Dr. Tulia Ackson, nani amekutuma? Unataka nini? Kwanini?

Dr. Tulia Ackson, nani amekutuma? Unataka nini? Kwanini?

Pasco

Ni kweli kwa sheria zetu huenda zinamruhusu kugombea uspika lakini kwa msomi kama yeye na kama usemavyo kwa kichwa kama yeye haingii akilini kwenda kugombea USPIKA kupitia CHAMA whether ni CCM au la. Akisha jifunga na CHAMA kwa level ya kugombea USPIKA hafai kuendelea kuwa Deputy AG au AG (tulilisema hili kuhusu Judge Ramadhani). Kwani ni wazi ni vigumu kuwa impartial hasa kwenye kesi za kisiasa au ushauri wa kisiasa. Lakini Tz yote yawezekana si unaona yanayoendelea Zanzibar?
 
Last edited by a moderator:
Huyu Mama...alinifundisha labour law UDSM...yupo vizuri mno....all the best
 
Nyie mna roho za kungunı na zımejaa kutu.Huyu dada ni brıght sana.Kila anapopewa nafası anaonesha uwezo na kwa kawaida anatakiwa kuwa rewarded.Hauwezı kumfananisha Dr Atson na mtu km Ndugaı,Nchmbi,Makinda,Zungu,Mwinyı,Mzamır,Blandes,Ikunda n.k.She is very determined ths madame!
Acha dharau ww kuna baadhi ya vyeo vinahitaji ukomavu wa Kisiasa sio midigrii ya darasani
 
Uwezo wake ni kawaida ila wale wenye uwezo mdogo wa kisheria wana muona ni kipanga. Alitumiwa sana na Asha Rose Migiro wakati wa Bunge la Katiba kuandika Rasimu Chakachuzi ya Chenge ambayo mwisho wa siku haikupita. Yeye ni mtu wa kutumiwa kutekeleza matakwa ya wakubwa. Hivyo kuweni macho naye.
 
Huoni kuwa dr atakuwa ana....kadi ya chama...na amejingiza kwenye maswala ya kisiasa alitakiwaa ajiuzulu....... sheria za utumishi wa uma zinaruhusu haya ???

Zinaruhusu kama ukiwa CCM,ona yule alitimuliwa na kurudishwa Kenya,alipokuwa anaifadhili CCM alikuwa MTANZANIA,alipobadili muelekeo na yeye ghafla akabadilishwa UTAIFA sasa ni MKENYA hii iko BONGO tu.
 
Zinaruhusu kama ukiwa CCM,ona yule alitimuliwa na kurudishwa Kenya,alipokuwa anaifadhili CCM alikuwa MTANZANIA,alipobadili muelekeo na yeye ghafla akabadilishwa UTAIFA sasa ni MKENYA hii iko BONGO tu.
Mwenye kanuni za utumishi wa uma zinazoprohibit mtumishi wa uma kujihusisha na siasa azimwage hapa.
 
@VUTA-NKUVUTE


  1. Kugombea nafasi yoyote ya uongozi ni moja ya haki za kiraia ambayo kila Mtanzania ana haki hiyo na yuko huru kugombea nafasi yoyote, hivyo Dr. Tulia Akson hajavunja sheria, taratibu wala kanuni yoyote!.
  2. Viongozi wakuu wa vyombo vya dola, wote ni makada wa CCM!, nikimaanisha hata CDF, IGP, Mkurugenzi wa TISS, Jaji Mkuu, Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru etc!. Tumemshuhudia Mboma akigombea ubunge!, Mahita akigombea ubunge!, Adadi sasa ni mbunge!, Apson akiongoza kamati ya EL!, etc, hivyo kama kosa ni kujionyesha, then Dr. Tulia ni too genuine kujificha nyuma ya cheo!.
  3. Nimetokea kumfahamu huyu dada, kwanza ni kichwa mbaya!. Nilijoin UDSM wakati yeye amemaliza LL.M na kuwa lecture, hivyo mwaka wangu wa kwanza, somo langu la kwanza ni Law of Contract, mwalimu wangu wa kwanza alikuwa huyu Tulia!. Kwa jinsi alivyo ki miss miss, enzi hizo akiwa mdogo, alionekana kama mtoto wa form Six anafundisha chuo kikuu, na sisi watu watu wa kanda ya Ziwa tunaudhaifu fulani, hivyo kila akifundisha watu wanaconcentrate na masomo, akina sisi mawazo yanatutuma kwenye mengine!, kufunga na kufungua somo lake nika supp, nikarudia nikashindwa ku clear!, hivyo nika carry over, mwalimu ndio huyo huyo!, nikashindwa ku clear nikazungusha!, yaani nikacheza DISCO!.
  4. Nadhani kwao wote ni vichwa!. Last born wao, ambaye pia ni binti, alitoka na 7 points O level, akatoka na 3 points A level na kuongoza kitaifa!.
  5. Kwa perfomance yake niliyoiona wakati wa BMK, kama CCM inataka tupate the best speaker, then watamteua Dr. Tulia, kitakachomponza labda ni ile flipy floppy ya Ana Makinda!.
  6. Tufike mahali moja ya sifa za nafasi ya uspika iwe kusomea sheria kiwango cha LL.M!.
Pasco

Yote uliyoyasema upo sahihi. Lakini angejiondoa kwanza kuwa NMS ndipo agombee uspika.
 
Ag ni mwanasiasa kwa nature ya nafasi yake.Spika sio mwanasiasa,hvyo hakuna kosa wa kasoro.Ameomba nafasi hyo kupitia CCM km ambavyo angeweza kuomba kupitia ACT,NLD n.k.

Kaka una uhakika na ulichokiandika hapo juu? Hefu fatilia fact zako vizuri
 
Si kosa la huyu Dada, ni mambo ya Rais mstaafu Mh. Dr Kikwete na uteuzi wake usio kuwa na mipango (not programmed). Dr Tulia Ackson alidhamiria kugombea Uspika kutokana na kuendesha Bunge la Katiba vizuri ktk nafasi yake. Ghafula anatunukiwa Unaibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Jamhuri wa Muungano wa Tanzania. Ukweli hiki ni cheo kikubwa kuliko uspika na hakina longolongo halafu uspika watu washasema wakikatwa wataenda mahakamani. Dr Tulia Ackson hakushauriwa vizuri angetakiwa aachie hii lengo lake maana tayari ni Deputy Attorney General. Pia ni kulinda heshima kwa aliyemteua. Dr Tulia Ackson I like you are educated you are not sick with Elimu Elimu Elimu disease. Merit your status you are Deputy Attorney General
 
Si kosa la huyu Dada, ni mambo ya Rais mstaafu Mh. Dr Kikwete na uteuzi wake usio kuwa na mipango (not programmed). Dr Tulia Ackson alidhamiria kugombea Uspika kutokana na kuendesha Bunge la Katiba vizuri ktk nafasi yake. Ghafula anatunukiwa Unaibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Jamhuri wa Muungano wa Tanzania. Ukweli hiki ni cheo kikubwa kuliko uspika na hakina longolongo halafu uspika watu washasema wakikatwa wataenda mahakamani. Dr Tulia Ackson hakushauriwa vizuri angetakiwa aachie hii lengo lake maana tayari ni Deputy Attorney General. Pia ni kulinda heshima kwa aliyemteua. Dr Tulia Ackson I like you are educated you are not sick with Elimu Elimu Elimu disease. Merit your status you are Deputy Attorney General

Ndugu Spika ni cheo kikubwa sana kuliko AG au Deputy AG. Dora ina mihimili mitatu, bunge, mahakama na serikali. Serikali na raisi, mahakama na jaji mkuu na bunge na Spika.
 
Kwa sababu hii nchi wajinga ni wengi kutokana na kunyimwa elimu. Acha tu iwe hivyo
 
yeyote anaejua sheria inasema nini hawezi bwana!!!katiba inasema nini!!!waziri,naibu wazir!!hana sifa za kuwa spika au naibu spika,AG ameshateuliwa je kuna mahari pameandika NAIBU AG ameteuliwa!!!alikuwa serikali iliyopita c sasa!!dr atkson anazo sifa kwani ni mtu yeyote awe mbunge au la!!atokane na chama chenye wabunge wengi au atakaungwa na 2/3 ya wabunge wengi!!JIPIMENI KWA HOJA ZENU HAFIFU!!!
 
Kaka kanuni na sheria ziko hivi, kwa cheo chake alichonacho cha kiserikali (naibu Mwanasheria Mkuu) hauruhusiwi kujihusisha na mambo ya kisisasa au kuwa mwanachama wa chama chochote cha kisiasa, sasa anapoenda kuchukua fomu za kugombea Uspika kwa mgongo wa CCM hili hali bado ajatoka serikalini hilo ni kosa
Hakuna sheria Tanzania iliyo juu ya CCM otherwise uchaguzi wa Zanzibar[sehemu ya JMT] usingekuwa batli lakini uchaguzi wa JMT uwe halali.
 
Back
Top Bottom