Dr. Slaa: Uongo ni dhambi na siko tayari kuishiriki!

Dr. Slaa: Uongo ni dhambi na siko tayari kuishiriki!

Dr. Willibrod Slaa

Public Figure
Joined
Jul 1, 2008
Posts
675
Reaction score
1,524
Yericko,

Siasa ya unafiki sipendi. Nimenyamaza lakini naona mnazidi kunichokoza. Ni afadhali mngelikaa kimya kama nilivyonyamaza mimi. Uwongo wowote na upotoshwaji wowote sitauvumilia. Nitaukanusha hapo hapo. Hata kama una lengo lako ambalo silifahamu naomba sana usitumie jina langu. Nimefundishwa uwongo ni dhambi siko tayari kushiriki dhambi hiyo.

sina kikao chochote cha Secretariat sina mpango wowote ninaopanga kuwasilisha popote. Naomba watanzania wapuuze propaganda zote zinazofanyika kwa jina langu.

Ningehitaji kutuma taarifa yoyote kwa umma ningeliita Press Conference Mwenyewe au ningelitumia utaratibu wowote uliouliozoeleka.

Naomba kutoa onyo kwa mtu yeyote awaye, matumizi ya jina la Dr Slaa yakome.
Jioni ya leo Dr. Slaa katibu mkuu wa CHADEMA atawasilisha mpango mkakati wa ushindi mbele ya sekretariet tayari kuelekea cc kesho.

Hatua hiyo inafuatia jopo la wataalamu nane likiongozwa na Dr Slaa kujichimbia kwa wiki nzima kuhariri na kuchakata taarifa mbalimbali za umoja wa vikosi kazi vya vyama vinavyounda UKAWA,

Japo maneno na uzushi mwingi umezagaa mitaani lakini Dr hayumbishwi na hilo, mida ya usiku wa leo atawasilisha ripoti hiyo katika vikao vinavyofanyika kwa siri kubwa ili kuepuka maadui ambao kwasasa tunapigana vita nao usiku na mchana.

Kesho ndio rasmi Dr. Slaa atawasilisha mbele ya cc mipango mkakati hiyo ikiwemo Ilani nk.

Pipoooooooz!!!!

==========
Moderator:
Baada ya wadau kutaka maoni ya Dr. Slaa yajitegemee na hoja ya Yericko ifungwe, tumeona ni vema kuiweka hoja hii ikijitegemea kama ilivyopendekezwa. Majibu ya msingi yapo hapa
 
Yeriko,

Siasa ya unafiki siipendi. Nimenyamaza lakini naona mnazidi kunichokoza. Ni afadhali mngelikaa kimya kama nilivyonyamaza mimi. Uwongo wowote na upotoshwaji wowote sitauvumilia. Nitaukanusha hapo hapo. Hata kama una lengo lako ambalo silifahamu naomba sana usitumie jina langu. Nimefundishwa uwongo ni dhambi siko tayari kushiriki dhambi hiyo.

Sina kikao chochote cha Secretariat, sina mpango wowote ninaopanga kuwasilisha popote. Naomba watanzania wapuuze propaganda zote zinazofanyika kwa jina langu.

Ningehitaji kutuma taarifa yeyote kwa umma ningeliita Press Conference Mwenyewe au ningelitumia utaratibu wowote uliouliozoeleka. Naomba kutoa onyo kwa mtu yeyote awaye, matumizi ya jina la Dr Slaa yakome.

Huyu ndiye Slaa ninayemfahamu! Pia tusome andiko la mdau Candid Scope hapo chini ambalo Dr Slaa kwa kutumia ID hii hii ali-like.



30th July 2015 15:21
#1 ​
JF Senior Expert Member


Join Date : 7th November 2010
Posts : 11,718
Rep Power : 366017298
Likes Received6553
Likes Given4596​


[h=2]Udikteta wa Mbowe: Msuguano Slaa na Mbowe waitikisa CHADEMA, Mafisadi wamteka Mbowe[/h]
LOWASA-2.jpg

Viongozi wakuu wa Chadema hawapo ila Mbowe peke anaonekana kubanana na Lowasa​
Wimbi la kuanzishwa chama cha ACT kulikuwa na mengi yaliuyoongelewa kuhusu udikteta ndani ya Chadema unaofanywa na Mbowe, pia kwamba kuna msuguano kati ya Mbowe na Slaa, ingawa ilikanushwa lakini ufa huo unaonekana kujitokeza sasa.

images

Kilichoendelea ni CHADEMA kuonekana kumwandaa Slaa kuwa mgombea wa Urais. Pia Slaa kuonekana kukubalika kimataifa hata kualikwa na mataifa makubwa au jumuia za kimataifa duniani kama Marekani, Ujerumani na Umoja wa nchi za Ulaya.


images

UKAWA ilionekana NCCR wako radhi Dr Slaa awe mgombea, ila upade wa CUF Lipumba hakuridhika na alitaka yeye agombee. Mbowe alipoonekana kumilikiwa na kisha kummiliki Lowassa kuwa mgombea, Lipumba akapoa kwa vile wote yeye na Slaa wamekosa, huko alikokuwa mafichoni akajifichua na kuanza kuonekana katika vikao vya UKAWA.


images
images

Mgawanyiko Kamati Kuu CHADEMA kutokana na Lowassa

Katibu Mkuu Slaa, makamu wake bara John Mnyika na Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA Tundu Lissu hawakushiriki mapokezi ya Lowassa wakati walionekana wako na moyo kwa mapokezi ya Lembeli na wengineo. Dalili kwamba Lowassa ni chaguo la Mbowe na kushinikiza kamati kuu waridhie matakwa yake.

images

Mbowe amkumbatia Lowasa anayewawakilisha Rostam na Chenge

CHADEMA ilijipambanua na kueleweka kwa umma kwamba wako kinyume kabisa na ufisadi na katu hawatakaa sahani moja na mafisadi, lakini leo Freeman Mbowe anakula sahani moja na fisadi Lowasa anayewakilisha mafisadi wenzake akina Rostam Aziz na Chenge.

mapacha-watatu-560x248.jpg

LOWASA AKWEPA MASWALI YA WAANDISHI KUHUSU KUWAKUMBATIA MAFISADI WENZAKE

Katika tukio la kukabidhiwa kadi za Chadema, Lowasa alipoulizwa na waandishi kuhusu yasemwayo na watu kwamba akiwa Rais atawakaribisha mafisadi wenzake Chenge na Rostam, hakujibu akakwepa na kusema tu anachukia ufukara na anataka watanzania wengi wawe matajiri. Hapo kuna jambo ambalo dhahiri analikwepa kuliweka wazi kuhusu uhusika wake kugombea urais nyuma yake wakiwamo mafisadi Chenge na Rostam. Akishakalia kiti cha magogoni ni mfalme nani wa kumnyoshea kidole?

images
images


Lowasa kukaribishwa CHADEMA na UKAWA badala ya uongozi CHADEMA

Lowasa akaribishwa na kukabidhiwa kadi ya Chadema na UKAWA badala ya safu ya uongozi wa Chadema. Jambo la kufikirisha na kuonyesha dhahiri kuna msuguano fulani na kwa vyo vyote jibu litapasuka maana uvundo huu hauwezi kuendelea muda mrefu.

Zengwe la kuteua mgombea urais CHADMA
Imedhihirika Mbowe ana kauli ya mwisho nani achukue fomu ya kugombea urais na bila yeye kuidhinisha haitafanyika na ndivyo ilivyotokea, wakati huo huo yeye Mbowe alishakuwa na mgombea wake fisadi Lowasa.

Wakati watanzania wakiwa na kiu ya kutangaziwa mgombea urais kwa tiketi ya Chadema mazingira tatanishi yameendelea kwa kuchelewesha kwa makusudi hadi Lowasa alipokatwa CCM Mbowe akamkumbatia.

CHADEMA IMEPASUA UFA MKUBWA MUHIMU KUZIBA HARAKA
Siyo siri na wengi wamebaki kunyamaza kuangalia movie inayoendelea huku Mbowe akijipongeza kumpata fisadi Lowasa huku wengi wa wanakamati kuonekana kutomwunga mkono na mgomo baridi ni pale waliposusia tukio la kumsafisha Lowasa Buguruni ofisi za CUF kisha kufuatiwa na tukio la Lowasa kukabidhiwa kadi za Chadema BahariBeach Hotel. Huko kote aliyekuwa kifua mbele toka Chadema alikuwa Mbowe wakati watendaji wakuu wengine wa chama wakisusia.

Mbowe na Lowassa watafanya nini mkutano mkuu wa CHADEMA ukimkata Lowassa?
Mkutano Mkuu wa Chadema una nafasi ya kumchagua mgombea kiti cha Urais kwa kura na si kwa shinikizo la mwenyekiti. Iwapo Dr Slaa ataamua kuchukua form za Kugombea Urais kadiri ya msukumo wa wanachama wengi wa Chadema na watanzania, kisha mkutano mkuu ikatokea kumkata Lowasa chaguo la Mbowe nini hatima ya Lowasa na Mbowe atajisikiaje ndani ya Chama?

MBOWE KAIDHALILISHA CHADEMA/TANZANIA NA KUKIPASUA VIPANDE VIWILI
Mbowe amekidhalilisha chama chake kwa kumkumbatia Lowasa kinyume cha maadili ya chama chake na bila ridhaa ya chama chake chenye haiba ya kupinga kwa nguvu zote ufisadi nchini. Asipokatwa Lowasa mpasuko huu umeshajidhihirisha kutoka ndani ya Kamati kuu, hakuna hasara ya kumtosa Lowasa kwa vile Chama kilikuwa na mshikamano kabla ya Lowasa. Kimsingi ujio wa Lowasa umesababisha mpasuko mkubwa wa wanachadema na watanzania wapenda mageuzi nchini.

CCM IMEWEZA KUWADHIBITI MAFISADI HAWA CHADEMA IMETEKWA NA MAFISADI
CCM waliweza kulithibiti hili kundi la mafisadi wanaotaka kumpitisha mmoja wao kuwa Rais wa nchi, lakini Mbowe kaingia kichawakichwa na hatimaye umakini usipokuwepo kumkata Lowasa utawala wake utakuwa wa maumivu kuliko tunachoshuhudia sasa hivi utawala wa Kikwete.
Lowasa ni mfalme si mtu wa kukaa kujadili na watu nini kifanyike ila anaonekana ni wa mfumo wa kifalme kutoa amri.

Akiwa rais atawaingiza na kuwapatia nafasi nyeti mafisadi wenzake, nani wa kumnyoshea kidole wakati katiba inamlinda?​



Udikteta wa Mbowe: Msuguano Slaa na Mbowe waitikisa CHADEMA, Mafisadi wamteka Mbowe
 
Last edited by a moderator:
Ndugu wa JF.
Bila kumung'ukumung'unya maneno na pia kutokana na propaganda chafu za wakina Yeriko na Makene mitandaoni, nalazimika kuusema ukweli. Dr. Slaa ameamua kupumzika kulinda Principals zake na heshima yake.

Mbaya ni kwamba, pamoja na kunyamaza, kuna kundi maalum chini ya mbowe, imewekwa kumdhuru huyu mzee ndio maana akaamua kutafuta usalama zaidi. Napinga kwa nguvu zote hii tabia. Kuna waraka wa siri unaozunguka kuhusiana na mkakati huu.

Kwa kifupi mbowe, jaribu kuwa na huruma. Madaraka ni ya muda tu. Endelea na Lowassa mchukue nchi. Slaa hana shida nanyi. Hawezi tu kukaa na mafisadi
 
Back
Top Bottom