Duh! Wapinzani wake wote wamegonga mwamba!

Duh! Wapinzani wake wote wamegonga mwamba!

Setfree

JF-Expert Member
Joined
Dec 25, 2024
Posts
6,104
Reaction score
8,038
Wamechallenge almost kila kitu alichosema. Wamehoji, wamefungua kesi, wamehamasisha wengine wawe wapinzani, wameleta arguments zao… wamepiga kelele.. lakini kuna statement yake moja wameshindwa kabisa kuipinga:

“Kwa maana u mavumbi wewe, nawe mavumbini utarudi.” (Mwanzo 3:19)

Ukweli ndio huo, no matter how powerful, educated or rich they may be, mwisho wa safari yao ni uleule: mwili unarudi mavumbini.

Hapo hakuna debate, hakuna escape route! Wale wanaompinga Mungu na Neno lake, kwenye hilo wamegonga mwamba. Kamwe hawawezi kuzuia kifo, hata wakila special diet au kwenda gym kila saa! Mbaya zaidi baada ya kifo ni hukumu (Ebr 9:27).
 
“Ee Bwana, Mfalme wetu, jina lako ni tukufu duniani mwote!” (Zaburi 8:1)

“Ee Bwana, ukuu ni wako, na uweza, na utukufu, na kushinda, na enzi; maana vitu vyote vilivyo mbinguni na duniani ni vyako.” (1 Mambo ya Nyakati 29:11)
 
Kwani binadamu tu ndo anakufa ? Kila kiumbe chenye uhai lazima kife ni nature
Nature yenyewe ilitoka wapi, na hizo laws za nature ziliwekwa na nani?

Ni kweli kwamba mtu anaweza kuita kifo “nature,” lakini hilo halijajibu point yangu. Mimi sijasema wanaokufa ni wanadamu tu; nazungumzia kile Mungu alichosema kuhusu hatima ya mwanadamu.

Hata kama kifo unakiita “nature,” ukweli unabaki pale pale kwamba kile Mungu alichosema kuhusu mwanadamu ndicho tunachokiona leo: mwanadamu anatoka mavumbini na anarudi mavumbini.

Kwa hiyo hoja sio kwamba “hata viumbe vingine vinakufa.” Hoja ni kwamba Mungu alitangaza mwisho wa maisha ya mwanadamu duniani ni kifo na kurudi mavumbini, na hakuna atheist aliyefanikiwa kupinga hilo.

Hiyo ndiyo maana yangu hasa kusema wapinzani wake wote wamegonga mwamba.
 
Wamechallenge almost kila kitu alichosema. Wamehoji, wamefungua kesi, wamehamasisha wengine wawe wapinzani, wameleta arguments zao… wamepiga kelele.. lakini kuna statement yake moja wameshindwa kabisa kuipinga:

“Kwa maana u mavumbi wewe, nawe mavumbini utarudi.” (Mwanzo 3:19)

Ukweli ndio huo, no matter how powerful, educated or rich they may be, mwisho wa safari yao ni uleule: mwili unarudi mavumbini.

Hapo hakuna debate, hakuna escape route! Wale wanaompinga Mungu na Neno lake, kwenye hilo wamegonga mwamba. Kamwe hawawezi kuzuia kifo, hata wakila special diet au kwenda gym kila saa! Mbaya zaidi baada ya kifo ni hukumu (Ebr 9:27).
Bab kubwa
 
Ndio, sasa hata huku mtaani sioni huyo wa kumfanya awe mke
Nilikuambia piga magoti umuombe Mungu atakupa.
Mt 7:7-8
"Ombeni, nanyi mtapewa; tafuteni, nanyi mtaona; bisheni, nanyi mtafunguliwa; kwa maana kila aombaye hupokea; naye atafutaye huona; naye abishaye atafunguliwa."
 
Davidmmarista
Hii mada vipi, bado unapekua makabrasha?

Bado sioni mantiki iliopo hapa Setfree unajitahidi mno kutumia ChatGpt lakini bila shaka logic na the way una prompt seems to vague.

Anyway hamna kiumbe hai asiyepoteza uhai. By any means uamini au usiamini wote tutapoteza uhai. Sasa sijui mantiki yako Iko wapi kwenye huu Uzi? Yaani point yako kuu ni nini hapa?
 
Ila Kuna watu 😅 anyway ndugu yangu Setfree kutokea kwa kifo hakuthibitishi uwepo wa Mungu wala ukweli wa kitabu fulani cha dini, kwa sababu kifo ni ukweli wa kiasili. Mtu kutokufa au kufa si hoja inayoweza kutumika kushinda mjadala wa kidini, kwa sababu hakuna mtu anayebisha kuwa viumbe hufa.

You got it Setfree
 
Bado sioni mantiki iliopo hapa Setfree unajitahidi mno kutumia ChatGpt lakini bila shaka logic na the way una prompt seems to vague.

Anyway hamna kiumbe hai asiyepoteza uhai. By any means uamini au usiamini wote tutapoteza uhai. Sasa sijui mantiki yako Iko wapi kwenye huu Uzi? Yaani point yako kuu ni nini hapa?
Wewe hoja zako si kila mara unasema "hakuna ushahidi"
Sasa ushahidi ndio huo: Mungu alisema "utarudi mavumbini" na hilo tunaliona likitimia hata kwa Atheists. Mimi nikifa nina tiketi ya kuingia mbinguni tayari. Kama wewe unadanganyika kwamba ukifa ndio mwisho wa maisha, basi subiri, utaona kitakachotokea ndani ya sekunde moja tu baada ya wewe kuiaga dunia. Utakumbuka nyuzi zangu na kujuta but it will be too late.
 
Davidmmarista
Hii mada vipi, bado unapekua makabrasha?
Htuwezi kujadiri Mad Isiyo na kichwa wala miguu.

Kusema Tu umetoka mvumbini na utarudi mvumbini kuna maajabu gani.

That is a fact, kwamba viumbe vinakufa, ili yeye ajione Mwamba abadiliahe huo ukweli ili watu wasiwe wanakufa ndio tutajua kweli ana nguvu hiyo.

Mfano mtu Akisema kwenye mazao ukimwagilia vizuri na kuweka mbolea utavuna mavuno mengi na mazuri, hii ni Kauli ya kupata Sifa? It's a matter of fact na haidhihirishi Ukuu wowote kwa masemaji/mtamkaji
 
That is a fact, kwamba viumbe vinakufa, ili yeye ajione Mwamba abadiliahe huo ukweli ili watu wasiwe wanakufa ndio tutajua kweli ana nguvu hiyo.
Hujui kwamba Yesu alikufa na kufufuka? Hapo tayari Yesu ameonyesha kuwa Yeye anaweza kuibadili hiyo unayodai ni nature. Yesu yuko juu ya nguvu ya mauti. Wewe jaribu ufe halafu ujifufue kama utaweza.
Halafu kama huna habari, siku ya ujio wa Yesu, waliokufa katika Kristo watafufuliwa (1 The 4:16-18)
 
Bada ya kufufuka Yuko wapi?

Habari za Yesu kufa na kufufuka zimekaa kimichongo Sana.

Nitkwambia kwanini? Habari za Yesu kuzaliwa, kufariki na kufufuka zinapatikana kwenye Biblia Pekee kana kwamba Yesu alizaliwa katika Dubai yake.
Peke yake isiyokuwa na watu wengine. Biblia ambayo nayo inatiliwa shaka kuhusu taarifa zake.

Yesu anazaliwa anakuta duniani kuna watu, watu walioishi kabla yake habari zao zimeandikwa na kuelezewa na Watu waliokuwepo, waandishi mbali mbali na vyanzo zaidi ya kimoja.

Leo hata picha ya Yesu au hata sanamu lake Tu hakuna, hakuna kumbukumbu alizaliwa lini na siku gani mwaka gani, kumejaa mabishano na Tarehe za kubuni, je Yesu alizawali hakukuta watu?

Tuje sasa wakati anafufuka watu wachache Sana tena wale wale 12 wafusi wake tu ndio walimwona, dunia nzima hakuna mtu Mwingine aliyeshuhudia, Nani atawaamini?

Tukio la kufa na kufufuka ni tukio kubwa sana, lingeandikwa na kusimuliwa kwa ufasaha kwa Vizazi vyoote.
Farida zake ni za kutilia Mashaka sana
 
Back
Top Bottom