Dr. Ulimboka: Hali ya afya (Updates)

Hawa Nipashe walitaka tu kuuza gazeti, hiyo habari haijisltoshelezi.
Lakini huo ndio uandishi wetu Tanzania.
 
Dk Ulimboka apata ahaueni

Geofrey Nyang'oro
AFYA ya Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari, Dk Steven Ulimboka imeanza kuimarika ingawa bado amelazwa katika Chumba cha Wanaohitaji Uangalizi Maalumu (ICU).


Dk Ulimboka alipelekwa Afrika Kusini Juni 30, mwaka huu baada ya jopo la madaktari lililokuwa likimtibu, likiongozwa na Profesa Joseph Kahamba kutoa taarifa za kubadilika ghafla kwa afya yake na kupendekeza apelekwa nje ya nchi kwa ajili ya vipimo na matibabu zaidi.


Jana, Katibu wa Jumuiya ya Madaktari, Dk Edwin Chitage alisema taarifa walizokuwa nazo zinasema: "Afya mwenyekiti wetu imeanza

kuimarikia, lakini bado yupo katika chumba cha wagonjwa mahututi kwani alikuwa naumwa sana."


Katika hatua nyingine, Dk Chitage alisema madaktari na wananchi wa kawaida wanaendelea kutoa mchango wa awamu ya pili

unaolenga kukusanya Dola za Marekani 30,000 kwa ajili ya kulipia gharama za matibabu za Dk Ulimboka.


"Sijapata kiwango sahihi kilichokusanywa hadi sasa, lakini michango inaendelea vizuri. Madaktari na wananchi wanaendelea kukusanya na tunawashukuru," alisema Dk Chitage.


Madaktari na ndugu wa Dk Ulimboka kwa pamoja, walikataa ofa iliyokuwa itolewe na Serikali ya kulipia gharama za matibabu za

mgonjwa huyo wakiishutumu kuhusika na tukio la kutekwa, kupigwa na kutupwa katika Msitu wa Pande kwa mwenyekiti huyo wa jumuiya ya madaktari.


Madaktari pia wamepinga tume ya polisi iliyoundwa na Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Kamishna Msaidizi wa

Polisi, Suleman Kova wakitaka kuundwa kwa tume huru kuchunguza tukio hilo.

Hilo ni miongoni mwa madai matano ya madaktari yaliyomo katika tamko la pamoja baina yao na viongozi wa dini na wanaharakati.

Madai mengine ni pamoja na Serikali kurejea katika meza ya majadiliano na madaktari, kufuta kesi iliyofungua mahakamani dhidi ya madaktari hao, kuwarejesha kazini waliofukuzwa na Rais Jakaya Kikwete kukutana na viongozi hao kujadili chanzo cha mgogoro huo.

Dk Ulimboka apata ahaueni

Mkuu Wimana na hili Gazeti la Mwananchi linasema maneno ya uongo Kuhusu hali ya Dr Ulimboka?
 
Last edited by a moderator:

hakika Mungu si mwanadamu hata akupungukie najuwa atakuponya nawe utarudi nyumbani salama kuungana na familia yako na kujenga taifa kwa ujumla
 
Asante kwa taarifa.

Wanamfuata mama wa watu wa nini tena jamani,
kama wajanja wamfuate mgonjwa mwenyewe.
 
WanaJF
Taarifa kutoka Afrika Kusini hospitalini alikolazwa Dr Ulimboka ni nzuri sana na za kutia matumaini.Kwa mujibu wa Katibu wa Jumuiya ya Madaktari Dr Edwin Chitage ni kwamba kwa sasa Dr Ulimboka anaweza kula chakula mwenyewe.

Source:Nipashe Jumanne.
 
Good news. Haikuwa mpango wa Mungu afe, ataishi miaka yake ya ahadi alopewa na Mungu wake.
 
Nashkuru kwa taarifa............kuna kundi la wapuuzi hawataki kusikia taarifa kama hizi
 
We pray for his earlier recovery, aje kujiunga na watanzania katika kusukuma gurudumu la kujitafutia maendeleo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…