Dullah Planet kuwa makini, Sepenga anakuharibia show

Ziroseventytwo

JF-Expert Member
Mar 27, 2011
6,725
2,000
Napendaga kuangalia friday night live show inayorushwa na East Africa TV na East Africa Radio na host wa show ni Dullah Planet. Sasa kuna jamaa yake wanakuwaga wote kwenye show. Huyu jamaa nadhani anaitwa Sepenga. Jamaa ni mshamba sana.

Kwanza sijui kama ni maarufu. Na kama ni maarufu sijui kaupata wapi. Pamoja na kuwa kwenye show na dullah kwa muda sasa jamaa bado tu hajaizoea camera. Anapenda kuonekana yeye kuliko hata wageni wanaokuja pale kwa ajili kuleta video zao mpya. Anaingilia sana maelezo ambayo mgeni anakuwa anayatoa. Kwa kifupi anamkatishakatisha wakati akiongea kwa maswali ya kibwege kabisa.

Kwa kifupi mle ndani jamaa anavyofanyafanya ni mambo ya kiduanzi. Dulla huyo mduanzi Sepenga usipokuwa makini atakuharibia kipindi. Kama vp mpige chini. Maana hana anachoongeza kwako. Zaidi sana anakuharibia.

Mpige chini.
 

Chen Hu

JF-Expert Member
Mar 27, 2012
4,318
2,000
Sio ataharibu shoo, sema ameharibu sho. Jamaa mpiga malele utafikiri wanaokunywa pombe ya kienyeji ambayo ukifika bandani mama muuza anakuja kukufunga suruali.
Yaani jamaa hana mpangilio wa kuongea, ana bwatuka bwatuka tu.
Halafu wenzangu mnamwonaje? Mbona kama
 

Its Pancho

JF-Expert Member
Sep 21, 2018
10,069
2,000
Nye nye nye" in sepenga voice.
Screenshot_20210709-210354.jpg
 

CHIZI VITABU

JF-Expert Member
Jun 12, 2021
940
1,000
Kwa waenda club maisha miaka hiyo mtakumbuka huyo chawa hadi ma-mende wakawa wanafanya yao kisa tamaaa,ghafla akawa mbeba pochi wa wema sepetu kipindi kile yuko juu akaanza kujiita bill sepetu siku hizi anairemba eti sepenga,yaaani kazi za media zimekuwa za kijinga sana
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom