Dr. Slaa ziarani Marekani

Dr. Slaa ziarani Marekani

Katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo - CHADEMA, Dk. Willibrod Slaa ameondoka nchini jana (Jumamosi Aprili 11, 2015) kuelekea nchini Marekani ambako atakuwa na ziara ya kikazi ya siku tisa. Dk. Slaa katika safari hiyo ameambatana na mkewe Josephine Mushumbusi.

Ziara hii ya siku tisa ni mwaliko wa Gavana wa Jimbo la Indiana Mike Pence pamoja na taasisi mbalimbali za nchini humo ikiwemo vyuo vikuu kutokana na kutambua mchango wa kisiasa na kijamii wa Dr Slaa na Chadema katika maendeleo ya bara la Afrika na kipekee nchini Tanzania. Ziara hiyo itamwezesha Dk. Slaa kushiriki mijadala mbalimbali inayohusu uwekezaji, elimu na uongozi iliyoandaliwa kwa ajili yake ambayo lengo lake kuu ni kuitangaza Tanzania kwa ukamilifu wake.

Kwa malengo hayo, Dk Slaa atafanya mihadhara (Public Lectures) kwenye vyuo vikuu vya Purdue, Indianapolis na Marion. Sanjari na mihadhara hiyo, Dk Slaa atakua na vikao vya mashauriano na baadhi ya Maprofesa waadhiri wa vyuo vikuu mbalimbali kwa lengo la kubadilishana uzoefu juu ya masuala ya kisiasa na maendeleo na kijamii na ushiriki wa Chadema katika siasa za Kimataifa.

Zaidi, ziara hii itamkutanisha pia Katibu Mkuu na viongozi na watendaji wakuu wa kiserikali na makampuni mbalimbali pamoja na taasisi kubwa za uwekezaji kwa lengo la kubadilishana uzoefu katika masuala ya uchumi na uwekezeji Barani Afrika na kwa kipekee Tanzania.

Imetolewa na:
Deogratias Munishi
Kurugenzi ya Mambo ya Nje
 
Nachukia viongozi wanaojikomba kwa wazungu naanza kimtilia mashaka nae maana wazungu watumia viongozi wete kutuibia tu watamwambia lipi lenye wema kwa waafrika, kwani ahamini sisi tutampeleke ikulu kwa kura zetu na sio kujikomba kwa misada ya kinafiki.yaleyale kama waliopita ujinga tu.
 
Dr. Slaa jana alianza ziara ya siku 9 chini Marekani ambako amealikwa na Gavana wa jimbo la Indiana.

Akiwa huko Dr. Slaa atakutana pia na maprofesa mbali mbali na kutoa mihadhara mbalimbali kuhusu masuala ya uwekezaji, uchumi nk. pia Dr. slaa atakutana na viongozi mbali mbali wa serikali ya Marekani.

Hongera sana Dr. Slaa...

Huyu Bubu kaenda lini America???
 
Nenda kyerwa ukaone wahaya wanachadema,kuanzia M/ kiti wa vitongoji,mtaa,kijiji na Madiwani,
Lwakatare ni Mhindi? Au unaongea bila kufanya utafiti?

Hao wote wamechanganya damu.
Sio wahaya Asili.
 
Rais wetu - go DR. goo....

Mwezi October si mbali - safari hii lazima watakaa.

Na mkileta Zile fujo zenu za Kitoto tutawapiga tu! Ndio ee! Manake adabu hamna, na We ndio wa kwanza kutiwa ndani ya FUSO na kandambili zako utazivaa mikononi.

Tunawasubiri tu CDM muanze fujo baada ya Huyo Slaa Kupigwa Chini Vibaya mno.
 
Last edited by a moderator:
Na Lipumba kakubali kuiua CUF kwa kuwapa nafasi kugombea urais watu wa chagadema! sasa UKAWA ndio umekwisha rasmi na chagadema mmeshateua mgombea wenu! poleni wana CUF.

Keweli mkuu cuf inapotea mda sio mrefu, hawa chadema wana hila sana. Cuf wasiposishituka watapotea kabisa
 
Keweli mkuu cuf inapotea mda sio mrefu, hawa chadema wana hila sana. Cuf wasiposishituka watapotea kabisa

Ndio wameshapotea hivyo! eti hata wanachama wa CUF wanaogopa kuitwa wasaliti na M/Kiti wa chama ambacho sio chao! yaani Mbowe akikohoa tu, wote kimyaaa!
 
Wanapopanga ziara za ng'ambo wakumbuke kuna viongozi wa chama wanajitolea. Wafikirie walau kuwapa posho kidogo, ruzuku isiishie kwenye ziara za ulaya na marekani.
 
Saccos kwa kuchoma pesa nawakubali.Ngoja October muone ruzuku yenu itakavyoporomoka.Lazima kila mtu atachagua mlango wa kutokea.Wamburu kivyao na Wachaga kivyao.

Unaumwa na nini au ndo umbea umbea tu. Na kwa staili hii wachaga wataendelea kuwa Superior class. Na watakuoa wakipenda. We kalia umbea!
 
Back
Top Bottom