Dunia ina majaribu makubwa, ninayopitia sasa ni mateso makali

njumu za kosovo

JF-Expert Member
Mar 9, 2017
1,721
3,857
Habarini wana jukwaa,poleni na majukumu yenu ya kila siku katika kujiongezea mkate ,awali ya yote niwatake radhi kwa maana nakiri wazi mimi si muandishi mzuri ila nimeona vyema tu niwape kisa changu kizito juu ya niliyoyapitia, ieleweke kwamba wapo watu humu kupitia maelezo yangu watanifahamu lakini kwa hatua niliyofikia sijali tena😪,Kwa kweli wanaume tunapitia mambo mengi sana sana na ndio maana naamini kwanini tunawahi kufa mapema,..

Kisa chenyewe kilianza miaka ya 2010 hivi pale nilipokutana na mdada mmoja mwenyewe wa mji kasoro bahari alikua ni single mother, wakati huo ndio nilikua namalizia malizia chuo na mwanae alikua mdogo sana ,hivyo baada ya kuwa nae kimahusiano yule mtoto mpaka anapata akili alikua anajua mimi ndo baba yake mzazi na hata alipewa ubini wangu(kosa hili) basi mimi kwa upande wangu niliona sawa tu lakini haikua bure kwa upande wa pili yule dada alikua ni mshirikina balaa hakuna mfano ..basi ndugu zangu kiukweli kabisa nilifanyiwa madawa nikawa zoba ndugu zangu hata mama mzazi alikua anaumia sana lakini dah uchawi?

Kweli upo hali iliendelea hivyo lakini balaa lilizidi baada ya kuzaa tena nje na mwanaume mwingine 😪😪na nikawa najua kabisaa lakini sikujali kabisa na ndio kwanza mimi nilikua wa kwanza kumficha yule mtoto wa pili ndugu wasijue, nb yule niliyemkuta nae niliwaeleza ndugu kuwa ni wa kwangu ,basi ndugu zangu yule dada ndio akakoleza madawa vibaya mno nikazidi kuwa fala kabisa..,hapo bado sikustuka baada ya miaka kupita ndipo akaja kunizalia mtoto mmoja mdogo na ieleweke kwamba hatukua tunaishi karibu sababu ya kikazi zangu kuhama hama ,hapo ikawa mbili moja akiwa anaongoza mbele kwa kufupisha kidogo basi siku moja nilienda dom kikazi nikakutana na binti mdogo tu na hapo kwa kweli moyo wangu ukaangukia kumbe ndio ukawa mwanzo wangu wa kufunguliwa ,amini nakueleza unaweza funuliwa kupitia matatizo.

Yule binti wa dodoma alipata ujauzito na baadae nikaletewa (kama kususiwa ) nitalieleza hilo siku nyingine kumbe kimbembe kilikuja yule dada niliyekua nae mwanzo alikua kila nnapomtumia hela ya matumizi alikua anawagawia wanaume zake huko na kisha hela hiyo hiyo niliyotuma akawa anapeleka kwa waganga azidi kuniroga na kuangalia kama nimestuka au laa, (inauma sana) baada ya kuona kwenye rada zake nina mwanamke ana mimba akaamua aue mtoto😢😢😩

Basi siku ya kuzaliwa mtoto kweli alifariki katika mazingira ya ajabu sana sana nikazika mwanangu kwa uchungu mwingi sana .Sasa niliyajuaje hayo iko hivi baada ya kuona kama kifo cha mwanangu kila uwalakini nilienda kwa mzee mmoja ,kufika tu aliniuliza majina na kumpa baaasi mzee akaflow kama ifuatavyo,..kwanza alinitajia kazi yangu mimi ni wangap kwetu kisha shida iliyonipeleka akanipa pole sana sana na kuanza kunielekeza.

Akaniambia mwanangu mwanamke uliyekua nae ni mbaya sana akanipa mpaka alipo na wanaishi wangapi ndani kwao kitu ambacho ni kweli ni hivi yule dada baada ya kuniona nishakua bwege akanizalia mtoto mwingine nje ya niliyemkuta nae na muhuni mmoja hivi, basi kumbe akaungana na huyo mwanaume wake kutaka kuniangamiza kabisa ili waje kurithi mali zangu na wao wawe na maisha yao(wanawake hawa) kumsaidia kote huko na hata hakuniwazia mema ndio kwanza akataka kuniangamiza na nakumbuka mara ya mwisho nilitaka nichukue mkopo nimalizie nyumba( amini usiamini nilimjengea nyumba kwao kwetu sina hata kibanda cha kuku)kisha akaniambia nikope alafu nimfungulie duka kubwa sana na biashara ya dala dala na nikakubali kumbe mtaalamu akaniambia baada ya kufanya hivyo ndio ungekua mwisho wako maana walipanga na huyo mwanaume wake ukishawafanyia mambo hayo tu wakumalize kabisa waishi kwa amani ,inauma sana ndugu zangu...,

Kingine mtaalam akasema kila unachokifanya lazima akijue kwa maana amekutangulia mbele na hakuna kitu naweza kumficha na kiukweli yule dada sikuwahi kuwa na hisia nae kabisa sijui yani yule mzee akaniambia, mwanangu hawa japo unatuma hela unalisha yeye wanaume zake ,wanae na kaka zake pia hela hiyo hiyo anatumia kukufanyia madawa😑😑 na baada ya kujua una mwanamke mwingine alitaka aue mwanamke na mtoto ila alimshindwa mama mtu akakaua kichanga na ili atimize hayo alilazimika kulala na chizi mmoja hivi ambae nilimfahamu lakini niliambiwa na mtu ambae hata hajawahi kukanyaga hapo mtaani,

Basi nilichoka vibaya mno kumbuka yule mtoto wa kwanza ananijua mimi ni baba yake mzazi mana tangia kachanga nahudumia mbaya zaidi aligombana na mke wa kaka nae akaenda kumroga akashindwa badala yake akamroga mtoto wa kaka yangu kama kisasi kwa mama yake ndugu zangu mtoto anaumwa kifua yule sijapata kuona hata kuhema kwa tabu ,pumu si pumu hospital hawaoni kitu kabisa 😪😪kumbe kaka aliwahi pita sehemu akaambiwa anayemuumiza mtoto ni yule dada wao wakaona wakiniambia ntawagombanisha lakini kumbe ndio nilizidi kupotea...

Kiukweli baada ya kuyajua yote hayo akili ikarudi kama mtu aliyemwagiwa maji hata ikafikia hatua tupo nyumbani amekaa anazinda kabisa sipiki upike wewe na kweli nikaanza kupika yeye ananitazama tu mama aliumia sana lakini hakusema kitu ni mambo mengi mengi sana nilifanyiwa kimazingara hata ikafikia hatua naenda kumuona mtoto wanaume zake wanakuja hapo hapo tunakaa wote kama mafala kabisa yani sikuona kama nimove on nilikua bwege haswa.

Naandika haya huku moyo unavuta vibaya mno mno asiyetaka kuamini silazimishi atakayeona nimetunga aamini hivyo hivyo ila ndio ukweli mgumu huo kwangu...,basi baada ya kujua hayo ndipo chuki ikaanza ingawa wazee na ndugu zangu niliwaeleza wakasema nitulie nisionyeshe kuwa nimejua lakini nashindwa kabisa kaka zake eti nao wananipigia wananigombeza kwanini nimebadilika sio kama zamani how? Wanashirikiana pia? Mungu si Athumani siku nimekaa ghetto akanipigia moja ya rafiki zake wakubwa ambae amemgeuka akanipa ukweli wote mwenyewe akaniambia "kaka mji mzima ukija mpaka tunatamani kulia jinsi anachokufanyia mtu wako na unavyomjali na aibu anazokutia mtaani😬😬 nikazidi kuchoka akaniambia kaone wazee kwenu umechezewa vibaya mno na hapo nishayajua kwa yule babu lakini bado nikaelezwa huko tena na rafiki yake...

Basi nna mambo makubwa mawili kwanza kutoka moyoni sitaki hata kumuona yule dada lakini mwanangu sasa nafanyaje na ndio kwanza ana miaka 2 hivi nimchukue au mana jana tu kaka alipita pita kwa wataaalam na yeye kwenye mambo yake akaona yule dada amenipangia aniue kwa ajali ya gari au aniue kwa kazini na mnaona hapo ndugu zangu?

Basi hayo ndio kwa ufupi sana nimeona leo niwaeleze mjue dunia ya sasa sio we mtu kila kitu ulipata leo malipo yangu ni hayo🤔🤔USHAURI wenu kwa sasa ni muhimu zaidi kama utataka kejeli tafadhali baki nazo tu niko serious katika hili na uzi huu ubaki hapa hapa mana kuna ndugu zangu wa kukufata jukwaa zingine kwa quotes zao..mkawe na siku njema
 
Pole mdogo wangu nimesoma kwa kwa kuchoka kidogo hila kama ushamngundua huyo mwanamke kwa ushirikina wake basi hachana mwanamke mshirikina hafai ata kwa kulimangia
 
Kaka pole sana kwa yaliyokukuta ila pamoja na yooote ayo uliyoyaeleza kikubwa now umeshajikomboa kumawazo kutoka kwa uyo mwanamke lkn kuna vitu naona unaviruhusu vikusumbue wakati sio vya msingi na ukienkdelea ivyo utapigwa na vitu vingine vizito zaid kichwani

Jambo LA kwanza ni iyo kauli ya kusema mtoto wako ambae kwanza ndio ana miaka miwili izo mentality zitakutesa zaid Fanya kutengeneza utaratibu mzr wa kuhudumia mwanao ila uko usiende na ikiwezekana umuhudumie kupitia MTU mwingine wa kati sio unaemuamini km baba yako

Kitu cha pili mm nakushauri usioe kwanza kwa sasa maana akili yako aiko sawa subir upepo upite kidogo ili upate kujipanga upya kimawazo na kiuchumi maana unaweza kuchukua MTU mwingine asie sahihi kwasababu ya maumivu uliyonayo kwa sasa.
Kitu cha tatu personally nakukaribisha kwenye chama la masingle father, na kua makini ulimwengu wa sasa usimwamini MTU ndio maana wengine tumeamua kua masingle father coz wanawake wa sasa awaaminiki walio wengi na kwa maelezo zaidi kamuone Mr Liverpool kwa ushauri.
 
Hapa kwanza subiri ninyonge dry moja kali ya orkokola af baadae nije nikazie na Embassy ili akili ikae sawa. Sa hv ntaishia kumwaga povu tu.

But in short, kama akili imefunguka bado unaomba ushauri wa nini? Nenda kamfungue huyo dem, mitama mingi, kata funua za kutosha, kelebu mujarab af beba kipande chako kalee na huyu mgogo wa dodoma.
 
Hamisha mali zote, mwambie zimeuzwa na bank pangisha hilo pagale aone mpangaji ndo kanunua (hakikisha wakati wa kupangisha mpangaji hakujui),,,,, uzuri kazi iko mbali mwambie unauza chips huko uliko.

Taratibu mwambie maisha yamebadrk akuvumilie kipindi ni kigumu sana kwa sasa.

km ulikuwa unatuma elfu kumi tuma elfu tano au elfu mbili

Mwisho usimtumbe uyo dada, wala usilale nae chumba kmoja.

NB: na weww mambo ya kujifanya unapittpta kwa mtaalamu kuna siku hao wataalamu watakuja na swala la mama yako ndiye mhusika mkuu sijui utafanyaje.
 
Sijaendelea mpaka mwisho...yaan kuona tu mtoto wa pili alizaa tena na mwingine moyo wangu umeugua.Haya mapenz tuyaache eti? Tutakufa jamen
 
ukimwona mwanamke yuko sngle na anamtoto jiulze kwann mwanaume mwenzio kamshindwa ww n nan ue bngwa m nshajfunza kuna sngle mama wa kuhurumia lakn sio wote 90% n ma mafia na tabia zao za ajabu ndio mana mwanaume wanawakimbia na wao wanatumia slogan ya kutelekezwa kua makin Mtoto wa kiume
 
Back
Top Bottom