Dunia haina usawa

Dunia haina usawa

SEHEMU YA 86

Hakuwa mtu wa siasa lakini hakuwa akiipenda serikali ya Chama cha Labour ambacho kilikuwa madarakani ambacho kazi yake kubwa kilikuwa ni kuwabana wafanyabiashara kwa kuwaongezea kodi.
Alikichukia chama hicho na hivyo kuwekeza nguvu zake kukisaidia chama pinzani cha Tanzania national Party kilichokuwa kimemuweka mwenyekiti wa chama hicho, Edward kuwa mgombea wa chama hicho.

Hawakushinda, walishindwa vibaya na hivyo Bokasa kuendelea kuiongoza Tanzania kwa miaka mingine mitano. Alikasrika, hakutaka kukiona chama hicho kikiendelea kuwa madarakani, aliawaandaa watu wake kwa ajili ya kufungua kesi ili kuyapinga matokeo hayo katika mahakama ya kimataifa lakini ilishindikana na hivyo kuamua kuachana na siasa na kufanya biashara zake.

Kila kitu kilichokuwa kikiendelea kwa Rosemary alikifahamu, moyo wake ulimuuma mno, alijua fika kwamba Mapoto hakuwa amekopa fedha hizo bali kulikuwa na mchezo ambao serikali ulitaka kuucheza, kumfilisi mwanamke huyo na kumuacha akiwa hana kitu kabisa.

Hakutaka kuona hilo likitokea, na hata nyumba ilipopigwa mnada, yeye ndiye aliyeinunua kwa kumtumia rafiki yake, Othman Ngolisho ili kusiwe na mtu yeyote ambaye angegundua kwamba yeye ndiye aliyeinunua nyumba hiyo.

Hakuishia hapo bali alichokifanya ni kupanga mikakati ya kumsaidia Rosemary kwa kila kitu. Alijua kwamba kama angemuweka ndani ya nyumba ileile ilikuwa ni lazima serikali kufahamu kilichotokea hivyo aliamua kuachana naye lakini mwisho wa siku amsaidie kumtunza na kumfanyia mambo mengine.

Wakati Rosemary hajui ni kitu gani kingeendeleakatika maisha yake, akamtuma kijana wake kwa ajili ya kumpa taarifa mwanamke huyo kwamba kulikuwa na nyumba iliyokuwa Kimara Stop Over ambayo alikuwa ameandaliwa kwa ajili ya kuishi na familia yake.
“Ni ya nani?” aliuliza Rosemary.
“Bosi wangu!”

“Nani?”
“Si lazima umfahamu! Ila ni yeye ndiye ameamua kukusaidia,” alisema kijana huyo aliyejitambulisha kwa jina la Juma Hassani.
“Sawa.”

Wakati Juma akizungumza na Rosemary, kulikuwa na wanaume watatu waliokuwa wakimfuatilia, walijua kwamba kulikuwa na kitu, walihisi hivyo kwa sababu kila walipomwangalia, kijana huyo alikuwa akiangalia huku na kule.
 
SEHEMU YA 87

Wakati Juma akiondoka, wanaume wale hawakutaka kumfuatilia kwa ukaribu, walichokifanya ni kutulia ndani ya gari lao kisha kumwacha mpaka atakapoingia ndani ya gari lake, alipofanya hivyo, wakaanza kumfuata.

“Kuna kitu!” alisema jamaa mmoja.
“Hata mimi nahisi! Hebu tumfuatilie, atatuambia ni kitu gani kinaendelea!” alisema jamaa mwingine.
Juma hakuwa na habari kama alikuwa akifuatiliwa kwa nyuma, akaingia kwenye barabara ya lami na kuondoka huku akielekea maeneo ya Namanga huku lengo lake likiwa ni kutaka kuelekea Kinondoni alipokuwa akiishi.

Wakati akiwa amekwishafika maeneo hayo ya Namanga, karibu na kona ya kuelekea ubalozi wa Marekani, akashtukia gari moja aina ya Range SUV jekundu likija na kusimama mbele yake.

“Kuna nini?’ alijiuliza lakini hata kabla hajajijibu, milango miwili ya gari lile ikafunguliwa, wanaume wawili waliokuwa na bastola mikononi mwao wakateremka na kumfuata Juma.
“Shuka chini,” alisema jamaa mmoja huku akiwa amevunja kioo.

“Nimefanya nini?”
“Paaa…” risasi ikapigwa hewani, watu wote waliokuwa wakishangaa huku wakitamani kujua kitu gani kinaendelea, wakaanza kukimbia.
“Jamani msiniue!”
“Basi teremka.”

“Sawa!” alisema Juma huku akitetemeka.
Akateremka, wakamchukua, wakamuingiza ndani ya gari lao na kuondoka naye mahali hapo. Watu wote waliokuwa wamejificha, wakaanza kujitokeza huku wengine wakilaumu kwamba kwa nini polisi wa Kituo cha Osterbay hawakutokea na wakati hawakuwa mbali na mahali ambapo risasi ilipigwa?

“Wale sio majambazi?” aliuliza jamaa mmoja.
“Majambazi! Majambazi gani wanavaa suti?” aliuliza jamaa mwingine, wakati huo gari lile lilifika ubalozini, likakata kulia na kuanza kuelekea Mikocheni huku muda wote huo Juma akilia kuomba msamaha japokuwa hakujua alifanya nini.

*** Bilionea Adam Matiku alikuwa nyumbani kwake ametulia, alichokuwa akikisubiri ni ripoti kutoka nyumbani kwa Mapoto ambapo nyumba ya marehemu huyo ilikuwa ikipigwa mnada huku akiwa amemuandaa rafiki yake, Othman Ngolisho kwa ajili ya kuinunua nyumba hiyo.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom