SEHEMU YA 101
“Sijajua! Sijui chochote kile. Nimekuwa nikionewa, hakuna anayenionea huruma, sijajua ni kwa sababu gani mambo haya nafanyiwa mimi. Kila siku mimi tu,” alisema mwanamke huyo huku akiendelea kulia.
“Nitafuatilia mama! Nakuahidi kwamba nitafuatilia!” alisema Bwana Massatu.
“Nitashukuru!”
Rosemary akaondoka ofisini kwa waziri wa elimu huku akiwa na matumaini ya kusaidiwa. Njiani, hakuacha kulia, kila alipokuwa akiiangalia barua ile moyo wake ulikuwa na maumivu makali mpaka kuhisi kama kulikuwa na kitu chenye ncha kali kilichokuwa kikimchoma.
“Mungu! Mbona kila siku hivi? Ni nani yupo nyuma ya mambo haya yote? Na kwa nini kila siku ni mimi tu? Mungu! Kuna kitu nimekukosea? Kuna kitu nimekifanya hakipo sawa na umeamua kunipiga namna hii?
Mungu, hili jaribu limekuwa kubwa sana kwangu, siwezi kulibeba, nitie nguvu ya kusonga mbele, nionyeshe njia kwani bila nguvu zako, siwezi, nitashindwa kusimama na kusonga mbele,” alisema Rosemary huku akiwa ameinama chini ndani ya daladala, machozi yaliendelea kumtiririka mashavuni mwake kama maji.
Je, nini kitaendelea?