Zanzibar 2020 Maalim, Wazanzibari na robo karne ya sanduku la kura

Mohamed Said

Verified Member
Nov 2, 2008
13,685
2,000
Naamini mmemsikia Maalim leo hii ni "final count down," tunaelekea kwenye, ‘’all systems go!’’ Chombo kinapaa angani.

Kwa upande wa pili ambao hawajaweza miaka yote kushinda uchaguzi, maneno ya Maalim ni "nightmare," jinamizi.

Wazanzibari wamechoka wanadai nchi yao na heshima yao ndani ya muungano wenye maslahi kwa Wazanzibari.

‘’Mark my words,’’ sijasema ‘’pande mbili.’’

Sababu ya kutosema ni kuwa upande mmoja unanufaika kwa kuwa maslahi yake yako vizuri.

Upande wa pili ikiwa watataka kusikilizwa lazima waje na kauli za kuwatia matumaini Wazanzibari wapiga kura.

"Zombies Strategy," waliyozoea kwao itakuwa balaa kubwa...’’the answer my friend is blowing in the wind.’’

Bob Dylan huyo.
Hii ni "protest song."

Sijui ni kitu gani lakini inanijia fikra kuwa wapigaji kura wa CCM watahama kuja upande wa pili sijajua ni kipi kinasukuma hili kwenye fikra zangu achilia mbali kuwa Maalim amepata kura upande huo taratibu miaka inavyosogea.

Maalim yuko ndani ya ‘’enemy’s camp,’’ anapumua ndani ya kambi ya adui.

Yawezeka ni hii kutaka umoja wa Wazanzibari ndiyo Maalim anafunguliwa milango
kuingia kwenye kambi ya adui zake.

Sijui kadi hii ya umoja wa Wazanzibar CCM wataichezaje kampeni zitakapoanza.
Bahati mbaya hili la umoja sijalisikia kutoka kwao.

Kitu kinachonitisha sana kila ninapowaangalia CCMZ ni kuwa wameshindwa kabisa kuamini kuwa Wazanzibari wamewakataa katika kila uchaguzi, wao wameshughulishwa na "kushinda," na kuendelea kutawala nje ya ridhaa ya Wazanzibari.

Hili ni tatizo kubwa sana na ajabu ni kuwa wao hawalioni.
Huu ni mfano wa lile pigano la George Foreman na Muhammad Ali.

Foreman akitegemea zile "rounds" zake tatu mpinzani anakuwa, "flat down and out."

Itawezekana kweli safari hii kufuta uchaguzi?
Itawezekama kweli safari hii tukawa tena na mfano wa yale yaliyotokea Pemba?

Miaka mingi baada ya ‘’Rumble in the Jungle,’’ Dr. Pacheco daktari wa Ali, walimhoji kuhusu lile pigano la Ali na Foreman, Zaire mwaka wa 1974.

Dr. Pacheco anasema ilipofika ''round'' ya 3 washabiki wa Foreman na ‘’handlers’’ wake pembeni ya ulingo walikuwa wanampigia kelele Foreman wanamwambia, ‘’George finish him off!’’ yaani, ‘’Foreman mmalize huyo!’’

Mimi katika pumziko la ile ''round,'' nikamwambia Ali, ‘’Unasikia maneno wanayomwambia Foreman?”

Ali akanijibu, ‘’Huyu mimi nampiga.’’

Mimi nikamwambia Ali, ‘’Basi mpige twende zetu nyumbani.’’

Ali akanijibu, ‘’Kuwa na subra ngoja tustarehe na huu mchezo kwanza.’’
Ali alimpiga Foreman kwenye ‘’knock out, ’’ ‘’round,’’ ya 8.

Kwa nini Foreman bondia wa kutisha aliyewapiga ‘’the best of the best,’’ kwa ‘’signature,’’ yake maarufu iliyowatisha mabondia wengi ya ‘’round’’ 3 alipigwa?

Wataalamu wa ngumi wanasema Foreman alipigwa kwa kuwa kwanza hakuwa na ‘’option,’’ hakuwa na ‘’Plan B,’’ yaani hakuwa na mpango je, ikiwa ‘’round,’’ zile 3 hazitamwangusha Ali, nini atafanya kupata ushindi?

Pili Foreman alitegemea kushinda tu akitegemea ngumi zake nzito zitamlaza Ali ‘’round,’’ ya 3 kama zilivyomlaza Joe Frazier na wenzake wengi tu.

Baada ya ‘’round’’ ya 3 Foreman, chembelecho Ali alikuwa anatembea katika barabara hakupata kuipita hata siku siku.

Foreman hakujitayarisha kwa hili.
Ali yeye alikuwa na ‘’option.’’

Ali alipanga safari ndefu ya round zaidi ya tatu ambako atahitaji stamina ya kukamilisha safari ya muda mrefu ya damu na vumbi.

CCMZ haina ‘’option,’’ ya kushinda uchaguzi ila kutumia ujanja wa miaka yote ya ‘’hatutoi, hatutoi, hatutoi,’’ na wakishangilia kwa kuwa wanajiamini kuwa uwezo huo wanao.

Kosa lililomwangamiza Foreman.

Ndiyo sababu hapasikiki lugha za kuvutia za kuleta matumaini kwa Wazanzibari ya kutaka umoja na kuangalia pale penye kasoro katika muungano patatengenezwa.

Hawana mipango ya kushinda uchaguzi kama chaguzi chama kinavyoweza kushinda kwa kuvutia wapiga kura kwa sera nzuri zinazotia wapiga kura moyo wa maendeleo.

Lugha ni kalikali za, ‘’Tutaulinda Muungano Wetu,’’ Mapinduzi Daima,’’ na mengi mengine mfano wa hayo.

Inashangaza vipi na kwa nini CCMZ haijatanabahi miaka hii yote kuwa kushindwa kwao katika sanduku la kura maana yake ni kuwa Wazanzibari wengi wameyakataa mapinduzi?
 

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
38,282
2,000
Maalim aongezewe tu ulinzi maana ku-deal na powerful individuals siku hizi kwao ndio mpango mzima wakiamini inawasaidia ingawa wanajidanganya tu.

Wenzetu hawa sasa waanaamini katika nguvu za wanasiasa badala ya nguvu ya wananchi, hivyo wanaweza kufikiri ku=deal na mtu mmoja ndio itakuwa suluhu ya kumaliza mchezo.

Wakishindwa kukushawishi uwe upande wao,basi wanakuja na Plan "B" ambayo kila mwenye akili anaielewa.
 

Mohamed Said

Verified Member
Nov 2, 2008
13,685
2,000
munajisumbua tu, hamna anaekusikilizeni
Dos,
Wapo wanaosikiliza kama hivi wewe na ukachukua tabu ya kuchangia fikra zako.
Hii inatosha sana.

Unajua uzuri wa mitandao ni kuwa kila sekunde kila nukta kuna mtu mpya anaingia na kusoma na kuanzia hapo huyo ni wako ushampata.

Mimi hakuna mtu aliyenijua kabla ya kuandika humu JF.
Leo sina la kusema na siwezi kuitoa shukurani JF.

Wewe usingenijua mimi kama si hapa barzani.
 

Proved

JF-Expert Member
Sep 10, 2018
9,107
2,000
Kinachowapa ushindi wahafidhina wa CCM huko Zanzibar ni mabavu ya dola bila kusahau figisu na fitna za Tanganyika.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom