Dr. Slaa: Sina Mpango wa kugombea Urais 2015

Dr. Slaa: Sina Mpango wa kugombea Urais 2015


Katibu Mkuu wa Chadema Dk Wilbrod Slaa



DK. Willbroad Slaa "Sifikirii kuelekeza nguvu zangu kwenye kuwania urais 2015 wapo watu wengi wenyesifa ktk kundi la UKAWA.Kila kitu kitafanywa kwa wakati muafaka,kazi iliyopo mbele yangu ni kupigania umoja wetu wa UKAWA ili kuleta ushindani wa kweli katika uchaguzi 2015.



Akizungumzia hatua ya UKAWA kususia Bunge Maalumu la Katiba Dk. Slaa alisema umoja huo uko sahihi kwani umesimama upande wa wananchi, niaheshimu uamuzi wa Viongozi wangu Mh Freeman Mbowe Prof Ibrahim Lipumba na James Mbatia.


UKAWA imebeba maoni ya wananchi na suala la kutengeneza Katiba sio suala la rais,serikali wala chama chochote bali ni la wananchi.


Serikali ina viongozi vigeugeu kwa sababu ni wao ndio waliosaini rasimu ya Katiba mpya, lkn cha ajaabu wao ndio wanageuka na kutaka yajadiliwe mambo ambayo hayamo ndani ya rasimu ya Tume ya Jaji Joseph Warioba."


Chanzo:Mtanzania Juni 11-2014


My take😀r slaa ni kiongozi mtiifu


mzee wa watu hana hata makuu na nokia yake ya tochi
 
nani kakwambia za ubunge hazikuibiwa,mlikimbia na masanduku ya kura na sehemu nyingine mmeua watu na kutangaza washindi kwa nguvu,sehemu mlizokubali kushindwa ni zile ambazo nguvu ya umma ilishinikiza mkaona hamna jinsi mkakubali yaishe....

kuna yule jamaa sijui anaitwa masele alishinda kwa tofauti ya kura moja,mwingine kule kusini alimshinda mpinzani wake kutoka CUF kwa tofauti ya kura Tatu.hii miccm ni we I sana wa kura.
 
hyo ndo sauti ya kamanda angurumapo magamba yote yanajikojolea.......
 
mkuu hivi ulishasikia kauli yoyote ya JK kumkandia DR??? kabla au hata baada ya Matokeo ya Uchaguzi 2010?

Tafakari... JK anaona mbali sana.

JK hawezi kumsema vibaya mtu aliye mpora Urais. Anajitahidi sana kumkwepa kwa maana Kila akimwona dhamiri inamshitaki
 
JK hawezi kumsema vibaya mtu aliye mpora Urais. Anajitahidi sana kumkwepa kwa maana Kila akimwona dhamiri inamshitaki

Tupe takwimu kula zilizo ibiwa ningapi? Acha upofu
 
Hata akigombea atapoteza muda wake bure watanzania wameisha wajua Chadema ni matapeli wa kisiasa.
Mkuu Ritz, hebu nipe darsa kuhusu uhusiano wa iliyokuwa TANU ya wazee wa Tambaza na CCM ya akina Nape.
 
Amejipima kakwama baada ya kusikia jina la Prof sasa anajiona kinda! Aliyeshindwa kanisani kwa Mungu leo aweze kuongoza ya duniani - "Ole wa Nchi na Bahari maana yule mshitaki wenu..." So, aliyefungiwa duniani awezeje kuongoza umma! Asiyeweza kuuza alichonacho na kuwagawia maskini leo eti aweze kuongoza watu!
 
Amechoka sana angalia ngozi ilivyochujuka duuh uzee wote huo kwanini asitulie?
 
Huyu mzee analipwa pesa za ubunge kama kawa na cdm.wewe hujui hilo kaa kimya.

Hizo pesa za ubunge analipwa na mama yako? Acha longolongo jadili jambo ulilo na uhakika nalo sio stori za mabanda ya kuuzia makubazi na kanzu
 
Back
Top Bottom