Dunia haina usawa

Dunia haina usawa

Mkwe unapoelekea utanipa ban shunie mm nikishusha mgazeti wangu yaani ni kweli hawana tofauti kabisa mwanzo walinipa ban et nachochea maandamo mods hawapendi sikia habari za maandamnao na sio kwamba napost thread za maandamano hapana nacomment tu habari za maandamano

Mara ya pili ban imeniuma mpaka nikawaandikia thread kama hawataki niende jukwaa la siasa waniambie ban waliyonipa wamenionea kuna thread ilipostiwa jukwaa la siasa jf ya sasa sio kama ya zamani nikacomment jf ya sasa inabidi tukae kimya tu nikala ban sababu waliyonipa eti comment yangu nazuia wengine kuchangia hoja nazuiaje sasa
Mkwe huna sababu ya kuogopa kama hakuna uhuru wa kuongea na kuchangia hoja Mtu anavyoona wafute mtandao wao bwana tutaogopana mpaka lini kama maandamano yapo yapo tuu tuongee tusiongee yatakuepo kama hayapo hayapo tuu hata tukakesha tukiongea hayapo sasa kama wao wanaamini wapo sahihi wanaogopa nini hawa mods nao washatishiwa wanakuja kuwapa Watu bani zisizo na maana nchi gani huru isiyo na uhuru?
 
Mkwe huna sababu ya kuogopa kama hakuna uhuru wa kuongea na kuchangia hoja Mtu anavyoona wafute mtandao wao bwana tutaogopana mpaka lini kama maandamano yapo yapo tuu tuongee tusiongee yatakuepo kama hayapo hayapo tuu hata tukakesha tukiongea hayapo sasa kama wao wanaamini wapo sahihi wanaogopa nini hawa mods nao washatishiwa wanakuja kuwapa Watu bani zisizo na maana nchi gani huru isiyo na uhuru?
Mkwe acha nibaki hivi
 
SEHEMU YA 43

Rais Bokasa akarudi hotelini, alikuwa amechanganyikiwa, hakujua ni kitu gani alitakiwa kufanya, ni kweli alifika nchini Marekani kwa ajili ya kuzungumza na Mapoto na kumwambia kuhusu kile alichotaka kukifanya lakini jambo baya kwake ni kwamba mtu huyo hakuweza kuzungumza chochote kwa kuwa alikuwa kwenye matatizo makubwa.

Alimuonea huruma lakini hakuwa na jinsi, alitakiwa kumalizana naye, aachane na barua hiyo na aendelee kufanya kazi kama balozi kwani kurudi kwake nchini Tanzania kungemaanisha kwamba upinzani ungepata nguvu na kujipanga tena kwa ajili ya uchaguzi ujao.

“Ni lazima nikae naye chini na kuzungumza. Hatakiwi kujiuzulu, nitamshawishi hata kwa kumlipa mshahara mnono,” alisema Rais Bokasa huku akiwa kitandani kwake.

Siku iliyofuata, haraka sana asubuhi akaelekea hospitalini kuonana na Mapoto, bado hakuwa sawa, alijitahidi kumchangamsha lakini mwanaume huyo hakuchangamka kabisa, alionekana kukata tamaa na kila alipomkumbuka mtoto wake, jinsi alivyokuwa amelala kitandani, moyo wake ulimuuma mno.

Godwin alikuwa mtu wa kulia tu, alikuwa na majonzi mazito, alitamani kumuona dada yake akisimama na kuzungumza tena, hali aliyokuwa nayo kitandani pale ilimuumiza mno.

Alizoea kuwa naye kila siku, kwenda shuleni pamoja, kucheza wote na kufanya mambo mengi lakini kwa kipindi hicho hali ilikuwa mbaya, kwani kwenda shuleni kwenyewe alikwenda peke yake na hata kurudi, alirudi peke yake bila Irene kitu kilichomfanya kukosa furaha kabisa.

“Mama! Nataka nimuone Irene,” alisema Godwin huku akifuta machozi yake.
“Utamuona! Daktari amesema kesho tutaingia na kumuona, ila utatakiwa kwenda shule kwanza. Umesoma nini leo?” aliuliza Rosemary swali ambalo lilionyesha ni kumtaka Godwin asiendelee kuuliza kuhusu Irene.

Wakati hayo yote yakiendelea nchini Marekani, Edward na viongozi wengine hawakujua ni kitu gani kilikuwa kikiendelea nchini humo. Waliambiwa na Mapoto kwamba angewaandikia barua ya kuomba kujiuzulu lakini kitu cha ajabu kabisa mpaka kipindi hicho alikuwa kimya kabisa.
 
Mistari ya kwanza tu imenivutia, acha nisubscribe ndovu zikiisha nitasoma.
 
SEHEMU YA 44

Wakawa na hofu kwa kuhisi kwamba mwanaume huyo aliwabadilikia, wakajaribu kuwasiliana naye, simu yake haikuwa ikipatikana, hawakujua ni kitu gani kilikuwa kikiendelea.

Rais Bokasa alipopata safari ya kuelekea nchini Marekani, wakajua kabisa kwamba mwanaume huyo alikuwa akienda kuonana na Mapoto, wakajua kabisa kwamba walibadilikiwa, mtu ambaye walimwamini kwa moyo mmoja, mtu ambaye walimpa dhamana kubwa ya kugombea urais kupitia chama chao, hatimaye aliamua kuwabadilikia na kuungana na chama tawala kinyemela.

“Huu ni usaliti! Sisi kama Tanzania National Party hatutoweza kukubali, ni lazima tulifute jina lake kama mwanachama wa chama hiki,” alisema Edward, alionekana kuwa na hasira sana.
Hilo halikupingwa, kila mmoja akamuunga mkono kwamba ni lazima Mapoto afutwe katika chama hicho. Hawakujua ni hatua gani alizokuwa akipitia nchini Marekani, hawakujua kama mwanaume huyo alikuwa kwenye hali mbaya, kwamba mtoto wake mpendwa, Irene alikuwa hoi kitandani.

Taarifa ya kufutwa kwake uanachama ikatangazwa kwenye vyombo vya habari na baada ya siku mbili, jina lake likakatwa. Kila mtu akahuzunika, wengi hawakuamini kama mwanaume huyo waliyemwamini aliamua kuwasaliti na kujiunga na chama tawala.

Chuki dhidi yake ikaingia mioyoni mwa kila mmoja, kila mtu akamchukia, kuanzia watoto, vijana mpaka wazee wote walionyesha chuki dhidi yake, hawakumpenda, walimuona kuwa msaliti mkubwa, hata habari ya kuumwa kwa Irene hawakuwa wakiijua. Kila mmoja alikubaliana na viongozi wa chama hicho kwamba jina lake lifutwe.

“Yule ni nyoka, ni mtu mbaya sana ambaye huwezi kuvumilia kuwa naye, kama ukiishi naye, anaweza kukuua,” alisema mwanaume mmoja, kwa kipindi hicho, hasa miaka hiyo hakukuwa na mitandao ya kijamii, watu walitegemea taarifa kutoka kwenye televisheni na magazeti, waandishi wa vyombo hivyo hawakujua kilichokuwa kikiendelea, hilo likawafanya wananchi kutokujua lolote lile kuhusu mtoto Irene.
 
SEHEMU YA 45

Kila kona nchini Tanzania kulikuwa na tetesi kuhusu kuandika barua ya kujiuzulu ya Bwana Mapoto, kila mtu aliyepata taarifa hiyo alimwambia mwenzake kwamba huo ndiyo ungekuwa mwisho wa mwanaume huyo kuwa balozi nchini Marekani na baada ya siku chache angerudi nchini Tanzania.

Mtu wa kwanza kupewa taarifa alikuwa Bwana Edward ambaye ni mwenyekiti wa Chama cha Tanzania National Party, kitendo cha kuwaambia viongozi wenzake tu, tayari taarifa hizo zikaanza kusambaa kila kona na ndani ya saa chache watu wengi wakajua kile kilichokuwa kikiendelea nchini Marekani.

Kila mmoja alikuwa na hamu ya kumuona Mapoto akirudi nchini Tanzania, watu walimpenda na waligundua kwamba mbinu za Rais Bokasa zilikuwa ni kumpoteza kisiasa kwa hiyo kitendo cha kuandika barua ya kujiuzulu kilikuwa ni kama kuwaambia kwamba alikuwa tayari kurudi katika uwanja wa vita mpaka kieleweke.

Viongozi wa chama tawala walichanganyikiwa, kwa kutumia usalama wa taifa ambao walikuwa mitaani, waliwapa mamlaka ya kuchunguza suala hilo kama lilikuwa na ukweli wowote, hilo halikuwa tatizo, wakaingia mitaani, wakachunguza kwa kina na kupeleka majibu kwamba kila kitu kilichozungumzwa kilikuwa ni cha kweli kabisa.

“Kwa hiyo?”
“Tumpeni taarifa rais,” alisema Waziri wa Mambo ya Ndani, Bwana Amani Kizutu.
Hakutaka kupoteza muda, haraka sana akampigia simu rais na kumwambia kilichokuwa kimetokea, rais mwenyewe hakuamini kama kweli jambo hilo lingeweza kutokea kwani aliamini kwa kumpa ubalozi Mapoto basi kila kitu kingekwenda kama kilivyotakiwa kwenda.

Alichanganyikiwa, huo ndiyo aliuona kuwa mwisho wa chama chake kwani aliamini kuwa kama mtu huyo angemwandikia barua ya kujizulu basi ingekuwa tatizo sana kwake.

Alichokifanya ni kumpigia simu, alitaka kuzungumza naye mambo mengi likiwa hilo la kutaka kujizulu kwa kumwandikia barua. Mapoto alipopokea simu, alimwambia kwamba hakuwa tayari kulizungumzia hilo kwani alikuwa kwenye matatizo makubwa kipindi hicho.
“Matatizo gani?”
 
SEHEMU YA 46

“Mtoto wangu anaumwa sana. Naomba umkumbuke katika maombi yako,” alisema Mapoto huku sauti yake tu ikisikika kama mtu aliyekuwa kwenye maumivu makali mno.

“Pole sana!”
Rais Bokasa hakutaka kubaki nchini Tanzania, hakutaka kulipuuzia jambo hilo, alichokifanya siku iliyofuata ni kuondoka nchini Tanzania na kwenda Marekani, alihitaji kuzungumza na Mapoto, alitaka kufahamu sababu iliyompelekea kutaka kufanya maamuzi hayo.

Ndani ya ndege, rais huyo alikuwa na mawazo lukuki, kichwa chake kilichanganyikiwa mno, alikuwa kimya, safari hiyo ilionekana kuwa ndefu na yenye kuchosha kuliko safari yoyote ile aliyowahi kufanya katika maisha yake.

Mara baada ya kufika jijini New York nchini Marekani, akaelekea katika Hoteli ya Bavarian iliyokuwa na hadhi ya nyota saba na kutulia huko. Usiku wa siku hiyo hakutaka kuwasiliana na Mapoto, kwa kuwa alimwambia juu ya hospitali waliyokuwepo, kesho yake akaelekea huko na kukutana naye.

“Pole sana! Jitie nguvu, natumaini Irene atapona na kurudi katika hali yake ya kawaida,” alisema Rais Bokasa huku akimkumbatia Mapoto.
“Nashukuru sana!” Matibabu yaliendelea hospitalini hapo, watu wengi walikuwa wakifika mahali hapo na kumpa pole.

Kila mmoja alionekana kumuonea huruma balozi huyo, hatua aliyokuwa akipitia katika maisha yake ilikuwa ngumu kupita kawaida.
Mke wake, Rosemary ambaye alipoteza fahamu baada ya kupewa taarifa juu ya mtoto wake kupata tatizo la kichwa hakuwa amerudiwa na fahamu huku tayari zikiwa zimepita saa arobaini na nane.

“Daktari! Mke wangu anaendeleaje?” aliuliza Mapoto huku akimwangalia mkewe aliyekuwa kimya kitandani, tena huku akisaidiwa kupumia kwa kutumia mashine ya oksijeni.
“Anaendelea vizuri! Natumaini atakwenda kuwa mzima wa afya ndani ya siku hizi chake,” alijibu Dk. Phellips.

Baada ya saa kadhaa, mke wake akarudiwa na fahamu, kitu cha kwanza kabisa kuuliza kilikuwa ni mtoto wake. Moyo wake ulikuwa kwenye maumivu makali, hakuamini kama kweli Irene, mtoto wake aliyekuwa akimpenda mno alikuwa kwenye hali hiyo.
 
SEHEMU YA 47

Kitandani pale alikuwa akilia tu, alimwangalia mume wake huku muda wote akiwa anamlaumu juu ya sababu iliyomfanya kutokumpa taarifa tangu alipokuwa nchini Tanzania.
“Ilikuwa vigumu kufanya hivyo mke wangu! Najua ni jinsi gani unawapenda watoto wetu, kama ningekwambia wakati upo Tanzania, ungepata tatizo zaidi.

Naomba unisamehe Rose,” alisema Mapoto huku akimwangalia mke wake.
Hali ya Irene haikuweza kubadilika kitandani hapo, japokuwa shuleni alionekana kuumia kidogo lakini alionekana kuwa na tatizo kubwa kichwani mwake kwani ilionekana kwamba alipokuwa ameanguka, kichwa chake kiliumia vibaya kwa ndani na kuifanya damu kuingia na kuvilia katika ubongo kitu kilichoonekana kuwa kibaya sana hasa kwa mtoto kama yeye.

“We must perfom craniotomy surgery,” (ni lazima tumfanyie upasuaji wa kichwa) alisema Dk. Phillips huku akiwaangalia madaktari wenzake.
“Will they agree with us?” (watakubaliana nasi?) aliuliza nesi mmoja.

“There are no other options,” (hakuna njia nyingine) alijibu Dk Phellips.
Hilo ndilo walilokubaliana, ilikuwa ni lazima Irene afanyiwe upasuaji wa kichwa kwani kulikuwa na donge dogo la damu lililovilia kwenye kichwa chake na kuganda.

Dk. Phellips akamuita Mapoto na mkewe na kwenda nao ofisini, walipofika huko, kwanza akawaelezea ugumu waliokuwa wakikutana nao, aliwaambia kuhusu donge dogo la damu na kwamba ilikuwa ni lazima wamfanyie upasuaji wa kichwa vinginevyo Irene angeweza kufa kitandani pale.

“Dokta....”
“Hakuna kitu kingine tunachoweza kufanya zaidi ya hicho! Hatuna jinsi, ni lazima tufanye kila liwezekanalo kuhakikisha kwamba Irene anapona kabisa,” alisema daktari huyo.
Hawakuwa na jinsi, walitamani kumuona mtoto wao akirudi katika hali yake ya kawaida. Walijua kwamba kulikuwa na hatari kubwa katika kufanyiwa upasuaji wa kichwa kwa mtoto wao lakini wakakubaliana na daktari huyo.

Hakukuwa na muda wa kupoteza, siku iliyofuata, Dk. Phellips na timu yake wakajipanga vilivyo kwa ajili ya kazi hiyo ambayo ingechukua saa ishirini na mbili mpaka kukamilika.
 
SEHEMU YA 48

Wakaweka kikao na kuanza kumjadili Irene, wakapitia ripoti ya tatizo lake lote na walipoona kamba wamepitia kila kitu, wakapanga muda wa kuanza upasuaji huo.
Si Mapoto wa Rosemary aliyeonekana kuwa na furaha, wote walikuwa na majonzi tele mioyoni mwao, kila walipokuwa wakimfikiria Irene na tatizo alilokuwa nalo wakahisi kabisa kwamba wangeweza kumpoteza mtoto wao kitu ambacho kingewauma mno.

Ilipofika saa 3:05 asubuhi, mlango wa chumba kile alicholazwa mtoto wao ukafunguliwa na kitana alicholazwa Irene kutolewa. Hawakuweza kubaki mahali walipokuwa, wakainuka na kukisogelea kitanda kile, wakainama na kumwangalia Irene.

“Irene mtoto wangu! Mungu akulinde, ninaumia moyoni, siamini kama wewe ndiye unayepitia hatua hii ngumu. Binti yangu, moyo wangu unaniuma sana, siwezi kuzuia jambo hili, siweza kufanya lolote lile zaidi ya kukukabidhi mikononi mwa Mungu aliye hai,” alisema Rosemary huku akibubujikwa na machozi.

“Mke wangu! Irene atapona. Ninamuamini Mungu wangu! Kama aliweza kumuokoa Daniel katika shimo lenye simba, kama aliweza kumfufua Lazaro, kama aliweza kumbadilisha Paulo kutoka kwenye ubaya mpaka utakatifu, amini hili ni jambo dogo sana kwa Mungu, ninaamini atamponya,” alisema Mapoto huku akimtoa mke wake kutoka katika kitanda alichokuwa Irene.

“Ninaumia mume wangu! Moyo wangu unachoma, moyo wangu unauma,” alisema Rosemary, machozi yake hayakukata. “Mungu atamponya tu,” alisema Mapoto na kumkumbatia mke wake.
Alimwamini Mungu wake aliyekuwa akimwabudu, alijipa nguvu moyoni mwake. Manesi wale wakakisukuma kitanda kile mpaka katika chumba cha upasuaji na kisha mlango kufungwa.

“Unahisi Mungu wako atamponya? Umesikia lini mtu anayefanyiwa upasuaji wa kichwa akapona kirahisi namna hii? Huo ndiyo mwisho wa mtoto wako, hatoweza kuamka tena, atakufa na kulala kaburini milele,” ilisikika sauti moyoni mwa Mapoto, kila alipoikemea sauti ile, iliendelea kuzungumza moyoni mwake kitu kilichomtia hofu kubwa. “Hatokufa…mtoto wangu hatokufa..” alisema kimoyomoyo kuijibu sauti ile.
“Endelea kujidanganya,” iliongezea sauti ile.

Je, nini kitaendelea?
 
SEHEMU YA 49

Mwandishi wa Gazeti la Siasa la Kioo, Samuel Matamshi alikuwa akifuatilia kila kitu kilichokuwa kikiendelea. Moyo wake ulihuzunika sana, hakuamini mtu kama Mapoto angeweza kufanya kitu kama kile, kuhamia katika chama tawala na wakati nyuma yake kulikuwa na idadi kubwa ya watu waliokuwa wakihitaji kumuona akiwa rais wa nchi hiyo.

Imani yake ilimwambia kwamba kulikuwa na kitu kilichokuwa kikiendelea, isingekuwa rahisi kwa mtu kama Mapoto kufanya uamuzi kama huo ambao ulikuwa mwiba mchungu kwa Watanzania wengi masikini.

Alitaka kufahamu kilichokuwa nyuma ya pazia, alisikia kwamba Mapoto aliachana na chama hicho, hizo zilikuwa tetesi lakini hakukuwa na taarifa iliyoandikwa kwenye gazeti lolote kuthibitisha ule uvumi uliokuwa ukiendelea kusikika.

Hakutaka kubaki nchini Tanzania, akazungumza na viongozi wake kwamba alitaka kuelekea nchini Marekani kufuatilia kile kilichokuwa kikiendelea kwa Mapoto nchini humo.
Hilo halikuwa tatizo hata kidogo, akaruhusiwa, akatafuta viza na vibali vingine vya kusafiria na alipotimiza masharti yote ya kuingia nchini Marekani, akaelekea huko kwa ajili ya kufanya kazi.

Waandishi wenzake walitaka kusikia taarifa kutoka kwake, walitaka kufahamu ni kitu gani kilichokuwa kimetokea, kwa kiasi fulani nchi haikuwa imetulia, kila kona ni jina la Mapoto tu ndilo lililokuwa likitajwa, halikukauka midomoni mwa watu na watu wengi waliokuwa wakilitaja, walilitaja kwa mabaya na si kwa mazuri.

Baada ya saa ishirini na tatu akaingia nchini Marekani, kipindi hicho kilikuwa ni cha baridi kali, akanunua koti kubwa na kuelekea katika hoteli ambayo aliweka oda ya chumba. Alipofika huko, akatulia kitandani na kupumzika kwani kesho yake alikuwa na jukumu zito la kumfikia Mapoto na kufanya naye mazungumzo huku akitaka kujua kila kitu.

Usiku ulipofika akalala, asubuhi na mapema akaamka na kuchukua teksi ambayo alihitaji impeleke katika ubalozi wa Tanzania hapo Marekani.

Hilo likafanyika, dereva akampeleka huko ambapo baada ya kufika, akateremka kutoka garini na kulifuata geti.
“Tukusaidie nini?” aliuliza jamaa mmoja mweusi, alikuwa Mtanzania.
“Ninahitaji kumuona balozi.”
 
SEHEMU YA 50

“Wewe ni nani?”
“Mwandishi! Samuel Matamshi!” alijibu huku akimuonyeshea kitambulisho.
“Ooh! Kumbe ndiye wewe? Nimefurahi kukuona, huwa ninasoma sana makala zako, hakika ni nzuri! Unafanya kazi safi sana, Mungu akubariki,” alisema jamaa huyo ambaye alikuwa mlinzi ubalozini hapo.

“Nashukuru sana.”
“Umesema umekuja kumuona balozi?”
“Ndiyo!”
“Ana wiki nzima hajafika ofisini!”
“Kwa nini?”
“Mtoto wake ni mgonjwa, juzi tu ametoka kufanyiwa upasuaji wa kichwa na hali yake si nzuri,” alijibu mlinzi yule.

Mlinzi huyo alimwambia Matamshi kila kitu kilichokuwa kimetokea. Mwandishi huyo akabaki kimya, alimwangalia mlinzi yule huku akionekana kutokuamini kile alichoambiwa.
Hapo ndipo alipogundua kwamba mwanaume huyo alikuwa kimya kutokana na matatizo aliyoyapata. Hakukuwa na mtu yeyote aliyejua hilo nchini Tanzania, kila mtu alimlaumu kwa kumuona msaliti aliyestahili kupigwa mawe na kufa kabisa.

Hakutaka kubaki hapo, alitaka kumsikia Mapoto mwenyewe, muda huohuo akapanda taksi na kuelekea katika hospitali aliyolazwa Irene. Njiani, kichwa chake kilichanganyikiwa, aliwalaumu viongozi wa Chama cha Tanzania National Party kwa kuamua kumfuta uanachama mtu huyo pasipo kujua kwamba kitu kilichomfanya kutokuandika barua ya kujiuzulu ni kwa sababu mtoto wake alikuwa kwenye matatizo makubwa.

Hakuchukua muda mrefu akafika katika hospitali hiyo. Akamlipa dereva na kuelekea huko. Aliliona kundi la wanafunzi wengi wakiwa hospitalini hapo, hakujua kama wanafunzi wote hao walifika hospitalini hapo kwa ajili ya kumjulia hali mwanafunzi mwenzao, Irene ambaye alikuwa katika hali mbaya hospitalini hapo.

Akaelekea mpaka mapokezini ambapo baada ya kuuliza, akaelekezwa chumba alicholazwa Irene na kwenda huko. Nje, macho yake yakatua kwa Mapoto, mkewe, mtoto wake, Rais Bokasa na walimu waliokuwa hapo nje. Akawasogelea, akamsalimia Mapoto na mkewe ambao walikuwa kwenye majonzi mazito.

“Pole sana Mapoto,” alimwambia huku akimkumbatia.
“Nashukuru sana Matamshi. Nashukuru sana kwa kuja kuniona,” alisema Mapoto huku akimwangalia akiwa amekumbatiana na mwanaume huyo.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom