Taarifa kwa Chama cha Madaktari MAT kuhusu Dr.Ulimboka | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Taarifa kwa Chama cha Madaktari MAT kuhusu Dr.Ulimboka

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzalendo2015, Aug 14, 2012.

 1. Mzalendo2015

  Mzalendo2015 JF-Expert Member

  #1
  Aug 14, 2012
  Joined: Aug 14, 2012
  Messages: 1,957
  Likes Received: 2,318
  Trophy Points: 280
  Napenda kuchukua nafasi hii kukipongeza Chama Cha Madaktari,MAT(Medical Association of Tanzania) kwa kazi nzuri waliyoionyesha kwa kumjali na kumhudumia kiongozi wao Dr.Ulimboka tangu alipotekwa na kupigwa na kuteswa na hatimaye kusafirishwa mpaka Afrika Kusini kwa matibabu bora zaidi ambayo ndiyo yamemwezesha kurudi Tanzania akiwa na afya iliyoimarika barabara. Hongereni sana Madaktari na Mungu awabariki.

  Hata hivyo nataka kutoa tahadhari kwa MAT na Madaktari wote kwa ujumla. Kwamba Dr. Ulimboka lazima apewe ulinzi imara na salama kwa masaa 24! Kama tu ambavyo MAT muliweza kuchangisha mamilioni ya Pesa kwa ajili ya matibabu ya kiongozi wa chama chenu basi ni wakti mwingine sasa kupanga mikakati ya ulinzi mkishirikiana na Familia namna ya kumpa ulinzi Dr. Ulimboka kwa wakti wote(24 hrs security). This will be another challenge to TMA. Jipangeni na mhakikishe hili la ulinzi linafanyika vinginevyo lolote laweza kutokea!

  Kila Mtanzania anajua sakata la Dr.Ulimboka lilivyoanza na nina amini bado sakata hili litaendelea maadamu wale wabaya wa Dr.Ulimboka hawajawekwa wazi kwa maana ya kukamatwa, kuwekwa ndani na kufunguliwa mashtaka na hatimaye mkondo wa sheria kuchukua mkondo wake.Mengi yamesemwa kuhusu wahusika wa kazi hii chafu,yapo yenye ukweli na yapo yaliyojaaa uongo mtupu ili kupoteza ukweli wa tukio lenyewe. Nashawishika kusema kuwa kazi hii chafu ambayo kwa sehemu kubwa inaonekana kuratibiwa na Serikali ya CCM bado haikufikia malengo yaliyokusudiwa!(Mwenye masikio na asikie). Bado hawa wakora na wahuni watataka kukamilisha kazi yao chafu baada ya Dr.Ulimboka kurudi Tanzania ili wapoteze ushahidi wa kesi hii ambayo inaweza kufananishwa na "Watergate scandal".

  Kumbukeni kuwa Dr.Ulimboka ndiye target na ndiye mwenye ushahidi wa kila kitu kama kesi itaanza kuunguruma. Dr. Ulimboka anawajua waliomteka kwa majina,sura na sauti na namba zao za simu.Hawa jamaa kwa namna yoyote ile watataka kufuta ushahidi huu kwa kumpoteza Dr.Ulimboka kwa gharama yoyote. They gonna strike back! Watatumia kila mbinu ili wamfikie au kumpata Dr.Ulimboka. It was confirmed by Dr. Uli himself that, they are trained soldires and killlers! Kwa hiyo watatumia mbinu zote walizofundishwa ili watimize adhima yao chafu. Kwa hiyo ulinzi ni jambo la msingi sana kwa usalama,uzima na uhai wa Dr. Ulimboka ili aendelee kutetea Afya bora kwa kila Mtanzania.

  Naomba kuwasilisha.
   
 2. Mark Francis

  Mark Francis Verified User

  #2
  Aug 14, 2012
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 605
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Wachange tu kwa ajili ya ulinzi wa miaka 3 iliyobaki kufika 2015 ambapo CDM itaingia madarakani. Baada ya hapo, hakutakua na ubabaishaji wowote maana kila idara ya serikali itafanya kazi yake kwa uhakika na ufasaha. 'Intelligence' itakua ya kweli na sio ya kizushi yenye lengo la kuwakandamiza baadhi ya watu au vikundi vya watu.
   
 3. Marire

  Marire JF-Expert Member

  #3
  Aug 14, 2012
  Joined: May 1, 2012
  Messages: 11,420
  Likes Received: 260
  Trophy Points: 180
  Ushuri murua, wahusika wauchukue na waufanyie kazi mapema ;hii movie imefika patamu sasa
   
 4. B

  Bobuk JF-Expert Member

  #4
  Aug 14, 2012
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 5,876
  Likes Received: 481
  Trophy Points: 180
  MAT na nyinyi mmekuwa wana siasa fanyeni mambo haya mawili
  1. Kwanza Dr. Ulimboka kuendelea kukaa na SIRI ya Watekaji moyoni ni MOTIVATION ya kuendelea kuwindwa, it is no brainer. Dr. Ulimboka inabidi aitishe PRESS CONFERENCE na kuweka wazi bila chenga MKASA mzima wa kutekwa na WATU waliomteka. Hiyo itaondoa motivation ya kuendelea kuwindwa.

  2. Kama mnakubali MKASA wa Dr. Ulimboka ni sawa na water gate. Basi MAT inabidi mratibu mpango wa kuchangisha pesa kwaajili ya kuwaleta SCOTLAND YARD ili watufanyie uchunguzi usio acha hata punje ya shaka. Tumuachie Kova na Ikulu waendelee na hiyo kangaroo tume yao. And you know report hizi mbili zikitoka unajua ni ipi itaaminiwa na wannachi.

  MAT na Dr. Ulimboka lazima mjue you're fighting with a powerful brutal enemy, Msfikiri kila siku watafanya makosa. I'm sure wakipata second chance they will not do mistakes! Sio nawatishwa ni UKWELI ulio dhahiri shairi!
   
 5. samora10

  samora10 JF-Expert Member

  #5
  Aug 14, 2012
  Joined: Jul 21, 2010
  Messages: 6,639
  Likes Received: 1,428
  Trophy Points: 280
  Navyojua mimi Dr Ulimboka sio kiongozi wa MAT, Ni kiongozi wa jumuiya ya Madaktari Tanzania!

  Hivyo ni vitu viwili tofauti sana
   
 6. Lyimo

  Lyimo JF-Expert Member

  #6
  Aug 14, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 3,828
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Ninaunga mkono hili la kuwapa kazi wachunguzi wa kimataifa waliobobea (Scotland yard). Kwa utata uliopo tusitegemee kupata taarifa/mapendekezo/maamuzi yasiyo na shaka kutoka kwenye hii tume ya Kova ama Mahakama zetu zinazochakachuliwa kila kukicha.
   
 7. Zogwale

  Zogwale JF-Expert Member

  #7
  Aug 14, 2012
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 11,613
  Likes Received: 825
  Trophy Points: 280
  Ninaunga mkono hoja kwa 200%. Ikiwezekana itisheni harambee ya kuchangia ulinzi wake na wengi watakuwa tayari kuchanga. Hatuwezi kuwa na wanyama kiasi kile.
   
 8. Nsabhi

  Nsabhi JF-Expert Member

  #8
  Aug 14, 2012
  Joined: Feb 23, 2011
  Messages: 1,096
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Kama ni ulinzi mimi napendekeza apewe ulinzi wa hali ya juu ikiwezekana ule wa kiwango cha mafia. Wale watekaji wake bado wana unaccomplished mision. Lazima alifahamu hilo na kujilinda zaidi.
   
 9. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #9
  Aug 14, 2012
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 11,373
  Likes Received: 3,136
  Trophy Points: 280
  Hoja nzito hii na wahusika wa pande zote yaani upande wa dr.ulimboka na upande pili(kikwete,cc,ikulu,serikali,polisi,tiss kwa umoja wao)....naamini kila mmoja atajitahidi kuhakikisha upande wake unashinda...serikali ina mkono mrefu kwenye kuua ama kutesa watetezi wahaki km uli lkn mkono wake mfupi km wa mbilikimo pale mafisadi wanapoliibia matrilioni wanaibtwiga kila siku wkt tuna rada ya bei mbaya.
  Hii ni nchi ya kusadikika, ni nani ataturudishia nchi yetu ya ahadi kwani nchi tuliyomo imenajisiwa na vjiongozi wa ccm wakiongozwa na kikwete
   
 10. N

  Ngoso JF-Expert Member

  #10
  Aug 14, 2012
  Joined: May 26, 2012
  Messages: 521
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 45
  Mimi nashauri mambo mawili kwanza ahojiwe na mwanasheria wake mbele kamati iliyoundwa ili mahojiano yawekwe kwenye kanda au Cd kwa matumizi ya baadae. Lakini mchawi mpe mtoto alee .muombeeni ulinzi .wasije kumvamia huko ikawa kwanini hamkuomba ulinzi
   
 11. phina

  phina JF-Expert Member

  #11
  Aug 14, 2012
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 414
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  mbona mwenzenu mbona sina imani na justice system yetu??ahh..liwalo na liwe!
   
 12. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #12
  Aug 14, 2012
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,976
  Likes Received: 688
  Trophy Points: 280
  Kinachotakiwa hapa ni Uli kuweka wazi watekaji wake, hadithi inyooke, tunajua Kova hatofanya kitu.

  Hiyo ndo msumari kwa serikali, wananchi wana akili, wabaona na watatoa hukumu muda utakapofika.
   
 13. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #13
  Aug 14, 2012
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,202
  Likes Received: 720
  Trophy Points: 280
  ni ushauri mzuri sana na MAT wanalijua hili la kuhusu ulinzi na wanalifanyia kazi na mpaka sasa yuko mahali salama..hukusu dr uli kujisema hadharani kilichomtokea hakuna shida hilo litafanyika tu... wacha kwanza apumzike
   
 14. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #14
  Aug 14, 2012
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,313
  Likes Received: 5,605
  Trophy Points: 280
  Asante sana kweli ukweli huwa haujifichi na hauchanganyiki na uongo kamwe!ni sawa na giza kutochanganyika na nuru pumzika Dr Uli uje umwage mboga.......
   
 15. a

  afwe JF-Expert Member

  #15
  Aug 14, 2012
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 4,087
  Likes Received: 109
  Trophy Points: 160
  Join Date : 14th August 2012
  Posts : 11
  Rep Power : 303
  Likes Received 7
  Likes Given 5
   
 16. D

  Deo JF-Expert Member

  #16
  Aug 14, 2012
  Joined: Nov 10, 2008
  Messages: 1,190
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Nashauri aombe hifadhi nchi za nje kama mkimbizi mpaka kipindi hiki kipete, hatakuwa salama sana akibaki labda awe kama Makembe aliyehongwa uwaziri.

  Tunamwomba autangazie ulumwengu kitu gani kilichompata!
   
 17. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #17
  Aug 14, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Inafaa mumuulize Ulimboka alikwenda kutatuwa mgomo upi bar saa 5 za usiku kwa kupigiwa simu wakaongelee mgomo. Au mgomo wa tumbo?
   
 18. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #18
  Aug 14, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Una maana kapata adabu stahiki na hatarudia? Amini kuwa kala kichapo usitake kujuwa mengine yaliyompata hayasemeki.
   
 19. Nyakageni

  Nyakageni JF-Expert Member

  #19
  Aug 14, 2012
  Joined: Feb 1, 2011
  Messages: 13,951
  Likes Received: 1,275
  Trophy Points: 280
  eagerly waiting . . . . . !
   
 20. D

  Determine JF-Expert Member

  #20
  Aug 14, 2012
  Joined: Apr 27, 2012
  Messages: 257
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  ninachojua mimi UN washailima Ikulu barua kuhusu tatizo lolote litakalomkuta DOCTOR wahusika watakuwa wao,huo ndo ulinzi tuliopata UN
   
Loading...