Duh, nimeumbuka, Naomba msaada wenu!

Mtambuzi

Platinum Member
Oct 29, 2008
8,806
15,379
senene.jpg

Jana usiku mwanangu Ngina kanistukiza na swali, akitaka kujua eti Senene wanaitwaje kwa kiingereza.

Nilijifaragua, kisha nikamwambia nitamjibu baadae, hata hivyo nikamtoroka nikaenda kulala, leo alfajiri nimewahi kuondoka bila hata kumuaga, maana nilijua atanikumbusha swali lake.
Najua nikirudi jioni nitapambana na hili swali, hebu wana JF niondoleeni hii fedheha!

Najuuta kusoma shule za Ngumbaru!

Masuala gani ya kitoto wewe Mtambuzi unatueleza hapa jamvini kumgwaya mtoto wako mdogo kiasi cha kuhofu kurudi nyumbani? Wahaya utawajua tu! Ukimlea huyo mwanao kwa kutompatia majibu ya maswali yake kwa wakati ndiyo unamfunza tabia ya usanii na kuahirisha ufumbuzi wa matatizo halafu baadaye anageuka kuwa janga la jamii/taifa kama ninavyowaona hawa wengine. Toa jibu, 'sijui wadudu hao wanaitwaje' na umuahidi kumtafutia jibu sahihi. Na bado suala la ubaba wako litabaki pale pale!!
 
Acha kumfundisha mwanao usanii bana,sikupenda hii kitu.Mwambie sifaham,au sikumbuki nakutaftia jibu sahh
 
Jibu ndo hilo katoa Babu wa Loliondo.Kiingereza cha nsenene ni cricket, jina kama ule mchezo wapendao wahindi na watu wa australia. sawa sio Mtambuzi?
 
Last edited by a moderator:
great green bush-cricket, Tettigonia viridissima (Orthoptera: Tettigoniidae). What about checking that link. Nahisi picha hii inashabihiana na senene japo naona huyo ni mkubwa (labda picha imekuzwa) ila kwa umbo ni sawa na senene. Ila lazima kujua huwezi kutumia jina green as if senene wote ni wa rangi ya kijani! Wapo wa kahawia, wenye mabaka na wengine kama wekundu kwa mbali! Sasa huo ukijani unakufa na rangi?
Jibu ndo hilo katoa Babu wa Loliondo.Kiingereza cha nsenene ni cricket, jina kama ule mchezo wapendao wahindi na watu wa australia. sawa sio Mtambuzi?
 
Similar Discussions

1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom