Dr. Steven Ulimboka anarudi leo saa sita mchana

Elishaosati

Member
Oct 31, 2010
8
5
Habari wadau, kwa taarifa za uhakika Dr.Steven Ulimboka anarudi nchini kesho, Madaktari wote na wadau wote mnaombwa kufika uwanja wa ndege saa sita na nusu mchana kwa ajili ya kumpokea jemedari, mtaarifu daktari mwingine!

Aliyekuwa M/kiti wa Jumuiya ya madaktari MAT anarudi leo siku ya Jumapili saa saba mchana kutoka Africa kusini alipokuwa akiendelea na matibabu, baada ya kutekwa na kuteswa vibaya na watu wanaosemekana kuwa hawajulikani. Akizungumza na wanahabari Katibu wa Jumuiya hiyo anasema kuwa leo kuanzia saa tano mchana madaktari wote pamoja na wanafamilia na wapenda haki wote tutakuwa viwanja vya ndege vya kimataifa vya mwl. Nyerere kwa ajili ya kumpokea kamanda wetu Dr. Steven Ulimboka.

Source Clouds radio




 
Ungeficha basi kaka..watategesha BEDFORD BOVU pale kipawa afe ajalini.BUT akaribie ila najua atapasua kila ki2.

Hiyo umeshaiona labda watumie mbinu nyingine!

Mkuu hatuwezi kuishi kwa kutishwa maana hiyo ndo mbinu ya adui(serikali ya CCM)

Tujitokeze tukampokee. Mapokezi tutakayompa ndo yatakayompa moyo zaidi wa kushirikiana na sisi wananchi kufichua ukatili wa vyombo vyetu vya usalama
 
kaka unamaanisha kesho ipi maana hivi sasa ni saa 6:50 usiku tarehe 12/8/2012 jumapili. maana wa TZ Wengi huwa hawatambui siku mpya mpaka waone jua. hebu tuweke wazi , shujaa ulimboka atawasili nchini jumapili au jumatatu?
 
Udaku mwingine bwana! Chanzo chako ni kipi? Au umetumwa na ikulu kupima mwitikio wa wadau? Shame on you!
 
Elisha nakufahamu sana, sidhani kama hii habari ni mahali pake hapa, kama vp itoe. Kama lengo ni kutupatia habari madaktari tunalo jukwaa letu pale fb ambalo ni closed. Mimi naomba utoe hii habari hapa.
Vp maandalizi ya harusi yako yanaendeleaje utaniona siku ya harusi yako. Nakumbuka tulikuwa tunasli wote pale JKM ila unakofungia ndoa nimechoka. Any way all the best na ufanye hivyo
 
Habari wadau, kwa taarifa za uhakika Dr.Steven Ulimboka anarudi nchini kesho, Madaktari wote na wadau wote mnaombwa kufika uwanja wa ndege saa sita na nusu mchana kwa ajili ya kumpokea jemedari, mtaarifu daktari mwingine!

Nasubiri mwendelezo wa ile filamu yetu iliyoko mahakamani
 
Unamaanisha atarudi jumatatu au jumapili leo. ULINZI upo vipi, mwambieni asipeane mkono na mtu yeyote ana avae bullet proof.
 
Ungeficha basi kaka..watategesha BEDFORD BOVU pale kipawa afe ajalini.BUT akaribie ila najua atapasua kila ki2.

Mmmmm..tulimsubiri Mwakyembe hivi hivi..mwisho akaja kusema tuviachie vyombo vya dola ambavyo awali alitamka wazi wazi kuwa hana iman nao..ha ha ha this z tz mpendwa wetu ulimboka keshapata kilema na kadri ninavyoona hakuna mtu aliyetayar ku reclaim damu fidia kwa ajil ya kilema alichokipa mpendwa wetu.
 
Nafanya intelejensia binafsi kuhakikisha Bwana Ahmed Msangi na Ramadhani Ighobu aka Rama,mtuhumiwa namb moja asionekane kitaa wala huko airport
 
Back
Top Bottom