Naantombe Mushi
JF-Expert Member
- Oct 16, 2015
- 6,253
- 15,746
Habarini wana jamvi na poleni katika harakati zenu za kulisukuma gurudumu la maisha. Si kazi rahisi kwa kweli, ni kazi ngumu sana. Ndo maana mi huwa nafikiri, kuishi tu ni moja ya ibada ya kutukuza ukuu wa mwenyezi MUNGU. Kwa sababu ndani ya masaa 24 kuna mambo mengi sana tunakuwa tunayafanya au kipitia lakini kwa hali isiyo ya kawaida unaona tu, usiku umefika ukaamka asubuhi na ukafika usiku tena. Hakika kuna nguvu ya ajabu inatenda kazi na inahitaji kupewa sifa na kutukuzwa.
Kwisha kusema hayo, ningependa kabisa kuja na hoja ambayo imekuwa na itaendelea kutawala maongezi katika jamii, hususani vijana. Nikiwa nimetoka kanisani, kitendo cha kufungua mlango tu ndipo likanijia wazo lililonipelekea kufikiri kidogo na kujiuliza swali, Hivi tafsiri haswa ya mke mwema ni ipi?
Wakati nikikua na mpaka sasa nipo hali ya kuitwa mtu mzima, nimekuwa nikishuhudia jamii kwa wakati mwingi ikitoa tafsiri ya mkwe mwema kwamba; ‘ni yule ambaye ataheshimu ndoa pasipo kutoka nje ya ndoa (kuzini nje). Ni mara nyingi tumesikia wanaume wakitoa kauli kama “Daah! Yule binti katulia, anafaa kuwa mke/ni mke mwema” na kauli nyingine nyingi, basi tu, kuonesha ni namna gani mwanamke asiye zini nje/kabla ya ndoa alivo mke mwema.
Kwa tafsiri hiyo ya jamii, wale wanawake ‘wakora’ waliokuwa wanaishi bila kutambua msingi huo wa jamii, hawakuwa wake wema na walivikwa maneno kede kede yenye taswira mbaya. Na hivo wakati tunakua ndani ya jamii tukajikuta na sisi tukiwa na mawazo hayo kwamba mke mwema ni mwanamke anayepaswa kuwa na sifa fulani tu.
Nimeona labda naweza kupambanua, ili kuwepo na fikra pana za ‘uke wema’. Na sio lengo langu nipotoshe wanachoamini jamii juu ya tafsiri ya ‘uke wema’. Ila najaribu kuangalia na uwezekano mwingine wa mwanamke kuwa mke mwema angali akiwa ametoka nje ya tafasiri ya jamii.
Hivyo basi, kwa uchungu mkubwa wa kutopenda kwenda kinyume na mafundisho ya jamii. Naamua sasa kutokuwa m(liberali) kwenye suala hili angalau kwa muda.
Kulingana na mwenendo wa maisha mpaka nilipofikia umri huu. Kuna mambo mengi nimeyashuhudia kwenye jamii na katika usawa wa familia. Mambo ambayo kwa namna moja ama nyingine yamepelekea kuwa na jamii yenye changamoto lukuki ikiwamo; umasikini, ukosefu wa maadili, jamii kukosa vipaumbele, upendo kukosekana, ujinga, chuki, hali ya kukosa kujitambua, na mengine mengi yanayoudhi.
Sio kwamba changamoto hizo ambazo zimeshamiri kwenye maisha ya sasa kwenye jamii zetu, eti zinatokea kwa sababu ya mipango na mapenzi ya MUNGU. Mimi nakataa kabisa, na ninaona ya kuwa changamoto hizi zimetokea katika jamii yetu baada ya kuwa na taasisi dhaifu ya familia ambayo uundwaji wake uliangalia msingi mmoja tu, pale bibi na bwana walipoamua kuoana ili kutengeneza familia.
Changamoto nilizozigusia kwenye aya ya juu ndani ya familia, hazihitaji ufahamu wa tafsiri ya jamii juu ya ‘mke mwema’ ni yupi ili kuziepuka. Penginepo kuna malaki na malaki ya familia ambayo nina uhakika thabiti kwamba zimetengenezwa kwa misingi ya jamii ya ‘uke wema’.
Lakini ni vipi sasa jamii inapitia changamoto chungu namna hii? Je, ni kweli kwamba kwa changamoto zilizopo na zinazotokea kwenye jamii upande wa familia nyingi, ndio haswa malengo ya waasisi wa familia (bwana na bibi harusi)?
Kama jibu ni hapana, basi nashawishika kujenga hoja kwamba, “ili mwanaume uweze kujenga familia bora iliyo huru dhidi ya changamoto nyingi zlizopo kwenye jamii, ni vema misingi ya kuchagua na kutafasiri maana hasa ya mke mwema wa kuunda hiyo familia, iwe kinyume na tafasiri ya jamii ambayo imeonesha kushindwa mpaka sasa”
Nikienda kumaliza na kukaribisha mahojiano juu ya hoja niliyoitoa hapo juu. Naomba niweke bayana kwamba; sishabikii wala suingi mkono vitendo vyovyote vya mwanamke kuzini kabla/nje ya ndoa eti kwa sababu sio sifa ya kumuondolea uke wema.
Ninachomaanisha hapa ni kwamba nataka jamii iwe na tafsiri pana pale tunapomuongelea “mke mwema”. Hivyo basi, natarajia kupata mapana hayo na tuyape uzito ili tuwe na machaguo sahihi pale tunapoenda kuanzisha familia na kuifanya taasisi ya familia iwe bora tena.
Ni kwa kujenga familia bora tu, ndiko kutatatua madhila yaliyo kwenye jamii yetu. Hiyo sio kazi ya serikali na wala sio kitu cha kusema “tusubiri mapenzi ya MUNGU yatimizwe”. Ni jambo ambalo tuna utawala nalo, nikiwa na maana tuna nguvu ya kulipanga na kulitekeleza. Na familia bora inaanza na “mke mwema” aliyepatikana pasipo misingi ya jamii.
******
Naomba kuwasilisha.
Wasalam,
Naantombe.