Duniani kuna mabara mangapi?

Nimeupitia huu mjadala kwanza nikaona na mimi nikachimbe wenzetu huko wanafundishwa nini kuhusu mabara

●Green Oaks Academy, UK



●St. Brigid Catholic Elementary School, Canada


●Marekani


Huko kote watoto wanafundishwa kuwa kuna mabara saba Africa, Asia, Australia (Ocenia), North America, South America na Antarctica.

Sijaona wakifundishwa bara la Eurasia

Ila hoja ya wanaosema Eurasia ni bara ina mashiko na iko kwenye mijadala ukizingatia definition ya Continent

KWA SASA ACADEMICALLY ILI TUSIWAPOTOSHE WANAFUNZI/WATOTO WETU MABARA NI SABA: Africa, Asia, Australia, Antarctica, North America na South America

Hayo mengine tuyaache kama mjadala tena wenye mantiki na tija
 
Ndio maana kuna mtu aliwai nambia kujua kuna mabara mangapi inategemea na elimu yako uliipata wapi..
 
Nafikiri hapo umeweka mfano wa elimu ya watoto. Ni kama watoto kufundishwa kuwa 0 kutoa moja haiwezekani lakini baadaye wanafundishwa kuwa sifuri kutoa moja ni negative moja. Mtu anayemaliza form 4 anatakiwa kufahamu kuna mabara ma 4 hadi 8 kulingana na criteria.
 
Kuna vitu havina cha level hiyo iko officially duniani kote mabara ni 7
 
Haya mambo yakijadiliwa na wabobezi huwa yanakuja na majibu mfano hilo suala la Eurasia bado lina mjadala ulio mezani kati ya geographers wanaosema ni bara wengine wanasema sio bara

Ni kama vile zamani tulisoma kuna sayari 9 ila sasa hivi mitaala duniani kote imebadilishwa kuwa sayari ziko 8 tu na hii ni baada ya wabobezi astronomers kukaa, kujadili na kukubaliana kuwa Pluto haikidhi vigezo vya kuwa Sayari

Kwa sasa haina haja ya kuforce kuwa Eurasia ni bara bado halijawa officially bara ni mjadala unaondelea kati ya geographers
 
Wewe unafikiri Europe ni bara kwa vigezo gani na Eurasia si bara kwa vigezo gani?
 
Africa
Europe
Asia
Australia
South America
North America
Antaktika
Ant-Arctic and hence the name Antarctica
Ni bara amalo limefunikwa na barafu na liko upande ulio opposite na Arctic Cicle ya dunia. Kule juu Sweden kama sehemu zile za Lulea; hizo ndiyo baadhi ya sehemu zilizo kwenye arctic cicle ya dunia. Kinyume cha arctic ni Ant-Arctic
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…