Dr.W.P.Slaa ndani ya EATV

Dr.W.P.Slaa ndani ya EATV

Naomba umuulize Dr kwanini anaogopa tahariri squire wakati akijua haki hutafutwa ata kwanguvu ikibidi yeye anaogopa nini kuhusu Hilo?

Tumekuwa tukitoa matamko mengi lakini serekali haisikii je cdm itaendelea kutoa matamko mpaka lini? Ni jitihada gani za dhati chadema inachukua baada ya serikali kupuuza matamko ya cdm?

Cdm wana mpango gani wa haraka dhidi ya wasaliti Kama akina shibuda na baadhi ya bavicha? Je tuhuma dhidi ya Zitto nini mtazamo wa Chama?

Ni hayo tuu Dr.
 
Muulize Dr Slaa maswali yafuatayo

Ni kwanini anaonekana kuungwa mkono sana ndani na nje ya chama chake mpaka kufikia kujadiliwa na kituo maarufu duniani CNN? Nini siri yake?

Swali la pili,Anazungumziaje kuwaandaa wanachama kupata viongozi madhubuti katika uchaguzi ndani ya chama?

Swali la tatu,Anatumia njia gani kudhibiti mamluki na maadui wa Chadema?

Swali la nne,Chadema kimekuwa chama kikubwa lakini hakina vyombo vya habari na hiyo ndiyo sababu vyombo vingi vinavyomilikiwa na washirika wa CCM kutumika kukishambulia chama.Chadema inakabili vipi changamoto hii?

Swali la tano,Ni lini Chadema itakuwa na makao makuu ya kisasa yanayoendana na hadhi ya chama chake?

Mkuu, ni lini alijadiliwa na Cnn naweza pata link kama inawezekana?
 
Atwambie kwanini CDM ni chama cha bara tu ila ikifika siku za uchaguzi mkuu wanaenda kutoa watu msikitini wakagombee nyadhifa za juu kabisa hata kama sifa ni dhaifu. Hapahatuitaji ubabaishaji wa kusema tuna wanachama kwani wananchi tunajua.Tunataka jibu makini
 
Frequency za iyo radio kwa dom ni ngapi?

ea%20radio%20part.png
 
Ni maswali mawili ya msingi kwa Dr Slaa.

1. Bavicha karibia wote wameishanunuliwa kwa kuendekeza njaa nani ataisaidia chama kushinda nafasi mbalimbali kwenye uchaguzi mkuu 2012.

2. Kwa nini unakuwa mwepesi wa kukusanya kadi za CCM kwenye mikutano yako huku wewe mwenyewe binafsi kadi yako ya CCM umeificha mchagoni na kuilipia ada kila mwezi.

Hiii single imechuja tena haraka kama ile single ya hajatulia tulia huyu demu mapepe! Tungeni nyingine
 
Binafsi ningependa waendesha kipindi wawe makini na maswali watakayokuwa wanamuuliza....wasije wakajisahau wakaona
kama wako na Lusinde au Shibuda na wakaanza kumuuliza maswali ya kiujinga ujinga au yakidakudaku. Watangazaji wa
kipindi yawapasa watambue kuwa huyu mtu ni VIP wa Watanzania....So watangazaji wa kipindi waendeshe kipindi kulingana
na heshima ya mgeni waliomualika hapo studio.

Mimi ni mpenzi mkubwa sana wa kipindi cha HOTMIX na huwa nawakubali sana watangazaji wake (Adrian​ na Fatna) kwa jinsi wanavyoendesha kipindi chao. So kama Adrian na Fatna watakuwa front line kumuhoji Dr Slaa basi nategemea kipindi
kitakuwa kizuri sana! Ila kama kitaendeshwa na watangazaji wengine ambao siwajui basi no coment.

Tbag Hatari uko juu na thnx for the info.
 
1) Anamshauri nini JK ili aweze kupunguza mfumuko wa bei na kushuka kwa thamani ya shilingi dhidi ya dola ya kimarekani?

2) Ziara za ufunguzi wa matawi nje ya nchi zinafadhiliwa na nani?

3) Ni lini viongozi wa CHADEMA watatangaza mali zao kwa umma wa wa Tanzania?

4) Ni kiasi gani analipwa na CHADEMA kwa mwezi akijumuisha na marupu rupu? Mbali na shughuli za kisiasa, ana shughuli yoyote nyigine ya kiuchumi anayoshiriki?
 
Binafsi ningependa waendesha kipindi wawe makini na maswali watakayokuwa wanamuuliza....wasije wakajisahau wakaona
kama wako na Lusinde au Shibuda na wakaanza kumuuliza maswali ya kiujinga ujinga au yakidakudaku. Watangazaji wa
kipindi yawapasa watambue kuwa huyu mtu ni VIP wa Watanzania....So watangazaji wa kipindi waendeshe kipindi kulingana
na heshima ya mgeni waliomualika hapo studio.

Mimi ni mpenzi mkubwa sana wa kipindi cha HOTMIX na huwa nawakubali sana watangazaji wake (Adrian​ na Fatna) kwa jinsi wanavyoendesha kipindi chao. So kama Adrian na Fatna watakuwa front line kumuhoji Dr Slaa basi nategemea kipindi
kitakuwa kizuri sana! Ila kama kitaendeshwa na watangazaji wengine ambao siwajui basi no coment.

Tbag Hatari uko juu na thnx for the info.
Mkuu,mbona unaanza kujihami kwani hata Dr Slaa mara nyingi anazungumza maneno ya kiudakudaku bila kuthibitisha ukweli ukimuuliza anakuambia uende mahakamani ili mkatopetezeane muda.
 
Binafsi ningependa waendesha kipindi wawe makini na maswali watakayokuwa wanamuuliza....wasije wakajisahau wakaona
kama wako na Lusinde au Shibuda na wakaanza kumuuliza maswali ya kiujinga ujinga au yakidakudaku. Watangazaji wa
kipindi yawapasa watambue kuwa huyu mtu ni VIP wa Watanzania....So watangazaji wa kipindi waendeshe kipindi kulingana
na heshima ya mgeni waliomualika hapo studio.

Mimi ni mpenzi mkubwa sana wa kipindi cha HOTMIX na huwa nawakubali sana watangazaji wake (Adrian​ na Fatna) kwa jinsi wanavyoendesha kipindi chao. So kama Adrian na Fatna watakuwa front line kumuhoji Dr Slaa basi nategemea kipindi
kitakuwa kizuri sana! Ila kama kitaendeshwa na watangazaji wengine ambao siwajui basi no coment.

Tbag Hatari uko juu na thnx for the info.

Heshima yako Boss wangu na ninafurahi kukuona u-hai!

Yale maswali ya Kiujinga Ujiunga kutoka kwa baadhi ya watangazaji hakika usitarie kuyaona ndani ya EATV..presenters are well informed..just relax and kudos kwako kwa kua mdau wa HotMix na wasalimie sana hapo ulipo..ha ha ha..
 
Mkuu,mbona unaanza kujihami kwani hata Dr Slaa mara nyingi anazungumza maneno ya kiudaudaku bila kuthibitisha ukweli ukimuuliza anakuambia uende mahakamani ili mkatopetezeane muda.
Anhaaa kumbe mulitaka aulizwe kama wanavyoulizwa wakina Dimond na Aunt Ezekiel? Basi imekula kwenu.
Huyo mtu anaheshima zake
 
DR. Slaa,

Wengi tuna uhakika CDM inaweza kuchaguliwa na watanzania na kuongoza dola baada ya uchaguzi mkuu 2015; maswali je?
a) Serikali mtakayounda itakuwa ni ya majimbo kama mlivyoanisha kwenye ilani yenu? mbona juzi nilikusikia pale Ilala
ukisema CDM itahitaji makada waadilifu ambao watakuwa wakuu wa mikoa na wilaya - hapo tunaomba ufafanuzi maana nafasi hizi ulisema hazitakuwepo mkiingia madarakani. kama unaweza kutupatika picha kidogo njinsi uongozi utakavyokuwa toka majimboni hadi taifa, je Halmashauri zetu itaingizwaje ndani ya serikali ya majimbo; Gusia kidogo Mamlaka ya mkuu wa jimbo (Gavana) na atapatikana vipi?

b) Tunaomba tuhafafanulie CDM ina kauli gani juu ya kundi la uamusho Zanzibar? fafanua zaidi kwa namna gani CDM
itakavyoshughulikia masuala yote (malalamiko) yanayohusu fursa mbalimbali za waislamu kukandamizwa - ie makahama ya kadhi, malalamiko baraza mitihani nk pia tupe msimamo wa CDM kuhusu uchomaji wa makanisa, bar na nyumba za wageni (Guest hse) kule Zanzibar

c) Mwisho DR. Slaa watanzania wanakuamini sana (70%) na unazidi kuaminiwa kila kukucha; na wanaokuamini si wana CDM tu bali watanzania kwa ujumla; je ukiingia madarakani utaweza kufuata nyayo za baba wa taifa kiuongozi? Je mfumo utakaoukuta serikalini hauwezi kukukwamisha kutimiza majukumu yako kama rais wa Tanzania? tunaomba mikakati ya kiuongozi uliyowekeana na wenzako kutimiza dhana nzima ya Kurudisha TUNU ya taifa iliyopotea.

Nimejikita sana kwenye uongozi wa nchi sababu wengi wetu hatujajua kiundani njinsi CDM mtakavyoongoza nchi, its time sasa taratibu tuanze kufahamishwa.

Nakutakia kazi njema na Mungu akulinde sababau wewe ndiyo tegemeo pekee la Watanzania kwa sasa.
 
Back
Top Bottom