meghan markle
JF-Expert Member
- May 22, 2018
- 483
- 1,166
Habari ya mapumziko wana JF...
Muda mchache uliopita nimetoka pharmacy kununua dawa za nyumbani,kwa utaratibu nikiojiwekea lazima nyumbani pasikose pain killers ,magnesium,flagyl,plasta etc kwa kifupi vitu cha huduma ya kwanza.
Nikiwa hapo pharmacy nikawa nabadilishana mawili matatu na kaka (pharmacist )wa hapo kwasabu tunafahamiana (wakunyumba).Wakaja wababa wawili kwa awamu mbili yani walipishana.Alivyokuja wa kwanza akamsalimia bila kuongea kaka akaingia ndani akatoka na dawa sikuziona akampatia yule baba akanywa kisha akaaga. Baada ya dk chache akaja mwingine kijana tu akasalimia pale kwa kutuchangamkia na yeye akapatiwa dawa na maji akanywa zake akasepa.
Nikamuuliza kaka kiutani "jamani dawa unatoa kwa upendeleo mbona nimekaa hapa muda wote hujanipa hata panadol" Akaguna tu akaniambia mdg wangu shukuru mungu huhitaji dawa ili uonekane una afya...watu wanaogopa kuvunja nyumba zao dawa wananywea pharmacy.Nikawa sijaelewa ,akasema yani siku hizi watu hawataki kukaa na dawa nyumbani wanakuja wanakunywa wanaenda af akacheka akasema mi kikubwa wananilipa kutunza dawa zao.Yani alikua anaongea very calm as if ni kitu cha kawaida sana.
Loooh nitabaki na butwaa moyo ukanyong'onyea.
Jamani dunia ina mambo....mtu anakuua hivi hivi ARV zake anatunzia pharmacy akija home huko vizuri hujui na maisha yanaenda .
Nimetafakari nimekosa raha ukizingatia hata kisheria nahisi ni kosa ila sasa ndo hivo mtu anatafuta riziki huku wenzie wanatunza siri ktk ndoa zao.
Nawaza hapo itokee uende kupima ugundue una VVU lijamaa litakavyo kunyanyasa kumbe limeungua kitambo dawa limefichia pharmacy.
Dunia nzito sana.
Wasalam.....Meghan!