Mbinu ya kulalia kamba: Mwakinyo Vs Tinampay sawa na Muhammad Ali Vs George Foreman

Titicomb

JF-Expert Member
Jan 27, 2012
11,306
17,772
Kaka yangu ndugu Matumla na watanzania naomba niwajulishe Hassan Mwakinyo kulalia kamba sio kosa na wala yeye sio wa kwanza.

Bondia wakubwa kadhaa wameshatumia sana hiyo mbinu lengo likiwa kuwapunguza nguvu washindani wao.
Kwa vile wanakuwa wameweka maeneo yao hatari mbali na mpinzani, basi mpinzani analazimika kutumia nguvu nyingi kwenye ngumi kujaribu kuyafikia maeneo hatari ya mpinzani wake hivyo kutumia nguvu nyingi.
Unaweza kuliona hilo round kadhaa za kati ilionesha Tinampay kuchoka kidogo.

Mbinu hii ilitumiwa pia na bondia maarufu na mkubwa sana kuwahi kutokea duniani Cassius Clay a.k.a Muhammad Ali alipo pambana na bondia mkongwe alie kuwa mkubwa na mzoefu kuliko yeye wakati wa pambano lao enzi hizo nchi Zaire au DRC ya sasa, ilikuwa mnamo tarehe 3 Oktoba 1974 mjini Kinshasa.
Pambano hilo lilienda kwa jina maarufu "Rumble in the Jungle ".


Muhammad Ali vs. George Foreman
Muhammad Ali appeared to be in way over his head when he got in the ring with George Foreman in 1974.
The fight in Kinshasa, Zaire, was a strange one. It featured explosive knockout power against an aging former champion who no longer appeared to have great skills.

Ali's charismatic personality made him a great favorite of the African fans, and they chanted his name everywhere Ali went.

On fight night, Ali appeared to have a curious strategy. He let the powerful Foreman whale away at him while he leaned on the ropes (source: Boxrec.com). While it looked like Ali was getting pummeled, he was leaning back on the ropes, and that took away much of the power in Foreman's punches.

Ali knew that his opponent had tired himself out. In the eighth round, Ali let loose with a series of lefts and rights, and the seemingly indestructible Foreman went down and was counted out.
Ali had regained his championship with the come-from-behind knockout.

Picha za pambano la Muhammad Ali dhidi ya George Foreman mwaka 1974
Ali-foreman-zaire-620x422.jpg

foreman-ali-zaire-ropes-3-crop-paint-4-620x460.jpg



#TUSIKARIRI _MAMBO
#TUACHE_WIVU_KWA_WALIOFANIKIWA
#TUSIINGIZE_SIASA_KWENYE_MICHEZO

BIG UP HASSAN MWAKINYO, UMETUWAKILISHA!
 
Kwa hiyo kwa akili yako unaona kuwa Rashid anamwonea wivu Hassan?
Hiyo ni mbinu lakin Ukweli dogo ana la kuimprove bhana Mwakinyo lazima aimprove maana akicheza kama alivyocheza na mabondia wakubwa atatapika malopa
 
Kwa hiyo kwa akili yako unaona kuwa Rashid anamwonea wivu Hassan?
Hiyo ni mbinu lakin Ukweli dogo ana la kuimprove bhana Mwakinyo lazima aimprove maana akicheza kama alivyocheza na mabondia wakubwa atatapika malopa
Kosa kubwa la Matumla ni kujaribu kupendekeza Mwakinyo atafute Mwalimu mwingine kwamba yule mwalimu wake sio mzuri.
 
Kwasababu watu waliona kapigwa ila walishangaa kuona majaji walimpa ushindi.
Fuatilia huommpambano nilio linganisha utaona kitu hicho hicho.
Kushambuliwa sana sio kupigwa ngumi za point.
 
Jiulize kwanini zinatumika nguvu nyingi kujaribu kupinga ushindi wake aliopewa na majaji?
ni Tanzania tu vinatokea vitu kinyume km hivi, Mwakinyo kapigwa sasa kwa vile alishaandaliwa Tamasha na Mkuu wake wa Mkoa kaja badala ya PM basi apewe vipoint
mwambienii aende akarudiane na Tinampey tena
kwa Mwendo huu wa bila mazoezi na Mwl mzuri HASHINDI TENA pambano lingine tupo hapahapa JF
 
Mwendo huu wa bila mazoezi na Mwl mzuri HASHINDI TENA pambano lingine tupo hapahapa JF
Weka akiba ya maneno, utakuja kuyakana maneno yako kwa aibu siku moja, tena sio muda mrefu.
 
Weka akiba ya maneno, utakuja kuyakana maneno yako kwa aibu siku moja, tena sio muda mrefu.
nimewasikiliza usiku huu sasa hivi Azam tv Mwakinyo, Kocha wake na pia Matumla pale hatuna Bondia
acha ushabiki wa namna hiyo jamaa yangu, bora hata yule Bondia wa Manzese atafika mbali
 
Tuombe iwe hivyo nitafurahia pia.
Mfaume Mfaume anatupa mawe mazito hasa left sijajua uzito wake na km wanaweza pambanishwa na Mwakinyo, Kiduku naye ni Mashine sema support hawana Govt ingesaidia tuwe na wengi
 
VAR HAINA USHAHIDI KAMA KAMARI
SO MSAHAU KULALAMIKIA USHINDI WAKE VAR ISJASEMA MSHINDI YEYE TOP
 
Matumla hakua akizungumza kwa chuki, Alizungumza kwa Weredi wa hali ya juu, Matumla anauzoefu mkubwa sana kuliko Makwinyo, Matumla ameibeba bendera ya Tanzania maranyingi na ilifanya vizuri , Matumla katika Ngumi za kulipwa pekee amepigana zaidi ya mara 70 na kushinda zaidi ya mara 40 na alipoteza 19 katika ngumi za kulipwa kuifikia iyo rekodi Makwinyo anahitaji usimamizi Mzuri na Nidhamu ya haliya juu.
Matumla ameanza kupigana Ngumi za ridhaa kwa muda kabla ya professional boxing. Ata yeye Matumla ali wai kukutana na halikama ile ya kukutana na mpinzani mwenye uwezo na sugu alikutana nayo mwaka 1996 wakati anapigana na David Potsane wa South Africa,
Sidhani kama kuna mtanzania aliyekua akifuatilia ngumi atakua amesha sahau kuhusu lile pambano pale Diamond Jubilee.
Baadhi ya watanzania tuliamini pambano lile Alipigwa ila majaji walimpa ushindi Rashid Matumla wakati uo Familia ya Malinzi ndio ilikua ikimdhamini Matumla.

Alichosema Matumla ni kweli, kwa namna Makwinyo alivyocheza lile pambano hakua amejiandaa kulingana na ubora aliokua nao mpinzani wake. Matumla alipendekeza ili bondia Makwinyo aimarike na acheze katika viwango bora kambi yake inahitaji waalimu wa ziada kumwongezea ujuzi na mbinu za kisasa.

Tuache unafiki kama tunahitaji Makwinyo afanikiwe yeye na kambi yake waelezwe wanahitaji msaada na lile pambano Makwinyo alishinda kwakua alikua nyumbani ata yeye makwinyo analijua ilo, Round ya 9 na 10 ata mimi sikujua alizimaliza vip Miguu ya Makwinyo ilionyesha tayari imelegea wakati kile kibabu/ Tinampey kilikua bado kiko fiti.
Makwinyo unabahati mbaya haku kubahatika kumuona Rashid akicheza ngumi, Atayeye Makwinyo japo amefanya vizuri mbaka sasa ila haujafikia kipaji/uwezo aliokua nao Rashidi au mdogowake Mbwana Matumla.
Awa jamaa kama wangepata watuwa kuwasimamia vizuri katika ngumi au wangekua marekani basi wangeacha historia kubwa duniani katika Ngumi. Ata Mambeya Bakari aliyekua bondia mzuri kutokea Tanga analifahamu ilo.
 
Back
Top Bottom