Muulize Dr Slaa maswali yafuatayo
Ni kwanini anaonekana kuungwa mkono sana ndani na nje ya chama chake mpaka kufikia kujadiliwa na kituo maarufu duniani CNN? Nini siri yake?
Swali la pili,Anazungumziaje kuwaandaa wanachama kupata viongozi madhubuti katika uchaguzi ndani ya chama?
Swali la tatu,Anatumia njia gani kudhibiti mamluki na maadui wa Chadema?
Swali la nne,Chadema kimekuwa chama kikubwa lakini hakina vyombo vya habari na hiyo ndiyo sababu vyombo vingi vinavyomilikiwa na washirika wa CCM kutumika kukishambulia chama.Chadema inakabili vipi changamoto hii?
Swali la tano,Ni lini Chadema itakuwa na makao makuu ya kisasa yanayoendana na hadhi ya chama chake?