Kimagege
JF-Expert Member
- Oct 28, 2010
- 283
- 88
Ni muda sasa umepita tangu Dr. Ulimboka aliporejea tena nchini akitokea katika matibabu na kupokelewa kifalmwe na madaktari wenzie.Katika vitu ambavyo watanzania na madaktari wenzie walitarajia kusikia kutoka kwake ni juu ya wale waliomteka na kumtesa kwani alidai mwenyewe kuwa anawajua na kwamba akirudi toka matibabuni angewataja wote.Akarudi na kutulia kwao pale Ubungo Maziwa akawa kimya na hadi sasa japo aliahidi mara nyingi kupasua jipu hadi leo sioni wala kuhisi dalili ya ulimboka kuwataja wabaya wake.
Naomba wana jamvi tusaidiane kujua ukweli kuhusu ukimya huu usiotarajiwa wa Dr. Ulimboka.
Naomba wana jamvi tusaidiane kujua ukweli kuhusu ukimya huu usiotarajiwa wa Dr. Ulimboka.