Duniani kuna mengi sikutegemea hili kunipata

Nimeishia Kuhuzunika tu........ nisijue cha kufanya Ufukara Mbaya sanaa.........................!!!!!!
Ni kweli inahuzunisha lakini tusiishie hapo, hebu tuone nini twaweza fanya kumsaidia huyu member mwenzetu.
 
Ni kweli usemayo mkuu, mimi nilikuwa na mgonjwa pale akaandikiwa dawa ambapo ilitakiwa awe anapatiwa dozi kila baada ya muda fulani, kila dozi ilikuwa 420,000/= ilikuwa kazi kweli kweli, maana dozi zilitakiwa ziwe nne, sasa jumlisha mwenyewe hicho kiasi mara nne
 
H
Pole sana ikiwa ni kweli unachosema. Umeandika kwa usitadi wa hali ya juu. Lakini huenda utahitaji namna bora zaidi kuthibitisha madai haya.
 
Pole sana Kaka. Nakushauri Umtafute FLORA LAUWO Wa kipindi cha "NITETEE SAUTI YA WANYONGE". Nauhakika kupitia yeye/kipindi chake utapata msaada Wa HARAKA SANA. POLE SANA, MUNGU AKAENDELEE KUWA UPANDE WAKO DAIMA
 
Matibabu pale ocean road naambiwa ni kama bure vile!
Sina uhakika.
Pole kwa mtihani unaokukabili.
Sio kweli mkuu, pale ocean road kama pesa huna utafia sakafuni. Fanya utafiti!!
 
Ni kweli inahuzunisha lakini tusiishie hapo, hebu tuone nini twaweza fanya kumsaidia huyu member mwenzetu.
kusaidia hapo panahitaji CHAI na siyo Pole tu..........Ni yale yale ya Ufakiri................!!!!
 
Mkuu pole sana na kuumwa nasi pengine tunaumwa lakini hatujajua Tu. Cha msingi weka uthibitisho wa vielelezo vya ugonjwa Kama barua za rufaa na majibu ya vipimo pamoja na kitambulisho chako Ili tuamini maana matapeli wengi nowdays. Binafsi ntakuchangia elfu 10 endapo ntapata uthibitisho wako
 
Kwanini haweki vielelezo na amepotea mazima? No offense, ila nadhani jibu linaweza kuwa computed hapo chini

-New member
-28 yr old
-married with one kid
-anakaa mbagala
-msaidizi wa Fundi ujenzi
(natamani kuelewa zaidi hapa)
-amegundulika na kansa
-aina ya uandishi (hii ni give-away kwa scenario hii, ya "kibarua wa Fundi")

-angalizo maana anatumia pc ya rafiki yake atakuwa hapatikani.



Pole sana
 
Si kasema hana smartphone,hivyo anaingia Jf kwa kuomba laptop ya jamaa, so subirini atawajibu,au bora mumpigie
 
Pole sana...matatizo tumeumbiwa wanadamu binafsi nitakusaidia nilichoojaliwa
 
Hapo umeongea vyema sana aisee,me pia am in
 
Ukipata uthibitisho wa hii issue nijulishe pia nione tutamsaidiaje.
 

Kwa mwandiko huu, inawezekana alifaulu vizuri sana kidato cha nne akakosa ada ya kwenda shule. [emoji3]
 
Pole ndugu, zaidi MUNGU ndo kimbilio lako na ndo faraja ya kweli kwako tafuta faraja iliyo ya kweli kutoka kwake yeye ndo kimbilio kwa ote na usihofu atakuponya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…