Dudu baya afunguka kuhusu tamko la BASATA

Hziyech22

JF-Expert Member
Jun 8, 2019
13,559
18,881
Msanii Dudu amefunguka baada ya kusikia kufungiwa mziki wake amesema sijapata wala kupokea barua yao so nitaendelea na mziki wangu Kama kawaida mpaka pale nitapopata barua yao alafu pia me sijafanya kosa lolote kwanini kuzungumzia kwangu na kukea matendo ya usagaji, ushoga na ufiraji ninaonekana nina kosa mbona Kuna watu wanavujisha video za ngono za kufanya kinyume na maumbile mitandaoni na hawachukuliwi hatua zozote na BASATA lakini me ninayekemea ninaonekana nimkosaji eti nimetukana je na wale watumishi wa Mungu wanaoongelea haya makanisani Kama mchungaji Lwakatare Napo mnazungumziaje?

Akaongezea pia ninatoa masaa 48 kwa BASATA wafungue leseni yangu ya kufanyia Sanaa la sivyo nitaenda mahakamani kuwashitaki yaani sisi wasanii tunalipia ada kila mwisho wa mwezi kwa BASATA alafu BASATA wanachojua wao ni kufungia kazi za wasanii lakini hawalindi haki za wasanii hivi karibuni Msanii mwenzangu CHIZBENZ amelalamika Kuna MEDIA moja ilikuwa inataka kumlipa elfu 50 kwenye show Cha ajabu wamekaa kimya Kama hawajui kinachoendelea lakini pia msanii Mbalamwezi amekufa kifo kibaya kwa kukatwa utumbo wake nje Cha kushangaza BASATA wameshindwa kutoa hata tamko la kinafiki kuoneshwa kuguswa na tukio Hilo.

Sasa hiv mambo ya uonyonywaji wa wasanii na media umekuwa mkubwa msanii akikataa offer ya kufanya show kwenye media ngoma zake hazipigwi inawafanya wasanii wengine wafanye show atakama hela wanaolipwa ni kidogo kuogopa kufungwa ngoma zao kupigwa redioni lakini BASATA wapo kimya.

Nini maoni yako kuhusu jibu la dudu baya kwa BASATA
 
maajabu ya Tz hayo,
huku amber rutty
penina & mwijaku
wema
sanchoka
rosa ree
mariam
nk. wapo ulaiani! huku konki afungiwe

hpa najiuliza hivi kumwambia mtu nitakupiga na kumpiga lipi ni kosa kubwa
itz shame
 
Dudubaya akaifanya hivi kweli nitaona mapinduzi kwenye mziki huu.Tatizo sheria za BASATA hazina sehemu ya kukata rufaa ,wakiamua wameamua.
 
Naona Amenza Kulegeza Sauti, Dawa Imeanza Kumuingia taratiibuu Anatafuta huruma ya Wananchi

Vishabiki vya WCb ndo Vinamshabia huyu Mibange
 
Kaongea kipi kibaya hapo?Wewe inaonyesha una vinasaba vya bunduki kwa hoja,pole.
Naona Amenza Kulegeza Sauti, Dawa Imeanza Kumuingia taratiibuu Anatafuta huruma ya Wananchi

Vishabiki vya WCb ndo Vinamshabia huyu Mibange
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom