Keynez
JF-Expert Member
- Feb 12, 2007
- 3,621
- 6,512
Kabla haujasoma ninachotaka kusema, embu tuelewane kidogo. Sijawahi kuisifia wala kuitetea CCM na serikali zake. Siungi mkono vitendo vyovyote vya unyanyasaji, utekaji, mauaji na uminywaji wa haki na uhuru wa raia wa Tanzania. Baada ya kusema hayo, naomba niendelee na mada yangu ya leo.
Hauwezi kutangaza takribani miezi miwili kabla kuwa unaenda kufanya maandamano ambayo nia yake ni kuiondoa serikali halafu uende kufanikiwa. Hivi mnadhani miezi hii yote hao CCM na serikali yake wamekaa tu wanawasubiri nyie hiyo October 29 muende kuwaondoa?
Maandamano ya kweli, yenye nguvu na yanayofanikiwa huwa yanaibuka tu "organically" na yanachochewa na hasira na hisia kali kutokana na matendo maovu ya wakati husika siyo haya ya kutangaza miezi miwili kabla.
Kwa Tanzania yametokea matendo mangapi ambayo yangeweza kuibua maandamano lakini kimya kikatanda mitaani hadi watu wakapoa? Watu wamebaki kugugumia na kunong'onezana tu ila hakuna action. Nguvu hiyo ya kuwavuta hao watu waingie road itatoka wapi wakati mmewapa watesi wenu muda wa kujiandaa na kujizatiti na wakati huo huo hisia za watu kupungua?
Kuna jambo nililisema kuhusu Polepole, Mpina na Mange wiki kadhaa nyuma katika post yangu ya mwisho na nasimama na maneno yangu maana baada ya nilichoandika ndiyo siku kadhaa nikasikia "ametekwa". Nasimama na kauli yangu ya awali.
Narudia jambo ambalo nimelisema mara kwa mara. Watanzania bila kuamua kusimama wenyewe bila kutegeana au kutegemea viongozi au watu fulani wawaongoze (au sasa hivi mmeingizwa chaka la eti jeshi lipo tayari kuwasaidia), hamtaiondoa CCM kamwe.