Dulla Makabila: Moyo wangu nahisi unawaka moto naumia sana sitaki tena mapenzi wala mahusiano sitaki

Gentlemen_

JF-Expert Member
Nov 24, 2019
3,563
10,548
Sina Maneno meengi

Mkiambiwa huwa HAMSIKIII..

=====

Mtu yeyote atakaekuja kuniskia nasema nampenda mwanamke yeyote basi mtu uyo kama nipo naye karibu yani uso kwa uso basi naruhusu anipige ata kofi sababu nimegundua mwanamke sio mtu wakumuamini ata kidogo.

Haijalishi atakuaminisha kiasi gani nafikili muda niliobaki nao ni bora nikautumia kupambania maisha yangu na kuhakikisha nakuwa na hela zaidi ya hapa ila sidhani kama ni sahihi kuwekeza tena hisia zangu kwa mwanamke yeyote yule tena uwenda ikawa nilichelewa kuligundua hili ila sasa nimeelewa.

Sio kama nimeamua hivi kwa hasira hapana ila ni kwa sababu kwenye maisha yangu alibakia mwanamke mmoja tu wa kumuamini mwanamke ambae niliamini atakuwa kwaajiri yangu tu na sio mtu mwengine ata kama tutapitia situation yeyote ambayo itampush kufanya kitu tofauti niliamini hawezi kuniumiza na hatokuja kuweza ila kama yeye kaweza basi hakuna ambae atashindwa.

Maana yeye ndo alikuwa wa mwisho kumuamini katika maisha yangu 😭😭

Nimeumizwa nimeumizwa niseme nimeumia sana hii sio kiki wala trending za mitandaoni ni maisha halisi kiukweli napitia kipindi kigumu sana nakumbuka @hassanmwakinyojr Aliwahi kuniambia mapenzi kwake ameyapa 5% tena ata izo 5 bado anaziona nyingi.

Ila naamini sasa ata akinipigia simu tutakuwa tunaongea lugha moja moyo wangu nahisi unawa moto naumia sana sitaki tena mapenzi wala mahusiano sitaki sitaki sitaki sitaki tena 🙌🙌😭😭😭😭

Another Satisfied Customer 😌

Screenshot_20230918-160546.png
 
Back
Top Bottom