Katika kulea, Kila jinsia ina nafasi yake.

livewise1

JF-Expert Member
May 25, 2019
837
952
Salaam.
Kwenye kulea mara nyingi Kila jinsia ina nafasi yake mahususi kwa watoto.
Mtoto wa kike analeleka vyema kwa mama na kidume kinaleleka vizuri mno kwa baba.

Katika kasi hii inayoendelea na kuongezeka mahusiano au ndoa kuharibika na kupelekea kutengana, ni vyema watoto wa kike wakaenda kikeni na watoto wa kiume waende kiumeni.
Wimbi la wanawake wanaothubutu kulea watoto wa kiume bila msaada wa baba linaharibu kizazi vibaya mno.

Wanaume tukiachiwa watoto wa kike fasta tu tunawapeleka kwa shangazi zao au bibi zao. Tunajua huko wataleleka vyema kuliko kiumeni.

Hata kama wanawake wamepewa jina la kuwapa nguvu na kuwafanya waone wanaweza (SINGLE MOTHERS), Haibadilishi uhalisia kuwa kulea watoto wa kiume kunahitaji zaidi baba.

Ukichunguza vizuri, utagundua watoto wa kiume waliolelewa na mama peke yao wana vichengamoto kama sio machengamoto.

✓ Wanapungukiwa au wanapoteza hulka ya kiume, KUJIAMINI.
✓Wanapenda kuwa upande wa kutetea kikeni bila kujali ukweli au uhalisia.
✓Wakipatwa na chengamoto kidogo tu hali zao za kisaikolojia tafrani.
✓Wanaridhika kirahisi sana kwenye hustle za maisha.
✓Wakifanikiwa BABA ataona rangi zote japo wengine walifichwa uhalisia (baba yao alikuwaje)
✓Na kufanikiwa kwao ni kama kisasi kwa BABA.
Hali inatisha saivi jamani.

"INFERIORITY COMPLEX"

Wapeni baba walee watoto wa kiume na nyie mlee wa kike ili kizazi kibaki salama.
(Wale mapoyoyo wasiotaka kulea watoto wao wa kiume yaacheni pelekeni kwa baba hata wa kufikia au Babu).

NB: Mshauri mkuu wa mtoto wa kiume ni baba katika namna Bora ya kuiendea Dunia na yaliyomo akiwa kama mwanaume.
Hali kadhalika kwa wanawake.
 
Back
Top Bottom