Landcruser
Senior Member
- Mar 24, 2017
- 179
- 344
Kuna mambo ya kijinga sana nchi hii. Kero nyingi sana zimeshindwa kutatuliwa Da es Salaam na maeneo mengi ya nchi. Issue ndogo sana ya wrong parking ndiyo inamfanya hadi mtu atumie risasi. Dunia iko busy na mijadala mikubwa sisi tunajadili pumba tupu. Hata wazungu wakiamia Afrika leo na sisi tukaenda Ulaya; baada ya miaka 50 tutadai kurudi kwetu maana tutawaaribia nchi zao na wao watafanya maajabu Afrika hadi tunapatamani.
Tuamke jamani. Dunia inasonga tajadili mambo mazito. Mfumo wa elimu yetu uwe mjadala wetu mkuu. Wengine wenye vyeti halali mitihani waliiba. Elimu yetu mbovu ndiyo inatufanya kutumia nguvu kubwa kwenye mambo yenye kuhitaji busara.