Dunia haina huruma | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dunia haina huruma

Discussion in 'Entertainment' started by Imany John, Sep 30, 2012.

 1. Imany John

  Imany John Verified User

  #1
  Sep 30, 2012
  Joined: Jul 30, 2011
  Messages: 2,776
  Likes Received: 262
  Trophy Points: 180
  Ni kisa kilichosimuliwa vizuri na kwa ubunifu mkubwa na mwanadada ajulikanaye kwa jina la BAHATI BUKUKU.

  Ni kibao kilichopigwa kwa hadhi ya kama charanga fulani,kina ujumbe ambao kwa dunia ya leo ni elimu tosha.
  Kama hujapata bahati ya kuusikiliza,ukipata nafasi hiyo itumie vizuri then uje utuambie umejifunza kipi toka katika wimbo huo!
   
 2. z

  zilakina JF-Expert Member

  #2
  Oct 1, 2012
  Joined: Sep 16, 2011
  Messages: 294
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 45
  Wimbo mzuri ila SIYO wa Mungu kwani hauna tofauti na nyimbo za kidunia eg "ZUWENA NITAMPATA WAPI".Bahati yupo kibiashara zaidi.
   
 3. Riwa

  Riwa JF-Expert Member

  #3
  Oct 1, 2012
  Joined: Oct 11, 2007
  Messages: 2,601
  Likes Received: 232
  Trophy Points: 160
  Naomba kutofautiana nawe kidogo kuhusu huu wimbo:
  1 - Japo nyimbo nyingi si visa vya ukweli, lakini huu wimbo kisa chake kiko mbali sana na ukweli kuliko visa vyote ambavyo nimewahi kuvisikia (atleast me personally). Labda nitoe mifano michache...si kitu kinachokaribiana na ukweli kuwa Daktari akatae kumpa matibabu mgonjwa wako (tene emergence case ICU) mpaka umhonge 'ngono', hiyo iko mbali kabisa na ukweli...kisha hongo hiyo ya ngono ifanyike bila protection (condom)...kisha hongo hiyo ya ngono izae mtoto.

  2 - Ukisikiliza nyimbo nyingi za Bahati Bukuku, solution zake zinakuwaga extreme..nikimaanisha, kwa mfano...kuna familia nyingi wanaume wanalea watoto wasio wao (rejea utafiti uliofanywa na ofisi ya mkemia mkuu wa serikali kupitia vinasaba au DNA test), lakini solution haijawahi kuwa kikao cha familia nzima iamue 'mtoto auawe, tena kwa mapanga'...kisa tu mama amezaa mtoto huyo nje ya ndoa.

  Nakubalina nawe kuwa Bahati Bukuku ni mwimbaji mwenye kipaji sana na sauti nzuri, lakini I cant help to think that...amejificha kwenye mwamvuli wa 'nyimbo za Injili' (labda kwa sababu ya soko) lakini anaimba nyimbo za kiDunia sana kuliko za kiInjili..

  NB: Ni mtazamo wangu tu nikiwa kama shabiki na msikilizaji mkubwa wa nyimbo za Injili toka kwa waimbaji tofauti.
   
 4. wanakopi

  wanakopi Senior Member

  #4
  Oct 1, 2012
  Joined: Sep 30, 2012
  Messages: 109
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  duuuh uyo ni mnyaki
   
 5. Scofied

  Scofied JF-Expert Member

  #5
  Oct 1, 2012
  Joined: Jun 5, 2012
  Messages: 2,017
  Likes Received: 197
  Trophy Points: 160
  mkuu mwisho wa siku anahimiza pamoja na hayo yote tunatakiwa tutengeneze(tutubu) kwa Mungu na watu tuliowatenda pia...ni nyimbo nzuri inamafunzo na kwa hili nampongeza sana bahati...kwa maudhui huwezi mlinganisha bahati na Rozi mhando...bahati anajitahidi sana...
   
 6. v

  valid statement JF-Expert Member

  #6
  Oct 1, 2012
  Joined: Sep 18, 2011
  Messages: 2,737
  Likes Received: 176
  Trophy Points: 160
  Umemaliza kabisa. Mengi aliyoyaimba katika wimbo huu ni ya kufikirika katika nadharia tu.
   
 7. hasason

  hasason JF-Expert Member

  #7
  Oct 1, 2012
  Joined: Sep 19, 2012
  Messages: 1,558
  Likes Received: 792
  Trophy Points: 280
  these are other types of blessing notes!
   
 8. Imany John

  Imany John Verified User

  #8
  Oct 2, 2012
  Joined: Jul 30, 2011
  Messages: 2,776
  Likes Received: 262
  Trophy Points: 180
  Gud say,uwo umetoa uchambuzi wako na mimi pia wala sikatai,je messagewise unauonaje je hadhira inachakujifunza?
   
 9. Imany John

  Imany John Verified User

  #9
  Oct 2, 2012
  Joined: Jul 30, 2011
  Messages: 2,776
  Likes Received: 262
  Trophy Points: 180
  Mbona hauweki nyama za kutosha hapa katika komenti yako? Zakidunia kwa namna ipi?
   
 10. Imany John

  Imany John Verified User

  #10
  Oct 2, 2012
  Joined: Jul 30, 2011
  Messages: 2,776
  Likes Received: 262
  Trophy Points: 180
  We kiongozi mtata,katika sehemu ya mtoto kucharangwa mapanga hatamimi najiuliza sana,ila hisia zinanituma kuwa alichukua aidia ya kuzaliwa kwa mtume MUSA,na kukua kwake.
   
 11. m

  mbano Member

  #11
  Oct 2, 2012
  Joined: Sep 9, 2011
  Messages: 46
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Huyoo nae Bukuku mie nilishamtoa kwenye orodha ya waimba nyimbo za injili baada ya kusikia yeye na Mheshimiwa EL kijana ya Richmond wana mambo yaleeeee kwa sita kwa sita.
  nikajitoa kwenye kundi la masahabiki wake.
   
 12. satellite

  satellite JF-Expert Member

  #12
  Oct 4, 2012
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 603
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Tupia link ya wimbo basi tupate kuusikiliza
   
 13. N

  NAJIAMINI New Member

  #13
  Oct 7, 2012
  Joined: Aug 11, 2012
  Messages: 3
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  uwekwni humu basi tuusikilize au tuuone
   
Loading...