Dubai kujenga Hotel yenye msitu wa mvua

Dubai kujenga Hotel yenye msitu wa mvua

Kwa umoja wetu bila kuogopa tuhamieni tukaijenge Dodoma iwe kama Dubai. Ukiangalia hali ya hewa ya Dodoma ni nzuri zaidi ya Dubai hivyo ipo siku Dodoma itakua kivutio cha utalii na kukuza uchumi wa nchi.
Kwa ujangwa.. Dubai ni jangwa zaidi ya Dom.
Hili la kuhamia Dodoma linaweza kuwa linaturudisha nyuma maana wengine watakuwa kama ndo wanaanza kazi kwa kununua vitanda na magodoro ilihali walishakaa kazini miaka 30 iliyopita !!!
 
Donald Trump alivyosema waafrika tunapaswa kutawaliwa ulidhani alikuwa anaropoka? Bado tuko kwenye Evolution of man, ndio maana muda WOTE tunawaza kuzaa, kula na pombe.MTU akipewa madaraka anaangalia tumbo lake, familia yake, ndugu zake,marafiki zake, CHAMA chake, kabila lake,dini yake na kisha mwisho ukoko ukibaki anaipa NCHI ile.Waafrika WOTE tunahii kasumba, bora tukubali wazungu washike nyazifa za juu serikalini kisha sisi kwakuwa bado yuko kwenye Evolution of man tushike za chini ili tunapobadilika huenda na akili ITAKUWA inakuja kichwani.

Ukitaka kuthibitisha hili angalia humu jukwaani, Kuna MTU hasomi kilichoandikwa Yeye nikupayuka anachoona kinamfaa, anasoma kichwa cha habari anaanza kuunhurumisha uharo na kupoteza maana ya Uzi NA jukwaa kwa ujumla.
 
Ivi dubai wana mafuta ....russia wana gesi na ndio inayomweka kifua mbele kwa usa..na wenzake!!!

Hao wooote hawana tanzanite..ipo tz tu!!!!

JE SISI SI TUNA GESI??? VIPI TANZANITE???? MBONA HATUFIKI HIKO??? VIPI MLIMA KILIMANJARO??? VIPI MBUGA ZA WANYAMA??? What is wrong???
Tafuta kingine cha kuwianisha na mafuta na gas lakini sio tanzanite.

Dunia inatumia 3,570,000,000 of oil gallons per second.

Marekani pekee inatumia average of about 384.74 million gallons ya gas per day

Tanzanite wanavaa wangapi shingoni kwa siku?
 
Safari ni hatua. Ukiona hatua za kitanzania huziwezi, hamia huko Dubai. Usitukatishe tamaa tunaojaribu kujikwamua humu humu Tz

Acha ujinga basi na wewe ....sio lazima kuchangia kila post.. Zingine tumia kujifunza na kupata munkari wa kujiongeza. Hatua ipi hiyo ya zaidi ya miaka 50? Hatua ipi hiyo mpaka leo tumeshindwa kupambana na kipindupindu,malaria nk? Hatua ipi hiyo wanafunzi wanasomea nje huku wanakaa chini. Hata kama ni mapenzi mara zingine tumia akili.
 
Mimi mbona kama sijaelewa? Msitu wa mvua ukoje? Nielewesheni kidogo!
 
Tanganyika ina laana ya kuvamia Zanzibar 1964 na kuuwa watu wasio na hatia kwa maelfu. Ni wakati wa kuwaachia wawe huru , tuwaombe msamaha tuishi maisha ya furahaya kusaidiana na ya ushindani wa kibiashara. Bila hivyo laana itaendelea kutula mpaka kiama
Na bado tunaongeza laana ya kung'ang'ania madaraka katika Zanzibar yao, lkn laana hii inatuumiza sisi walala hoi.
 
Na bado tunaongeza laana ya kung'ang'ania madaraka katika Zanzibar yao, lkn laana hii inatuumiza sisi walala hoi.


Na wao wanaumia huoni namna wanavyolindwa na majeshi kama vile gaidi ??? MJI UMEWASHINDA WANAKIMBILIA PORINI
 
halafu wale twiga wetu ndo watakuwa wanakaa huko.nshashtuka. jamaa wana endelea kuprove kwamba KAZI YA KICHWA SIO KUFUGIA NYWELE
 

Attachments

  • indexss.jpg
    indexss.jpg
    6.8 KB · Views: 41
  • sss.jpg
    sss.jpg
    5.2 KB · Views: 55
Hiyo nayo ni point mkuu. Ila Dom napo patajengwa airport kubwa itakahoweza accomodate ndege kubwa kama za Emirates na Qatar airways. Wale waarabu weupe tu hawatushindi.. Wenyewe wana mafuta sisi tuna gas, dhahabu, almas, tanzanite, mbuga za wanyama nzuri na za kuvutia.. Mlima kilimanjaro, n.k


Mmmmh, ilikuwa Kigoma kama Dubai sasa ni Dodoma kama Dubai. Nafikiri bado hatujaamua Mkuu, ila Tunaweza tukiamua kuipita Kenya, Rwanda then Ethiopia......... South Africa na baada ya hapo ndo Dubai
 
Kupatikana maji safi kila kijiji shida seuze makubwa haya....hebu niendelee kuvuta shuka mie, ukiwaka moto mnistue niokoe uhai wangu manake usingizi mzito mno...


Huo ukungu sio hatarishi kwa afya lakini?..
 
Sisi tumeambiwa tufyatue tu,ha ha ha haaaaaaaaa
 
Back
Top Bottom