Dunia haina usawa

Dunia haina usawa

Nilijua tu kule hapatufai watu kama sisi wenye hasira za haraka haraka maana kuna mimtu INA majibu yanakera sana
Hapana wala sijagombana na mtu nimeambia nachochea maandamano nikicomment
 
SEHEMU YA 31

Alipomaliza, akaisoma, aliporidhika, akapeleka kasa katika kitufe cha kutuma barua pepe hiyo lakini hata kabla hajaibonyeza, simu yake ya mezani ikaanza kuita. Akaacha kuituma, harakaharaka akachukua mkonga wa simu na kuupeleka sikioni, alichokisikia ni sauti ya mwanamke iliyokuwa ikilia.

“What is going on?” (nini kinaendelea?)
“Don’t tell him that she has died,” (usimwambie kama amekufa) alisikia sauti ya mtu aliyekuwa pembeni ya mtu aliyepiga simu hiyo kutoka shuleni walipokuwa wakisoma watoto wake.

Kijasho chembamba kikaanza kumtoka.
“Who has died?” (nani amekufa?) aliuliza lakini hata kabla hajajibiwa, simu ikakatwa. Akachanganyikiwa kupita kawaida. Kilichomjia akilini ni binti yake Irene tu.

Je, nini kitaendelea?
 
SEHEMU YA 32

Ofisini hakukukalika tena, Mapoto alichanganyikiwa, kwa simu aliyopigiwa, alihisi kabisa kulikuwa na tatizo shuleni hasa kwa mtoto wake Irene. Akachukua koti lake, hata kuuweka mkonga wa simu sehemu husika hakukumbuka, akatoka, hakumuaga ‘secretary’ wake, akatoka na kwenda nje ambapo akaingia ndani ya gari lake.

Dereva hakuwemo garini, alikuwa katika mgahawa uliokuwa hapo ofisini akinywa kahawa. Hakutaka kusubiri na wala hakutaka kumuita, akachukua ufunguo mwingine aliokuwanao, akaliwasha na kuondoka mahali hapo.
Alichanganyikiwa, hata uondokaji wake haukuwa wa kawaida, watu wote waliouona uondokaji ule wakawa na wasiwasi kwamba kulikuwa na kitu kimetokea.

Njiani, aliendesha kwa mwendo wa kasi, akaingia katika barabara iliyokuwa ikiruhusu magari kwenda kwa mwendokasi kuanzia 90 na kuendelea, akakanyaga mafuta kwa kasi, alichokuwa akikihitaji ni kuwahi huko, alitaka kuona ni kitu gani kilitokea.

Alichukua dakika kumi mpaka kufika shuleni ambapo geti likafunguliwa, hata hakuzima gari, akateremka na kuelekea katika ofisi ya mwalimu mkuu, alitaka kujua ni kitu gani kilitokea.

Alipofika huko, macho yake yakatua kwa mtoto wake, Godwin ambaye baada ya kumuona, akainuka kitini, akamkimbilia na kumkumbatia huku akilia mno.
“Kuna nini?” alimuuliza lakini Godwin hakujibu zaidi ya kuendelea kulia tu.

Mwalimu mkuu wa shule hiyo akamkaribisha, hakutaka kuzungumza kitu chochote kuhusu Irene, alimwangalia Mapoto, kwa jinsi alivyoonekana, alionekana kuwa na hofu kubwa.
“Mtoto wangu yupo wapi?” aliuliza Mapoto.

“Kuna kitu inabidi tuzungumze,” alisema mwalimu mkuu.
“Kitu gani? Kwanza niambieni mtoto wangu yupo wapi,” alisema Mapoto kwa sauti kubwa iliyowafanya walimu wawili kuingia humo kwani walihisi kwamba kulikuwa na fujo.

“Ndiyo tunahitaji kuzungumza kuhusu hilo,” alisema mwalimu mkuu.
“Ila yupo hai?”
“Ndiyo! Yupo hai! Cha msingi nisikilize kwanza,” alisema mwalimu huyo.
Hakutaka kumficha, alimwambia ukweli kwamba mtoto wake, Irene hakuwa kwenye hali nzuri.

Wakati wakiwa darasani, alipanda juu ya kiti huku akicheza na wenzake lakini kwa bahati mbaya alidondoka baada ya viatu vyake kuteleza.
 
SEHEMU YA 33

Lilikuwa tukio baya, japokuwa kuteleza kulionekana kuwa kwa kawaida kwa watoto wengi shuleni hapo lakini kitu ambacho kilionekana kuwa kibaya kwake ni kwamba alipoanguka, aliangukia kichwa na kukipigiza kwenye marumaru kisogoni hali iliyosababisha damu kutoka na kupoteza fahamu hapohapo.

“Nilisikia kwamba amekufa!” alisema Mapoto huku machozi yakianza kumtoka.
“Nani alikwambia?”
“Nilisikia kwa masikio yangu kwenye simu, mmoja wa walimu alisema hivyo!” alisema Mapoto.
“Hapana! Ila wote walihisi kwamba amekufa kutokana na mazingira yaliyokuwa yametokea ajali hiyo,” alisema mwalimu mkuu.

Hawakuongea sana, kitu alichokitaka Mapoto ni kumuona mtoto wake hivyo mwalimu mkuu alimwambia kwamba ni lazima waondoke na kuelekea katika Hospitali ya St. Monica Medical Center ambayo haikuwa mbali na mahali hapo.
Wakaondoka, njiani, Godwin alikuwa akilia tu, alitaka kumuona dada yake, alikuwa kwenye tukio, kila alipokumbuka jinsi Irene alivyoanguka na kuumia vibaya kichwani, moyo wake ulimuuma mno.

Hawakuchukua muda mwingi wakafika hospitalini hapo na kuanza kuelekea katika chumba kile alicholazwa Irene, walipofika, hawakuruhusiwa kwani mgonjwa hakuwa kwenye hali nzuri, alihitaji muda mrefu wa mapumziko.
“Dokta! Mtoto wangu atapona?” aliuliza Mapoto huku akionekana kuumia moyoni mwake.

“Tunamwamini Mungu!”
“Kwa hiyo atapona?”
“Hebu nifuateni ofisini!” Wakamfuata daktari huyo mpaka ofisini ambapo wakakaa na kuanza kuwaelekezea tatizo alilokuwa nalo Irene.

Lilikuwa tatizo kubwa ambalo huwatokea watu wengi, wakati Irene alipoanguka chini, alikipigiza kichwa chake kwenye sakafu na hivyo kushtua mishipa ya fahamu hali iliyompelekea kupoteza fahamu na kuwahishwa hospitalini.
“Atarudiwa na fahamu zake?” aliuliza Mapoto.

“Ndiyo japokuwa anatakiwa kuwa chini ya uangalizi wetu kwani tatizo ambalo amekutana nalo ni kubwa sana, kama itachukua muda mrefu zaidi na hakuna mafanikio basi itabidi afanyiwe upasuaji wa kichwa,” alisema daktari huyo aliyekuwa na kichuma kifuani mwake kilichoandikwa Dr. Phellips.
 
SEHEMU YA 34

Hilo ndilo waliloambiwa na daktari, hawakutakiwa kumuona Irene kipindi hicho kwa kuwa tu hali yake haikuwa nzuri na baada ya kutolewa kwenye chumba cha upasuaji, haraka sana akahamishwa na kupelekwa katika chumba cha wagonjwa mahututi.

Hilo lilimuuma sana Mapoto, hakujua ni kwa jinsi gani angeweza kukabiliana na hali hiyo ambayo ilikuwa ni yenye kuumiza sana, mbali na hayo yote, pia hakujua ni kwa jinsi gani angeweza kumwambia mke wake juu ya lile lililokuwa limetokea.

Alimfahamu Rosemary, aliwapenda sana watoto wake, kwake, hao walikuwa kila kitu katika maisha yake, alijua kwamba kama angempa taarifa moja kwa moja basi hali ingekuwa mbaya zaidi na angeweza kumsababishia matatizo.

“Nitamwambia tu, ila sitotaka kumpa taarifa akiwa nchini Tanzania, ni lazima aje huku,” alisema Mapoto.
Siku hiyo walikaa hospitalini hapo, hawakuruhusiwa kumuona mgonjwa mpaka ilipofika majira ya saa 2:00 usiku ndipo wakaruhusiwa na kwenda katika chumba maalum alicholazwa mtoto huyo.

Walipomuona kitandani, kila mmoja alionekana kuumia mno. Irene alikuwa kimya kitandani pale, mdomoni alikuwa na mashine ya oksijeni iliyokuwa ikimsaidia kupumulia huku pembeni kukiwa na mashine nyingine ambayo ilikuwa ikionyesha mapigo ya moyo kwa jinsi yalivyokuwa yakidunda.

Mapoto na Godwin wakamsogelea Irene pale kitandani alipokuwa, walipomfikia, wakasimama na kumwangalia. Alikuwa kimya kabisa kiasi kwamba ilikuwa ni rahisi kusema kuwa tayari aliaga dunia, walikuwa kama wakimwangalia mtu ambaye tayari alikuwa amekwishafariki dunia.

“Irene…We came for you, open your eyes and look at us,” (Irene…tumekuja kwa ajili yako, fumbua macho yako utuangalie) alisema Mapoto huku akimwangalia mtoto wake kitandani pale.
Walihuzunika, waliendelea kukaa ndani ya chumba kile kwa saa mbili ndipo wakaondoka na kurudi nyumbani.

Hakukuwa na mtu aliyelala, kila mmoja alikuwa kimya, walimkumbuka Irene, kitendo cha kutokuwa ndani ya nyumba ile kiliwapa mawazo mazito mno.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom