Dr.Ulimboka kasalimu amri kwa wabaya wake?

Kimagege

JF-Expert Member
Oct 28, 2010
283
225
Ni muda sasa umepita tangu Dr. Ulimboka aliporejea tena nchini akitokea katika matibabu na kupokelewa kifalmwe na madaktari wenzie.Katika vitu ambavyo watanzania na madaktari wenzie walitarajia kusikia kutoka kwake ni juu ya wale waliomteka na kumtesa kwani alidai mwenyewe kuwa anawajua na kwamba akirudi toka matibabuni angewataja wote.Akarudi na kutulia kwao pale Ubungo Maziwa akawa kimya na hadi sasa japo aliahidi mara nyingi kupasua jipu hadi leo sioni wala kuhisi dalili ya ulimboka kuwataja wabaya wake.

Naomba wana jamvi tusaidiane kujua ukweli kuhusu ukimya huu usiotarajiwa wa Dr. Ulimboka.
 
Lwesye

JF-Expert Member
Sep 29, 2012
5,292
0
Ramadhani Inqondu,Abeid Msuya,Selemani Kova hivi hawa ni dini gani vile ,kawaulize watakupa majibu
 
yegella

JF-Expert Member
Nov 18, 2010
3,113
1,250
sasa ulitaka usikie nini zaidi mbona alisha sema ni nani alimteka kuwa ni Ikulu..
 
Zogwale

JF-Expert Member
Jul 10, 2008
14,908
2,000
Hivi aisee huyu daktari niliyemtetea kwa mapovu karibia nipata ban hapa aliishia wapi? Kuna tetesi alipewa manoti mengi sana!!!!! Naweza kukubaliana na tetesi kuwa ni kweli!!
 
Githeri

JF-Expert Member
Apr 2, 2012
813
500
Yaelekea unajua anapoishi. Kwa nini usimfuate ukamuuliza? Hapo huoni kama utapata majibu ya swali lako?
 
Mheshimiwa Mwl Steve

Senior Member
Nov 3, 2012
139
0
Mi nina uliza kesi ya yule mkenya aliyedaiwa kumteka ulimboka imefikia wapi wadau? Vipi kesi ya dakt mkopi pia? Kuhusu ulimboka kunywea nadhani ni katka kuokoa maisha yake baada ya kuona anapigana kivyake.
 
Concrete

JF-Expert Member
Mar 12, 2011
3,605
0
Hivi aisee huyu daktari niliyemtetea kwa mapovu karibia nipata ban hapa aliishia wapi? Kuna tetesi alipewa manoti mengi sana!!!!! Naweza kukubaliana na tetesi kuwa ni kweli!!
Leo hautalipwa posho na usije kabisa hapa Lumumba.
UmeandiKa utumbo mwingi sana.
 
Mnyakatari

JF-Expert Member
Oct 25, 2010
1,919
2,000
Hakuna ambacho Dr.Ulimboka hajakisema kuhusu waliomteka,kumsukumiza kwenye gari,kumtesa kinyama na hatimaye kuitupa 'maiti' yake kwenye msitu wa Mabwepande.Kuanzia siku ya kwanza alipookotwa alifanyiwa mahojiano na mwanakijiji na kuwataja waliohusika.

Akiwa hospitali alihojiwa na mahojiano yale kwanza kabisa yalikuja hapa jf kabla ya kusambaa hadi U-tube.Haikuishia hapo yameandikwa mengi na ya ukweli kuhusu sakata lake(rejea sababu ya kufungiwa mwanahalisi) na kufanywa mazingaombwe mengi tu(rejea picha ya Kova pale kwa Gwajima).

Hata yeye mwenyewe baada ya kurudi alisema yote yalioandikwa na mwanahalisi ni kweli na kwamba majina yote yaliyotajwa na mwanahalisi ni ya wahusika halisi.Ulimboka amejua unafiki unaowatawala wale wanaojifanya kufuatilia mkasa wake huku wakimlaumu yeye.Kipi ambacho hajakisema?Tuache unafiki,Ulimboka aliponywa na Mungu wake na ni yeye ambaye amepata machungu yote.

Endelea na maisha yako muache nae aendelee na maisha yake.Kama yeye asivyoweza kukupangia la kufanya na wewe vilevile huna haki ya kumtaka afanye unavyotaka.Umejua kila kitu huna unachokifanya zaidi ya kuendeleza unafiki hapa.Washabiki wote waligeuka wanafiki pale Ulimboka alivyorudi mzima kutoka SA hasa walipoanza kumtaka aseme yale ambayo tayari ameshayasema.Ulimboka angepoteza maisha ungepungukiwa na kitu gani wewe kwenye maisha yako?

Hata baada ya muda kupita na yeye kutoa andiko la kuthibitisha kuhusu wahusika bado wanafiki kama wewe hawafanyi lolote ila mnaendelea kumtaka aseme tu.Aseme nini zaidi.Muachie Ulimboka maisha yake.Ameponywa na Mungu sio wewe,hivyo huna haki ya kujifanya kujuajua kwani wakati yeye anateswa kule kwenye zile nyumba nzuri kule,wewe ulikuwa umelala ma mke/mme wako.Muache Ulimboka ,fuata yako.
 
Bijou

JF-Expert Member
Feb 25, 2011
1,193
1,500

Need you say more?? EmeUngumza KWA uchungu na hisia Kali, ni kweli Kabisa, yaliyobaki ni Maisha yake na aachiwe MWENYEWE
 
schwester

Member
Apr 7, 2012
69
0
Ni muda sasa umepita tangu Dr. Ulimboka aliporejea tena nchini akitokea katika matibabu na kupokelewa kifalmwe na madaktari wenzie.Katika vitu ambavyo watanzania na madaktari wenzie walitarajia kusikia kutoka kwake ni juu ya wale waliomteka na kumtesa kwani alidai mwenyewe kuwa anawajua na kwamba akirudi toka matibabuni angewataja wote.Akarudi na kutulia kwao pale Ubungo Maziwa akawa kimya na hadi sasa japo aliahidi mara nyingi kupasua jipu hadi leo sioni wala kuhisi dalili ya ulimboka kuwataja wabaya wake.

Naomba wana jamvi tusaidiane kujua ukweli kuhusu ukimya huu usiotarajiwa wa Dr. Ulimboka.

Ndg kwa mfano akaamua kusema yote na kuwTAJA HAO WAHUSIKA WEWE AU HILO KUNDI MNALOSHABIKIA MTAFANYA NINIß mMEFANYA NINI KWA MLIO WAONA WAKIFANYA UNYAMA KAMA HUU: MMESAIDIAJE MATATIZO YAKUWEPO SASA: ACHA USHABIKI FANYA KAZI SHUGHULIKA NA MIPANGO YAKO YA FUTURE:
 
uwoya

Senior Member
Oct 18, 2012
166
195
Hivi aisee huyu daktari niliyemtetea kwa mapovu karibia nipata ban hapa aliishia wapi? Kuna tetesi alipewa manoti mengi sana!!!!! Naweza kukubaliana na tetesi kuwa ni kweli!!

Dr. Uli mateso ulipata wewe mwenyewe na hatimaye unaendelea kuteseka na familia yako. wewe songa mbele na maisha yako
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom