NALIA NGWENA
JF-Expert Member
- Oct 6, 2016
- 10,206
- 12,747
Timu za Simba na Yanga zitawajua wapinzani wao katika makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika kupitia droo itakayochezeshwa leo jijini Johannesburg, Afrika Kusini.
Droo za hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa na Kombe la Shirikisho Afrika inachezeshwa leo saa 9:00 alasiri kwa saa za Afrika Kusini na saa 10:00 jioni kwa saa za Tanzania.
Hatua hii ya droo ni baada ya timu zote kufanya vizuri kwenye hatua ya awali katika mashindano yote (Ligi ya Mabingwa na Kombe la Shirikisho Afrika) isipokuwa mabingwa Al Ahly (Ligi ya Mabingwa) na USM Alger (Shirikisho) wakianzia katika makundi.
Kitendo cha Simba na Yanga kuwekwa katika vyungu tofauti katika zoezi la upangaji wa makundi, linazua uwezekano mkubwa wa wawakilishi hao wa Tanzania kukutana katika hatua hiyo msimu huu.
Kwa mujibu wa kanuni za mashindano hayo, kila kundi litaundwa na timu moja moja kutoka kila chungu kati ya vinne ambavyo vitakuwepo katika uchezeshaji wa droo na hakuna zuio kwa timu za nchi moja kukutana.
Source
Mwananchi.