Dr. Slaa tolea maelezo hii picha tafadhali

Dr. Slaa tolea maelezo hii picha tafadhali

Status
Not open for further replies.
siasa za kitoto sana hizi,hivi dr slaa haruhusiwi kuongea na mtu yeyote wa ccm?kwani siasa ni ugomvi?kuna jamaa aliposti picha na maelezo kwamba dr slaa na prof lipumba walialikwa na kiongozi wa ujerumani ktk hoteli ya hyatt kuwakilisha vyama vyao na ukiangalia hizo picha zote utaona tu ni zile zile.tatizo chadema mmekubali kutawaliwa akili zenu na mbowe,hiki chama mbowe anakiuwa.mtakuja kushtuka mkiwa mmechelewa sana.
 
Ukweli wa huu upuuzi wa Mungi ni huu hapa. Mungi na wenzako njooni mjikanyage. Angalieni hizo suti za kwenye picha ya Mungi na hii niliyoweka

image.jpg
 
Alijua tutaunga mkono..mtu anasema ameacha kazi Chadema wakati salary ya August kavuta na karamba.rudisha mshahara wetu mzee

Tena bila aibu eti nimeacha kazi tangu July,huku anajua fika kabisa kavuta mshahara wa August,Mungu hamfichi mnafiki,shame on him!
 
Hii ni kweli???Wapige kampaign bwana waache babu akapumzike...mabadiliko kwanza mabadiliko baadae...Sasa baada ya kustaafu siasa nyumba na gar la CDM anarudisha au?

Lazima arudishe msaliti mkubwa huyo
 
Siasa ni mchezo kama michezo mingine. Na kila mchezo lengo ni ushindi. Tunapokuja kwenye siasa lengo la chama cha siasa ni kushika dola. Mfano vyama ambavyo vilipata dola kwa njia tofauti ni kama FRELIMO, SWAPO, ANC na wengineo wengi. Hivi vilikuwa ni vyama ambavyo vilishindwa kwenye medani ya democrasia vikaingia kwa njia ya mapambano. Lakini kuna vyama vingine kama TANU, UNIP na vingine vyenyewe viliendeleza harakati zake kwa mdomo tu lakini vyote lengo ilikuwa ni kushika dola na kila kimoja kilifanikisha kwa kupitia njia yake na waliposhika dola kila chama kilianza kufanya kile walichokiamini kina manufaa kwa wananchi wake. Tukija kwenye mpira mchezo ni ule ule. Mfano timu inapopanda daraja utakuta wachezaji wale walioipandisha wanaachwa hata kocha pia wakati mwingine huachwa. Wakati mwingine wanasajili wachezaji kutoka timu pinzani ili waweze kushindana na kushinda mechi. Tulitegemea wale waliopandisha timu wachukuliwe lakini hutokea baadhi huachwa.

Sasa tukirudi kwenye siasa vyama vya upinzani hapa nchini vilifikiria ufisadi au kinyesi kwa jamii yetu ni kitu amabacho hakikubaliki. Lakini vyama kama CHADEMA, CUF, NCCR, NLD na vingine vilihubiri kwa zaidi ya miaka 8 vikitaja mafisadi papa na chama kikaitwa ni chama cha mafisadi (CCM) lakini jamii katika chaguzi tatu ambazo zimefanika kutokea 2007 hadi 2015 kumefanika chaguzi 3 mbili za serikali za mitaa na moja serikali kuu. Na katika wakati huo Dr. Slaa aliongoza kuhamasisha mafisadi na chama cha mafisadi wanyimwe kura lakini wananchi waliwapa hao hao mafisadi na chama kile kile cha mafisadi. Kwa maana nyingine kile ambacho Dr. Slaa anaona ni choo au kinyesi wananchi ndiyo ilikuwa chaguo lao na wao huku waliokuwa chumba kizuri chenye kiyoyozi na manukato (kwa Dr. Slaa) wananchi hawakwenda au hawakuchagua kukipigia kura.

Hivyo, nafikiri wakati huu ni wa kutambua wananchi wanataka nini? Sio wakati wa kuchagua choo au chumba yenye manukato. Kwani wananchi wenyewe wameishachagua choo ndio mahali muafaka. Na mimi ningependekeza wale mafisadi papa wangeongezeka wengine 7, maana wamekuja wawili tu. Wakiongezeka tutakuwa na uhakika wa UKAWA kupata ushindi.

HITIMISHO: Dr. Slaa anatakiwa atambue kuwa hapa alipoifikisha CHADEMA inatosha hivyo inabidi awaachie wengine waendeleze na siyo kulalamika kwa sababu huu ni mchezo na kinachotakiwa ni ushindi. Hatuhitaji habari za KUFUNGWA TWAFUNGWA LAKINI CHENGA TWAWALA!
 
Masaa machache yamebakia ili (UKAWA) Waongee na wanahabari juu ya Tuhuma dhidi yao zilizotolewa na Dr. Slaa.
Updates...
Mbatia anaongea sasa
Fuatilia matangazo ya moja kwa moja AZAM TZ
AZAM Media Flash Page
Dr. Slaa anaendesha siasa za mitaroni.
Tanzania ni yetu sote na siyo mali ya chama cha mapinduzi
Kamati kuu ya CHADEMA walishamteu Dr. Slaa kuwania uraisi, CUF walimtea Pro. Lipumba kabla ya Lowassa kabla kuhamia CHADEMA
Dr. Slaa alisema yeye alikuwa bora kuliko wagombea wengine hivyo lazima apewe kijiti cha UKAWA
============
Dr Slaa alisema yeye ni bora kuliko wengine na alikuwa anaulilia Urais kwa nguvu kubwa, karibu kikao kivunjike kwa kutokukubaliana. Colisium hotel tulitakiwa tutangaze mgombea urais, Slaa aliomba msinitangaze leo, leo anasema hajawahi kutia nia, anasema siasa ni sayansi. Nilikuwa nimtangaze tarehe 14 wakati huo Lowassa hajaingia CHADEMA. Aliyeenda hadhari kumtaka Lowassa agombanie urais 27/7/2015 alikuwa James Mbatia, aliehariri alikuwa Pro Lipumba na namheshimu kwelikweli mpaka kesho.
Hizi hoja nyepesi za kutaka kulipasua taifa la Tanzania badala ya kuleta umoja wa kitaifa. UKAWA tunasimamia uadilifu, umoja, uwazi, uwajibikaji, tunawataka watanzania wote tuje pamoja, tuwe kitu kimoja. Niwaombe watanzania kwa nia njema, kila mtu ana haki ya kutoa mawazo yake lakini wanansiasa hasa wa CCM, nawakaribisha kwenye midahalo Mzee sitta alijenga ofisi ya spika Urambo, Je kuna ofisi ya spika Urambo, ndio maana nawaambia hakuna atakaepona hapa. Magufuli ni rafiki yange sana tangu chuo kikuu, alichangia harusi lakini leo hii tukimwambia aeleze kashfa ya uuzaji wa nyumba za serikali, atapona?.
 
siasa za kitoto sana hizi,hivi dr slaa haruhusiwi kuongea na mtu yeyote wa ccm?kwani siasa ni ugomvi?kuna jamaa aliposti picha na maelezo kwamba dr slaa na prof lipumba walialikwa na kiongozi wa ujerumani ktk hoteli ya hyatt kuwakilisha vyama vyao na ukiangalia hizo picha zote utaona tu ni zile zile.tatizo chadema mmekubali kutawaliwa akili zenu na mbowe,hiki chama mbowe anakiuwa.mtakuja kushtuka mkiwa mmechelewa sana.

Wewe ndiyo umefungiwa ndani ya box na ccm
 
Waswahili wanasema, wekeni akiba ya maneno.

attachment.php

Ahh ndugu hii picha yaani kabisa I adobe \

La kwanza picha ya lipuba haiwezekani kichwa kihongeke nyuma kama picha ya kchora
La pili Mkono wa Lipumba wa Kulia haiwezekani ugusane na slaa kiasi hiko wakati haw watu wao katika motion ya mazuumzo
tuifunze ku edit picture
 
siasa za kitoto sana hizi,hivi dr slaa haruhusiwi kuongea na mtu yeyote wa ccm?kwani siasa ni ugomvi?kuna jamaa aliposti picha na maelezo kwamba dr slaa na prof lipumba walialikwa na kiongozi wa ujerumani ktk hoteli ya hyatt kuwakilisha vyama vyao na ukiangalia hizo picha zote utaona tu ni zile zile.tatizo chadema mmekubali kutawaliwa akili zenu na mbowe,hiki chama mbowe anakiuwa.mtakuja kushtuka mkiwa mmechelewa sana.

mkuu usiyaamshe acha yatoe povu lakn mwisho wa siku watakuja kujiona wapumbavu
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom