Kwa habari nilizo nazo, Dr. Ulimboka anapaswa kuwa mwangalifu na hao wakubwa wa serikali. Damage aliyoisababishia hii serikali na idara nzima ya TISS ni kubwa mno, na kwa uhakika, kuna watu wameapa "Hawatamsamehe".
Hakuna shirika lolote la kijasusi ulimwenguni linaloweza kuvumilia mtu aliye na siri zake bila control ya namna fulani. Yeye kuahidi kukaa kimya haiwahakikishii majasusi wetu kuamini kuwa daima atakaa kimya. Dawa ya hili katika mashirika yote, huwa ni kumalizana ili kuwa na uhakika kuwa ushahidi umekufa. Ndiyo maana, wakati wa Coup de'tat, rais anayeingia huwa anawamaliza waliomsaidia mmoja baada ya mwingine kwa sababu hawezi kuwa salama kwa kuwa na subordinates wanaofahamu udhaifu wake.
Ni suala la muda tu, Dr. Ulimboka ama atapoteza uwezo wa kusema wala kuandika; au atalazimika kuandika taarifa ya uwongo na kisha apotezwe kisha taarifa hiyo itumiwe kuisafisha serikali; au tu - atapotea na huo utakuwa mwisho wa hadithi hii. Worst scenario ni pale atakapojengewa mazingira ya kuchukiwa na wenzake, kisha amalizwe na ndipo wenzake watakaposingiziwa kuwa ndiyo wamemmaliza ili kulipiza kisasi cha kusalitiwa. Kukaa karibu na Dr. Ulimboka ni risk sana kwa sasa.
Mimi si nabii wala mtoto wa nabii!
Mnataka aseme ili tuje humu kwa majina feki kumgongea "like" huku akiishi kwa mashaka bila msaada? Tunataka kujua nini zaidi ya kilichomtokea?
Tuliambiwa ripoti itatoka haraka kurudisha imani kwa wananchi mpaka leo kuna wanaharakati au wanahabari wanaohoji mbona ripoti imechelewa na hiyo kamati haijamhoji hata mtuhumiwa mmoja! Madaktari ndio wasaliti namba moja wa Dr Ulimboka!
Ulimboka aseme nini zaidi ya aliyokwisha sema tena alitaja mpaka majina!
Tumeshasema habari za Dr. Ulimboka zimetuchosha hapa JF pelekeni Issa Michuzi Blog hizo habari
Umechoka wewe Mfuasi wa magamba; sisi tunatamani amani ya kweli nchini tunaendelea kupashana habari hadi kieleweke.
Kwa hili ninakubaliana nawe JJB, bora anyamaze yaishe. Sisi tunaotaka aseme sio kwa sababu yoyote zaidi ya kutaka kusoma umbea tu. Watanzania sote tumemsaliti Dr.Ulimboka na wanaharakati wote waliowahi kuthubutu kulenga jiwe la kwanza lakini sisi tukaficha mikono yetu.
Moja ya maneno na rai aliyoitoa Dr. baada ya kudhulumiwa afya na uhuru wake yalikuwa kuwataka Madaktari wenzake (na Watanzania kwa jumla) kuwa yeye yamemfika yaliyomfika, lakini waliobaki wanendelee na mapambano; matokeo yake, Madaktari walifanya nini na Watanzania tumefanya nini?
Baada ya Mwanahalisi kulezea kile ilichokijua na kuwataja watu na ubini wao na nambari zao za simu, Watanzania tumefanya nini? Tuseme Dr. Ulimboka aje na habari zile zile za Mwanahalisi, Watanzania tutafanya nini? Kama tuwatendaji kweli na sio wambea tu, tuchukue hatua juu ya yale ambayo tayari tunayajua kabla ya kutaka mengine mapya.
Tumwache Dr. apumue na sisi tuendelee na woga na blah blah blah zetu. Uchune Dokta, uchune!
sisi tuliopigania maisha yake kipindi rama anataka kummalizia pale moi anatuona mafala sio!!!!
Tumejitoa mpaka kuhatarisha usalama wetu kwa ajili yake, huyu ulimboka vipi!!!
Siyo kama amezimwa bali baada ya tafakuri mwanana aliyoifanya kuhusu kadhia nzima na jinsi ilivyomfikisha hapo, ametambua kuwa mwisho wa yote hatma yake na ya familia yake imo mikononi mwake yeye mwenyewe...na haipo mikononi mwa hao wanaojiita wanaharakati, ambao km walivyo duniani kote wanatumia watu km akina Ulimboka km turufu la muda kukidhi mahitaji ya muda.
Na wakishayapata hao wanaondoka zao bila ya kujali athari walizomsababishia kinara wao! ndio siasa za kila uchao karne hii ya viini macho!. Na ukizubaa kidogo tu umeumia! lakini wenzako watakuwa wameshapa mradi wao!.
Ulimboka, ni dhambi kubwa kuudanganya uma wa watu wote waliolia kwaajiri yako na kukuona kama mpigania haki,then leo unanunuliwa.fanya maamuzi mazuri la sivyo hautokaa kwa amani rohono mwako.hata mungu hapendi.
Shauri yako.
Akisema atakuwa ameusaliti uhai wake. Kipi Bora? Sifa za kijinga au Uhai wake?
Kama kweli Dr.Ulimboka anafanya mawasiliano na watu wazito(vigogo) wa serikali kwa kumhadaa kuwa anyamaze maana swala lake linashughulikiwa basi hakuna kesi tena!
Hawa jamaa wako very smart kwenye kumafanya manipulation ya mambo. Nina uhakika kabisa kuwa kile kikundi kilichokuwa kimeandaliwa kummaliza na kwa bahati ya Mungu akaweza ku-survive kwa muujiza wa Mungu bado kinafanya kila mbinu za kumfikia kwa mbinu za hali ya juu.
Kama hawa jamaa TISS/Vigogo wa serikali watashindwa kumweka sawa kwa maana ya kumnyamazisha kwa rushwa ya namna yoyote ile iwe pesa au cheo fulani basi hatua ya mwisho itakuwa kummaliza kwa kumuua! Nina mashaka sana na security ya huyu Dr.Ulimboka. Maana hata hawa vigogo wanaoenda kuzungumza naye yawezekana kabisa wako kazini kwa ajili ya kuandaa mazingira ya kummaliza.
Ushauri wangu kwa huyu Dr. Ulimboka ni kuamua moja: Kuweka mambo hadharani kwa kusema ukweli wote anaoujua kuhusu walio mteka halafu aishie majuu kama mkimbizi wa kisiasa. Kukaa kimya kwake naona ni hatari zaidi kuliko kama atajitokeza na kuweka ukweli hadharani.
Ni afadhali akafanya hivyo na akaomba hifadhi ya kisiasa kama mkimbizi katika nchi za Ulaya au USA. Kuendelea kukaa kimya hakutamsaidia! TISS huwa hawana msamaha na hawasahau. Watamzubaisha na kumlaghailaghai lakini mwisho wa siku they'll strike back! Kina Sokoine,Kombe,Kolimba,Amina Chifupa na wengineo wako wapi?
Dr.Ulimboka watch out,the hunters are after you.