Acheni kututengenezea kizazi cha wanaume legelege

Loading failed

JF-Expert Member
Sep 14, 2023
1,945
5,849
Heri ndugu zangu.

Ukifanya tathimini za haraka haraka mpaka kufikia mwaka 2045 kama tutakua hai tutashuhudia kizazi cha hovyo sana kinacho nyumbishwa huku na huko na wanawake zaidi ya sasa na haya yote ni kutokana na malezi mabovu ya watoto wa kiume.

Katika familia zetu watoto wa kike wamekua strong sana na wajanja zaidi kuliko hata watoto wakiume, unakuta mtoto wa kiume kalainika lainika, mjinga mjinga, mvivu, mwoga wa giza , hana nguvu , anakula vyakula laini laini , wazazi wanamdekeza dekeza hovyo hovyo tuu huku wakimnyoa kiduku mara afro, hujakaa hivi pank ni vurugu mechi kila uchwao

Mtoto wa kiume analelewa kimayai mayai kupita kiasi hata kupigana na maadui huko njiani ma mashuleni hawezi, mtoto wa kiume kutoka nje saa mbili usiku ni mwoga wa giza kuliko kawaida , ila hapo hapo binti mdogo tuu anatoka nje na kwenda dukani na kurudi salama salmini .


Unakuta mtoto wakiume anachimbwa mkwara na machalii hata kukaza sauti hawezi anaongea huku kalegeza macho kama ka binti ni balaa tupu kwa kweli

Mtoto wa kiume kwenda chooni usiku ni hadi asindikizwe, mara alale taa ikiwaka eti ana ogopa mende . Hivi mnatutengenezea kizazi cha aina gani zaidi ya kututengenezea wanaume legelege na wazee wasio na sauti miaka ijayo kwenye jamii zetu.

Unakuta baba anamwachia mama mtoto wa kiume wa miaka 13 bado acheze cheze na mama yake na dada zake badala ya kumkaza kijana aache kufata hulka za kike za mama na dada zake yeye anaona ni sawa tuu.

Ni balaa tuu malezi ya mtoto wa kiume yamevamiwa acheni kututengenezea kizazi cha wanaume legelege makaburi yenu yatakuja kuchapwa fimbo na watoto wa mabepari.

Wajomba na mabinamu wasaidieni hata na hao single maza kukaza hao watoto wa kiume waliotelekezewa huko na wanaume kwa ujinga wao au kwa makusudi.
 
Ndo vizuri ili watoto wetu sisi tunaowalea kigumu waje kuwa lulu baadaye
 
Watoto wa kiume wamekuwa mlenda mlenda wanajinyea Hadi kitandani wanaambiwa pole na mama zao.
 
Huu ni ukweli bila shaka yeyote.
Na kwa mwenendo jinsi ulivyo 2045 ni mbali sana hili janga lita anza kuonekana wazi ikifika 2030 tu hapo.
 
Back
Top Bottom