Kete Ngumu
JF-Expert Member
- Nov 21, 2014
- 6,661
- 6,909
Hata tuhamishiwe Dubai Watanzania wooote na wao Waarabu waje huku, tutabakia hapo tulipoikuta Dubai huku wao wakitumia rasilimali zilizopo kuijenga Tanzania yao mpaka Tanzania ikue na kuizidi Dubai huku tukijiuliza tena hivi sisi tupo karne ya ngapi na Dubai yetu embuona Tanzania inavyoongoza kwa majengo marefu duniani. Ulevi wa kisiasa ndio maendeleo yetu, tumebakia kupiga domo na kuwindana ktk lingo za kisiasa nani kasema nini na nani ashughulikiwe. Majizi yanalindana humo kwa humo yakijilimbikizia mali na familia zao bila kujali binadamu wenzao. Elimu imenyimwa mbolea haikui na sio kipaumbele, mitahala ya elimu ni butu sana inazalisha wanaoitwa vilaza lakini wapo vyuoni. Dubai haijengwi kwa kutunishiana mishuli baina ya chama tawala na upinzani, haijengwi ktk majukwaa ya siasa wala kwa maneno ya kwenye kanga. Tubakie kuwa watizamaji maana wote tukiwa wajenzi wa miji mikubwa tutashindwa kuheshimiana.