Drip Irrigation System

Mkuu nimependa maelezo yako toka awali.
Naomba unijulishe zile ulizoziita irrigation zones ambazo zipo mikoani...particularly maeneo ya Mwanza nilipo mimi.
Natanguliza shukrani.

Nashukuru sana,ngoja nifanye uchunguzi maeneo hayo alafu ntakuletea jibu haraka niwezavyo!! karibu.
 
Hii system si tuliambiwa unapandisha tenk juu maji yanatililika yenyewe kutoka kwenye tenk kwenda kwyenye mipira iliyolazwa shambani, haiitaji pamp kuyasukuma shambani. Sasa hayo mafuta ya pampu yanatumika kwa kazi ipi tena??
 
Hayo maji kwenda kwenye Tenki lililoko juu yanapanda yenyewe??!!
 
mkuu lordville hii system ya drip irrigation inafaa kwa kilimo cha mahindi?
Ndugu mzawa, jibu ni ndio!!! drip inaeza fanya kazi katika mazao mengi sana!! na katika mahindi ni uhakika kwamba itafanya vizuri!!

Hii system si tuliambiwa unapandisha tenk juu maji yanatililika yenyewe kutoka kwenye tenk kwenda kwyenye mipira iliyolazwa shambani,
Ndugu yangu ibra, ulichosema ni sahihi lakini hii haiwezekani kwenye kilimo kikubwa (large scale farming), na mara nyingi wanatumia kwenye gadeni ndogo za majumbani...kwa case hii ina maana maji yatakua yanasambazwa kwa kani mvutano (force of gravity) na ni vyema ukawa eneo la mwinuko kidogo!! kwa kifupi ni ngumu sana na hata ufanisi wake utakua chini tu!! hamna jinsi utahitaji pump ndugu!!
haiitaji pamp kuyasukuma shambani. Sasa hayo mafuta ya pampu yanatumika kwa kazi ipi tena??
Ni vigumu kuweka lita zaidi ya 10000 kwenye tanki juu bila pump!! kama nilivyosema kwa eneo kubwa na ufanisi bora utahitaji pump na sio pump tu, pump ambayo itatoa presha stahiki kwenye mazao shambani bila ya uharibifu wa mazao au udongo!!
 
Mkuu nimependa maelezo yako toka awali.
Naomba unijulishe zile ulizoziita irrigation zones ambazo zipo mikoani...particularly maeneo ya Mwanza nilipo mimi.
Natanguliza shukrani.

Mkuu hapo jijini Mwanza zonal office ya umwagiliaji iliyo chini ya wizara ya kilimo ipo Nyakato. Nenda hadi kituo cha daladala cha Iloganzala kisha fuata barabara inayokufikisha Nyakato shule ya msingi. Kutoka hapo shule hadi hizo ofisi za Irrigation ni kama mita 300 hivi.
 
Ndugu mzawa, jibu ni ndio!!! drip inaeza fanya kazi katika mazao mengi sana!! na katika mahindi ni uhakika kwamba itafanya vizuri!!

Ndugu yangu ibra, ulichosema ni sahihi lakini hii haiwezekani kwenye kilimo kikubwa (large scale farming), na mara nyingi wanatumia kwenye gadeni ndogo za majumbani...kwa case hii ina maana maji yatakua yanasambazwa kwa kani mvutano (force of gravity) na ni vyema ukawa eneo la mwinuko kidogo!! kwa kifupi ni ngumu sana na hata ufanisi wake utakua chini tu!! hamna jinsi utahitaji pump ndugu!!

Ni vigumu kuweka lita zaidi ya 10000 kwenye tanki juu bila pump!! kama nilivyosema kwa eneo kubwa na ufanisi bora utahitaji pump na sio pump tu, pump ambayo itatoa presha stahiki kwenye mazao shambani bila ya uharibifu wa mazao au udongo!!

nina tenki la lita takribani 23'000 ambalo.nimelijenga kwenye muinuko sambamba na shamba ambalo pia pia lina muinuko. nimetengeneza teras na kupanda nyanya ilihali nimetumia drip ambapo lakini nilipata mavuno hafifu. je unanipa ushauri gani eneo kama hili?
 
Naona wahandisi wa kilimo mnashusha nondo. Safi. Nimejifunza kitu kwenye hii thread
 
Tenki la lita 10000 likijazwa maji yale maji yanakandamizana then yanatengeneza presha+kulipandisha juu mita2 bado nitahitaji pamp?
 
shukrani Mr LORDVILLE!chanzo cha maji ni mto RUAHA , landscape ya shamba sio almost perfectly flat kuna sehemu zingine ina slope kidogo na nyingine tambarare!

Hawa watalaamu wa kupima soil moisture nitawapata wapi Tanzania , na wanatest udongo wa mda gan!
Ingekuwa vizuri ungenielekeza kwa watu waliofanya drip irrigation project on large scale farms ili niwavisit na kupata maujuzi
 
Naimani wako wengi mkuu, ila ambao nna uhakika nao kuna wa pale SUA kwenye idara ya udongo, SUA idara ya uhandisi kilimo, kama SUA ni mbali unaweza pitia irrigation zone ambayo iko karibu nawe nadhani watakupa mwangaza zaidi. Kuhusu mashamba, naiman yako mengi ila kuna Mtibwa kama si kilombero sugar na hata TPC wanatumia sana drip irrigation, kuna watu binafsi pia ila hawa sijabahaitika kutana nao ila am sure wapo!!.Maelezo mengine tutapata kwa wadau..

Karibu.
 
New world kama unataka kuona shamba kubwa la umwagiliaji wa drip njoo Songea kuna shamba karibu na kijiji cha liganga shamba la Kahawa lina eka zaidi ya 1000, shamba lote wanamwagilia kwa drip.
 
Hiyo ni nzuri ila ni muhim sana kuwa na pump kwa maana huwez kupata level moja shambani ni ngumu Labda iwe ni kwa bistan tu kwa matumiz ya nyumbani
 
  1. View attachment 216681Furrow irrigation is conducted by creating small parallel channels along the field length in the direction of predominant slope. Water is applied to the top end of each furrow and flows down the field under the influence of gravity.

Mais
hii si uandaaji wake gharama sana hadi eneo liwe level ?
 
Last edited by a moderator:
Barton mkuu wako vizuri halafu unataka drip ipi ya pressure ama gravity kama ni gravity mkuu waone Barton
 
Salaam wana JF wote! je ni kampuni gani hapa Tanzania inaweza kufunga "efficient drip irrigation system" maana hii teknolojia ya umwagiliaji inasekana kuwa ya ufanisi mkubwa. Nakarisha wadau wote wenye ujuzi na teknolojia.
Green agriculture company, tupo Morogoro mjini, contact 0763347985 Eng Octavian Lasway (irrigation engineer)
 
Back
Top Bottom