Mawazo ya Zitto kuhusiana na issue hii:
Zitto Kabwe
Guys, how much does it cost to put a 30 seconds advert on CNN? Brazil - Stars match will be watched in 160 countries for 90 minutes. It is worth it. Sasa jamani sisi miaka 4 tunapiga kelele ufisadi ufisadi, maalbino, indecisiveness, power blackouts etc..... tuache Watanzania wafurahi japo kidogo na wao. waende Taifa kuwaona Brazil nk. Relax guys relax
Kwanza kabisa hii hela imetoka kwenye bajeti gani?
Nani kakwambia kwamba hayo matangazo ya CNN tunaafikiana nayo? Mimi naona nayo ni ufujaji wa mali ya umma tu. Huwezi kutangaza sekta ya utalii kabla ya kuwa na sekta ya utalii madhubuti.
Tanzania hakuna sekta ya utalii ya kusema, weka miundombinu, piga sabuni sehemu zinazohusika, then unaita watalii.
Sio wewe unataka kutumia $ 6 m kwa "kutangaza" Tanzania katika mechi moja, halafu ukipiga hesabu mapato ya utalii 2009 ni $ 1.35 billion. Tayari mshaondoa 0.45% ya mapato -mapato, si faida- ya utalii ya mwaka jana.
Msitake kutumia kigezo cha utalii hapa, kama mnataka kutangaza utalii tangazeni mbuga, mpira kwa nchi isiyojulikana kwa mpira kama Tanzania na utalii wapi na wapi?
There are more cost effective ways to advertise Tanzania's tourism sector, certainly not by this extravagant excuse of extracurriculum excesses.
Hawa ndio opposition wanaotaka kuchukua nchi hawa? Je wana uchungu na pesa ya nchi hawa? Au ni kama hao hao CCM B tu, wanasubiri kufika Ikulu na kuchukua serikali na kuanza kununua mirada, midege kochokocho, migari ya mibunge kila muhula, mihela mpaka iwapalie waote vitambi hata kutembea washindwe wawe wanapelekwa bungeni na mi wheelchair ya dhahabu inayosukumwa na umeme.
Wakati watu wao hata maji safi hawayajui.
Hivi Zitto wewe mbunge au si mbunge? Si umesoma uchumi wewe? Ina maana kama unaambiwa ni namna gani ya kuzitumia hizi hela in the most economic way ungeona kuleta Brazil?
Huyu atakuwa yule **** Kikwete tu mwenye kupenda mijezi jezi ya wachezaji soka na miatu atu ya NBA.Akili hamna kutwa kuwaza ngoma na michezo tu utafikiri Mkulu wa madogoli vile.Hiyo FA ya bongo hata haina hela hizo.
Hata kama unasema wewe unapenda michezo, kama hizo hela ungezipeleka katika mashule kuimarisha timu za vijana ungeweza kufanya makubwa sana.In three to five years tayari tungeona mabadiliko katika michezo yetu.
Ila kama kawaida yetui, tuko radhi kuchangia harusi kuuuuuuubwa ya siku moja, halafu baada ya harusi bwana na bibi harusi wanaenda kujibanza kwenye kibanda cha mbavu za mbwa.Ili mradi na wao waonekane kwamba wapo duniani kwa siku moja.
Tuko tayari kumlipa mgeni hela nyiiingi, wakati watu wetu wanakufa njaa.
It is ironic that the two countries Brazil will play in are Tanzania and Zimbabwe, that says a lot about our state of affairs.Ina maana tunaenda ki-Mugabe Mugabe tu, presidaa anatoa mihela kwenye state coffers, hamna anayeuliza wala kujua mpaka after the fact, $ 6 million. Akiweza kufanya hivi katika kuleta timu ya soka kipi kitamzuia kufanya hivyo hivyo na kupeleka mihela Uswizi?
Halafu wabunge wa upinzani nao wanashabikia upuuzi huu. Wabunge wasomi eti.
Pumbaf kabisa.