Salama Jabir "Ecejay"

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,016
9,885
Salama Jabiri "Ecejay"

Nilimfahamia kwenye kipindi cha Planet Bongo ambacho kiliurithi moto wa Hip Hop Base HOP kutoka kwa mwana Hip Hop, Saigon ambaye alikifanya kwa namna ya tofauti, kisha Salama akakiacha kwenye mikono ya Abdallah Khamis Ambua " Dulla Planet" ambaye naye akakibadilisha na kukifanya kwa namna yake mpaka kupewa wiki nzima (Jumatatu mpaka Ijumaa).

Akiwa hapohapo East Africa TV, alipita kwenye kipindi kiitwacho Friday Night Live (FNL) ambacho kilitupa ladha za watangazaji wengine kama Ssebo, Jimmy Kabwe (JK), Sam Misago, na wengineo.

Akatemana na utangazaji na kuendelea na mishe nyingine lakini baadaye akakaa chimbo na AY na Josh na kuibuka na kipindi maarufu cha Mahojiano kilichoitwa Mkasi.

Akaibuka na segment ya kuzungumzia kabumbu na baada ya hapo akaibuka na Salama na.

Salama alisifika sana kwa ukosoaji wa videos na nakumbuka mwaka 2006 alimchana QJ kwenye ngoma yake ya Sifai kuwa alivaa tisheti ya mikono mifupi na kuonesha kiwiko ambacho kilipauka.

Videos nyingi zilipitiwa na alikumbana na misukosuko MINGI. Bila shaka, ukiniambia nikutajie mtu ambaye amekuza thamani ya videos za Muziki wetu basi nitasema ni Salama.

Nilikuwa nikisikia tu kuwa kuna "mmama" wa kizungu ambaye Salama anamgeza kuanzia uvaaji na mtindo wake mzima wa maisha wa kujiweka kama mwanaume. Nikajua ni kamba tu, nilipomwona Ellen Degeneres kwenye kipindi chake kiitwacho The hellen Show ndipo nilipoamini kwamba kila mtu ana anayefanana naye kwenye dunia hii.

Salama amesikika kwenye intro ya wimbo wa Jay Moe unaoitwa Tutakukumbuka, wimbo ambao Moe aliuandika baada ya kifo cha Mutie Rodney Abraham Mengi.

Salama alisikika kwenye intro ya Agost 13 ya Fid Q na nilimsikia Fid akisema kwamba Majani alimzingua sana kwamba inakuwaje anawapeleka watu ambao ni "Miyeyusho" studioni lakini Fid akasisitiza kuwa angefanya kitu poa, Majani akakata kamba na Salama akafanya alichokifanya.

Salama aliwahi kushindanishwa na Fatma Hassan "Fetylicious, DJ Fetty" wa Clouds FM lakini wawili hao hawakuwahi kulumbana na zaidi ni " wana" Ila kiukweli wawili hawa walielekeana kwa vingi; jinsia, maumbo, vionjo vyao vya kipekee wakiwa hewani, maswali chokozi na chonganishi na uchangamfu wakiwa nyuma ya mic. Nilitamani sana kuwasikia wakitangaza pamoja.

Akimhoji Adam Mchomvu, Salama alisema alifuatwa na Ruge ili ahamie Clouds lakini alipotaja dau alilolitaka, wakashindwana.

KALI ZA KUSISIMUA KUHUSU SALAMA
1. Kutekwa na Kikosi (Pina) kwa sababu ya kuponda video yao, halafu akanyolewa nywele na kushindwa kutokea kwenye kipindi. Je ilikuwa kweli hii?

2. Kuwa na mtoto na kumficha Sauzi. Je ni kweli hii??

3. Salama ni shabiki wa timu "nyekundu" hivyo umeshajua kwa wale pacha wa Kariakoo, anashabikia timu gani.

4. Salama alidaiwa kuwa aliwahi kutoka na Fid. Wengine walidai Salama alimtoa Fid nishai kwa ule mwonekano wake wa zamani na ndiye aliyechochea Fid kubadilika, lakini pia Salama alimponda Ngosha kuwa alivaa mguo wa kulalia kwenye video ya Hapo vipi ya Prof. Jay, Je ni kweli? Lakini Nikki Mbishi ana line inayosema, "Mkasi haukukata rasta za kubanda " Kuna uhusiano na nilichokiuliza.

5. SALAMA aliiponda Bongo Star Search kwa kila kitu. Madam Ritha Paulsen akapata habari hiyo na kukutana na Salama akiwa amefura kama mbogo.

Walipokutana, Salama akabaki na msimamo wake na kumpa ramani nzima Ritha ya namna ambavyo BSS ilitakiwa kuwa.

Ritha akafurahi na kumpa shavu Salama na kuanzia hapo Salama amekuwa jaji wa mashindano hayo ya kuibua vipaji mpaka leo.

Usiogope kukosoa kwa kuogopa kukosea, usiogope kukosoa unapoona upo sahihi, unaweza kuinuka kwa ukosoaji wako.

Napenda Kiswahili chenye marashi ya Zenji, napenda Kiingereza chake, napenda " kauli kubwa" anazozitoa akivurigwa, napenda vile anavyoonesha hisia zake halisi pasipo kujali utajisikiaje. Napenda vile alivyo.

Napenda namna alivyoulinda mwonekano wake na kuonekana "Forever Young"

Nampenda Salama.

Una kipi cha kusema kuhusu Salama?
1678090616717.jpeg

1678090628958.jpeg

1678090640730.jpeg
 
The Ellen Show ni kipindi cha WATOTO!!?
Hebu rekebisha kwanza hapo ili tuendelee na mengine...

Kuhusu Salama kutekwa na Kikosi cha Mizinga uongo,
Salama kudate na Fid Q uongo mengine sijui zaidi,

Nampenda jinsi alivyo real hajui kufake,
Nampenda anavyoshikilia Misimamo yake,
Sio Mtu rahisi kua rafiki yake lakini once akikukubali ni rafiki mzuri sana ambaye huwezi kutamani kumkosa,

Salama ana mchango mkubwa sana kwenye sanaa ya bongo hasa upande wa video, aliwahi kumchana 20% kwenye video ya wimbo wake kisa aliacha kifua wazi wakati ana kifua na tumbo baya

Aliwahi pia kua na kipindi cha Ngazi kwa Ngazi ambacho aliwaachia wasanii wakiendeshe na kuchagua nyimbo zao 10 wazipendazo na kuzipiga,

Hivi ni wapi naweza kupata vile vipindi vya mwanzo kabisa alivyokua anatangaza eatv bonga na salama kitu kama hicho.
 
Napokea Dr. Mariposa ,
 
Salama anafanya vitu vingi incomplete maana huwa hawezi kufabya kitu Hadi amalize yaani ni mwepesi saana wa kuishia njiani kwenye mchongo wake.

Ukianzia Planet Bongo Hadi Mkasi na vinginevyo vingi huwa vinaishia njiani.
 
The Hellen Show sio kipindi cha watoto .
Sioni la zaidi juu ya Salama ila nachoweza kusema alivyo Salama kihisia na kimsimamo ni vitu ambavyo kila mtanzania inabidi kujielewa na kujisimamia sio kuwa bendera fuata upepo .

Issue ya kuwa na mtoto aliyefichwa South Africa sio kweli sababu nilimjua Salama akiwa binti kabla ya leo katika historia na stori za maisha yake hakuwahi kunieleza hayo na pia ningejua maana sikumjulia Tanzania ila huko wanakosema alikuwa na mtoto sikuwahi kumuona na mtoto wa kuficha popote pale.

Salama ni aina ya binti ambaye baadhi ya wanaume wanatakiwa kujifunza kwake juu ya nini maana ya msimamo.
 
Only kama huo msimamo unakupa mkate.
Walamba nyayo wa kibongo hawapendi ila ndio vile hawana " uwezo" tofauti na kulamba Nyayo.
 
Salama anafanya vitu vingi incomplete maana huwa hawezi kufabya kitu Hadi amalize yaani ni mwepesi saana wa kuishia njiani kwenye mchongo wake.

Ukianzia Planet Bongo Hadi Mkasi na vinginevyo vingi huwa vinaishia njiani.
Huo ni mwisho sio vinaishia njiani, she is creative, huwezi ukafanya jambo moja muda mrefu watu watakuchoka, hata juzi kuna mtu alilalamika kuhusu hili,Salama akamjibu kama anapenda Mkasi basi atazame Mkasi vipindi vilivofuata aache

Sent from my TECNO KA7 using JamiiForums mobile app
 
Salama hata wanaokaa nae wanajua she's getting bored easily. Yaani akifanya kitu anakuwa bored easily afu anaanzisha kitu kingine tena.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom