazima znz wawajibike katika muungano katika kuuendeleza, si kufanya Tanganyika shamba la mavuno.
Hakuna haki isiyo na wajibu, na waznz sasa ni wakati watambue kuwa Watanganyika wamechoka si kuudumia muungano peke yao bali pia uzito walioubeba ambao return yajke ni questionable
Kwa kila dimension, Tanganyika inaumizwa sana na mfumo wa sasa. Kwa mfano, tukiangalia hesabu rahisi tu tena in practice (mapato na matumizi) ni hivi:
Mapato ya Zanzibar kwa mwaka(ndani, nje, na kutoka tanganyika) ni kama tsh 700b. Hizi ndio fedha za bajeti ya znz kwa mfano kwa mwaka huu wa fedha. Ukigawanya hii kwa kila mzanzibari (1.3mil) unapata mgao wa bajeti kwa kila mzanzibari ni tsh kama 540,000. Ukiondoa waznz kama 500,000 ambao wapo Tanganyika, ni kama tsh 870,000 per mzanzibari. Kwa watanganyika, mapato yao ni kama sh.19 trillion. Hii ndio bajeti ya muungano pia. Ukigawanya hii kwa kila mtanganyika, unapata ni kama tsh 440,000. Katika hizi, bado nyingine nyingi tu zinaenda znz wakati zile 540,000 za znz n kwa ajili ya matumizi yao wenyewe tu. Mtanganganyika hagusi kitu hapo.
Last edited by a moderator: