Droo ya Hatua ya Makundi CAF: Yanga yapangwa na TP Mazembe, Simba wapangwa na Raja Casablanca

Greatest Of All Time

JF-Expert Member
Jan 1, 2017
20,722
45,126
Wawakilishi wa Tanzania katika michuano ya ligi ya mabingwa pamoja na shirikisho Africa, Simba na Yanga mchana huu watakuwa wakifuatilia droo ambapo makundi yatapangwa.

Droo hii itaanza saa 8:00 kwa masaa ya hapa nyumbani. Hivyo karibu jukwaani ujue nani kapangwa na nani?

Droo itakuwa live kupitia AzamTv chaneli namba 106 na DStv kupitia chaneli namba 229.

Nafikiri na YouTube kwenye account rasmi ya CAF.

===

KOMBE LA SHIRIKISHO
GROUP A
USMA (ALG)
M. GALLANTS (RSA)
AL AKHDER (LBY)
ST. ELOI LUPOPO (RDC)

GROUP B
ASEC MIMOSAS (CIV)
DIABLES NOIRS (CGO)
RIVERS UTD FC (NGR)
DC M. PEMBE (RDC)

GROUP C
PYRAMIDS FC (EGY)
ASKO DE KARA (TGO)
FUTURE FC (EGY)
ASFAR (MAR)

GROUP D
MAZEMBE (RDC)
US MONASTIR (TUN)
Y. AFRICANS (TAN)
REAL BAMAKO (MLI)


Shirikisho la Soka la Afrika (CAF) limekamilisha droo ya Hatua ya Makundi ya Kombe la Shirikisho, Yanga ya Tanzania ikiwa Kundi D pamoja na US Monastir ya Tunisia, TP Mazembe ya DRC na Real Bamako ya Mali.

Kuna jumla ya makundi manne yaliyopangwa ambapo michezo ya Hatua ya Makundi inatarajiwa kuanza Februari 2, 2023 na kuendelea hadi Aprili 2, 2022.

LIGI YA MABINGWA
GROUP A
W.A.C (MAR)
A. PETROLEOS (ANG)
JS KABYLIE (ALG)
AS VITA CLUB (RDC)

GROUP B
AHLY SC (EGY)
M.SUNDOWNS (RSA)
O EL HILAL (SUD)
COTON SPORT (CMR)

GROUP C
RAJA C.A (MAR)
HOROYA A.C (GUI)
SIMBA SC (TAN)
VIPERS SC (UGA)

GROUP D
E.S.T (TUN)
ZAMALEK SC (EGY)
CR BELOUIZDAD (ALGI
AL MERRIKH (SUD)
 
saa kumi na mbili jioni ni droo ya shirikisho na saa moja usiku n droo ya club bingwa
 
Tuendelee kusubiri timu zetu zinapangwa na nani maana zoezi liko linaendelea
 
Back
Top Bottom