Duniani kuna mengi sikutegemea hili kunipata

Pole sana ndg ila kuna wachangiaji wamekuambia, weka wazi vielelezo vyako. Usione ati kuna mtu anataka kukudhalilisha bali kuaminiana kumepotea kabisa leo. Wewe weka hapa vifaa vyako kama hivyo vyeti na kadhalika uoane misaada utakayo mwagiwa.
Mfano: Ni Juzi tu alinipigia sim kama vile ni ku beep. Nikampigia. Akawa analia kabisa kuwa yupo kijijini, mahali fulani, anashida kubwa. akasema hawajala siku 3 yeye pamoja na watoto wake wachanga 4 aliachwa na bwanake akakimbia wala hawajui aliko. Nikamuuliza vizuri, upo wapi, akanitajia kile kijiji. Kumbe ni mahali napafaham sana. Nikamwambia, njoo kwenye njia ya kwenda shule ya sekondari hapa nakungoja nitakupa msaada. Ukifika tu hapo njiani, ni beep ntakuja kukusaidia. Akaanza; Oh! Kwani lazima unifaham?? Nikamwambia, sharti ni kumpa msaada ninaye mfaham. Akakata sim na hadi leo hajawahi nipigia tena. Toa vielelezo utasaidiwa
 
Point
 
Naunga mkono hoja awe muwazi na mi nipo tayali kumchangia mkuu pole sana ebu msikilize Nemo alivyosema
 
Mungu atakukipa nemo kwa moyo wako
 
Yatapita Mkuu, kwanza anza kuweka mwili wako katika mazingira ya kula na kupumzika vizuri, stress inasababisha ugonjwa kuwa mkubwa zaidi, fanya mipango ya finacial status na omba MUNGU akuvukishe katika hili, POLE SANA Mkuu& ugua pole
 
Dohhh[emoji26]pole mno mkuu,
Inasikitisha
 
Pole sana kaka yangu mungu atakusaidia kuwa naimani tu...nenda hospital usisikilize watu wanao kuambia uende kanisani kwenye maombi. Hakuna kitu kama hicho. Nenda ocean road matibabu ya cancer ni bure. Nitakutafuta kwa namba yako kwa msaada zaidi

 
Ocean road kwa matangazo ni bure ila pata mgonywa au umwa uende hapo utajuta kuzaliwa hakuna cha bure pale ndugu zangu watanzani vitu vya bure pale ni vidogo vidogo sana hakuna dawa za kumpa mtu bure pale za bei kubwa utapewa panado hata dawa ya kikohozi benline hawana utaambiwa ukanunue hapo nje duka la dawa na nje inauzwa 14500 ni hatari sana
 
Pôle sana mkuu ni sehemu ya maisha ila ingekuwa vizuri ukapost vielelezo /documents Za diagnosis na refferal hapo itakuwa rahisi watu kukusaidia maana siku hizi utapeli umekuwa mwingi watu si rahisi kuamini bila hizo nyaraka
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…