Dunia haieleweki, maisha hayaeleweki

Dunia haieleweki, maisha hayaeleweki

Jeremiah Stephin

Senior Member
Joined
Feb 6, 2014
Posts
123
Reaction score
137
1. Maisha ya kwenye Ndoto ukiwa umesinzia si halisi,ila utagundua si halisi pale utakapo zinduka kutoka usingizini.Ndoto ni Illusional..unadanganywa.

2. Video games kama zile za FIFA,GTA n.k wahusika wa kwenye zile games mfano unacheza PS5 kuna muda wachezaji wanalalamika,wanaumia,wanahuzunika na Kushangilia ila hawajui kwamba kila wanachokifanya ni Program,wao ni program ya computer inayo chezeshwa na binadamu.

3. Kwa Kuzingatia 1 na 2 hapo juu nashawishika kwamba hata sisi binadamu na viumbe wengine kwenye huu ulimwengu Tunaishi maisha yasiyo na uhalisia..tunaishi maisha danganyifu kama wale wachezaji wa kwenye PS au yale maisha ya ndoto.

4. Kila tunachokiona sio halisi(illusional) na maisha yote ni kama simulation za games..Sisi tupo kwenye Program inayoendeshwa na aliyeiunda.Maisha yetu ni program ndio maana hayaeleweki.

5. Tunazaliwa Then Tunakufa bila kujua hata lengo la kuwepo duniani ni lipi(achana na falsafa za dini).Magonjwa,Vita na kila uharibifu unaofanyika ni sehemu ya simulation za mcheza game..

6. Mwisho wa haya maisha ni pale anayetuchezesha Game Akiacha kucheza au akashindwa kuendesha program yake vizuri. #Ongeza na wewe
7.
8.
 
Ukitumia hoja yake ya 1 na 2 kama kueleleza kielelezo cha maisha yetu ndugu itakuwa umepotea sana!, vipo vitu vingi sana tunatofautiana na huo ulimwengu unaojaribu kuulezea!. ni ulimwengu usiokuwa na hisia na si halisia!. maisha yetu halisi yamegubikwa na kanuni zake ambazo ukizivunja utavunjika ama zitakudhuru moja kwa moja!.. mfano katuni kwenye game hawezi kula na wala sio shida zake na wala hapambanii kuishi!!.
Kiufupi niseme umetumia mfano mbaya sana katika kuangalia uhalisia wetu!.

Kutoyaelewa maisha haimanishi ya kwamba tupo program vilevile kuyaelewa maisha haimanishi tuwe au tusiwe kwenye program!.
yani kuwa program ama kutokuwa yote yanawezekana!, sema bado hatuna majibu ndio tunaweza kuchagua jibu lolote ila sio kwamba jibu halipo ni vile hatujalivumbua tu!.

Nadharia yako ya kuwa tunachezeshwa unaweza kuithibitisha ama unafuata hisia zako ktk kuwaza tu..?
 
Human beings are trapped in illusional World
Everything we experience through the senses appears real… yet it ...
 
hakuna illusionary (udanganyifu), kila kitu ni halisi katika mtazamo wa kitu chenyewe. hakuna anaetuchezesha ila ni ufahamu wenyewe unaojichezesha. kwa macho ya kawaida inaonekana kua sisi tupo, ila kiuhalisia hatupo na hata ulimwengu wenyewe haupo ila ni ufahamu unaojionyesha katika miili tofauti na hii ni kwa sababu kitu pekee ambacho kinaweza kua, ni ufahamu tu
 
Back
Top Bottom