Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 20,925
- 30,273
DUA YA MUHAMMAD ALI KINSHASA 1974
Kwenye kitabu cha maisha yake, "The Greatest My Own Story," Ali anaeleza vipi mzee mmoja kutoka Cuba mchuaji wake misuli alivyokuwa anamnanga kuhusu yeye kujiita, "The Greatest."
Akimwambia kama kweli wewe ni Greatest mpige Foreman siyo ajisifu kwa kumpiga Sonny Liston aliyekuwa kachoka anasubiri mtu atokee ampige.
"Foreman ni simba ndani ya tundu na nyama yake anakula. Ingia ndani ya tundu lake mpore hiyo nyama kama kweli wewe ni Greatest.
Ukiliweza hilo ulimwengu mzima utakutambua kweli wewe ni Greatest. "
Ali alimleta kambini kwake mtu mmoja anaitwa Bossman.
Huyu alipatakuwa "sparring partner," wa Foreman. Katika kitabu kampa sura nzima: "Bossman Comes."
Alisubiriwa kwa hamu kubwa.
Alipowasili Ali na timu yake akiwepo kocha wake Angelo Dundee na Drew Bundini na handlers wakenda faragha.
Ali akamuuliza Bossman amueleze kwa ukweli wa nafsi yake. "Bossman niambie kweli ikiwa leo nitapigana na Foreman nani atapigwa?"
"Utapigwa wewe."
"Toka, toka ondoka hapa msaliti mkubwa wewe."
Bundini kaghadhibika.
Ali akamtuliza Bundini.
"Nimemuuliza swali kwa ukweli na Bossman kajibu kwa ukweli wa nafsi yake.
"Sasa Bossman nataka unifundishe kila kitu unachokijua vipi Foreman anavyopigana."
Kuna mengi sana katika sura hii siwezi kueleza yote. Lakini Ali anasema silaha yake kubwa iliyomwangusha Foreman ni stamina.
Ali alijitayarisha kwa kupigana raundi 30 akiwatumia sparring partner watatu.
Katikati ya pambano mtangazaji alimuuliza Joe Frazier anaonaje pambano linavyokwenda?
Frazier alijibu, "Foreman hatofika mbali kwani naziona dalili za kuchoka."
Waingereza wanasema, "The rest is history."